Ijumaa, 24 Julai 2026

Kutumika kwa mda wa sasa. Kuomba kwa ajili ya wakati ujao

 








    Jambo kwa wote. Naitwa Dean Davis, na munasikiliza ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Wakulima na wapandaji wa makanisa wanakuwa na vitu vingi vya kufanana.

Wote wawili wanatumika kwa imani. Moja kama mwengine hakuna anayejuwa kwa uhakika kama kazi wanayoifanya leo itazaa mavuno kwa myezi inayokuja.

Ijapokuwa, wote wawili wanatumika kwa bidii leo kwa matumaini yakupata mavuno mengi kwa Siku chache baadaye.

Wakulima wanalima udongo siku baada ya siku ili kuitayarisha kwa kupanda mbegu. Wanapanda kwa makini sababu mbegu zipate kukomaa na kutowa mavuno. Wanaboresha ukulima ili kuondowa majani mabaya, na wakati wamavuno inapofika, wanatumika kwa bidii ili kuvuna kila mbegu.

Ni kwa namna hiyo, wapandaji wa makanisa wanatumika kwa juhudi leo kwa matumaini yakupata mavuno mengi kwa myezi inayokuja. Wanatayarisha eneo wakiomba ili kwamba Mungu awakutanishe na watu wa amani. Wanapanda kwa hekima na kwa uhakika mbegu njema ya Injili kwa namna iweze kuzaa matunda. Wakati mbegu inapo pokelewa, inalinda mioyo ya waamini wapya kwa kuwafundisha kumtii Kristo. Wanawasaidia pia kuondowa majani mabaya ya shaka na kutokutii wale wanaotafuta kuzimisha imani yao kabla haijazaa matunda.

Wakulima wanatumainia mavuno mengi yatakayoleta chakula cha kutosha. Wanatarajia kwamba yote yatatendeka vizuri. Wanapendelea mvuwa inyeshe kwa mda muhafaka na kiwango cha kutosha. Wanatarajia mavuno mazuri ili waweze kufurahi pamoja na jamaa zao wakati mavuno yatakuwa  yamekusanywa.

Kwa namna hiyo, wapandaji wa makanisa wanapendelea kuona makanisa yenye afya yanapandwa, yakikomaa, kwa hesabu ya kila Siku watu wengi wanamjuwa Yesu na wanajifunza kuishi kama wanafunzi waaminifu. Wakipendelea hivo kwa siku zijazo, tunaomba. Tunaomba kwa ajili ya mavuno yajayo, tukimsihi Mungu kwa makini abariki, kwa kurizisha maitaji na kukingia kazi yake.

Kwa hiyo, wapandaji wamoja wanachukuwa mda mwingi wakifikiria siku zijazo, kwa kupangilia na kuomba juu ya baraka zijazo wakizarau kazi itakayotekelezwa leo. Wengine, kwa kinyume, wanamezwa na majukumu ya sasa hadi kusahau kupangilia na kuomba kwa kile kinastahili kutendeka kwa majuma wala kwa myezi michache ijayo.

 Tunastahili kupata usawa kati ya hizi hatuwa. Lakini ni kwa namna gani tutaifikilia ?

Namna gani wapandaji wapya wa makanisa wanaweza kupata usawa kati ya kazi inayotekelezwa leo na mpangilio pamoja na maombi ya siku zijazo ?

Mfano wa mashamba ine unaweza kukusaidia kuifikilia.

Wapandaji wanaofuata mfano wa mashamba ine wanajuwa kwa uhakikisho yake wanastahili kufanya leo. Wanatambuwa ''eneo'' ambako wanatumikia na kutekeleza majukumu yanayowastahili. Kwa wakati huo, wanatazamia kwa wasimamizi wanaowangoja kwa shamba mpya. Kwa hiyo, wanaweza kuomba ili Mungu atende, afunguwe milango na kuwabariki, ili wawe tayari kutekeleza haya majukumu mapya wakati mda utaruhusu.

Mtindo wa mashamba ine ni mwongozo wetu. Unatusaidia kukusanya nguvu zetu juu ya kazi ya leo pamoja na kupangilia na kuomba juu siku zijazo. Sasa, fuata mtindo wa mashamba ine katika kazi yako na katika maombi yako. Itakuongoza kwenye huduma ya upandaji wa makanisa ya kina zaidi.

Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis. Nawaacha na hili swali :

''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?''

Maendeleo ya Uongozi - Peter na Fidélité

 









            Tazama Chuck Rapp, na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji na viongozi wa makanisa katika vijiji.

Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Katika podikasti zangu tatu za nyuma, nilizungumuzia mawazo ya Claude, Kasisi wa VCP, kuhusu mchakato wa maendeleo ya Uongozi.

Wakati wa shauri tulilokuwa nalo hapa karibuni ya wa kurugenzi wa VCP pa Nairobi, nilimualika Peter Baraka, kasisi makamo wa VCP, pamoja na mke wake, Fidélité Ramla, Mkurugenzi wa Dynamic women kwa Bara la Afrika, ili kugawanya pamoja nami mawazo juu ya maendeleo ya Uongozi. Ni muhimu sana kwangu kuelewa na kuwasilisha mtazamo wa Kiafrika kuhusu mada hii.

Tulianza kujadili baadhi ya tabia za muhimu za kiongozi. Vipengele vya kwanza vilivyo onyeshwa ilikuwa : ''ni mnyenyekevu ? Anaongoza kwa upendo ? Ni mwaminifu ?''

Baadaye tuliongoza maojiano kwenye mchakato wa maendeleo ya Uongozi, na Peter alikazia nukta mbili za muhimu sana.

Anafundisha wale anao watayarisha kwa uongozi ''kulingana na mpango'' na anawachunguza ili kuona kwamba wanafuata vizuri mafundisho.

Pia Peter alieleza kwamba, kwa jukumu lake la Mkurugenzi wa VCP, anachukuwa mda mwingi kuelekea eneo la kazi ''akichunguza''.

Anauliza mara nyingi kwa waratibu kumwelekeza kwenye vituo vya mafunzo pia na kwenye makanisa yaliyopandwa, baadaye anachunguza kwa makini kama wanafahamu eneo zote. Kama hawazijue, hiyo inaweza kuonyesha kama hawatembelee eneo za kazi mara kwa mara.

