Hamjambo nyote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutia moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Ikiwa umekuwa ukipanda na kuzidisha makanisa kwa zaidi ya miaka mitatu au minne, umechukua majukumu muhimu. Kwa mwanzo, unaweza kuwa ulilenga katika kuomba mitaani, kutafuta watu wa amani, na kushiriki Habari Njema katika nyumba na vikundi vya nyumbani. Lakini sasa, majukumu yako yamekua. Unatumia muda mwingi kutoa maono, kufunza wengine, kuandaa matukio, na kusimamia upandaji wa makanisa mengi katika maeneo mbalimbali. Pengine unahisi kuondolewa kidogo kutoka kwa furaha na msisimko wa uinjilisti wa moja kwa moja na ufuasi wa waumini wapya. Umechukua madaraka makubwa zaidi, na wale walio karibu yako wanashukuru kwa kazi unayofanya, lakini ukweli ni kwamba, umeondolewa kidogo kutoka kwenye eneo la kukomaa kwa Ufalme.
Katika nyakati kama hizi, lazima uwe macho. Linda moyo wako. Hakikisha huruma yako kwa waliopotea haipungui. Linda moyo wako. Hakikisha unamwamini Mungu kila siku kwa ajili ya riziki, hekima, nguvu, kibali, na neema. Linda moyo wako, uwe macho msijisifu kwa nguvu zenu wenyewe; mtukuzeni Bwana, rehema zake, na wema wake. Unapopanda makanisa zaidi na zaidi na kugawa majukumu zaidi na zaidi kwa wanafunzi wako, njia moja ya kulinda moyo wako ni kusikiliza kwa makini ripoti za wanafunzi wako. Yesu alifanya hivi. Alipowatuma mitume katika huduma yao, alisikiliza ripoti zao waliporudi.
Mathayo 9:10 inatuambia, “Wale mitume waliporudi walimweleza Yesu yote waliyoyafanya. Kama unavyojua, kusikiliza sio kusikia tu. Kusikiliza ni kuwa makini. Kusikiliza ni kutafuta kuelewa. Yesu alisikiliza ripoti za wanafunzi wake, nasi ni lazima tufanye vivyo hivyo. Lazima tuwaache waseme hadithi zao kwa maneno yao wenyewe. Lazima tuulize maswali ya wazi ili kuongeza kuelewa kwetu na wao. Ni lazima tuwe na subira wanapozungumza. Kwa kufanya hivyo, tunaonyesha heshima kwa wanaume na wanawake hawa wenye bidii ambao wanajaribiwa katika huduma yao ya kufanya wanafunzi na kupanda makanisa. Tunapata maarifa na kuelewa katika hali halisi ambazo hatujapata.
Tunapata hekima ya muhimu ili kuwashindikiza wanafunzi wetu vizuri. Na wanafunzi wetu wenyewe wanafaidika kwa hekima na kufikiria kwa uzoefu wao wa huduma.
Sasa, mufanye kama vile Yesu. Mchukuwe mda wa kusikia ripoti za wanafunzi wenu, mkifanya hivo, pande zote mbili mtapokea nguvu. Mukisikiliza kwa makini, roho zenu zitaunganishwa. Mungu atatukuzwa na mtakuwa timu iliyo nguvu. Kwa kusikia, Bwana atawaongoza pamoja mbali zaidi, na kuwa na imani zaidi, ya hekima na maoni.
Ilikuwa Ongezeka na mimi Dean Davis nawauliza, ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?







