Jumatatu, 31 Agosti 2026

Usikawize ubatizo

 










Karibu kwenye ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, kwa wachungaji na viongozi wa Kikristo.

Mimi ni muhamasishaji wenu leo, Daneille Snowden.

Tutaendelea na mjadala wetu kuhusu ubatizo wa maji na kujadiliana kwa swali lifuatalo :Sababu gani watu wamoja wanakawiza ubatizo wao ?

Wakati ukiuliza watu tofauti kuhusu swali hili, wanatoa sababu nyingi : woga, hisia ya kutukuwa kamili, mila zinazotofautiyana, ao tena wazo kwamba inafaa kujiandaa vizuri, kuwa na sare rasmi, nk.

Neno "kukawiza" linamaanisha kupeleka utendaji wa jambo kwa mda wa baadaye, kuizuwia wala kufanya namna jambo litendeke pole pole na ilivyo tarajiwa.

Tendo la kigriki linaloambatana na "kukawiza" linatokana na "chrono" ikimaanisha kuchukuwa mda, kukawa ao kukawia.

Japokuwa, tunaona ndani ya Neno la Mungu kwamba hapakuwa na mda wa kubatiza mtu baada ya yeye kukubali Yesu kama Mwokozi wake.

Katika Matendo 16.31-33, Mitume hawakukawiza ubatizo wakati watu walipo amini.

Paulo, aliyeitwa mbele Sauli, alibatizwa hapo hapo, kama tunavyoona katika Matendo 9.17-19.

Na katika Matendo 2:41, tunasoma : "Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu."

Tunapashwa sote kukumbuka yale yanayofanyika kabisa wakati mtu anabatizwa.

Tunaweza kuanza na ubatizo wa Yesu.

Tendo hili kubwa lilifunua utambulisho wake kama Mwana wa Mungu ; alionyesha utatu utakatifu na alitangaza kifo chake na ufufuko wake kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.

Baada ya ubatizo wake, Yesu aliachana na maisha yake ya ubinafsi ili kuingia wazi wazi katika umisheni wake.

Kama inavyosemeka : "ubatizo unakamilisha ushirika wa kila mwamini na Kristo. Ni tendo la imani linalotangaza mawasiliano mapya ya kila mwamini pamoja na Kristo. Ni tendo la imani linalotangaza mawasiliano mapya na Mungu." 

(Mwongozo wa Mkufunzi ? NVP, muhula 1, kipindi cha 2)

Katika myezi ya kipwa, mimi namume wangu tulikuwa ndani ya kikundi kinachoitwa "kongamano juu ya Yesu" tulishuhudia watu wengi waliotowa maisha yao kwa Yesu.

Kwa mwisho wa kipindi cha sifa, tunakuwa na beseni la maji mahali ambapo kwa miaka iliyopita, tuliona watu wengi wakibatizwa.

Wakati tunapobatizwa, tunatambulika kwa kifo na kwa ufufuo wa Yesu-Kristo.

"Ubatizo unakamilisha imani ndani ya Kristo, musamaha wa dhambi, na umoja ndani ya Kristo." (Fundisha na Ongezeka muhula 2)

Uzoefu wa ubatizo ni uzoefu wa kweli unaobadilisha maisha ya mwamini, pamoja pia na wale wanao shuhudia.

Unaimarisha imani ya wengine waamini na kushuhudia mbele ya wale ambao bado wanatafuta tumaini.

Kwa upande wangu, wakati nilipobatizwa, nafsi yangu ilijisikia hakika kuwa na ushirika pamoja na Yesu. Nilijisikia nikiwa karibu sana naye kwa kufanya hatuwa hii ya utii na upendo.

Ilikuwa Ongezeka.

Utapendelea kugawanya podikasti pamoja na wengine ?

Tayarisha waamini wapya kwa ubatizo

 









      Jambo kwa wote ! Naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Shurti lililotolewa na Yesu katika Mathayo 28 linatupa maelekezo ya umisheni. Bwana wetu alisema : "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 

na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari"

Wakati tunaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume, tunaona ni kwa namna gani Mitume pamoja na wanafunzi wao, walivyotii Agizo. Sehemu moja muhimu ya mafundisho ya wanafunzi inahusu kubatiza. Na katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kanuni thabiti inajitokeza :

Kubatiza bila kupoteza mda.

Siku ya Pentekoste, Petro liuliza wasikilizaji wake pa Yerusalemu kwamba "watubu na kila moja wenu abatizwe kwa Jina la Yesu-Kristo, kwa ajili ya musamaha wa dhambi zenu" (Matendo ya Mitume 2:38). Baadaye kidogo, watu 3000 wakabatizwa.

Wakati Filipo alihubiri wakaaji wa Samaria, wengi waliamini. Biblia inasema katika Matendo 8:12 : "Matendo ya Mitume 8:12

[12]Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake."

Baadaye kidogo, wakati yule Towashi mwethiopia alipo elewa Habari Njema ambayo Filipo alimueleza, akasema : "tazama maji ; ni nini basi kinanizuiya nisibatizwe ?" Na Filipo akambatiza.

Ubatizo wa Sauli katika Matendo 9, pia ule wa Kornelio pamoja na nyumba yake yote katika Matendo 10, pia ubatizo wa Lidia pamoja na nyumba yake, pia ule wa mlinda Gereza pa mji wa Filipi, akibatizwa pamoja na familia yake, wote wawili wakiripotiwa katika Matendo 16, pia ubatizo wa Crispus pamoja na nyumba yake yote katika Matendo 18, zinasimulia zote hadisi ya kufanana. Mitume na wanafunzi wao walibatiza wale walio sikia na kuelewa Habari Njema ya Yesu bila kupoteza mda.

Lakini ubatizo wa bila kupoteza mda, haukufanyika katika makanisa yaliyopandwa baada ya kipindi cha Mitume.

Makanisa mengi yalishurutisha vipindi virefu vya katekismu ao mafundisho ya kutayatisha ubatizo mbele ya kubatiza waamini. Wengine walipitisha mda mbele ya kubatiza sababu walitarajia kusubiri kuona matunda ya toba, wala tu hawakuwa na uaminifu na waamini wapya. Lakini hiyo haikuwa mtindo wala matendo ya Mitume.

Kanisa lako linatumika namna gani ? Wazee wanafundisha nini, wachungaji, wasimamizi ao maaskofu wa kanisa lako kuhusu mda unaofaa kubatiza na matayarisho yanayostahili kwa ubatizo ?

Kama haujue, nakuhimiza kutafuta hiyo habari kwa makini.

Lakini angalia kanuni moja ambayo naweza kuwapendekezea ili kuwasaidia kuhusu mda unaofaa kubatiza waamini wapya : muwabatize bila kupoteza mda.

Muhakikishe kama wameelewa injili.

Muongee nao ili muhakikishe kama wanamjuwa Yesu vizuri akiwa Mfalme wa maisha yao.

Muwafundishe ubatizo na maana yake.

Muhakikishe kama wameelewa damu inaosha roho zetu na kwamba maji ya ubatizo inamaanisha huo utakaso.

Muwasaidiye kuelewa kuwa wakati wanapotoka ndani ya maji baada ya wao kubatizwa, wanasimama ili kuishi maisha mapya ndani ya Kristo.

Muwasaidiye pia kugawanya Habari Njema pamoja na jamaa zao.

Lakini musikawize ubatizo wao.

Muhubiri Habari Njema. Mutayarishe kwa ubatizo wale wanaoelewa Habari Njema na wanaoweka tumaini lao kwa Kristo.

Muhakikishe kama hawa wanafunzi wapya wa Kristo wanabatizwa bila kukawa.

Ilikuwa ''ongezeka'' na mimi Dean Davis na ninawauliza swali hili : ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Amini Habari Njema

 










          Jambo kwa wote ! Naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Injili ya Marko ni mfupi kuliko hadisi ine za maisha ya Yesu ambayo tunaita '' Injili ''. Marko anaingia moja kwa moja ndani ya hadisi ya Yesu kwa sura 1, vesi 14, akisema :

'Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akihubiri Habari Njema ya Mungu,'' alikuwa akisema : '' mda umefika. Ufalme wa Mungu umekaribiya. Tubuni na kuamini Habari njema !"

Agizo la kutubu na kuamini Habari Njema, ndiyo ya kwanza miongoni mwa zile tunazoita leo Agizo saba za msingi za Kristo.

Tunafundisha Agizo hizi saba za msingi ili kusaidia watu kuishi kama wanafunzi wa Yesu.

Sisi kama wapandaji wa makanisa, tunajuwa kama maisha ya watu yatabadilishwa kama wakiweka tumaini lao kwa Kristo na kumtii. Tunaelewa kama ''Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. (Yohana 10:10)

Na tunajuwa kwamba watu wa kila aina wanapenda maisha bora : maisha ya amani, ya tumaini na yenye mwelekeo, maisha yanayojaa upendo.

Kwa hiyo, sababu gani inakuwa vigumu kwa baadhi ya watu wanao sikia hadisi kubwa ya Mungu, pamoja pia na hadisi ya Yesu na upendo wake, kutubu na kuamini Habari Njema ?

Pengine ni sababu hawaamini kabisa kama Ufalme wa Mungu umekaribia.

Watu wanao shiriki madhehebu ya kiasili wanaamini Mungu, lakini wanazania kama iko mbali nao. Watu wanaoshiriki dini ya Uislamu wanakazia sana juu ya ukoo wa Mungu, yaani yeye yuko juu sana na ulimwengu ulio umbwa Wala hahusiki nayo. Wakristo wengi wa jina wanazania kama Mungu anashugulikia sana maswala makubwa ya muhimu kwa hiyo hausike kabisa nawao. Lakini Yesu alisema kama Ufalme wa Mungu umekaribiya.

Kama watu wanaweza kuamini kwamba ufalme wa Mungu umekaribiya, itakuwa kwao rahisi sana kutubu na kuamini Habari Njema.

Kwa hiyo, sehemu kubwa ya kazi yetu sisi kama Wainjilisti walio jitolea na upandaji wa makanisa unahusu kusaidia watu kuelewa kama Ufalme wa Mungu umekaribiya.

Kazi yetu ya uinjilisti inahusu kutangaza kama Mfalme mwenye nguvu na mwenye upendo, Yesu, yuko hapa pamoja nasi sasa : ili kusamea na kuponya, ili kununuwa na kuokowa.

Kama watu wanaweza kuamini tu ya kwamba Ufalme wa Mungu umekaribiya, itakuwa kwao rahisi sana kutubu na kuamini Habari Njema.

Kuko hatuwa tatu maalum kupitiya hizo tunawasaidia watu kuamini kwamba ufalme wa Mungu umekaribiya : tunagawanya ushuhuda wetu, tunasimulia hadisi ya Yesu na tunaomba. Tunahadisia yale ambayo Yesu alifanya kwetu.

Tutasema kwa wazi kuhusu uwezo na upendo wake ukitenda kazi ndani ya maisha yetu.

Tunahadisia pia matendo yake yenye nguvu na upendo wake wa ajabu wakati aliposhinda mwili hapa duniani, imepita miaka 2000.

Na tunaomba pamoja na watu na kuombea watu, ili waone uwezo wa Mungu ukionekana kupitiya maombi yaliyojibiwa.

Wakati watu wanasikia ushuhuda wetu na hadisi ya Yesu, wakati wanaona Mungu akijibu maombi, imani inaanza kukomaa ndani yao.Wanaanza sasa kusemezana :

 Pengine ni kweli Ufalme wa Mungu umekaribiya. Pengine Yesu anaweza hakika kunipa maisha tele, yenye kujaa tumaini, ya furaha, ya upendo na mwelekeo."

Ndipo kwa wakati huo tunaweza kuwaalika wazi wazi, lakini kwa upole, kutubu na kuamini Habari Njema kuhusu maisha, kifo na ufufuko wa Yesu.

Wakati rafiki zetu wanajuwa kama Ufalme wa Mungu umekaribiya, nawao pia watatubu, wataamini na watabadilishwa kupitiya uwezo wa Mungu.

Ilikuwa " Ongezeka."

Na mimi, Dean Davis, nawauliza swali hili : 

Ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Maendeleo ya Uongozi - Uchaguzi wa Yesu katika maombi na wito wake kupitiya kura

 









             Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti iliyo na shabaha ya kuleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi katika vijiji.

Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi.

Katika podikasti zangu zilizopita, niligawanya mawazo juu ya maendeleo ya Uongozi kupitiya maneno ya Claude, Kasisi wa upandaji wa makanisa katika vijiji (VCP), Peter Kasisi makamo wa VCP na Fidélité, Mkurugenzi wetu wa Dynamic women katika Bara la Afrika.

Leo, na katika mtiririko wa podikasti zinazokuja, napendelea kupekuwa kwa ndani mafundisho ya Yesu kulingana na maendeleo ya Uongozi. Tunaanza na Kutambuwa kwamba, wakati ilipofikia kipindi cha kuchaguwa wa Mitume wake kumi na mbili, Yesu aliifanya akiwa katika maombi. Kwa kulinganisha na hayo, wito wake ulikuwa wa kuchagua.

Katika Luka 6:12-13, tunasoma : "Luka 6:12-13

[12]Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. 

[13]Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume"

Yesu kuchaguwa Mitume kumi na mbili, ilikuwa azimio kubwa ya muhimu kwa Kristo.

Walikuwa watu ambao pamoja nao atakuwa nawao miaka tatu ijayo, watu atakabizi kuendelea na kazi yake baada ya kurudi kwake mbinguni. Ni muhimu kuonyesha kwamba Yesu alikuwa Mungu pia Mwanadamu katika maisha yake yote hapa duniani. Na mbele ya kuchaguwa viongozi hawa, maandiko yanatuonyesha kwamba alikesha katika maombi usiku mzima.

Shurti ambalo tunaweza kuchukuwa hapa ni kwamba, tukiwa viongozi, tunapashwa kuomba wakati tunachaguwa viongozi wanaojitokeza 

watakao alikwa kujiunga kwa kazi.

Vile miaka inavyopita, niligunduwa mara nyingi kama azimio hizi zilichukuliwa kwa urahisi sana ndani ya kanisa. Ni muhimu mtu kutekeleza kazi ndani ya huduma, na apatikane "mtu aliye tayari ", msemwa unaomaanisha mtu anayejikuta kuwa tayari kwa mda huo na kumuweka katika kazi bila kuchukuwa mda wa kuomba na kufikiria vizuri uchaguzi wake. Mchakato kama huu wa uchaguzi mara nyingi unaleta matokeo mabaya.

Kwa kuunganisha na uchaguzi wa maombi, tunapata shurti la pili : Yesu alitangaza wito wa uchaguzi. Maelezo ya vesi ya 13 inatuonyesha kama Yesu alikuwa pamoja na kundi ya wanafunzi wake, inamaanisha wale walio mfuata. Kupitiya kwa kundi hili kubwa zaidi, Yesu alichaguwa ndani yao kumi na mbili ili wawe Mitume wake.Shurti ya maendeleo ya Uongozi ninayo chunguza hapa ni kwamba : wakati tunatarajia kuchaguwa viongozi wanaojitokeza, tunastahili kuwapitisha kwa kura.

Ninawatuma katika podikasti yangu ya tarehe 24 Aprili, ambamo ndani yake nilionyesha kwa kifupi baadhi ya tabia ninazo zitafuta kwa viongozi waliyo tayari. Pengine unawezakuwa na horoza yenye utofauti mdogo.

Ya muhimu ni kwamba tufanye kura, tukizingatiya juu ya tabia za muhimu ambazo tunatarajia kuona kwa viongozi wanaokuja.

utambulisho wenye mizizi ndani ya Kristo 

 mnyenyekevu  kazi zao walizofanya Siku za nyuma na uchuzi wao uliopita

 ushupavu wao katika kazi mbali mbali

 uwezo wao wakuchukuwa uwamuzi

- wito mkubwa wa kujifunza na kukomaa

- moyo uliyo tayari kupokea mafundisho 

- mtu mwema

- sifa yao, ndani ya kanisa hata karibu na watu walio inje na kanisa

- ndoa iliyo nguvu na yenye msingi juu ya Kristo 

Ni neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi katika vijiji.

Tubuni na kuamini Habari Njema : Tubuni

 









           Jambo, tazama ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji. Mimi ni Brad Snowden.

Juma lililopita, podikasti yetu ilihusika na : "sababu gani kufundisha amri 7 za msingi za Kristo ?"

Amri ya kwanza ya Yesu ni  : tubuni.

Neno la Mungu katika Mathayo 4:17 : 

""Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.""

Yesu alianza huduma yake na neno hili : TUBUNI.

Hiyo inamaanisha kubadilisha namna ya kufikiri. Ni mabadiliko makubwa na yenye nguvu ambayo yanastahili kuwepo.

Maisha yetu ndani ya Yesu inaanza wakati tunakubali dhambi kwa huzuni na kumuomba atusamehe. Anatuosha sasa na damu yake na kubadilisha roho zetu kuwa mweupe kama balafu kwa hali ya kiroho.

Kwa hiyo, siyo jambo linalotokea mara moja tu ndani ya maisha yetu. Namna yetu ya kufikiri inastahili kuendelea kubadilishwa kila siku.

Tunaweza kuwasaidia wengine kubadilisha namna yao tu, kwa kuwahubiri Habari Njema. Wakati wanasikia kwamba wanaweza kuwa na maisha tofauti, maswali mengi yanatokea : namna gani naweza kuwa na maisha tofauti ? Sina namna ya kuwa na maisha mengine. Ni mpaka kwa hatuwa gani haya maisha mapya yatanibadilisha ?

Horoza ya maswali inaweza kuwa ndefu, lakini kila mojawapo inatupa fursa ya kugawanya Habari Njema ya Yesu-Kristo.

Roho zinaweza kubadilishwa wakati wanaelewa ukweli huu rahisi : neno "toba" siyo neno mbaya. Kinyume chake, ni habari nzuri, sababu inafunguwa roho ya kupokea Habari Njema ya upendo, ya musamaha kwa ajili ya kesho.

Ni nani asingependelea kujuwa tumaini hili ?

Kwa dunia, kuwa na matumaini inamaanisha mara nyingi kuwa na pesa nyingi ili chakula kisikosekane. Japo hiyo, tumaini inayotolewa na Mungu inaenda mbali zaidi ya hayo.

Kwa kuwa Mwanafunzi wa Yesu, inafaa mabadiliko makubwa ndani ya namna yetu ya kufikiri.

Kumepita miaka mingi, msemwa moja umekuwa maarufu : WWJD-- "What would Jesus Do " yaani Yesu angefanya nini ?

Nafikiri kwamba swali hili lilihusika na kutusaidia kubadilisha namna yetu ya kuishi. Lakini linaweza pia kwenda mbali : linaweza kubadilisha namna yetu ya kufikiri.

Tunaweza kuomba namna hii :

"Bwana Mungu, natubu sababu mawazo yangu hayakukuwa na mwelekeo kwa Neno lako, na maisha yangu hayajaonyesha kabisa kwamba namna yangu ya kufikiri imebadilika."

Tusikie pia 2Mambo ya nyakati 7:14 :

""ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.""

Toba inahusu kugeuka kuacha maisha yako ya zamani ya dhambi ili kuishi maisha ya ujazo wa Yesu-Kristo. Ni kujinyenyekeza mbele ya Mungu na kusema :

" Bwana Mungu, nasikitika. Nisaidie kuzingatiya kwa namna nyingine maisha mapya ambayo umenipa. Nakubali hii Habari Njema, hii tumaini na haya maisha ambayo umenipa. "

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Saidia watu kujibu kwa hadisi kubwa ya Mungu

 








        Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na munasikiliza ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Moja ya majukumu ya muhimu zaidi tuliyo nayo sisi kama wapandaji wa makanisa ni kuwa musimuliaji wa hadisi. Kila mutu hapendelei kabisa kujilinganisha kuwa musimuliaji wa hadisi. Ijapokuwa, mbele ya kuwa mwinjilisti, mbele ya kuweza kupanda kanisa, tunapashwa kuwa wasimuliaji wa hadisi.

Wakati Yesu alipoanza huduma ya kuhubiri, kufundisha na kuandaa wanafunzi, alisema : ''tubuni na kuamini Habari Njema.'' Habari Njema ni hadisi ya mpango wa Mungu wa wokovu, uliotekelezwa na Yesu kupitiya mfano wa maisha yake, kifo chake cha msalaba na ufufuko wa ushindi.

Kuko haina nzuri nyingi za kugawanya hadisi hii kubwa ya Mungu inayotendeka duniani. Tunaweza kusimulia mtiririko wa hadisi za kibiblia juu ya uumbaji wa Mungu wa kushangaza kuhusu uhasi wa binadamu zidi ya Mungu, juu ya namna Mungu alivyo chaguwa binadamu, Ibrahimu, ili kurejesha baraka duniani, juu ya uhasi wa binadamu unaoendelea, juu ya itaji lake la kujitowa sadaka na kuungama.

Tunaweza kusimulia hadisi kubwa ya Mungu kwa kuonyesha filamu ya YESU, inayoanza na uumbaji na inamalizika na ahadi ya Mungu kwamba Yesu atarudi. Tunaweza kugawanya Habari Njema kwa kuchora miviringo tatu na kwa kueleza uhasi wetu pia na kushindwa kwetu kuepuka kwa nguvu zetu wenyewe kanuni iliyovunjika ya dunia yetu. Tunaweza kusema juu ya maisha, ya kifo na ufufuko wa Yesu.

Mitindo yote hii ni namna bora ya kugawanya Habari njema, lakini kusimulia tu hadisi hii haitoshe. Tunaweza kusaidia watu kuishi hadisi hii ndani ya maisha yao binafsi ili waweze kugeuzwa kupitiya neema iletayo wokovu ya Mungu.

Munaona, watu wengi wanafikiri kwamba hadisi kubwa ya Mungu inahusu watu wengine. Wanazania kama ni hadisi inayohusu Mungu, Adamu na Hawa, Nuhu na watoto wake, Abrahamu, Isaka na Yakobo. Na wana haki : watu hawa wote wamefanya kazi muhimu ndani ya hadisi ya Mungu.

Lakini kama ukisikia hadisi kubwa ya Mungu kama muhuzuriaji tu wa inje, ukijihusisha tu na watu mashuhuri walio onyeshwa ndani ya hadisi hii, utakuwa umepita kando ya ujumbe muhimu.

Jambo la muhimu katika hadisi ya Mungu ni vile alivyotuma Mwana wake wa pekee aje kufa ajili ya kukuokowa aje kufa ajili ya kuniokowa. Ndiyo, kuko watu wengine wengi ndani ya hadisi hii. Lakini kama bado weye mwenyewe hautajihisi kuwa kama mutu muhimu wa hadisi hii kubwa ya Mungu, hauwezi bubadilishwa.

Siyo tu kujuwa kama Mungu anapenda ulimwengu. Siyo tu kujuwa kama Yesu alikuja kuokowa watenda dhambi. Kile tunastahili kusaidia watu kuelewa, ni kuwa Yesu alikuja kwa ajili yao na kwamba Yesu alikuja kukutana nao.

Kama tunaweza saidia watu kuona nafasi yao ndani ya hadisi hii kubwa ya Mungu, vitu vingi vitatokea.

Wakati watu wanasikia kwa mara yao ya kwanza hadisi kubwa ya Mungu, mwangaza unaanza kujitokeza. Wakati watatambuwa kwambi dhambi yao iliyosababisha Yesu kuja duniani, siku inageuka kuwa na mwangaza zaidi. Wakati wataelewa kwamba Yesu alikufa na kufufuka kwa ajili ya kuwaokowa, mwangaza wa injili unawaka zaidi.

Lakini wakati watu wataelewa ni kwa kutubu na kuamini Habari Njema, wanaweza kusamehewa, kununuliwa na kubadilishwa, hapo sasa mwangaza wa injili unakuwa na utukufu.

Sasa, simulia hadisi kubwa ya Mungu. Uisimuliye vizuri. Isimulie mara nyingi. Isimulie na hadisi, pamoja na filamu, pamoja na taswira.

Isimulie kwa mtu  moja kama vile kwa watu wengi.

Lakini ukumbuke kila siku kitu kimoja : wakati unapo simulia hadisi hii kubwa, wasaidie watu kuelewa kwamba jibu lao kwa upendo wa Mungu ni kama wakifanya hadisi hii iwe yenye kuenea.

Ukifanya hivo, utaona maisha ya watu wengi yakibadilishwa.

Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis, nawauliza swali hii : ni kwa nani utagawanya nao neno hili la kutiya moyo ?

Alhamisi, 13 Agosti 2026

Sababu gani kufundisha amri 7 za msingi za Kristo ?

 










Karibu kwenye ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, wachungaji na viongozi wakikristo.

Mimi ni muhamasishaji wenu Daneille Snowden kwa siku ya leo.

Mathayo 28:18-20 inasema : 

''Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 

[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 

[20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.''

Mada maalum ya mfikiri yetu ya leo ni kufundisha utii kwa amri za Kristo. Neno la Mungu linatafsiri utii kama tendo la kusikiliza kwa makini Mungu, kumtegemea na kunyenyekea chini ya mapenzi yake. Kwa kutii amri za Yesu, mwamini anaonyesha uaminifu wake kwake na kujitolea kwake.

Tusisahau kamwe mfano kamili wa utii ambao Yesu alituonyesha, kama tunavyosoma katika Wafilipi 2:8 :

''tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.''

Shabaa ya Mchungaji wa kanisa, Mchungaji wala kiongozi wowote ule wakikristo ni kufundisha utii. Kwa kutii amri za Yesu, tunakuwa pia mashahidi wa namna anavyobadilisha maisha na vizazi vyote, ndio maana ya kufanya wanafunzi !

Wakati Yesu alipowaita kila moja wa wanafunzi wake, alikuwa akisema ''nifuate.'' kwa kumufuata, tunapendelea kumpendeza na kumtii.

Tufanye kifupi cha amri saba za msingi za Kristo :

1. Tubuni na muamini (Marko 1:15)

2. Mubatize waamini wapya (Mathayo 28:19)

3. Mpende Jirani yako (Mathayo 22:37-39)

4. Shiriki Meza ya Bwana (Luka 22:19-22)

5. Ombeni na kutafakari Neno la Mungu (Mathayo 6:9-13)

6. Towa (Luka 6:38)

7. Fanya wanafunzi (Mathayo 28:19-20)

Wakati nilipokuwa shuleni ndani ya shuke letu la Biblia na wakati walipotufundisha amri za Kristo, moyo wangu ulijaa na huruma mwingi : jambo la kwenda tu na kuzingatiya amri hizo, maisha yangu yote !

Nikiwa bado binti kwa mda ule, na leo nakuwa mwanamuke mwenye uzoefu, naweza kushuhudia kwamba amri 7 za msingi za Kristo bado zingali muhimu sana ninapo shuhidia maisha ya wengi yakibadilishwa kwa utukufu wa Mungu. Ninapo fundisha amri hizo, tunaleta TUMAINI duniani mzima kwa utii wetu.

Ilikuwa Ongezeka.

Usikose kugawanya podikasti hii pamoja na wengine.

Usikawize ubatizo

  Karibu kwenye ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, kwa wachungaji na viongozi wa Kikristo. Mimi...