Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wa Kikristo.
Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Kwa kipindi cha myezi mbili iliyopita, niligawanya tabia 10 ambazo nazitafuta kwa viongozi wanaojitokeza. Leo, napendelea kutowa kifupi cha tabia hizi. Mbele siyafanya hivo, napenda kusisitiza kwamba, ni viongozi wanaojitokeza wachache wataonyesha tabia hizo 10.
Ninajuwa pia kwamba horoza hii siyo ya kutosha wala ya mwisho.
Hii ni mawazo yangu tu.
Tazama horoza yangu :
* Utambuzi ulio na mizizi ndani ya Kristo - ninatowa kipaumbele cha juu kwa tabia hii, sababu kwa miaka mingi iliyopita , nilichunguza matatizo makubwa yaliyosababishwa na viongozi ambao hawajiamini wenyewe. Mara nyingi, Motisha zao zimechanganyika katika uongozi wao, sababu wanatafuta kujipendekeza machoni pa wengine pahali ya kutafuta kutumikia Yesu-Kristo na ufalme wake. Wanajiusisha wenyewe pahali pa kujihisisha juu ya ufalme.
* Unyenyekevu - inashikamana moja kwa moja na tabia hii, sababu viongozi wanaojiamini hawasukumwi kujipendekeza kwa macho ya wengine. Mithali 27:2 inatafsiri vizuri : ''Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe;
Mtu mgeni wala si midomo yako wewe''
* Hali yao ya zamani ao matendo yao ya zamani - pengine utakumbuka kama katika mtiririko wa mwaka jana kuhusu Uongozi wa uwakili, nilisema kuhusu mfano wa Mtumishi Mwaminifu ambaye Yesu alisema : ''ni vema, Mtumishi Mwaminifu na bora ; ulikuwa mwaminifu katika mambo machache , nitakupa zaidi''. (Mathayo 25:21)
* mambo ya uzoefu wala uwezo - wakati tunapo chunguza na kuendeleza viongozi wapya, ni muhimu kutathmini matendo yao ujuzi na kuwapa fursa ya kuongoza kwenye misheni zinazotumikisha nguvu hizo.
* Mpango - mwezi uliyopita, niliitafsiri kama vile ''uwezo wa kukaguwa na kuchukuwa matendo kwa namna ya uhuru''. Viongozi wanaojitokeza hawabaki wavivu wakingojea kuambiwa nini cha kufanya. Wanaonyesha mwenendo mzuri na wanatenda.
* Hamu kubwa ya kujifunza na kukuwa - viongozi wanaokuja hapo baadaye hawatosheki na hatuwa yao ya kukomaa kiroho, ya kuelewa ao ya ujuzi.
* Moyo wa kufunzwa - kwa kujifunza na kukomaa, viongozi wanaojitokeza wanastahili kuwa wanyenyekevu, na kuwa tayari kujifunza kwa wengine.
* Bora kwa kuwasiliana - naongeza tabia hii sababu watu wabaya hawawezi kufuatwa, na hauwezi kuwa kiongozi kama hakuna mtu anayetufuata.
* Sifa yao, iwe ndani ya kanisa ao inje - kama mtu iko na sifa mbaya kwa wale wanao mjuwa vizuri, kwangu mimi ni alama ya tahazari muhimu.
* Ndoa ya kudumu yenye kujengwa juu ya Kristo - imepita sasa miaka 40, nilisikia muhubiri moja akitowa shauri hili : ''kama haindeki nyumbani, usiitoe inje.'' wala tunaweza sema, kama ndoa ya mtu haina nguvu, kipaumbele ni kurudisha kwanza mawasiliano nyumbani mbeye ya kujaribu kuongoza wengine.
Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni