Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji na kwa viongozi wa Kikristo katika vijiji.
Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi.
Wakati wa toleo zangu tatu za nyuma, niliongea nanyi kuhusu tabia mbali mbali ambazo nazitafuta kwa viongozi tayari wanaojitokeza. Mbili kati ya hizo zilizo za muhimu zaidi kwangu ni utambulisho wa nguvu wenye mizizi ndani ya Yesu-Kristo na unyenyekevu.
Leo, natarajia kugawanya mawazo mamoja kuhusu tabia tatu za ziada ambazo nazitafuta kwa viongozi wanaojitokeza. Ni utu wa kupendeza, ambao wengine wanasifia, kwa sifa zao, (hiyo ikifanyika ndani ya kanisa na inje ya kanisa), na ndoa yenye nguvu ikiwa na mizizi ndani ya Kristo. (Kama ni wenye ndoa).
Hiyo inajumulisha tabia 10 ambazo nazitafuta kwa viongozi wapya ao kwa wale wanaojitokeza. Mbele ya kuendelea mbele zaidi, ninakazia kwamba maendeleo ya Uongozi ni mchakato unaoendelea, na kwa mwanzo, haiwezekani kungojea kupata mtu anaye eneza tabia hizi 10. Nitarudilia kwenye Mada hii kwa podikasti yangu ijayo.
Kwa kufafanuwa vizuri tabia hizi tatu, nawaza munaweza kuelewa kama :
Mtu aliye na sifa mbaya iko na bahati kidogo ya kukusanya wanafunzi.
Kwa hiyo, wakati ninapo mchunguza mtu, ninapendelea kumuona awe mtu ambaye wengine wanavutiwa na hali yake, na kama hapendi watu kumusogelea. Ikiwa hivo, ni vigumu kwake kutarajia kuwa kiongozi bora. Tunda la Roho, katika Wagalatia 5:22-23, inahusu ''upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, upole na kiasi''. Kila moja ya tabia hizi inahusu namna mtu anavyoishi pamoja na wengine.
Tukiunganisha pamoja na hayo, napendelea kupata taarifa juu ya sifa zao. Wanazingatiwa na wasimamizi wao wa kiroho na washiriki wa kanisa ? Wako na sifa njema zidi ya wakubwa wao wa kazi, waliyo juu yao wala viongozi wakijamii? Katika 1Timotheo, Mtume Paulo anatowa tabia za wasimamizi wa kanisa : ''Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi''. (3:7). Walio na sifa njema wako ao na rikodi nzuri, kama nilivyo onyesha katika podikasti yangu ya nyuma) wako na uwezekano mdogo wa kuanguka katika sifa mbaya na athari mbaya kwa kanisa zao wala shirika zao.
Kwa mwisho, wako na ndoa zilizo nguvu zenye mizizi ndani ya Kristo ? Katika 1Timotheo 3, Paulo anasema : ''Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, ....'' (3:2). Kila wakati ambao hiyo inawezekana, napenda kuangalia nyumba ya kiongozi aliye tayari wala kuchukuwa mda wa kuwa pamoja naye ao jamaa lake, sababu tunaweza kujifunza mengi kupitiya uchunguzi huo.
Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wa Kikristo katika vijiji.
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)



