Jumatatu, 23 Septemba 2024

Kutembea Katika Maombi - Siku 90 za Maombi na Kufunga




 Tazama ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo makanisa, wapandaji wa makanisa katika vijiji, wachungaji na viongozi wa Kikristo, ni mimi mgeni wenu, Danielle Snowden.


Kumbukumbu 11;24 inasema :''Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu .......''


Makanisa mamoja ya ki Anglikane wanatembea katika maombi kando kando ya kanisa zao, wanazoziita ''piga viungo'', tendo linalo dai uwanja kwa ajili ya Mungu katika maombi.


Ndivyo tunavyofanya, kwa kudai ahadi hii tukiwa watoto wa Mungu ili kwenda kuomba kwa eneo na kikundi la watu. Baada ya hapo, anaamsha Roho wake ndani ya maisha ili wapokee Neno la Injili ambalo mutakalo waletea ninyi kama wapandaji wa makanisa.


Kuomba kunatuletea mbele ya yote roho na moyo uliyo wazi ili kusikia kwa makini mwongozo wa Mungu na kusikia nguvu zake ili kutekeleza mpango wake mkuu ndani ya Kijiji hicho na wakaaji wake. Itakuwa kwa shabaa iliyojuu ya Mungu ya kuleta Roho na wokovu wake kwa wote wasio mujuwa Yesu kama Bwana na Mwokozi.


Katika kipindi cha siku 90 za maombi na kifungo, tunafanya hivo kwa kujikusanya katika maombi kwa shabaa hiyo moja !

Kuleta injili kwa kila Kijiji cha Afrika.


Ilikuwa ongezeka, ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Mungu awabariki !

Ombea Wagonjwa Na Wanaoonewa Na Mapepo - Siku 90 za Maombi na Kufunga




 Jambo kwa wote, tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wa Kikristo katika vijiji.

Naitwa Brad Snowden. Wakati Yesu alipowaita Mitume wake, aliwaambia ''njoni, munifuate''. Wangestahili kujifunza kujuwa roho. Nguvu ya injili inahusu kubadilisha roho. Yesu alipendelea kuwapa moyo kwakuwaambia kuwa, ijapokuwa njia yoyote atakayo ifuata, ilihusu tu mbele ya yote kubadilisha roho. Tunapashwa kujuwa kwamba Mungu anatumikisha namna nyingi tofauti ili kututiya moyo kwa  kumtegemea. Wakati Yesu alipotembee juu ya hii inchi, maisha ya wengi yalibadilishwa sababu aliponya magonjwa yao ya kimwili. Mathayo 14:14 ''Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.'' Yesu anatamani kwambo mioyo iguswe ili iweze kujuwa upendo wake na uwezo wa Neno lake. Oh, Acha Mungu apate fursa ya kubadilisha maisha ya wengi kiroho na kimwili. Roho wa Mungu ni ajili ya kugusa na kuponya wagonjwa, Yakobo 5:14-16 inatupa moyo kututumikisha kwa karama hiyo. Wakati tukimwomba fursa hii, atafanya kazi. Shuhuda zenye nguvu nitagawanywa sababu uruma ndani ya roho ya mwanafunzi wa Yesu-Kristo iliwaombea na wakaponywa. Kuko watu wengi wanaosumbuliwa na magonjwa ya kimwili na tunasoma Luka 4:18 Yesu anasema kuwaweka huru mateka wanaofungwa na utumwa wa kimwili. Alikuja pia kuwaweka huru wanaoonewa na adui. Shetani anapendelea kugandamiza roho zinazoteseka ili wapoteze matumaini. Nawaomba leo kama hatukupokea matumaini kwa Yesu ? Tumaini hii inapashwa kuonekana na kufanyika. Neno la Mungu linajaa na matumaini na tuko na fursa kubwa ya kugawanya tumaini hii pamoja na wale walio na itaji kwamba Yesu aponye miili yao.

Kuko mioyo inayoweza kubadilishwa, ndoa na vijiji ambavyo vinaweza kubadilishwa kwa maombi rahisi kwa wale wanaoitaji uponyaji. Oh, acha tuwe sauti hiyo na tendo hilo la tumaini.

Ilikuwa Neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili ? Bwana Mungu awabariki !

Kupata Watu Wa Amani - Siku 90 za Maombi na Kufunga




 Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Yesu alimwambia Petro na marafiki zake: ''munifuate na nitawafanya kuwa wavuvi wa watu''. Pengine uliwai kama mimi kusikia hadisi na kujibu ''napenda kuwa muvuvi wa watu. Nifanye na mimi kuwa muvuvi wa watu. Kuvuwa watu siyo rahisi. Kuita wanaume na wanawake, wavulana na wasichana kutubu na kuamini Habari Njema mara nyingi ni kazi ngumu.

Najuwa ilinifikia kutumika nguvu kwa kujitayarisha kwenda kutangaza injili. Nilitayarisha vizuri sana ujumbe wangu. Niliomba sana. Na baadaye, nilipofika kwenye mahali, nikahubiri na sikuona matokeo yoyote. Umekwisha wai kuishi tokeo hili?

Inavunja moyo. Lakini baada ya miaka 30 tangia nilipoanza kuhubiri Habari Njema, nilijifunza kuwajuwa wa amani. Luka 10:1-12 inatufundisha kuwa Mungu anatusaidia kupata wanaume na wanawake walio na kiu ya kumjuwa. Wakati tunagawanya Habari Njema, wanasikia. Wakati tunapo wapendekeza kuomba, wanafurahia Sisi kuifanya. Wakati wanapokuwa na maswali juu ya Biblia, wanayauliza... na wanasikia baadaye kila neno tunalotamka kama jibu. Wakati tunapowafundisha kutii Yesu wanafanya hivo. Watu hawa wanaitwa ''watu wa amani ''.

Wakati naenda kuvuwa watu na kama nawapata watu wa amani, ni kama vile sikuweza kutupa wavu na kuikokota. ''samaki'' hawa wanafanana kurukia ndani ya mtumbu wangu ! Ni sababu Mungu kwa neema yake, alitayarisha watu wa amani kujibu kwa Habari Njema.

Wakati wa mwezi wamunane, wakenda na wakumi, mutatumika kwa upandaji wa makanisa mapya. Lakini Mungu hakungojea mwezi wa munane ili kuanzisha huu mradi. Mbele ya mwezi wa munane, alitumika katika roho za wanaume na wanawake walio na njaa ya kumjuwa Mungu. Ni kwenu kuwapata.

Kupata watu wa amani ni fungulo kwa kupanda makanisa mapya katika vijiji visivyo na kanisa.

Lakini muliwafundisha wanafunzi wenu kutafuta watu wa ?

Muliwahafisia hadisi ya mwanamuke kwenye kisima. Alikuwa akiisha kwa ukahaba, lakini alipokutana na Yesu, roho yake ilibadilishwa na, kupitiya yeye, kijiji chake kilibadilishwa pia (Yohana 4).

Muliwaambia wanafunzi wenu kuhusu Kornelio, askari wa kirumi aliye muita Petro kufika nyumbani kwake?

Kupitiya Kornelio, jamaa yake yote ilipokea Habari Njema na Roho Mtakatifu akawashuka kwao wote. (Matendo 10). Muliwafundisha wanafunzi wenu kutafuta watu wa amani kwa kugawanya ushuhuda wa sekundi 15 ? Muliwaonyesha namna ya kuwapendekezea kuombea wagonjwa na maitaji mengine ya watu walio mbali na Mungu ? Mulikwenda pamoja na wanafunzi wako wakati ulipo muuliza mtu moja ''naweza kukuhadisia hadisi ya Biblia ambayo imenigusa sana ?

Umekwisha kuwaonyesha tu namna ya kuhadisia hadisi ya Biblia na baadaye kuwaambia maana kwa kuuliza maswali sita rahisi ?

Wanafunzi wako wanajuwa kutafuta watu wa amani ? Ni mda wakuwafundisha. Ni mda wakuwasaidiya wa kujaribu tendo la Mungu kwa kutafuta na kupata watu wa amani ! Tuko katika mwezi wa kwanza wa Siku 90 za kifungo na maombi kanisani. Ni wakati wa kufundisha wanafunzi wako ginsi ya kupata watu wa amani. Ni wakati wa kwenda pamoja nao katika vijiji ambako hakuna kanisa ili waweze pamoja nawe, kuvuwa watu. Ni kwa mda huu unastahili kufurahi pamoja wakati wewe pamoja na wanafunzi munawapata watu wa amani.


Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis nawauliza ''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Kuhadisia Hadishi Za Biblia - Siku 90 za Maombi na Kufunga




 

Jambo  wapenzi wapandaji wa makanisa, Kaka na dada.

Nawasalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu-Kristo. Mimi ni Mtumishi wenu, Mchungaji Douti Claude, Kasisi wa VCP. Asubui ya leo, ningependelea kukuambia kuhusu Mada  ya ''kuhadisia hadisi za Biblia ''. Kama mujuavyo , Biblia ni kitabu cha hadisi za Mungu kuhusu Mungu na wanadamu. Ili kuelewa vizuri kile ninataka kusema na kuwa na ujuzi wakati wa kuhadisia hadisi za Mungu, unaweza kusoma '' Fundisha na ongezeka '' muhula wa 1 katika ukurasa wa 65-02 hadi ukurasa wa 65-38. Lakini kwa ufupi, napendelea kuwaambia kuwa Yesu-Kristo, ambaye alikuja kama Mwana wa Mungu, yeye mwenyewe alihadisia hadisi za Mungu na alitupa moyo kuifanya, kuhadisia hadisi za Mungu. Katika Mathayo 28, vesi 19 na 20, Marko 16, vesi 15, Yesu alitupa moyo kwenda kuhubiri Habari Njema kwa viumbe vyote.

Katika Mathayo, anasema kwenda kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi. Na ni wazi kuwa ni hadisi za Biblia ambazo tunastahili kuhadisia watu. Sasa ni nani anastahili kuhadisia hadisi ya Mungu? Ni sisi, kama vile wanafunzi wa Yesu-Kristo. Na kwa wanani tutawahadisia hadisi? Kwa viumbe, kwa wote ambao Mungu aliumba : kwa kila binadamu aliye juu ya inchi, kwa wote ambao wanawaza kusikia Neno la Mungu ambalo Yesu-Kristo aliita Habari Njema, Injili. Sasa, kaka na dada wapenzi, napendelea kuwatiya moyo kusoma zaidi kitabu na kupata maelekezo juu ya namna ya kuhadisia hadisi na sababu gani kuhadisia hadisi za Mungu, hadisi za Biblia.

Namna gani unaijuwa, katika jamaa zetu, watu wanapenda kusikia hadisi. Na unajuwa kama hadisi za Mungu zinafanana kuwa hadisi zisizo na madhara, hazigombane na mtu, haziwatukane wengine. Na mara nyingi, hadisi za Mungu ni za kuchekesha, lakini zinaleta pia tahadhari. Na ziko nzuri kuzisikia.

Inafaa tu kujuwa namna yakuzitangaza kwa wengine. Inastahili kujuwa kuzitangaza kwa ufupi, kwa makini sana, kwa usahihi. Hivo, ili kusimamisha agano lako, inastahili kutayarisha hadisi yako, mara nyingi ukitumikisha picha ndogo, vyombo vya kuleta mifano vinavyoitwa storyboard, kwa kujenga storyboard yako, ao wakati unapo hadisia hadisi, unaweza kumbuka nukta muhimu, sehemu muhimu za hadisi, ili kwamba hadisi iwe hai, ya kweli na ya kufurahisha. Nawapa moyo kwa kujitayarisha vizuri wakati unachaguwa hadisi ndani ya Biblia. Kuko hadisi nyingi katika Biblia, na kama unachaguwa ile ambayo unapendelea kuhadisia, uwe umejitayarisha vizuri sana, uwe na uhakika, na kuwa na uwezo wa kuhamasisha watu kukufuata ili kwamba hadisi izae matunda.

