Karibu kwenye ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, kwa wachungaji na viongozi wa Kikristo.
Mimi ni muhamasishaji wenu leo, Daneille Snowden.
Tutaendelea na mjadala wetu kuhusu ubatizo wa maji na kujadiliana kwa swali lifuatalo :Sababu gani watu wamoja wanakawiza ubatizo wao ?
Wakati ukiuliza watu tofauti kuhusu swali hili, wanatoa sababu nyingi : woga, hisia ya kutukuwa kamili, mila zinazotofautiyana, ao tena wazo kwamba inafaa kujiandaa vizuri, kuwa na sare rasmi, nk.
Neno "kukawiza" linamaanisha kupeleka utendaji wa jambo kwa mda wa baadaye, kuizuwia wala kufanya namna jambo litendeke pole pole na ilivyo tarajiwa.
Tendo la kigriki linaloambatana na "kukawiza" linatokana na "chrono" ikimaanisha kuchukuwa mda, kukawa ao kukawia.
Japokuwa, tunaona ndani ya Neno la Mungu kwamba hapakuwa na mda wa kubatiza mtu baada ya yeye kukubali Yesu kama Mwokozi wake.
Katika Matendo 16.31-33, Mitume hawakukawiza ubatizo wakati watu walipo amini.
Paulo, aliyeitwa mbele Sauli, alibatizwa hapo hapo, kama tunavyoona katika Matendo 9.17-19.
Na katika Matendo 2:41, tunasoma : "Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu."
Tunapashwa sote kukumbuka yale yanayofanyika kabisa wakati mtu anabatizwa.
Tunaweza kuanza na ubatizo wa Yesu.
Tendo hili kubwa lilifunua utambulisho wake kama Mwana wa Mungu ; alionyesha utatu utakatifu na alitangaza kifo chake na ufufuko wake kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.
Baada ya ubatizo wake, Yesu aliachana na maisha yake ya ubinafsi ili kuingia wazi wazi katika umisheni wake.
Kama inavyosemeka : "ubatizo unakamilisha ushirika wa kila mwamini na Kristo. Ni tendo la imani linalotangaza mawasiliano mapya ya kila mwamini pamoja na Kristo. Ni tendo la imani linalotangaza mawasiliano mapya na Mungu."
(Mwongozo wa Mkufunzi ? NVP, muhula 1, kipindi cha 2)
Katika myezi ya kipwa, mimi namume wangu tulikuwa ndani ya kikundi kinachoitwa "kongamano juu ya Yesu" tulishuhudia watu wengi waliotowa maisha yao kwa Yesu.
Kwa mwisho wa kipindi cha sifa, tunakuwa na beseni la maji mahali ambapo kwa miaka iliyopita, tuliona watu wengi wakibatizwa.
Wakati tunapobatizwa, tunatambulika kwa kifo na kwa ufufuo wa Yesu-Kristo.
"Ubatizo unakamilisha imani ndani ya Kristo, musamaha wa dhambi, na umoja ndani ya Kristo." (Fundisha na Ongezeka muhula 2)
Uzoefu wa ubatizo ni uzoefu wa kweli unaobadilisha maisha ya mwamini, pamoja pia na wale wanao shuhudia.
Unaimarisha imani ya wengine waamini na kushuhudia mbele ya wale ambao bado wanatafuta tumaini.
Kwa upande wangu, wakati nilipobatizwa, nafsi yangu ilijisikia hakika kuwa na ushirika pamoja na Yesu. Nilijisikia nikiwa karibu sana naye kwa kufanya hatuwa hii ya utii na upendo.
Ilikuwa Ongezeka.
Utapendelea kugawanya podikasti pamoja na wengine ?










