Jumanne, 9 Desemba 2025

UONGOZI WA MUWAKILI - Umuhimu wa Kujenga Mawasiliano


 

           Mimi ni Chuck Rapp, na ongezeka. Ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji na wasimamizi wa makanisa katika vijiji.

Kwa ukumbusho, Muwakili anatafsiriwa kama ''mtu anayesimamia rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali''. Kwa mtazamo wetu tunaongoza rasilimali tulizopewa na Bwana kwa ajili ya kazi yetu ya upandaji wa makanisa katika vijiji.


Kwa kipindi kilichopita, nilionyesha Mada tano kubwa za uwakili :

1. Tabia inahusika 

2. Mawakili wanaombwa kutowa ripoti ya uwakili wao 

3. Muwakili anastahili kujenga mawasiliano.

4. Muwakili anapashwa kugawanya malengo ya ukuaji ya bwana wake.

5. Mawakili waaminifu wanaendelea katika hatuwa zao za usimamizi.


Hadi sasa, tulijadili Mada mbili za mwanzo. 

Leo, tutaangalia kwa makini kuhusu ukweli ulio muhimu :

👉 Uongozi wa Muwakili unahitaji kujenga mawasiliano pamoja na Bwana, wanafunzi wetu pamoja na rasilimali tunazo ongoza.


1. Kujenga mawasiliano na Bwana.


Kama tukiwa viongozi -mawakili, tunastahili kutekeleza malengo ya Bwana, ni muhimu sana kujenga mawasiliano binafsi naye.

Katika muelekeo wetu, Bwana wetu ni Yesu-Kristo.


Tunastahili kumjuwa vizuri, kuelewa Roho yake kwa ajili ya mioyo na shabaha yake, ambayo inaonyeshwa waziwazi katika Mathayo 28:19-20a:


 Mathayo 28:19-20 

[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 

[20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi''


Kwa hiyo, tunapashwa kumjuwa kwa undani Bwana na mipango yake kwa maisha yetu na kwa huduma zetu.


2. Kujenga mawasiliano pamoja na wanafunzi wetu


Tukiwa kama viongozi-mawakili, tunastahili pia kuendelesha mawasiliano yenye nguvu pamoja na wale wanaotufuata.


Mtaalamu wa uongozi, Mchungaji na Mwandishi John Maxwell, siku moja aliandika :


''anayefikiriya kuongoza na kama hana wanafunzi ni kama mtu anaye jitembeza.''


Kwa namna nyingine, kwa kuwa Muwakili wa kweli, unapashwa kuwa na wanafunzi 

_ na hiyo inawezekana tu kama tunajenga mawasiliano na wao.


Ningesema kwamba kuendelesha mawasiliano inaomba kwa pamoja kuwa na ukaribu na mda.

Kiongozi VCP, nakuhimiza kufuata mashauri ya Mithali 27:23: 


''Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; 

Na kuwaangalia sana ng’ombe zako.''


3. Jenga mawasiliano na rasilimali 


Kwa mwisho, kiongozi Muwakili anapashwa pia kujenga mawasiliano mazuri na rasilimali.


Ninajuwa kwamba nilistahili kufanya utafiti kuhusu Mada hii, na tazama niliyogunduwa :


''kujenga mawasiliano na rasilimali inahusisha siyo tu kujenga urafiki, bali pia kuyaweka kwa faida ili kwa mwisho yalete mafanikio na mapato.

Hiyo inahusu pia ugawaji wa ujuzi, wa uzoefu, pamoja pia na kutowa mashauri na msaada kwa wengine. Inatokana na kujenga njia ya uaminifu ambayo kwa hiyo tunaweza tegemea ili kupata mwelekeo na majadiliano, zaidi kwa wakati rasilimali ni ndogo.''


Viongozi mawakili wako na nguvu zaidi na uhodari sana wakati wanatumika kwa pamoja.


Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji na kwa viongozi wa makanisa katika vijiji

UONGOZI WA MUWAKILI - Mawakili waaminifu wanaendelea katika hatuwa zao za usimamizi


 

    Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji na wasimamizi wa makanisa katika vijiji 

Mada yetu kwa mwaka huu wa 2025 ni Uongozi wa Muwakili.


Kwa ukumbusho, Muwakili anatafsiriwa kama ''mtu anayesimamia rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali'' kwa mtazamo wetu, tunaongoza rasilimali tulizopewa na Bwana kwa ajili ya kazi yetu ya upandaji wa makanisa katika vijiji.


Katika vipindi vilivyopita, nilionyesha Mada tano kubwa za uwakili:


1. Tabia inahusika.

2. Mawakili wanaombwa kutowa ripoti ya uwakili wao 

3. Muwakili anapashwa kujuwa kujenga mawasiliano 

4. Muwakili anastahili kugawanya malengo ya ukuaji ya bwana wake.

5. Mawakili waaminifu wanaendelea katika hatuwa zao za usimamizi.


Leo, tutajadili Mada hii ya mwisho, iliyo ya muhimu sana, na tunarudilia mfano wa talanta katika kitabu cha Mathayo 25:14-30

Kumbukeni : watumishi waliyo pokea mifuko tano na mbili za zahabu walikuwa mawakili waaminifu na walizidisha rasilimali zao.


Napenda tuangalie kwenye vesi za 28 na 29.

Wakati Mtumishi mvivu hakuleta chochote kwa bwana wake, bwana wake alisema hivi:


Ondoeni kwake ule mfuko wa zahabu, na mumupe yule aliye na mifuko kumi.

Sababu kwake aliye na vingi, atapewa mengine, na atakuwa na mali mingi...''


Nataka kurudilia huyu msemwa, sababu ni wa muhimu sana;


''kwake aliye na vingi, atapewa mengine, na atakuwa na mali mingi.''


Kanuni iko wazi;

✓ mawakili waaminifu watapewa zaidi.


Kanuni hii inafanyika sana ndani ya kazi yetu ya upandaji wa makanisa katika vijiji.


Tunaona vuguvugu ya ajabu na upendeleo wa Mungu unaonekana kupitiya Afrika kwa mpango wa shirika la VCP (village church planting) angalia matokeo fulani:


Kwa miaka tano, tulizidisha mara mbili hesabu ya inchi ambamo tunatumikia ndani.


Kwa miaka tano, tumezidisha mara mbili hesabu ya vituo vya mafunzo vya VCP.


Kwa miaka tano, bajeti yetu (tukiongeza pesa za miradi muhimu) ilizidishwa mara mbili



Kwa mwaka wa 2024, zaidi ya waamini wapya 250 000 walimpokea Kristo, ripoti ikitolewa ndani ya makanisa yaliyopandwa na mpango wa VCP.


Tuna moyo wa shukurani kwa upendeleo na mpangilio wa Mungu, na tunastahili kuongoza vizuri yote hayo.


Pamoja na kuongezeka huku kwa VCP, inatupasha kuwa na watendakazi na wasimamizi. Hii inamaanisha kwamba kuwa na waalimu wapya, waratibu wapya, na  makasisi watakao ongezwa kwenye timu _ na watachaguliwa miongoni mwa wale walio onyesha uwakili wa uaminifu.


Mawakili waaminifu wanaendelea katika hatuwa zao za usimamizi.


Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wa makanisa katika vijiji.

UONGOZI WA MUWAKILI - Anapashwa kugawanya ukuaji wa malengo ya Bwana wake


 

    Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji na kwa viongozi.


Mada yetu leo ni Uongozi kama vile Muwakili. Kwa kukumbusha haraka, Muwakili anatafsiriwa kama ''mtu anayesimamia rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali''. Kwa mwelekeo wetu tunaongoza rasilimali tulizopewa na Bwana kwa ajili ya kazi yetu ya upandaji wa makanisa katika vijiji.


Kwa mwanzo wa mwaka, katika kiingilio changu kuhusu swala hili, nilisema kama tutachunguza Mada tano kubwa za uongozi ;


1. Tabia inahusika


2. Mawakili wanashurutishwa kutowa ripoti ya uwakili wao


3. Muwakili anastahili kujenga mawasiliano


4. Muwakili anastahili kugawanya malengo ya maendeleo ya bwana wake


5. Mawakili waaminifu wanaendelea katika hatuwa zao za usimamizi


Mada ya leo ni kwamba Muwakili anapashwa kugawanya malengo ya maendeleo ya bwana wake, na tutaijadili katika mwelekeo wetu wa upandaji wa makanisa katika vijiji.


Ya kwanza, tuzingatiye maono yetu ya VCP ambayo ni : ''kanisa katika kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2025'' haitawezekana kufikia lengo hili bila ukuaji. Kama tunapenda kuongoza vizuri rasilimali na utoaji kwa Mungu kupitiya VCP, tunastahili kutamani kuwa na ukuaji (Na tumsifu Mungu, sababu VCP imepata maendeleo makubwa ya kushangaza, sababu kwa leo tunatumika sasa katika mataifa 36 za Afrika na kuwa na zaidi ya vituo vya mafunzo 800.)


Ya pili, tuzingatiye Mada hii kwa maoni ya Bwana wetu. Sababu gani Bwana wetu angekuwa na maoni ya ukuaji ?

Tuangalie maandiko.


2Petro 3:9 inatuambiya : ''Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.'' mapenzi ya Bwana ya kuona ''wote wamefikilie toba'' inafanana kabisa na lengo la ukuaji wa Ufalme. 


Tunaona ujumbe mwengine wa kufanana na huu wa Mtume Paulo anaye andika kwa 1Timotheo 2:3b-4 : 

''... Mungu Mwokozi wetu; 

ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.'' hapo pia, tunaona lengo la maendeleo la Bwana wetu, sababu matakwa yake ni kwamba watu wote wafikilie ujuzi wa wokovu wa Yesu-Kristo.


Kwa mwisho, katika Ufunuo wa Yohana, tuzingatiye maono haya kwa sura ya 7, vesi 9 : ''Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao ...''


Mkutano mkubwa ambaye hakuna mtu awezaye kuuhesabu wa waabiduo katika mbingu, ''wa kila taifa, wa kila lugha, wa kila jamaa na Kabila '' inaonyesha ukuaji wa Ufalme wa Bwana wetu, na ndiyo shabaha yake kwetu ili tushiriki kwa hilo kusanyiko kubwa.


Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji na kwa viongozi wao.

UONGOZI WA MUWAKILI - Uwajibikaji


 

  Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji na kwa viongozi.


Mada yetu leo ni Uongozi kama vile Muwakili. Kwa kukumbusha haraka, Muwakili anatafsiriwa kama ''mtu anayesimamia rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali''. Kwa mwelekeo wetu tunaongoza rasilimali tulizopewa na Bwana kwa ajili ya kazi yetu ya upandaji wa makanisa katika vijiji.


Kwa mwanzo wa mwaka, katika kiingilio changu kuhusu swala hili, nilisema kama tutachunguza Mada tano kubwa za uongozi ;


1. Tabia inahusika


2. Mawakili wanashurutishwa kutowa ripoti ya uwakili wao


3. Muwakili anastahili kujenga mawasiliano


4. Muwakili anastahili kugawanya malengo ya maendeleo ya bwana wake


5. Mawakili waaminifu wanaendelea katika hatuwa zao za usimamizi


Katika podikasti ya mwanzo wa mwezi wa juni, nilijadili Mada ya kwanza : Tabia inahusika.

Leo tutajadili Mada ya pili : Usimamizi. Tuliiona katika mifano ine tuliyojifunza, na zaidi kwa upekee ndani ya mfano wa talanta katika Mathayo 25:14-30


Kwa mwanzo, kuko zawadi kwa uwakili bora. Angalia katika vesi za 21 na 23, kuhusu wale waliopata talanta tano na talanta mbili, kwa mara moja, maneno ya bwana yanafanana : ni vema, Mtumishi mwema na mwaminifu !

Ulikuwa mwaminifu kwa mambo madogo, nitakupa mengi.''


Mara nyingi, ''usimamizi'' unatumikishwa tu kwa mwelekeo mbaya, lakini siamini kuwa hii inastahili kuwa vile.

Kama kiongozi, utumishi bora wa usimamizi ni kukamilisha mwenendo, tendo ao matokeo binafsi. Inafanishwa na kiongozi wa michezo (kocha) anayewapa moyo na kuimarisha vizuri mchezaji wakati anapofaulu.


Kwa hiyo, anapashwa pia kuonekane usimamizi hata wakati wa kushindwa.

Katika mfano wetu, Muwakili mbaya alihamakiwa na kuhazibiwa. Tunayaona hayo kwa vesi za 24-30.

Mtumishi ambaye hakufanya chochote na talanta yake moja, alionekana kuwa ''mbaya '' na ''mvivu'', na talanta aliyokuwa nayo ilinyanganywa.


Viongozi bora wachaMungu wanastahili kuwa na hekima na utambuzi muhimu ili kujuwa ni kwa wakati gani na kwa namna gani kuwafanya wengine kuwa wasimamizi wa mwenendo wao mbaya, matendo mabaya Wala matokeo mabaya. Napendekeza kwamba sababu maalm ni wakati mtu anajuwa anacho stahili kufanya lakini haifanye. ( Angalia Yakobo 4:17.) Ndani ya mfano wa talanta, Mtumishi ''mbaya'' alijuwa kama bwana alitarajia matokeo kwa yale aliyompa.


Kwa namna ingine, ningesema kwamba wakati makosa yanapotendeka sababu mtu moja hakujuwa kilicho tarajiwa ao kile angestahili kufanya, hiyo ingestahili kutumikishwa kama fursa ya mafundisho kwa kiongozi.


Mawakili wanaombwa kutowa ripoti ya uwakili wao, na viongozi wanatumikisha usimamizi moja kwa moja kwa washirika wao.


Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji na kwa viongozi wao.

UONGOZI WA MUWAKILI - Kuhamakia kwa mamlaka kama ikiitajika


 

  Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji na kwa viongozi wa makanisa.

Tunaendelea na mfululizo wetu juu ya uongozi. Leo, napendelea kugawanya nanyi maelekezo ya ziada kuhusu kitu nilicho shiriki imepita sasa wiki mbili.


''Muwakili'' anatafsiriwa kama ''mtu anayesimamia rasilimali alizopewa na mtu mwengine, ili kufikia malengo ya mwenye mali''. Katika muelekeo wetu, tunasimamia rasilimali na tunatumikisha mamlaka tuliyopewa na Bwana kwa ajili ya kazi yetu ya upandaji wa makanisa katika vijiji.


Tazama mara ingine ombi ya hapa karibu ya moja kati ya rafiki zangu makasisi wa OMS :

''Bwana, tusaidie kuongoza madaraka tuliyopewa.''


Katika vipindi vyangu vilivyopita. Niligawanya haya mafundisho kuhusu uongozi yaliyotolewa katika Tito 2:15 : ''Fanya mambo hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka. Mtu yeyote asikuzarau. 


Kwa kutafakari juu ya mafundisho ya Mtume Paulo, nilijiuliza maswali mengi :


Ni kwa matokeo gani viongozi wanastahili ''kukaripia kwa mamlaka ?


Ni kwa hatuwa gani viongozi wanastahili kujizuwia kuhamakia mtu?


Kama ni muhimu kukaripia, ni kwa namna gani tunastahili kuitenda?


Kwa mwisho, Paulo anapendelea kusema nini wakati anasema kwamba tunastahili kukaripia kwa mamlaka?


Mbele ya yote, kukaripia ni sahisho linalo elekea kwa mtu anayejidanganya katika mafundisho wala katika mwenendo wake. Shabaa ya kukaripia kwa haki ni kumrudisha kwa ukweli ; siyo kumfezehesha. Viongozi wazuri wachaMungu wanastahili kuwa tayari kuhamakia wengine ili kuwafanya upya ao kuwakingia na yale ambayo yangeleta shida kutokana na tukio.


Baadaye, ningependekeza kama kungekuwa mda ambao tungeweza kujizuwia kuhamakia.

Kwa jumla, ninafikiria matokeo mawili. Ya kwanza ni wakati kaka wala dada mkosaji haiko kwenye mamlaka yetu : yeye ni Msimamizi mbele ya wengine. Hiyo inajumlisha pia matokeo ambayo sisi hatuna mawasiliano na yule anayepotea kwa mafundisho ao kwa mwenendo. (Angalia Mithali 27:6)


Hii inanielekeza kwa hatuwa zimoja juu ya namna, viongozi wa kiroho wanastahili kukaripia. Waefeso 4:15 inatusii ''kusema ukweli kwa upendo '' kwa hatuwa hii, ningependekeza kwamba wakati tunachaguwa kuachilia mwenendo wa dhambi wala mafundisho potevu, hatutendi kwa upendo zidi ya mtu mwovu ; kinyume chake ni kwamba, tunajihuzuru kwa majukumu ya kiongozi.


Kwa mwisho, Paulo anafundisha viongozi wa kiroho kukaripia kwa ''mamlaka yote'' inamaanisha nini ? Mamlaka yote'' yanatolewa na Mungu, na wamoja wetu wanatumia madaraka ni wasimamizi mbele ya Mungu.


Kwa kuhitimisha, Yakobo 5:20 anasema : 

''Jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.''


Mara ingine, tutaendelea na somo letu kuhusu uongozi wa Muwakili.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wa makanisa katika vijiji.

UONGOZI WA MUWAKILI - Kuongoza madaraka tuliyopewa



 

Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi katika vijiji.

Tunaendelea na mfululizo wetu juu ya uongozi wa Muwakili kwa kutafakari sehemu ya mada kubwa zinazoshikamana na hatuwa hili. Leo, napendelea kugawanya nanyi maombi ambayo niliyasikia hapa karibuni kutoka kwa mmoja wa watumishi wenzangu makasisi wa O.M.S.


Kwa ukumbusho wa haraka, Muwakili anatafsiriwa kama ''mtu anayesimamia rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali''.

Kwa mwelekeo wetu, tunaongoza rasilimali na madaraka ambayo Bwana alitupatiya kwa ajili yetu ya upandaji wa makanisa katika vijiji.


Tazama maombi yake: ''Bwana, tafazali,  tusaidie kuongoza madaraka yetu vizuri tuliyopewa.''

Ombi hili liligusa moyo wangu, sababu kwa mda wote wa majifunzo ya mfululizo juu ya uongozi, nilijihusisha sana juu ya uongozi wa rasilimali za kiuchumi wala za binadamu. Mungu anatupatia watu wazuri ili tutumike pamoja nao, wanasaidia kwa pesa za kutosha kwa ajili ya huduma.


Lakini anatupatiya pia madaraka yake.

Tujifunze jambo hili leo. Tazama vesi mbili za Biblia zinazozungumzia Mada hii:


''Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.''

Waebrania 13:17


Sisi kama viongozi, Mungu alituweka katika hatuwa za madaraka.

Lakini, kama watumishi-viongozi, madaraka haya yanapashwa kutumikishwa kwa ajili ya kuwahidumia wengine na kuhudumia Ufalme. Napenda kukazia nukta mbili hapa :


1. Tunastahili kukesha kwa ajili ya wale tunaowaongoza.

2. Mungu anatudai mbele zake kwa namna tunavyokesha kwa ajili yao.


**"Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 

nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 

Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote".

 _ Tito 2:11-12,15


Kwa mara ingine tena, napenda kukazia sehemu ya hatuwa ambazo tunapata katika mafundisho ya Mtume Paulo :


1. Ujumbe wa wokovu wa Mungu unawahusu watu wote.

2. Neema ya Mungu haistahili kutumikishwa vibaya. Tunastahili madaraka tuliyopewa kwa kufundisha wanafunzi kuzikataa tamaa za dunia na kuishi maisha matakatifu.

3. Kwa utumishi wa madaraka yetu, tunastahili kutiya moyo pia kuhamakia, kwa usawa. Kuhimarisha kwa zaidi kunaweza kuzuwa kiburi kwa wengine. Kuhamakia kwa zaidi kunaweza kuwavunja moyo. Walio chini ya madaraka yetu wanaitaji hivi vitu viwili, na tunaitaji roho ya utambuzi kwa kujuwa kile nilicho cha muhimu kwa kila nyakati na majira.


Kwa turu nyingine, tutaendelea na somo letu kuhusu uongozi wa Muwakili.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wao

Uongozi Wa Muwankili - Kuzaa matunda



 

     Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji na kwa viongozi


Tunaendelea na mfululizo wetu juu ya uongozi wa Muwakili kwa kutafakari sehemu ya mada kubwa kuhusu uwakili.

Leo, napendelea kugawanya nanyi maombi ambayo hapa karibuni niliyasikia kutokea kwa Mchungaji moja kutoka Nigeria.


Kwa kukumbusha, Muwakili anatafsiriwa  kama : ''mtu anayesimamia rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali''. Kwa mtazamo wetu, tunaongoza rasilimali tulizopewa na Bwana kwa ajili ya kazi ya upandaji wa makanisa katika vijiji.


Tazama maombi ya Mchungaji Isaac, niliyoyasikia imepita sasa wiki chache:

"Kuwa juu ya kila kitu, tunaomba ili tuwe wenye kuzaa matunda mengi zaidi kwa Ufalme wako.''


Kwa kugawanya maneno ya maombi haya, ninaona alama tatu za muhimu alizotaja.


Anaanza na ''kwa kuwa juu ya kila kitu''. Hii inamaanisha kwamba ni kipaumbele cha kwanza katika uongozi wetu. Kiongozi Muwakili aliye mfano atakazia sana juu kuzaa matunda. Nitaongea mengi katika podikasti yangu ya kufuata juu ya hatuwa hii, kwa kipekee juu ya umuhimu wa  uwajibikaji.

''kipaumbele'' chetu, Mungu, kama ndani ya mfano wa Talanta (Angalia Mathayo 25:14-30), anatarajia kupokea marudilio ya kile alichotupatiya.


Kwa sehemu ya pili, katika maombi yake, Mchungaji Isaac aliomba ili tuwe ''wenye kuzaa matunda mengi zaidi''. Kuzaa matunda ni itaji kubwa ya kiongozi Muwakili. Moja ya vesi inayonigusa sana ni kwa kipekee ile ya Luka 12:48b :

''... Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.''

Neno ''kuomba'' katika toleo la New international Version liko nguvu. Tafsiri zingine, kama vile New English Version, inatumia maneno '' hitaji'', ''kungoja'' ao ''kuwajibisha''. Ujumbe uko wazi : Bwana ataomba kwa  viongozi yale waliyatenda, namna walivyotumikisha rasilimali walizopewa.


Kwa mwisho, alimalizia maombi yake ''kwa ajili ya Ufalme wako''. Nafurahia hiyo zaidi sana. Munaona, ni Ufalme wa Kristo ambao utafaidika na kazi yetu. Hatutumiki ilikujijengea umaarufu wetu ao kuangalia ajili ya huduma yetu binafsi.

Viongozi mawakili hawatumiki sababu ya kupandishwa vyeo. Yesu alifundisha hivo katika hotuba yake juu ya mlima : ''utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na mengine mtazidishwa baadaye.'' (Mathayo 6:33)

Mara nyingi, ujuzi wala kupandishwa cheo vinaweza kutokea baada ya kazi yetu, lakini ni matokeo tu, wala siyo malengo za uongozi wa Muwakili.


Wakati ujao, tutaendelea na somo letu kuhusu uongozi wa Muwakili.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi katika vijiji.

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...