Na kwa Wale wanaokusikiliza, ili kwamba upate watu wanaokusikia na wanapokea Neno la Mungu ndani ya roho zao. Kaka na dada wapenzi, neema ya Mungu iwe juu yenu na iongezeke.

Jifunzeni na kufanya mazoezi kuhadisia hadisi za Mungu.

Mungu awabariki.

Gawanya Ushuhuda Wako Wa Sekundi 15 - Siku 90 za Maombi na Kufunga




 

Hamjambo wandugu wapenzi Kaka na dada wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Nawasalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu-Kristo. Napendelea kuwaambia asubui ya leo kuhusu ushuhuda wa sekundi 15.

Tunaweza kupata Mada hii ndani ya kitabu cha VCP Fundisha na ongezeka muhula wa 1 katika ukurasa wa 66-18 hadi 66-27.

Wandugu wapenzi Kaka na dada, wakristo wengi hawajuwe namna ya kutangaza injili. Namna gani kuwakaribia watu ?

Wakristo wamoja wanasema kama watu hawatajiamini wenyewe, wengine wanasema hawajuwe nini watasema, wengine wakristo wako na haya na mtindo huu wa tabia unapunguza mwendo wa kazi ya Mungu.

Muniruhusu niwakumbushe, wapandaji wapenzi kwamba ushuhuda wenu wa sekundi 15 unaweza kuleta msisimuko wa mawazo, kufunguwa vifungo vya roho zilizo ngumu.

Ushuhuda wa sekundi 15 ni nini ?

Wakati unapenda kutumikisha ushuhuda wa sekundi 15, Utakutana kwanza na mtu, unakutana na msikilizaji wako baadaye unamusalimia, na unamwambia : tafazali, naweza kugawanya nawe hadisi ndogo ? Watu wote wanapenda hadisi, sherti watakubali kukusikiliza kwa makini na baadaye utawaambia ''kwa wakati mwengine ilifikia kwa maisha''.

Kila ushuhuda wa sekundi 15 unaanza na msemwa huu ''ilifikia wakati mwengine ndani ya maisha yangu''. Baadaye utawaambia kuhusu maisha Yako kabla haujampokea Yesu, kisha utasema namna gani rafiki ao ndugu yako alikueleza kuhusu Yesu na ukampokea kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako binafsi, baadaye utamuhadisia namna gani Yesu alibadilisha maisha yako.

Usisahau kumuuliza swali hili:

Je! Unaweza kuwa na hadisi kama hii ya kugawanya nami ?


Akisema ''ndiyo'' utajuwa kama ni ndugu katika Kristo na hapo utaweza kusherekea na kumsifu Mungu pamoja naye.

Akisema ''hapana'', endelea maongezi naye ukimuuliza ''unaweza kuniruhusu nigawanye nawe uzoefu mzuri niliopata ndani ya Yesu? Akijibu ''ndiyo'', unapata tena fursa ya kumwambia kuhusu Yesu kama Bwana na Mwokozi. Akisema ''hapana'', usimukaze. Kubali maamuzi yake. Baadaye, munaweza kubadilishana namba za simu na kuendelea kumuombea.

Hiyo ndiyo ushuhuda wa sekundi 15. Chombo hiki kinanguvu sana, usichoke.

Uko na hatuwa ine za kutenda wakati unaendelea kuongea kuhusu ushuhuda wa sekundi 15.

- kipindi cha 1: ilifikia wakati mwengine katika maisha yangu wakati niliteseka mbele ya kumjuwa Yesu-Kristo .

- kipindi cha 2: rafiki ao ndugu yangu alinieleza kuhusu Yesu.

- kipindi cha 3: nilimukubali kuwa Bwana na Mwokozi wangu binafsi, ni mageuzi yaliyo tendeka ndani ya maisha yangu. Leo, nina amani rohoni mwangu.

- kipindi cha 4: swali la muhimu : je! Unayo hadisi kama hii ya kuhadisia ?

. Mungu awabariki, wapenzi wapandaji wa makanisa.

. Nafurahia kazi yenu ngumu kwenye vijiji ili kuwapata watu wa amani na kugawanya ushuhuda wa sekundi 15.

Amani ya Mungu iwe pamoja nanyi. Mimi ni Mtumishi wenu, Mchungaji Douti Claude, Kasisi wa VCP.

Ulikuwa ongezeka.

Shalom.

Hamasisha Wapandaji Wa Makanisa Kupanda Makanisa Mapya - Siku 90 za Maombi na Kufunga




 

Jambo ! Tazama ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wa Kikristo katika vijiji.

Mimi ni Brad Snowden na ndani ya podikasti hii, napendelea kuangalia mapigo ya moyo ya siku hizi 90 za kifungo moto moto, jina la podikasti hii ni ongezeka, msingi wa VCP ili kuwa na uwezo wa kufikilia lengo letu la 2050 ya kuwa na kanisa katika kila Kijiji cha Afrika. Hiyo inawezekana tu kwa kuzidisha. Kwa hiyo, wakati wa mda maombi yetu, sehemu moja ya hiyo ni kuhamasisha wapandaji wa makanisa kwa ajili ya Yesu.

Wakati tunapo fuata mwelekeo wake, yote inahusu kuhamasisha na wakati Mpandaji wa kanisa anapopanda kanisa kulingana na mfumo wa shamba ine, anafanya uanafunzi kwa furaha kuona wanafunzi wakikomaa na baadaye uwezo wa kuzidisha unakuja ndani ya ujumbe wa furaha kwa Wale wanaojihamasisha kwenda kupanda makanisa mapya. Kama tukienenda kwa moyo wa furaha unaotusukuma kupanda kanisa letu, wengine wataelewa na kufuata.

Kwa furaha ya kutekeleza Neno la Mungu kupitiya maisha yao binafsi, makanisa mapya yatapandwa. Tunaomba ili kwamba moyo huu uwashe zaidi ya moja ili kutekeleza mpango wa Mungu ili kufikia kila Kijiji cha Bara hili kubwa. Maandiko inasema kwamba pamoja na Mungu yote yanawezekana na anapenda kutumikisha kila Mpandaji wa kanisa kuwakilisha zawadi hii kubwa. Mungu alitupa kuangalia ufalme wake kuongezeka katika kila Kijiji. Ni msukumo gani ulio bora kujuwa hayo. Ulipokea bahati kubwa na uwajibikaji wa kuzidisha ufalme wake. Mungu anapenda twende kuwafundisha watu wengine kupanda makanisa mapya na kufanya uzoefu wa baraka hii kubwa.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Omba Kwa Imani - Siku 90 za Maombi na Kufunga




 

Jambo kwa wote ! Wapendwa wapandaji wa makanisa.

Nawasalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Ni mimi Mtumishi wenu, Mchungaji Douti Claude Kasisi wa VCP.

Hii ni ongezeka, Neno letu la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa. Imepita mda mchache, tuliongelea kuhusu Siku 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa.

Mumepokea ujumbe nyingi kwa kipindi hiki.

Kwa hiyo, asubui ya leo, napenda kuwaambia kuhusu ''maombi ya imani''. Kuomba kwa imani. Muniruhusu kwanza nisome kifungu cha Waebrania 11:1-6 inayosema :''Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. 

[2]Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. 

[3]Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. 

[4]Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena. 

[5]Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. 

[6]Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao''.

Tazama, wandugu wapendwa, Neno hili, muniruhusu ni anze kwa vesi ya mwisho. kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko.

Muwajulishe kwamba maombi munayo elekeza kwa Mungu, Mungu ataitekeleza. Nawapa moyo kupitiya vesi hii kuomba kwa imani. Muwe na Imani ndani yenu. Uhakikisho. Imani ni hakikisho ya mambo yatarajiwayo. Tunatarajia nini ?

Tunatarajia kupata makanisa mengi yaliyopandwa, mioyo mingi iokolewe katika Bara la Afrika katika mda wa miezi tatu ambayo tumeitowa kwa Mungu wakati tunapo enenda mbele zake.

Ndugu wapendwa, Imani ni ya muhimu sana, Mtume Yakobo anasema haina maana kuomba wakati tunakuwa na mashaka.

Nina Imani kwenu pia, wapandaji wa makanisa, tumepitiya mambo mengi, tuko na ushuhuda zinazoleta nguvu kwa imani yetu.

Ninajuwa kwamba baada ya miezi hii mitatu za maombi tutapata matokeo mazuri kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Munastahili kuwa na imani, kuomba kwa imani. Ombeni kwa kujitolea.

Amini kwamba maombi yenu yatakuwa na matokeo makubwa na kwamba jina la Mungu litatukuzwa.

Ilikuwa ongezeka, podikasti yetu ya kutiya moyo kila Siku.

Jifunze Upya Misingi Ya Upandaji Wa Kansisa - Siku 90 za Maombi na Kufunga



 Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Imenifikia mara nyingi kwenda kwenye ibada pamoja na binti wangu na kumuonyesha kuhusu ujumbe : ''ni ujumbe gani mzuri ! Ilikuwa kujazwa na injili tofauti na kingine isipokuwa tu injili''.

Yeye na mimi tunapendelea kusikia ujumbe wa kiinjili inayosema kuhusu nguvu za wokovu za Yesu-Kristo. Ni hadisi ya kimsingi ya wakristo wote.

Kwa namna hiyo, napenda kushiriki kwa mafundisho ya kimsingi ya wapandaji wa makanisa. Napenda kuona tena vipindi vya muhimu vinavyosaidia kupanda kanisa chembechembe itakayo komaa na kujizidisha. Ninaamini kwamba kwa mwezi wa nane, wapandaji wa makanisa wa Afrika nzima watakutana katika vituo vyao vya majifunzo VCP vya kawaida pamoja na wakufunzi wao ili kurudilia misingi ya upandaji wa makanisa.

Ni nini misingi ya upandaji wa makanisa ?

Ni ujuzi zinazo onyeshwa ndani ya muhula wa 1 na wa 2 ya mpango mpya wa VCP .

- pambanuwa, tafuta vijiji visivyo na kanisa 

- omba kwa ajili ya vijiji, pamoja na kuendelea katika maombi katika vijiji.

- tafuta na kupata watu wa amani 

- Gawanya Habari Njema ya Yesu pamoja na watu wa amani, jamaa zao na marafiki wao

- Fanya wanafunzi kwa kufundisha waamini wapya kutii Agizo Saba za msingi za Kristo,

Ndizo kazi za muhimu za wapandaji wa makanisa. Wakati tukienenda kwa imani na kufanya kazi hizi 5 za msingi za upandaji wa makanisa, Tunakutana na Mungu. Anatupa nguvu. Anatusaidia kujenga mawasiliano mema.

Wakati tunatekeleza kazi hizi kwa kuweka Imani yetu kwa Mungu na kwa upendo wake mukubwa kwa watu waliopotea, anatujaza upendo na nguvu.

Ni ujuzi wa msingi ambao wapandaji wote wa makanisa katika vijiji wanastahili kujifunza, kutumika na kuboresha.

Lakini kwa wengi ndani yetu, kazi hizi ziko ngumu sana. Tunapata basi zingine kazi zilizo rahisi zaidi ambazo tunahusika.

Siku zetu 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa ziko na lengo ya kubadilisha hayo yote. Mbele ya yote, tunaomba. Tunaomba ili tujazwe na upendo. Tunaomba ili madaraka ya ondoke. Tunaomba ili Mungu atuonyeshe watu wa amani na kuwavuta kwake. Tunaomba ili Mungu awavute kwake watu waliopotea. Kwa kuendelea kuomba, tunaboresha ujuzi wetu wa msingi kwa hatuwa ya upandaji wa makanisa.

Kisha tunaendelea.

Kwa mda wa mwezi wa nane, wewe, pamoja na wapandaji wa makanisa wa VCP kwa Afrika mzima, watakutayarisha kwa vitendo. Kwa maombi, utatengeneza Imani yako na kufikia nguvu za Mungu ili kuwa mashahidi wake.

Kupitiya mafundisho, utaimarisha uwezo wako kwa misingi ya upandaji wa makanisa.

Baadaye, utaondoka pamoja na washiriki wa kanisa ambao utachukuwa kama wapandaji wa makanisa mapya. Wakati utaenda pamoja nao ndani ya vijiji visivyo na kanisa, Utakutana na Mungu. Atakuwa pamoja nawe atakufanya uwe na matunda. Kumbuka ahadi ya Yesu. Alisema : ''Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni''.

(Yohana 15:16).


Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis nawauliza : ''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Ongeza Kijungo Kwa Maombi Yetu - Siku 90 za Maombi na Kufunga





Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Tayari umekwisha kusikia ikisemwa Siku 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa, ambazo Kasisi wetu Mchungaji Claude, alitangaza kwa mwezi wa nane hadi wa kumi wa mwaka huu.

Maombi, kifungo na upandaji wa makanisa ni kazi tatu zinazo muheshimu Mungu na tunatumika pamoja.

Siyo kazi za uchawi. Hazimushurutishi Mungu kutenda. Lakini ziko na nguvu.

Mbele ya yote, kwa kuomba, kwa kufanya kifungo na kwa kwenda kupanda makanisa katika vijiji ambako hakuna kanisa, tunatangaza tegemeo yetu yote kwa Mungu mwenye nguvu zote. Tunajuwa kwamba ni kazi yake, bali siyo yetu. Yeye ni kiongozi wetu, sisi ni wasaidizi wake. Tunatumika pamoja na Kristo na tunamtegemea yeye. Sisi tuko zaifu lakini yeye ni mwenye nguvu. Tunaomba sasa. Tunajikumbusha ahadi za Mungu. Tunaunguma mazaifu yetu. Tunakumbuka namna gani aliwapa Mitume Agano jipya. Tunamwaminia ili kwamba atupe nasi uwezo huo huo.

Lakini siku zetu 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa siyo tu siku za maombi kwa ajili ya nguvu za Mungu.

Zinajionyesha siku zilizo andikwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 1 na 2, ambazo Mitume waliingia ndani ya chumba cha juu wakati wa kula karamu ya mwisho mbele ya siku ya Pentekoste. Waliomba kwanza, baadaye wakajazwa na Roho Mtakatifu.

Walitoka na kutangaza maajabu ya Mungu kwa watu ambao walikuwa bado kuamini Habari Njema.

Kwa mwisho, Bwana aliongeza kila siku hesabu ya wale waliokoka.

Sasa kwa nini kuongeza kifungo kwa maombi yetu ? Kifungo siyo uchawi. Haishurutishi Mungu kutenda.

Lakini ni ya muhimu ? Kama ni ndiyo, kwa namna gani ?

Kifungo ni cha muhimu, ni vema kujizuwiya kula wakati  wa Siku moja wala Siku nyingi ili kumtafuta Mungu. Lakini tunajuwa kwamba tunakutana na Mungu wakati tunapo acha kiburi chetu na tukimtafuta kwa unyenyekevu.

Anapingana na wenye kiburi, lakini anawapa wanyenyekevu neema.

Yesu alitarajia kifungo  kwa wanafunzi wake, lakini mwelekeo maalmu aliyowapa kuhusu kifungo ni kuepuka kifungo kinacho sababisha kuleta maabudu kwa wanadamu.

Hatufanyi kifungo ajili ya kupata ukubalifu kwa wengine. Tunafanya kifungo ajili ya kujiweka kwa Mungu, ili kusikia sauti yake na kukubali atuongoze maishani mwetu.

Kwa mda wa siku 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa, hakuna mtu atakaye tushurutisha kufanya kifungo. Kifungo ni tendo la kujitolea.

Lakini kama ni turu ya kwanza unafanya kifungo na ukiwa mwenye afya njema, nakupa moyo kujaribu kifungo.

Mtafute Bwana kwa moyo wako wote. Onyesha upendo wako kwa Mungu kwa nafsi yako yote. Ukionyesha kwa maneno tegemeo lako kwa Mungu, uionyeshe kwa wakati wa mda fulani, kwa kumtafuta Mungu ukijizuwiya kula.

Wakati wa kifungo chako na zaidi baada ya kifungo chako, Utakutana na Mungu. Atakuongoza, atakupa uwezo. Na nguvu za Mungu ni kila Siku kitu cha ajabu !

Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi ni Dean Davis nawauliza : ''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Tumikisha Mwongozo Wa Maombi - Siku 90 za Maombi na Kufunga


 Tazama ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji, wachungaji na viongozi wa Kikristo. Mimi ni mgeni wenu wa leo, Danielle Snowden.


Zaidi ya 10 000 ya wapandaji wa makanisa katika vijiji walihamasishwa katika inchi 32 tangia mwaka wa 2020. Tunaamini kuwa Mungu alitayarisha wanaume na wanawake wa amani kwa vijiji hivi vyote, ili wapokee Habari Njema.


Wapandaji wetu wa makanisa katika vijiji wanakabiliana na matatizo mbali mbali wakati wanapoitikia wito wa kupeleka injili ndani ya maeneo haya yaliyo mbali na miji.


Ni muhimu kwamba wote miongoni mwetu wanaogawanya maono mamoja ya upandaji wa makanisa waunganishwe ndani ya maombi, kwa makubaliano yenye nguvu (wakati Sisi tunaomba).

Kwa hiyo, mwongozo wa maombi iliyo andikwa kwa udondozi kwa ajili ya siku 90 za maombi, inayoitwa : Siku 90 za maombi, kifungo na za upandaji wa makanisa, ni kitabu kinacho tusaidiya sote kuomba.


Wakati tunapokuwa katika kifungo, tunajihusisha kwa ajili ya kila siku na ya maombi inayo onyweshwa, angalieni kwamba inashindikizwa na kifungu cha Biblia.


Ninataka kuwapa moyo kuomba na kujuwa kwamba watu wengine wanaomba maombi haya kila siku na kukariri maandiko ya ahadi juu ya mwongozo wa maombi.


Chukuwa kila ombi, ikariri, iangalie vesi inayo ambatana na maombi. Ngojea Bwana, baadaye omba kwa ajili ya kazi yako, ya wapandaji wako wa makanisa, viongozi wako, makanisa yako, wachungaji wako na wewe mwenyewe. Tunakutiya moyo kuifanya mara mbili kwa siku, wewe mwenyewe na baadaye na vituo vyako vya majifunzo wakati munapo kusanyika, na hivo pia pamoja na makanisa yenu. Omba tafazali, tafakari, na ngojea Bwana Ili kusikia. Ingestahili kuwa mda ambao Mungu atakupa ahadi, maono na mwelekeo.


Muwe waaminifu na kubaki ukitafakari, sababu maandiko yanasema : 

''Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya.''  (Isaya 50:7).

Uwe mwaminifu kwa Mungu na utangaze kwamba hautarudia nyuma mbele ya wajibu wako ambao Mungu amekupangia !


Asante kwa kutusikiliza leo!

Je! Unajuwa kwamba tuko na mtandao : vcpencourangement.org ?

Tuko pia kwenye mitandao mingi ya podikasti, na unaweza kutupata kwenye Facebook : na You tube, kwa anwani hii :

''Encouragement pour les planteurs d'églises de village/Multiplier ''.


Ilikuwa ongezeka, asante na Mungu awabariki !

Hamasisha Waombaji - Siku 90 za Maombi na Kufunga



 

Hamjambo nyote !

Hamjambo wapandaji wapendwa. Tazama ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wote wa makanisa katika vijiji.

Mimi ni Mchungaji Douti Claude Kasisi wa VCP.

Turu ya mwisho, niliongelea kuhusu unyenyekevu ndani ya upandaji wa makanisa.

Tangia mda uliyopita, maneno yetu yote ya kutiya moyo yanahusika na siku 90 za kifungo, maombi na upandaji wa makanisa.

Asubui hii, nitaongelea kuhusu maombezi. Ninaipa jina la ''kuhamasisha waombaji''.

Kwa kipindi hiki cha siku 90 za kifungo, maombi na upandaji wa makanisa. Nitawapa moyo, Kaka na dada wapendwa kwa kuhamasisha waombaji wote.

Muombaji ni nani ?

Muombaji ni yule anayekuwa katikati ya Mungu na wanadamu ili kutetea itaji za watu. Ukiwa muombaji, uko msaada unayejiweka karibu na mtu.

Tunastahili kuonyesha maono ya VCP kwa makanisa shirika, kwa ndugu zetu, ndani ya kila kanisa, katika Afrika nzima. Kwenye Tik tok, Facebook ....

Tuongelee kuhusu maombi. Ni maombi ndiyo inayoweza kuokowa Afrika.

Kuanza leo, viongozi wa inchi zetu za Afrika wanaonyesha uzaifu mwingi usio weza kusaidiya makanisa, isipokuwa kuyasumbuwa.

Nguvu yetu kwa kipindi hiki ingekuwa maombezi, maombi tu ili kubaki kwenye uwepo wa Mungu na Mungu atagusa roho za viongozi.

Alibadilisha viongozi wote ili kwamba watu watoe maisha yao yote kwa Yesu ili kwamba Afrika iokolewe. Maombezi yako na nguvu.

Mtume mkubwa Paulo aliomba maombezi kwa makanisa. Akatuma baruwa kwa kanisa la Efeso katika kitabu cha Waefeso 6 :18-19 

''kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; 

[19]pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili.''

Kaka na dada, nawapa moyo kupitiya maneno haya kuhamasisha hesabu kubwa ya waombaji hata kama wengine miongoni mwao hawawezi kufunga, washirikiane wote kwa maombi kwa mda huu wa siku 90 kwa ajili ya Afrika. Ni kwa ajili ya wokovu wa Afrika. Pandeni makanisa mengi inamaanisha kuleta suluhusho kwa wa Afrika wengi.

Ninawapa moyo kuifanya kwa moyo wa kuchangamka na upendo mkubwa.

Hamasisha waombaji kwa ajili ya vijiji vyenu, nyumba zenu, kwa marafiki zenu.  Sababu gani kuangalia podikasti za mambo ambayo hayakuletei faida yoyote kwenye Tik tok mahali wanaongelea tu siasa, ununuzi wa vifaa vya vita, mahali ambako tunaona tu vita, lakini mahali ambako tunaweza simamisha vita kuipa tena Afrika amani kupitiya maombi, kifungo, kupitiya nguvu ya kanisa. Ninawapa moyo, Kaka na dada, kwakujiweka sawasawa kwa ajili ya maombi.

Acha Mungu awabariki, awape nguvu kwa mda huu wa siku 90 za kifungo, maombi na upandaji wa makanisa ili kuona matokeo ya maombezi.

Amani kwenu

Muhtasari Wa Mukutano Wa Siku 90 Za Maombi - Siku 90 za Maombi na Kufunga




 Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji 

Mkutano wa Siku 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa ! Ni bora zaidi !

Ni nini Mungu angefanya kwa kujibu maombi yetu ?

Ni milango gani itafunguliwa wakati tutajielekeza kwenye vijiji visivyo na kanisa ?

Ni roho gani ngumu zitatulizwa ? Ni nani ataokolewa wala kuponywa ?

Siku 90 za maombi, za kifungo na upandaji wa makanisa zitaanza tarehe 01/08/2024.

Wapandaji wa makanisa na washirika wao katika inchi 32 za Afrika wataomba hawa wakiombea wengine.

Kipindi cha kwanza kinahusu  kuhamasisha waombaji kuanza sasa. Waambie kuanza hivi sasa washiriki wa kanisa lako na kwa wasimamizi wa makanisa jirani kuhusu kuzingatia kwa kujitowa juu ya maombi kuanza, tarehe 01 Agosti 24. Tunapendelea kuleta Habari Njema ya Yesu na uwezo wake wa wokovu kwa maelfu ya vijiji vya Afrika visivyo na kanisa.

Waombe washiriki wa kanisa lako na wachungaji wa makanisa mengine wajiunge nanyi kwa maombi.

Soma mwongozo wa maombi inayotumwa na hii podikasti.

Baadaye gawanya kupitiya WhatsApp kwa waombaji wengi. Waambie waombe mara tatu kwa hizi itaji 30 za siku 90 kuanza tarehe 01 Agosti 24.

Ndani ya mukutano yenu ya maombi, waombe washiriki wenu wajihusishe juu ya maombi kwa ajili ya waliopotea na kwa ajili ya wapandaji wa makanisa mapya ya kizazi cha kwanza, cha pili na cha tatu watakao kwenda kwenye vijiji visivyo na kanisa ili kuenenda kwa maombi na kupata watu wa amani. Sema kwa wanaume na wanawake hawa kuanza leo.

Gawanya maoni !

Usisahau kwamba lengo letu ni kila kanisa la VCP lianze kanisa lingine mpya katika Kijiji kisicho na kanisa.

Tunapenda kufikia lengo hili ifikapo tarehe 29 oktoba 24. Makanisa mpya yatakayopandwa yatendelea kukomaa na kuendelea baada ya mwezi wa Oktoba. Lakini lengo letu ni kuanzisha maelfu ya makanisa mapya katika kipindi hiki cha Siku 90.

Ndani ya mwezi wa Agosti, fuata maelekezo ya Mkufunzi wako wa VCP. Mukutanane na marafiki wenzenu wapandaji wa makanisa katika vituo vya majifunzo. Kama uko na afya njema, fanya kifungo. Watu wote wataomba. Nyenyekeeni mbele za Mungu. Mungu anapingana na wenye kiburi, lakini anawapa wanyenyekevu neema. (Yakobo 4 :6). Kama uko na dhambi maishani mwako, uihungame. Fanya uzoefu wa utakaso wa Mungu.

Baadaye, waite kwa ajili ya vijiji vilivyo karibu na kituo chako cha majifunzo, visivyo na kanisa.

Baada ya kipindi cha maombi, Mkufunzi wako atakuongoza kwenye mtiani wa kanuni za msingi za upandaji wa makanisa.

Wakati unapo rudilia mfano wa shamba ine kwa kujihusisha juu ya shamba la kwanza na la pili, acha moyo wako ujae na imani kwa kugunduwa watu wa amani na uanzishaji wa makanisa mapya. Kila Juma ya mwezi wa munane, mutakutana ndani ya kituo cha majifunzo ili kuomba na kupata misingi ya upandaji wa makanisa.

Ndani ya mwezi wa munane na wa kenda, wewe na wapandaji wa makanisa mapya mutatembea ndani ya maombi kwenye vijiji visivyo na kanisa. Mutaomba kwa ajili ya maitaji ya watu, mutahadisia hadisi za Biblia, mutagawanya filamu ya Yesu na kutumikisha miviringo tatu ili kuita watu kwa toba na kwa imani ya Kristo. Hapa Mwezi wa Oktoba, kila Mpandaji wa kanisa ataombwa kutafuta mahali ambako waamini wapya wataweza kukutanana kwa ajili ya ibada na kujifunza namna ya kumtii Mungu na Agizo Saba za msingi za Kristo.

Na usisahau kama wapandaji wa makanisa 13 000 wanakusaidia katika maombi, kama vile naweye unavyo wasaidia !


Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi ni Dean Davis nikiwauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Unyenyekevu Na Upandaji Wa Makanisa - - Siku 90 za Maombi na Kufunga




Jambo wapendwa Kaka na dada, wapandaji wa makanisa.

Mimi ni Mchungaji Douti Claude , Kasisi wa VCP. Hii ongezeka ni podikasti inayoleta maneno ya kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa.

Ninapenda kuwa Kaka na dada wawatiye moyo kuhusu hizi siku zetu 90 za kifungo, maombi na upandaji wa makanisa.

Ninawatiya moyo kwamba musichukuwe siku hizi kwa zarau, bali kuwa na bidii na kujinyenyekeza mbele za Mungu.

Napendelea kuwaambia juu ya unyenyekevu ndani ya upandaji wa makanisa.

Unyenyekevu ni wa muhimu ndani ya upandaji wa makanisa.

Unyenyekevu mbele za Mungu na unyenyekevu mbele za watu unaowahudumia.

Unyenyekevu katikati ya watumishi wa Mungu.

Unyenyekevu ni nini?

Unyenyekevu, ni kujishusha binafsi ; unyenyekevu, ni kujishusha mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu.

Ni mda ambao tunashikamana ndani ya kifungo na maombi. Ni mda ambao tunajitenga na dunia hii, na kushikamana kwa uaminifu na unyenyekevu kwa Mungu.

Yakobo anasema katika Yakobo 4:4 urafiki wa dunia hii ni uadui na Mungu, lakini Mungu anapenda wanyenyekevu.

Mungu anatoa neema zaidi kwa wanyenyekevu. Mungu anapingana na wenye kiburi lakini anawapa wanyenyekevu neema, kwa vesi ya 6 ya Yakobo sura 4.

Nyenyekeeni mbele za Mungu kwa mda wa siku 90, hivo mutapata neema zaidi ndani ya maisha yenu, vijiji vitafikiwa, utapokea zaidi ndani ya huduma yenu, mutaono ubora katika huduma.

Petro anarudilia haya kwa wazee ndani ya 1Petro 5:5 anasema kuhusu neema ambayo Mungu anatowa kwa wanyenyekevu na kupingana na wenye kiburi.

Ndugu, uwe mnyenyekevu kwa mda huu wa siku 90 za kifungo na za maombi mbele ya Mungu.

Siku 90 Za Maombi, Mafungo Na Upandaji Wa Makanisa - Siku 90 za Maombi na Kufunga




 Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Umekwisha kusikia ikisemwa Siku 90 za maombi, na kifungo na upandaji wa makanisa itakayotekelezwa katika inchi 32 za Afrika kuanza tarehe 01/Agosti hadi tarehe 29/oktoba 2024? Nina furaha kwa ajili ya fursa hii kwa kujinyenyekeza na kuita Mungu kwa ajili ya neema yake, msaada wake na wokovu wake vijae vijijini ambako hakuna kanisa kupitiya Afrika nzima. Ninafuraha kubwa kwa wazo kwamba kanisa 13 000 zimeweza kupandwa na wapandaji wa makanisa wa VCP kama vile zinaweza kugeuka kuwa kanisa 26 000 kwa myezi ifuatayo.

Wakati unaposikia ikisemwa kipindi cha Siku 90 zilizotengwa juu ya upandaji wa makanisa, kuanza tarehe 01 Agosti, umeifikiria nini? Ulisikia boga? Ulichanganyikiwa? Tangazo lilikuwa pengine la kuchanganya. Sababu gani tutasimamisha majifunzo yetu ya kawaida katika vituo vyetu vya majifunzo ya VCP ili kujiusisha na maombi na kifungo ?

Sababu gani tunastahili kuifanya sote kwa mda moja? Sababu gani Siku 90? Ni kipindi kirefu! Wanatarajia kabisa nifanye kifungo cha Siku 90 za kufuatana ?

Muniruhusu kujibu kwa baadhi ya swali hizi za muhimu sana. Kasisi wa VCP, Claude Douti, alituomba kusimamisha masomo katika vituo vya majifunzo ya VCP

Mwanainchi Douti alituomba kusimamisha masomo yetu ya kawaida katika vituo vya majifunzo ya VCP ili wapandaji wote wa makanisa, waalimu, waratibu, na wa superviseurs na wa wezeshaji wa kuzidisha makanisa ya VCP ili waweze kujinyenyekeza na kuhusisha roho zao katika maombi. Tutatoa wito kwa Mungu ili kwamba kila kanisa lianze kanisa lingine mpya.

Tunafurahia makanisa yote iliyokwisha kupandwa tangia mwaka wa 2020, tarehe ambayo mfumo mpya wa VCP ulianzishwa kwa mara ya kwanza. Lakini tunatarajia sana watu ndani ya vijiji zaidi wajue upendo wa Yesu na wafanye uzoefu wa kuzaliwa upya ndani ya jamaa ya Mungu. Tunafurahia yale tuliofanya ili kupanda makanisa, lakini tunashugulikia yale bado kutekelezwa. Tunaitaji nguvu na uwezo wa Mungu. Tunaitaji milango ifunguliwe. Tunastahili kupata watu wa amani.

Tunastahili kuonyesha kupitiya kifungo siyo kwa nguvu, wala uwezo, lakini kwa Roho wa Mungu ambayo maoni ya VCP yatatimizwa.

Tunasimamisha hivo masomo yetu ya kawaida na tutarudilia kwenye vituo vyetu vya masomo kwa mwezi wanane kwa kufanya mambo yafuatayo :

Mtiani wa huduma juu shamba 1 na 2, tukiendelea na maombi, kutafuta watu wa amani na ugawaji wa Habari njema. Na tunaomba, Sisi wenyewe, kwa vikundi kidogo vidogo na vile vikubwa. Tutaandaa na ibada za maombi ndani ya kanisa zetu binafsi na ndani ya makanisa tunayoshirikiana nayo.

Na ikiwa tuna afya njema, tunafunga pamoja na maombi, tukijizuiza kula.

Mara nyingi tunafunga na wengine, Mara nyingi Sisi wenyewe.

Zaidi tena tunafunga kwa mda wa Siku nyingi. Mara nyingi, tunasimamisha ili kuanzisha kifungo inga ijayo. Hatuko chini ya sheria, lakini chini ya neema. Mufunge vile munajisikia kusukumwa kuifanya. Mujinyenyekeze mbele ya Bwana. Kama hauna afya njema, usifunge, lakini uombe.

Mwezi wa munane, tumika pamoja na Mwalimu wako ili ku orozesha vijiji ambavyo havina makanisa mahali ambako weye na rafiki zako mutakwenda kutafuta watu wa amani. Baadaye, pamoja na wapandaji wako vijana, muchukue mda mwingi uwezekanayo ndani ya vijiji hivyo kwa mwezi wa kenda na wakumi.

Mutafute watu wa amani, muombee wagonjwa, mugawanye ushuhuda wenu, mugawanye miviringo tatu. Ikiwezekana, muonyeshe filamu ya Yesu. Muwasaidiye waamini wapya kukusanyika ili kupokea Neno la Mungu na kuabudu Mwenye nguvu zote.

Na usisahau kwamba kupitiya Afrika, wapandaji wa makanisa 13 000 wanapatana ndani ya maombi pamoja nanyi.

Katika Marekani, waombaji wanapatana ndani ya maombi ili usaidiye kila kanisa ambalo utatumika nalo kuanzisha kanisa lingine mpya ambalo pamoja nalo pia mutatumika kuunda kanisa lingine mpya.

Mujae matumaini. Mujae nguvu za Kristo aliye hai. Yeye aliye waita ni mwaminifu ! Hatawaacha wenyewe!


Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis na ninawauliza; ''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...