Baadaye Fidélité alionyesha mtindo wa kutowa mfano, kusaidia, Kuchunguza na kuachilia. Kama kipindi cha muhimu kwa mafundisho ya viongozi wapya.

Haya mawazo yanashikamana na 1wakorinto 11:1, Paulo anaandika : "munifuaye mimi kama ninavyo mfuata Kristo.''

Alieleza kama anatayarisha kila siku mtu moja mwenye uwezo wa kuchukuwa wazifa wake kama akizuwilika. Akiwa Mwalimu, anawasilisha watu wengine kwenye mafundisho na kazi tofauti ili waweze kuangalia ginsi anavyotenda kazi. Kisha, anawaalika kumchunguza wakati anapoongoza.

Kwa mwanzo, anawapa majukumu yaliyo rahisi ili waendeleze pole pole ujuzi na uhakikisho wao.

Kipindi cha kufuata, Kuchunguza, kwa upekee ni kipindi muhimu kwa maendeleo ya viongozi wanaojitokeza.

Fidélité anawapa wanafunzi wake majukumu maalum ya mafundisho ao kazi ingine.

Japo hiyo, hana budi tu ya kuchunguza bila kusudi : anawashindikiza na mashauri na marudilio ya kujenga.

Anakazia kwa yale yaliotendeka vizuri na kuwapendekezea njia za kuboresha.

Baadaye kunakuja mda wa kuachilia. Kipindi hiki kinaweza kuwa kigumu, lakini ni cha muhimu sana. Tutaieleza zaidi kwa udondozi mtindo wa kutowa mfano, kusaidia, Kuchunguza na kuachilia katika podikasti ijayo.

Nafurahia sana Uongozi wa Peter na Fidélité, pamoja na utayari wao wa kugawanya haya mawazo pamoja nasi.


Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wa makanisa katika vijiji.

Maendeleo ya Uongozi - Maendeleo ya Uongozi

 










     Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Katika podikasti yangu ya nyuma, nilizungumuza na Peter Baraka, ni Kasisi makamo wa VCP, upandaji wa makanisa, pamoja pia na mke wake Fidélité Ramla, Mkurugenzi wa Dynamic women kwa Bara la Afrika, ili kupokea mawazo yao kuhusu maendeleo ya Uongozi.

Wakati wa majadiliano yetu, wamenisumilia hadisi ya kuchangamsha inayofanana na Mathayo 25. 14-30. Kwenye vesi ya 21na 23, tunasoma : ''

[21]Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 

[22]Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. 

[23]Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. 

Nilikutana na Robert kwa mara ya kwanza imepita sasa miaka saba, wakati wa safari ya CMF pamoja na Peter na Fidélité. Kwa kipindi hicho, alikuwa mkufunzi aliyetumika bila malipo, inamaanisha hakuwa na mshahara. Pamoja na mda kuwa mwingi alionyesha kuwa mwaminifu na mchapakazi. Miaka mingi iliyopita, Mkurugenzi wetu na Mratibu wa upandaji wa makanisa katika vijiji, Peter na Fidélité, walinieleza kwamba walitumika na kuchapa kazi  kwa makini.

Fidélité alionyesha kuwa kwa wakati fulani, Robert alitumikisha pesa zake kwa kugaramia kazi za huduma ya upandaji wa makanisa katika vijiji, ambayo inaonyesha kujitolea na upendo wake kwa kazi hii.

Mara nyingi alikuwa akisema : " hata kama hakuna mshahara, wataendelea japo hiyo kutumika ?''

Kwa miaka hii, Robert alionekana mwenye uaminifu katika majukumu aliyopewa, kama vile kutunza kuku alizopewa. Peter na Fidélité malinieleza pia kuwa mara nyingi waliuliza mashauri, sababu walitamani sana kuwa na ujuzi mwingi katika kazi ya kuwa Mkufunzi. Kwa kuambatanisha na podikasti za mwaka huu, alionyesha kiu kubwa ya kujifunza na kuendelea'' pamoja na moyo wa kukubali kufunzwa ''.

Peter na Fidélité pia waliniambia kwamba mawasiliano yao na huyu bwana, hata pamoja na watu wengine anaowaongoza, hayaishii tu kwa kazi. Wanachukuwa pia mda wa kuongea kuhusu maisha, kuendelesha mawasiliano ya kirafiki na kuwa shindikiza kwa jukumu la upastori.

Kwa kuhitimisha, turudilie kwa hadisi ya Robert. Wakati fidélité hapa karibu alikubali jukumu la kuwa Mkurugenzi wa Dinamic Women kwa Afrika, ilikuwa muhimu ku ajiri Mratibu mwengine wa upandaji wa makanisa katika vijiji katika inchi ya Ouganda. Robert, ambaye alikuwa kwa wakati ule Mratibu, alionekana kuwa mtarajiwa bora kwa kazi hiyo, sababu alionyesha uaminifu kwa majukumu aliyopewa.

Wakati walimpendekeza wazifa huo mpya, walimweleza wakati wa majadiliano na Robert pamoja na mke wake. Waliuliza mke wake kama alikubali, akijuwa kama haya majukumu mapya yatakuwa na athari kwa maisha yake. Kwa bahati nzuri, wote wawili walikubali wazifa huo.

Je ! Tunaweza sote kuwa waaminifu katika majukumu ambayo Mungu alitupatia. Kwa kutenda hivi, tunajiandaa kupokea wazifa mpya na kupandishwa vyeo wakati mda utafika.

Nafurahia sana Uongozi wa Pater na Fidélité, pamoja utayari wao wa kuongea pamoja nasi  haya mawazo yao mazuri.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji na viongozi wa upandaji wa makanisa katika vijiji.

Mwongozo wa mtindo wa mashamba ine

 








     Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis. Na munasikiliza ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Imewai kukufikia kuuliza kwa mwana muziki maarufu ''ni kwa namna gani unafanya ili kucheza namna hii?'' kama ni ndio, pengine alikujibu kwa swali lingine : ''namna gani ninafanya nini ?'' unamaanisha sasa : ''namna gani unajuwa ni kwa sauti gani utaimba ? Kufata mtindo gani ? Ni kwa namna gani unafikia kutunga muziki muzuri kwa kutumia chombo hiki ?

Wasaani wamoja watakujibu : '' hakika sijue. Niliangalia tu watu wengine wakicheza. Baadaye nikanunuwa chombo, nikaanza kujifunza, na sasa ninacheza tu.''

Mtindo huu unastahili kwa watu ambao kwa asilia ni wazoefu wa muziki, lakini siyo hivo kwa watu wengi. Baadhi ya watu wengi wanaitaji kufunzwa kwa mtindo maalum kama wangependa kucheza na chombo.

Ni hivo pia kwa wapandaji wa makanisa. Kuko wapandaji wa makanisa wenye uzoefu ambao walianza tu kuhubiri na kuwakusanya watu ili kuabudu Mungu. Waliangalia tu wachungaji katika huduma yao na wakaanza tu kupitiya hisia zao namna gani ya kupanda makanisa mapya, bila kupata mafundisho mengi. Lakini haina ya hawa wapandaji wa makanisa wako nadra, na, mara nyingi, hawajue ginsi ya kufundisha watu wengine kupanda makanisa. Kama vile wengi miongoni mwa wasaani wako na haja ya kujifunza kuchezesha chombo. Wapandaji wengi wa makanisa wanaitaji kufundishwa ili wajue kupanda kanisa.

Haina ya mashamba ine inahusu mafundisho ya msingi ambayo wakristo wakawaida wanaitaji ili kupanda na kuzidisha makanisa. Ni mtindo bora, sababu iko rahisi kuelewa na kurahisisha kuzalisha. Wote wanaoitaji kupanda makanisa watazidishwa nguvu kama wakichukuwa kila mara mtindo wa mashamba ine. Ndio kwa maana imechapishwa nyuma ya vitabu vya VCP kwa kila muhula. Imetengenezwa ili ichukuliwe kila mara na kugawanywa pamoja na wanafunzi.

Mtindo wa mashamba ine inajibu swali la ''ni wapi kwa kuanzia ?''

Utaanza na kuomba ili Mungu akusaidiye kupata watu wa amani ndani ya Kijiji ambako hakuna kanisa. Utaanza na hatuwa ya maombi. Hiyo inamaanisha kama utatembea Kijiji chote, macho yakiwa wazi na moyo mwangalifu, katika kuomba ndani ya Kijiji kilicho na itaji ya kanisa. Utaomba kwa  Mungu akuongoze kuelekea watu wa amani : watu wasikivu, wakaribishaji na wenye haja ya kumjuwa Mungu.

Mtindo wa mashamba ine inakuonyesha pia kile unastahili kufanya wakati unapata watu wa amani : msaidie kuweka tumaini lake kwa Yesu Kristo kama Mwokozi wake. Mufundishe Ku alika jamaa lake na maraflki kuja kusikia Habari Njema ya Yesu. Saidia kikundi hiki kujifunza kutii kwa yote Yesu aliyo amuru.

Kwa mwisho, mtindo wa mashamba ine inakufundisha kuandaa viongozi kwa ajili ya kanisa lako mpya na kuwatuma kwa vijiji vingine ambavyo havina kanisa ili waanze mchakato wote wakiomba na kutafuta watu wengine wa amani.

Kwa hiyo, mtindo wa mashamba ine ni mwongozo lakini pia ni mwongozo wa maombi. Tunastahili kumuomba Roho Mtakatifu atende kazi ndani ya kila moja ya  shamba hizi ine.  Tunaitaji msaada wa Mungu ili kupata watu wa amani. Tunaitaji msaada wake ili kutangaza waziwazi na nguvu Habari njema. Tunaitaji hekima ya juu ili kufanya wanafunzi na kufundisha na kuunda vikundi vipya vya maabudu. Na tunaitaji hakika msaada wa Mungu ili kuandaa na kutuma viongozi ili watumike ndani ya kanisa letu Jipya na wanapanda makanisa mengine ndani ya vijiji vingine.

Wakati unaendelesha kazi yako ya upandaji wa makanisa, acha mtindo wa mashamba ine ukuongoze. Pengine unajisikia kama hauna uzoefu, lakini Mungu atakusaidia kama ukiwa mwaminifu kwake na kutumikisha kwa mwisho mtindo wa mashamba ine kwa upendo mkubwa kwa watu wanaopotea.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Mimi ni Dean Davis, nawaacha na hili swali, ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

KANISA KATIKA KILA KIJIJI CHA AFRIKA

 









    Jambo kwa wote. Naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Kila mpandaji wa makanisa anajuwa maono ya VCP : "kanisa katika kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2050". Maono haya, inayojengwa juu ya Agizo kubwa ya Bwana wetu Yesu Kristo, inatowa mwelekeo kwa jumla na msingi kwa yote tunayoyafanya wakati tunatumika pamoja kwa kuzidisha wanafunzi, wasimamizi na makanisa.

Wapandaji wa makanisa, kwa mfano wa Mungu, hawapendi hata mtu apotee. Tunapenda wote wafikie toba. Tunajuwa kwamba Mungu hana upendeleo. Anapenda watu wote, popote. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtowa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. (Yohana 3:16). Tunapenda kuishi katika utakaso ; ndio maana tunachaguwa pia kupenda watu wa mataifa yote na kila mahali.

Kwa hiyo, ikifikia wakati wa kuhubiri Habari njema, mara nyingi vijiji vinazarauliwa. Wakaaji wa miji wako na fursa nyingi ya kusikia Habari Njema. Katika mikutano mikubwa, katika barabara kubwa, tunaona makanisa mengi. Lakini kupitiya hadisi, inachukuwa mda mrefu mbela ya Injili kufika katika vijiji. Waundaji wa huduma ya upandaji wa makanisa walijuwa hiyo.

Ndio maana waliweka kipaumbele upandaji wa makanisa katika vijiji.

Leo, uko miongoni wa hii vuguvugu inayosaidiwa na msemwa huu rahisi : "kanisa katika kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2050". Kila mpandaji wa makanisa VCP, kila mwanafunzi wa VCP, kila Mwalimu na Mratibu, kila kasisi, Mkurugenzi na mrahisishaji wa kuzidisha makanisa iko na kazi ya kufanya ili kubadilisha haya maono kuwa ukweli.

Mbele ya yote, tunastahili kuomba, tunapashwa kuomba Mungu ili ufalme wake uje na mapenzi yake yafanyike ndani ya kila Kijiji cha Afrika.

Tunastahili kumuomba ili kuwe kanisa katika kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2050. Baadaye, tunapashwa kujumulisha maombi kwa matendo. Kwa namna ingine, tunastahili kutenda kama wafanyakazi pamoja na Kristo ili kuona maono haya yakitekelezwa.

Kila mpandaji wa makanisa anaye chukuwa maono haya kwa uaminifu atajuwa ni vijiji gani vilivyo karibu na kituo cha mafundisho tayari viko na kanisa na ni vijiji ngapi havina kanisa. Kama weye na rafiki zako wapandaji hamujuwe kama ni vijiji ngapi vilivyo kandokando ya km 10 ao 20 ya kituo chako cha  mafundisho ambavyo bado havijakuwa na kanisa, uliza habari, wende katika kila Kijiji cha kutembea kutwa mzima kutoka kwenye kituo cha mafundisho na ugunduwe kama kuko kanisa ao hakuna.

Gawanya habari hizo pamoja na mkufunzi wako na wanafunzi wenzako. Ikiwezekana, uonyeshe hiyo kwenye ramani.

Baadaye, zidisha maombi kwa ajili ya vijiji vya kandokando ambavyo bado havina kanisa. Kila mwanafunzi wa VCP anastahili kuchukuwa majukumu ya kupanda makanisa ndani ya vijiji vinavyojulikana kuwa havijafikiwa. Tembelea vijiji hivyo kwa maombi. Muombe Mungu akuonyeshe watu wa amani, wanaume na wanawake walio na kiu ya kumjuwa Mungu na wako wazi kusikia Habari Njema. Gawanya ushuhuda wako, ombea wakaaji, uwasimulie hadisi za Biblia, onyesha filamu ya Yesu kwa baadhi ya watu ao kwa Kijiji chote. Uwe mwaminifu kwa Mungu ili akutumikishe, wewe pamoja na wenzako wa huduma, ili muanze kupanda makanisa yenye afya ndani ya vijiji ambavyo havina kanisa. 

Unaweza kufikiri kwamba juhudi yako haitabadilisha Afrika. Lakini wakati itajumulishwa na yale ya wengine maelfu ya wapandaji wa makanisa katika vijiji, watafanya utafauti. Mungu atakutumikisha kama chombo kubwa cha kazi yake kwa ajili ya kuleta maisha tele ndani ya Kristo kila mahali. Sababu inchi itajaa na ujuzi wa utukufu wa Bwana, kama maji yazavyo vilindi vya bahari (Habakuki 2;14). Amini hayo!

Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis. Nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

MIVIRINGO TATU ZINAMTAWAZA YESU KAMA MFALME

 









Miviringo tatu zinamtawaza Yesu kama Mfalme. Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Wakati nilijaribu kwa mara ya kwanza kuelewa Habari Njema ya Yesu, nilisikia kila mara wahubiri na waalimu wakisema kama ''tunastahili kumwamini Yesu''. Nilikuwa nikiona kupitiya shauku yao na marudilio ya msemwa huo, ya kwamba ni muhimu sana ''kumwamini Yesu''. Lakini sikuelewa kabisa nini walimaanisha hapo.

Walitaka kusema kwamba tunastahili kuamini mtu aliyeitwa Yesu aliyeishi imepita sasa miaka 2000? Niliamini hivo, na nilipenda sana yale aliyoyatenda na mafundisho yake.

Walipenda hakika kusema kama Yesu alifufuka kutoka wafu ? 

Sikuamini kabisa hayo.

Walipenda, wakati wakihakikisha kama tunastahili kumwamini Yesu, kama tunapashwa kufuata mafundisho yake ? Nilipenda mafundisho yake, lakini sikuwa tayari kuyafuata yote.

Hapo nilikosa msimamo. Waalimu wangu waliniambia kuwa ningestahili kuamini Yesu. Waliniambia pia ningemfanya awe Bwana wa maisha yangu.

Nilijuwa kama yale walioniambia yalikuwa ya muhimu, lakini sikujuwa nifanye nini.

Baadaye siku moja, kupitiya maombi na usomi wa Agano Jipya, niliielewa kwamba hakika Yesu alifufuka kutoka wafu. Nilikubali kwamba ningestahili kumwamini.

Nilistahili kuamini Yesu na kumtii sababu ni mwema, amejaa upendo, na yuko hai.

Na kisha nikaomba hivi :

''Bwana Yesu, ninasikitika kwa namna nimeishi. Tafazali, unisamehe. Nifanye kuwa kiumbe kipya. Nakupokea kama Bwana na Mwokozi wangu. Amen''.

Ombi langu lilikuwa rahisi, lakini lilibadilisha kila kitu. Sasa, nilijuwa kama nilimwamini Yesu. Sio tu niliamini kwamba aliishi, na akafa na akafufuka, lakini nilimwamini. Nilezaliwa upya !

Wakati tunapotangaza injili ya miviringo tatu, tunawaalika watu, ''kugeuka kutoka uasi wao na kumtawaza Yesu kama Mfalme wa maisha yao ''.

Ni kweli, tayari Yesu ni Mfalme. Siku ya Pentekoste, Petro alisema :

 ''Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake. 

Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia. 

 Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye mwenyewe anasema, 

Bwana alimwambia Bwana wangu, 

Keti upande wa mkono wangu wa kuume. 

Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako. 

Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.''

Yesu ni Bwana ; Yesu ni Mfalme ! Lakini taifa lake linaasi. Wakati tunapo waomba watu kumtawaza Yesu kama Mfalme wa maisha yao, tunawaomba kuacha uasi zidi ya Mungu na kisha kuweka tumaini lao kwake na kumtii.

Je ! Utachukuwa mda mchache ili kumwambia Yesu kama ni Mfalme wako ?

Kumwambia pia kama unampenda, na kumwamini na unapenda kumufuata ? Acha Roho Mtakatifu aseme nawe wakati unapofanya hivo.

Baadaye, kwa upendo mkubwa na furaha kubwa, alika watu wengine kumtawaza Yesu kama Mfalme wa maisha yao.

Ilikuwa ''ongezeka'' na mimi Dean Davis, nawauliza : ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Maendeleo ya Uongozi - Mafikiri ya Kasisi Claude kwa ajili ya mchakato wa maendeleo ya Uongozi - 2

 








        Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji na wasimamizi wa makanisa katika vijiji.

Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Katika podikasti yangu ya nyuma, niligawanya mawazo ya kasisi Claude kuhusu mchakato wa maendeleo ya Uongozi. Leo, napenda kuendelea na yale mawazo na mafundisho yake.

Niliuliza Kasisi Claude ni kwa namna gani anawasaidia viongozi wapya kukomaa kama wanaume wa kiroho. Hiyo haikunishituwa kwa vile alianza na uchunguzi wa utu wao na mwenendo wao. Hiyo inamsaidia kwa kumupa picha ya namna atakavyo muombea kila m'moja wao. Ijapokuwa, kwa kumchunguza mtu, tunastahili kuwa karibu ya huyo mtu ; tunastahili kuchukuwa mda wa kuwa karibu yake ; hata kama iwe nguvu kuwa ana kwa ana pamoja, kama hiyo haiwezekani, teknolojia inaweza kutusaidia.

Swali langu lakufuata kwa Kasisi Claude lilihusu namna anahusika kama ikitokea tukio la kukosowa wala kama kurudiya nyuma kutaitajika.

Pengine mtu moja ataonyesha uzaifu wa tabia katika mwenendo wake. Pengine angeona kwamba kuko jukumu ambalo halikutekelezwa vizuri. Sikiliza jibu lake.

Claude anapenda kushiriki maoni yake kwa njia isiyo rasmi. Hiyo inaweza kufanyika mezani wakati wa chakula. Hapendelei kufanya namna ya majadiliano ndani ya ofisi kubwa, akiwa na mtu. Alieleza kama anapenda kufanya hivo sababu ya kutowa moyo zidi ya kutowa maonyo.

Baadaye nilimuuliza ni wakati gani ulio mzuri wa kutowa sahisho. Alinijibu kuwa, wakati mtu anatenda jambo mbaya, pahali ya kuongea naye hapo hapo, anapendelea kungoja mda muhafaka. Aliniambia ; ''kama uko mgumu sana, watakuwa na woga na kisha watajificha. Iliyo ya muhimu ni kwamba waendelee kuwa wazi kwako.''

Ni hekima kubwa : ''ya muhimu ni kwamba waendelee kuwa wazi kwako.'' kama mtu akijifunga kwetu sisi kama wasimamizi, kwa hiyo hatuko tena na uwezo wa kumsaidia kuendelea kwake.

Kitabu cha Mithali 27:6 inatufundisha : ''Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; 

Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.''

Wakati tunapo towa onyo (sahisho) kwa kiongozi anayetayarishwa,  kwa hatuwa ya mawasiliano ao urafiki, mtu huyo anaelewa kuwa, hata kama maneno yetu yangemchoma kwa mda huo, yalisemwa kwa ajili ya ubora wake wa baadaye.

Kasisi Claude aliendelea na majibu yake kwa kueleza,  kama kosa ni kitu ambacho kinaweza ''kuhatarisha kazi'', anaishuhulikia hapo hapo. Mifano mbili aliyotowa ilikuwa mawasiliano mabaya kati ya kasisi na mratibu, ao tena matumizi mabaya ya pesa. Mara nyingi, hiyo ikitokea, anaishuhulikia swala hilo faragani.


Hii ni neno la kutiya moyo kwa wapandaji na viongozi wa makanisa katika vijiji.

MIVIRINGO TATU NA TOBA

 










        Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Wakati nilipoanza kuelewa Habari Njema ya Yesu, nilipenda kusikia ujumbe kuhusu ''maisha tele''. Moja ya vesi za Biblia za kwanza nilizo kariri,  ilikuwa Yohana 10:10;

Biblia

''Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.''

Nilipendelea maisha tele, maisha inayojaa isia za matumaini.

Lakini ilikuwa kama watu wote walio tangaza injili pamoja nami walikuwa wakinieleza kuwa ningestahili kuachana na dhambi zangu na kuweka tumaini langu kwa Kristo. Basi ningejaribu kuishi maisha tele.

Shida, nilipendelea kuishi maisha tele bila toba.

Nakumbuka kwamba turu nyingi, Muhubiri alisema kuhusu baraka ya kuwa mwana wa Mungu. Ujumbe hizi zilileta matumaini ndani yangu, lakini baadaye alitamka neno hili :"tubuni.'' nilisikia woga moyoni mwangu.

Kwa mwisho, nilitubu. Nilimwambia Mungu kama nasikitikia namna ya maisha yangu mabaya ya kuishi. Nilimwambia kama napenda kuachana na dhambi zangu. Nilimuomba Yesu kunisamee. Ndipo wakati huo maisha tele ndani yangu yalianza.

Nilikua na amani pamoja na Mungu. Nilijuwa kama nilikuwa mtoto wake. Wakati nilikuwa nikisoma Biblia, niliielewa. Maneno yaliyokuwa yakitoka kinywani mwangu yalibadilika, hata pia na namna nilivyokuwa nikiwatenda marafiki zangu. Nilizaliwa upya.

Moja ya sehemu nzuri ya kutangaza injili ya miviringo tatu ni mkuki unaoelekea kwenye dunia iliyovunjika kuelekea mviringo wa chini, hiyo inayosimulia hadisi ya maisha, ya kifo na kufufuka kwa Yesu.

Mkuki huu unamaanisha toba.

Wakati tunapo tangaza miviringo tatu, tunasema :"ukitubu dhambi zako na kumtawaza Yesu kama Mfalme wa maisha yako, na atakupatanisha na Mungu.''

Hii inamaanisha kama ukiachana na uasi wako zidi ya Mungu na kuweka tumaini lako kwa Kristo, Mungu atakusamehe na atakupa maisha tele.

Watu wengi wanashangaa kama Mungu anakubali kutupokea mara tena baada ya sisi kumuasi. Na ni ajabu kweli. Lakini kilicho cha ajabu zaidi, ni kwamba Mungu anatupa neema na nguvu yakutosha kwa sisi kutubu.

Kwa ajili ya upendo wa Mungu, tunaweza kubadilika. Hatushurutishwi kuendelea kuishi maisha hayo hayo mabaya tuliyoyaishi wakati tulipokuwa waasi zidi ya Mungu. Tunaweza kuachana na ubaya, uzalimu na dhambi.

Tunaweza kuanza kuishi maisha ya haki, yenye kujaa upendo kama tukiweka tumaini letu kwa Yesu.

Sasa, wakati unapotangaza injili ya miviringo tatu, chora mkuki huu kwa kuonyesha mwisho wa uasi na kumrudilia Mungu. Ambia watu kama wanaweza kutubu, wanaweza kubadilika, wanaweza kuachana na mabaya na kumuelekea Mungu. Wajulishe kama anafurahi kutupatia nguvu inayotustahili ili tumtumainie na kumtii.

Maisha ya Kikristo ya toba na imani ni kitu kizuri.

Nashukuru sana vile nilivyo tubu ; na ninaomba ili kwamba mamia, hata maelfu ya watu watubu na kuweka tumaini lao kwa Kristo. Wakati unapo tangaza Habari Njema kwa kuchora miviringo tatu na kusimulia hadisi kubwa ya Mungu.

Ilikuwa ''ongezeka'' na mimi Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

MIVIRINGO TATU MUNGU HUINGILIA KATI

 









     Jambo kaka na dada. Naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Inatendeka namna gani kwenu, wakati munapo tangaza injili ya miviringo tatu ? Nafikiria kwamba munapo tangaza injili ya miviringo tatu, munaona kama watu wengi wanakubaliana nanyi wakati munapo waeleza kwamba dunia ambamo tunaishi ndani imevunjika. Inanisikitisha kusema kama mateso ya dunia yetu yanakuwa kweli kila siku. Wakati nilipokuwa nikitayatisha podikasti hii, inchi yangu imepitiya katika kipindi cha machafuko magumu ya kisiasa tena yakusikitisha. Utajiri na elimu yote ya inchi yetu hazikutusaidia kuziwiya mgawanyiko mkubwa ambao tumo ndani.

Ndiyo, dunia ambamo tunaishi ndani imevunjika. Lakini wakati tunapo tazama uumbaji, tunaelewa japo hiyo kwa machache kama Mungu ni mwema. Wema wake unaonekana ndani ya uumbaji.

Kwa hiyo, ukweli unaotangazwa katika miviringo mbili ya mwanzo ni wa ukweli kwa watu wote : dunia imevunjika, lakini mateso na uharibifu havikuwa na sehemu kwa mpango wa asili wa Mungu kwa dunia. Ukweli unaotangazwa katika mviringo wa tatu unaeleweka kidogo, lakini miongoni mwa miviringo tatu, ni hiyo inayoleta matumaini zaidi.

Mviringo wote wa tatu unasema juu ya Yesu : namna gani alivyokuja duniani, namna gani alivyoishi maisha ya upendo, namna gani alivyokubali kusulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu, na namna gani alivyofufuka ndani ya wafu, akiwa mshindaji juu ya dhambi, zidi ya kifo na mateso.

Mviringo wa tatu unasema juu ya uajibikaji wa Mungu. Inatuambia juu ya mkombozi aliyetokea inje ya dunia yetu iliyo vunjika ili kuleta uponyaji na matumaini. 

Hadisi hii ni ya ajabu sana ambayo Yesu mwenyewe aliita Habari Njema. Japo hiyo, mviringo wa tatu ni sehemu ya hadisi ya Mungu isiyo eleweka vizuri na watu waliovunjika ndani ya dunia hii.

Kama wapandaji wa makanisa, pengine mutajiuliza : ''nifanye nini ili kuwasaidia watu kuelewa mviringo wa tatu ili waweke tumaini lao kwa Kristo na waokolewe na mateso tunayoyaishi ndani ya dunia hii?''

Muniruhusu kugawanya pamoja nanyi kinacho nisaidia zaidi :

Omba. Omba kwa ajili yako ili usimulie hadisi vizuri. Omba kwa ajili ya wasikilizaji wako ili Mungu ajifunue kwao wakati wanaposikia Habari Njema. Omba ili kusiwe mtu atakaye kusumbuwa wakati ukisimulia, na kusiwe chochote kitawapotosha wakati wanaposikiliza. Omba ili ujazwe na upendo mkubwa kwa watu unao ongea nao. Weka tumaini kwa Mungu ili akujaze na Roho wake Mtakatifu.

Sijisikie huru. Pengine unaogopa na kuwaza kama utasimulia hadisi yote vizuri. Usiogope. Ujisikie huru na ufanye tu kila iwezekanayo kwako. Mungu iko pamoja nawe, ni yeye anayetumika ili kuwasaidia wasikilizaji wako kuweka tumaini lao kwake.

Ujue kile unataka kuongea, lakini usiwe haraka. Baki mwangalifu na usimulie hadisi ya Yesu wakati unapochora mviringo wa tatu. Usipotoshwe na chochote ; tangaza Habari Njema. Baadaye, acha matokeo mikononi mwa Mungu. Wamoja watatubu na kuamini hapo hapo. Wengine watakuzarau, wewe pamoja na ujumbe wako. Wengine wataitaji kujuwa zaidi. Weka tumaini kwa Mungu. Anatenda kazi.

Na ukumbuke : wakati unapo gawanya Habari Njema, unaleta utukufu kwa yeye aliyekuja kukuokowa. Na hiyo kila siku ni kitu kizuri. Usiache!

Hii ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

UUMBAJI UNATANGAZA WEMA WA MUNGU

 
















     Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Wakati nilipoanza kupanda makanisa kwa Bara la Marekani ya kusini, nilitumika pamoja na ndugu aliyeitwa Pedro.

Ijapokuwa upole wake na uaminifu wake katika kutowa injili, mara nyingi alipigwa, kutukanwa na kuzarauliwa kwa ajili ya imani yake kwa Kristo. Japo hiyo, alibaki mvumilivu, akijazwa na upendo, na akitafuta kila siku kusaidia wengine kutambuwa mwangaza wa Yesu. Pedro alirudilia mara kwa mara, hata kama watu wanamuasi Mungu, Mungu anabaki mwema : anaagiza mvula na juwa, na kutowa chakula. Alionyesha hivo kuwa Mungu anaendelea kuonyesha upendo wake ijapokuwa kutokuamini kwetu.
Ujumbe huo sio mpya ndani ya 
Matendo ya Mitume 14:17, Paulo na Barnaba wanasema mambo hayo : Mungu anafanya vema kwa kutowa mvula, mavuno na chakula, akijaza kwa namna hiyo mioyo na furaha.
Wakati tunapotangaza injili kupitiya miviringo tatu, tunakumbusha hivo pia kwamba dunia, hata kama imevunjika, ingali na alama za wema wa Mungu: wema kujitokeza kwa juwa, tabasamu la mtoto, mvuwa inayo otesha mavuno.

Kwa kutowa injili, usipite haraka bila kuonyesha ukweli huo. Inafaa kualika watu kutambuwa wema wa Mungu katika uumbaji, kusikiliza uzoefu wao na kuwaleta kufikiria.
Lakini dunia imevunjika sababu ya dhambi. Watu wanajaribu kuikwepa, lakini Yesu pekee ni njia inayoelekeza kwa Mungu. Kupitiya yeye, tunaweza kupata uzoefu wa kweli wa wema wa Mungu.
Wakati tunapo mrudiliya Mungu kwa imani na kwa toba, tunaanza tayari kuonja kwa mpango wake wa asili, kama kionjo cha mbingu mpya na inchi mpya.

Siku moja, tutaishi furaha hii pamoja na Mungu, katika ushirika wa kweli na siku kuu tukiwa naye.
(Ufunuo 19).

Ni hadisi kubwa ya Mungu. Muigawanye kwa uaminifu.

Maendeleo ya Uongozi - Mafikiri ya Kasisi Claude kwa ajili ya mchakato wa maendeleo ya Uongozi - 1

 









   Chuck Rapp anawatolea podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji na viongozi.

Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Kwa kipindi cha myiezi mbili iliyopita, niligawanya tabia 10 ambazo nazitafuta kwa viongozi wanaojitokeza. Leo, natarajia kuanza kujifunza mchakato wa maendeleo ya Uongozi. Kwa hiyo, asubui moja, tukiwa tukila chakula cha asubui, niliuliza mtiririko wa maswali kwa Kasisi Claude.

Nilianza kumuuliza aeleze namna gani anawasaidia viongozi wapya tayari wanaojitokeza. Jibu lake la kwanza ilikuwa kwamba anawauliza maswali mengi na anasikiliza kwa makini majibu yao. Kwa kufanya hivo, anaanza kuelewa nguvu yao na uzaifu wao. Kupitiya ujuzi huo, iko sasa na uwezo wa kutambua ni majukumu gani ya kuwapa. Wakati wanapotekeleza majukumu haya, anawachunguza kwa makini.

Nilimuuliza kwa namna gani anatambuwa majukumu bora ya kuwapa viongozi wanaojitokeza. Namna gani anatafautisha ubora wa majukumu ambayo wanaweza kutekeleza kwa urahisi, kile kinachozidisha uaminifu wao na majukumu ya nguvu zaidi zitakazo wasaidia kupokea uwezo mpya.

Claude alinieleza kwamba, kuhusu hii hatuwa ya pili ya majukumu, anapenda kutowa majukumu muhimu kwa ajili ya kazi ya kila mtu. Alitowa kama mfano wa uandishi wa ripoti ao majukumu fulani yanayoshikamana na mtandao (informatique). Anapendelea kuwapa viongozi wanaojitokeza fursa ya kujifunza na kukomaa katika ujuzi wao.

Mara nyingine tena, anachunguza kwa makini namna wanavyotekeleza majukumu hayo. Wakiitaji msaada, anawashindikiza yeye mwenyewe ao anawaweka kwa mawasiliano na mtu aliye na uwezo wa kuwasaidia vizuri kuelewa.

Kwa mda huo, nilimuuliza namna gani anawasaidia makasisi wa VCP kukomaa kama viongozi. Alitowa mifano tatu za namna anavyowasaidia kujiendelesha kwa mara moja kama viongozi wa kiroho na katika ujuzi wao wa utendaji kazi.

Kasisi Claude anauliza kila wakati makasisi wa VCP kwa namna gani wanatambuwa waratibu wao. Mithali 27:23 inasema ''Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; 

Na kuwaangalia sana ng’ombe zako.'' kama vile viongozi, tuko kama wachungaji wa kondoo wanaostahili kutunza maitaji ya wale wanaotufuata, na kwa hiyo, tunapashwa kujuwa namna wanavyotembea.

Kasisi Claude anawasaidia makasisi pia kutambuwa nama gani ya kutekeleza majukumu muhimu, kama vile kutowa vikaratasi vya maelezo ya namna pesa zilivyotumikishwa. Anagawanya pia uzoefu wake na kuwapa moyo kuwa waangalifu kwa hiyo.

Ujuzi wa tatu anaofundisha ni namna ya kufanya bajeti. Ni pia ujuzi wa utendaji kazi wa muhimu.

Kwa kumsikiliza Kasisi Claude, nilitambuwa Mada iliyotokea kila mra kwa namna yake ya kuendeleza viongozi : anasikiliza sana na anachunguza sana. Nitairudiliya : anasikiliza sana na anachunguza sana.

Kama tukikusudia kuendeleza viongozi wanaojitokeza, hatuwezi kwenda haraka; tunapashwa kuwa wavumilivu.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji na kwa viongozi.

AMRI KUBWA

 









        Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Kupitiya Afrika, watalii, wanasema kuhusu ''Big Five''. Ni haina 5 ya mbuga za wanayama. Wanapendelea kuona : ndovu, vifaru, simba, chui na nyati.

Wakati ninapofikiria kuhusu  jumla ya ujumbe wa Biblia na mafundisho yake, ninasema ''Big Three''. Ni amri tatu ambazo ninastahili kutii. Kwangu mimi, ni tatu za muhimu:

Mika 6:8 inajulikana kama mamlaka ya Mika : ''Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!''.

Mathayo 22:36-39 ni amri kubwa : ''

[36]Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 

[37]Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 

[38]Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 

[39]Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.''

Mathayo 28:18-20 ni misheni kubwa : ''Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 

[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 

[20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.''

Nastahili kutii amri hizi kuzidi zingine zote. Je! Wewe vipi?

Wakati tunapo tii amri hizi tatu za Biblia, tunaishi maisha bora ambayo Yesu ali ahidi. Maisha yetu yanajaa na haja pamoja na malengo. Tunakaribia Mungu. Tabia yetu inageuka Ku ambatana na tabia yake. Upendo wetu unakomaa. Tunabariki wengine na sisi tunabarikiwa.

Huduma ya upandaji wa makanisa katika vijiji imetengenezwa kusudi ya kutekeleza amri kubwa. Tumejitolea kufanya wanafunzi wa Yesu Kristo. Tunafundisha wanafunzi kwa kusudi wa tii kwa yote Yesu aliyo tu agiza. Wakati tunapo sema kwamba tunatumika ili kuwe kanisa kwa kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2050, tunajitolea kutekeleza amri kubwa. 

Tunajuwa kwamba makanisa zenye afya njema ni jamii maalum ambazo Mungu anatumikisha kufanya wanafunzi. Wakati tusemapo "kanisa katika kila Kijiji cha Afrika, ifikapo mwaka wa 2050", tunahakikisha kama tunapenda kila Kijiji kijae wanafunzi wanaojuwa, wanaopenda na kumtii Yesu.

Kwa hiyo, tunaomba : ''mimi hapa Bwana, nitume''. Tunapokea mafundisho ili tuelewe injili. Tunakuza vipawa ili kutangaza Habari Njema na kufundisha watu kumtii Yesu. Tunajitolea kwa watu na kuwaita kuishi kama wanafunzi wa Yesu ndani ya ushirika wa kanisa la mahali.

VCP imetengenezwa tu kwa kutekeleza amri kubwa. Nafurahi sana kwa vile mumechaguwa kwenda, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kufanya wanafunzi katika mataifa yote. Muko kwenye njia nzuri; musiache !

Ilikuwa ''ongezeka'' na mimi Dean Davis, nawauliza : ni pamoja na wanani utagawanya nao leo ujumbe huu wa kutiya moyo ?

Maendeleo ya Uongozi - Baadhi ya tabia za ziada za kutafuta kwa viongozi wanaojitokeza (3)

 









      Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wa Kikristo.

Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Kwa kipindi cha myezi mbili iliyopita, niligawanya tabia 10 ambazo nazitafuta kwa viongozi  wanaojitokeza. Leo, napendelea kutowa kifupi cha tabia hizi. Mbele siyafanya hivo, napenda kusisitiza kwamba, ni viongozi wanaojitokeza wachache wataonyesha tabia hizo 10.

Ninajuwa pia kwamba horoza hii siyo ya kutosha wala ya mwisho.

Hii ni mawazo yangu tu.

Tazama horoza yangu :

* Utambuzi ulio na mizizi ndani ya Kristo - ninatowa kipaumbele cha juu kwa tabia hii, sababu kwa miaka mingi iliyopita , nilichunguza matatizo makubwa yaliyosababishwa na viongozi ambao hawajiamini wenyewe. Mara nyingi, Motisha zao zimechanganyika katika uongozi wao, sababu wanatafuta kujipendekeza machoni pa wengine pahali ya kutafuta kutumikia Yesu-Kristo na ufalme wake. Wanajiusisha wenyewe pahali pa kujihisisha juu ya ufalme.

* Unyenyekevu - inashikamana moja kwa moja na tabia hii, sababu viongozi wanaojiamini hawasukumwi kujipendekeza kwa macho ya wengine. Mithali 27:2 inatafsiri vizuri : ''Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; 

Mtu mgeni wala si midomo yako wewe''

* Hali yao ya zamani ao matendo yao ya zamani - pengine utakumbuka kama katika mtiririko wa mwaka jana kuhusu Uongozi wa uwakili, nilisema kuhusu mfano wa Mtumishi Mwaminifu ambaye Yesu alisema : ''ni vema, Mtumishi Mwaminifu na bora ; ulikuwa mwaminifu katika mambo machache , nitakupa zaidi''. (Mathayo 25:21)

* mambo ya uzoefu wala uwezo - wakati tunapo chunguza na kuendeleza viongozi wapya, ni muhimu kutathmini matendo yao ujuzi na kuwapa fursa ya kuongoza kwenye misheni zinazotumikisha nguvu hizo.

* Mpango - mwezi uliyopita, niliitafsiri kama vile ''uwezo wa kukaguwa na kuchukuwa matendo kwa namna ya uhuru''. Viongozi wanaojitokeza hawabaki wavivu wakingojea kuambiwa nini cha kufanya. Wanaonyesha mwenendo mzuri na wanatenda.

* Hamu kubwa ya kujifunza na kukuwa - viongozi wanaokuja hapo baadaye hawatosheki na hatuwa yao ya kukomaa kiroho, ya kuelewa ao ya ujuzi.

* Moyo wa kufunzwa - kwa kujifunza na kukomaa, viongozi wanaojitokeza wanastahili kuwa wanyenyekevu, na kuwa tayari kujifunza kwa wengine.

* Bora kwa kuwasiliana - naongeza tabia hii sababu watu wabaya hawawezi kufuatwa, na hauwezi kuwa kiongozi kama hakuna mtu anayetufuata.

* Sifa yao, iwe ndani ya kanisa ao inje - kama mtu iko na sifa mbaya kwa wale wanao mjuwa vizuri, kwangu mimi ni alama ya tahazari muhimu.

* Ndoa ya kudumu yenye kujengwa juu ya Kristo - imepita sasa miaka 40, nilisikia muhubiri moja akitowa shauri hili : ''kama haindeki nyumbani, usiitoe inje.'' wala tunaweza sema, kama ndoa ya mtu haina nguvu, kipaumbele ni kurudisha kwanza mawasiliano nyumbani mbeye ya kujaribu kuongoza wengine.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo.

Kutumika kwa mda wa sasa. Kuomba kwa ajili ya wakati ujao

      Jambo kwa wote. Naitwa Dean Davis, na munasikiliza ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapand...