Jumamosi, 12 Aprili 2025

Hakikisho la wokovu



      Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Niliongea leo na ndugu moja anaye mtumikia Kristo katika inchi ya Afrika ya Mangaribi. Aliniambia kama aliwauliza zaidi ya watu 1000 ya kwamba wanajuwa sehemu ambayo watakaa milele baada ya kifo chao.

Katika hao watu 1000 aliowauliza, ambao baadhi yao wanashiriki kanisa kila jumapili, ni watu Saba tu ndio walio hakikisha kwamba wataishi milele pamoja na Kristo kufuatana na vile alivyofanya

Wengine walisema kama wanajuwa kama wataishi milele jahanamu. Ndugu yangu alijihusisha sana kwa vile wengi wa wale wanaoshiriki ibada hawakuwa na uhakika wa wokovu wao ndani ya Kristo.

Neno langu la kutiya moyo leo ni kwamba tunaweza kuishi ndani ya dunia hii inayovunjika tukiwa na uhakika kwamba tu wana wa Mungu, warithi pamoja na Kristo, walio samehewa dhambi, wakiwa na uhakika kwamba wako na maisha mapya na ya milele ndani ya Kristo. Hatuna cha kuogopa kifo ao jehanamu.

Nilipata uhakikisho wa wokovu nikiwa na umri wa miaka 13. Nimeishi katika uhakikisho huo tokea sasa miaka 55. Tazama namna gani nilivyo upata.

Niliambia ndugu moja katika Kristo kama sikuwa na uhakika wakuwa mukristo. Alifunguwa Biblia yake kwa kitabu cha 1Yohana 5:10 na akanisomea maneno haya: 1 Yohana 5:10

[10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. Na tazama ushuhuda huo, ni kwamba Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huo uko ndani ya Mwana wake. Yeye aliye na Mwana yuko na uzima; yeye asiye na Mwana wa Mungu hana uzima.

Ndugu akaniuliza sasa : ''Dean, uko na Mwana wa Mungu ndani ya maisha Yako?''

Nilifikiri kiasi kidogo, kisha nikajibu : ''ndiyo, nilitumainia Yesu kama Mwokozi wangu. Anaishi ndani yangu.''

Kisha ndugu akasoma tena 1Yohana 5:11,12 : ''Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. 

Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.'' baadaye akauliza, Dean, watu walio na Mwana wa Mungu ndani ya maisha yao wako na uzima wa milele? Nilikubali, ''ndiyo.'' kisha akaniuliza : ''uko na uzima wa milele ?'' nilijibu : ''ndiyo'' niko na Yesu; niko na uzima wa milele ''. Ndugu huyo ananiambia akiwa na uhakikisho : ''Dean, unaweza kwenda na usiwe na shaka ya kwamba wewe ni Mwana wa Mungu, mkristo aliye na uzima wa milele ''. Je! Munajuwa ? Nilitoka mahali hapo nikijaa uhakika kwamba niko Mwana wa Mungu na kwamba niko na uzima wa milele.

Tokea hapo, nilikwisha kuona woga mara nyingi. Lakini sijawai kupata woga wa kuingia jehanamu ao kutengwa na Yesu. Niko naye.

Uko na uhakika wa kuokolewa ndani ya Kristo ? Unaweza kuokolewa. Wanafunzi wako wanao uhakika wa kuokolewa ndani ya Yesu-Kristo ?

Wanaweza kuokolewa pia. Tafazali, bila kukawia, gawanya nao ukweli wa ajabu wa wokovu, uliotolewa ndani ya Neno la Mungu 1Yohana 5:10-12.

Mimi ni Dean Davis na ninaomba ili kuwe kanisa katika kila Kijiji cha Afika, na kila mtu ndani ya kanisa hizi aishi kila siku akiwa na uhakika ya uwepo wa wokovu wa Kristo ndani yao, na tumaini ya utukufu na upendo wa Mungu.

Kujitolea kufundisha na kuongezeka




   Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Huduma mpya ya upandaji wa makanisa katika vijiji inaanza wakati Mkufunzi wa VCP anapokusanya wanafunzi ili kupanda makanisa katika vijiji visivyokuwa na kanisa.

Shabaha ya mukufunzi ni kukusanya wanaume na wanawake 15 waaminifu, waliyo tayari na wenye uwezo wa kufundisha. Kaka na dada hao walio tayari na wenye uwezo wa kufundisha wanajitolea kufuata miaka ine ya mafundisho ndani ya vituo vya mafunzo juu ya namna ya kupanda makanisa. Lakini wanajitolea kwa mema zaidi ya kujifunza. Wanajitolea katika kazi ya Mungu : kutumika kwa nguvu kwa kusudi ya kuzidisha wanafunzi, viongozi na makanisa.

Wanafunzi wa VCP wanakumbuka kujitolea kwao kwa fundisha na ongezeka waliyo chukuwa wakati walipoanza  kutumika katika kituo cha mafunzo.

Lakini ..., Tuchukuwe mda kidogo kwa kukukumbuka kujitolea huko kunakopatikana kwenye ukurasa 24-32 ya kitabu ''mafunzo ya watumishi wachungaji na wewe''. Vile utakavyoendelea kusoma, chaguwa alama iliyo muhimu zaidi kwako ambayo pia kwako ni vigumu kuitekeleza.

Kujitolea kwa mwanafunzi wa Fundisha na ongezeka pamoja na msaada wa Mungu, najitolea kwa :

- kumpenda Yesu-Kristo na kuweka kipaombele utii kwa amri zake.

- kufundisha wengine kutii amri zote za Yesu.

- kutunza jamaa langu kwa upendo wa kweli (waefeso 5:25-33)

- kuombea kila siku Kondoo, rafiki zangu na wale ambao bado wangali na itaji ya kujuwa Kristo.

- kutumika kwa nguvu pamoja na wengine kwa umoja na upendo, kwa upeke pamoja na kanisa langu, na kusikilia Mwalimu wangu Fundisha na ongezeka na kuongeza kujulisha kazi zangu (Warumi 12:9-11)

- kutowa kiasi cha mda na pesa zangu ili kueneza Ufalme wa Kristo popote anaponiita kwenda (Mathayo 28:18-20)

- kuwa mwaminifu kwa uwezo wa Mungu ili kuruhusu kanisa kukomaa na kujizidisha (Marko 4).

- kufanya nguvu kutii shurti zinazo stahili kwa viongozi wa kanisa, kama vile zinavyoonyeshwa ndani ya 1Timotheo 3:1-7.

- Tangaza injili kwa bidii, upendo na uwazi ili watu waamini Bwana na kumtii. (Mathayo 28:19-20).

- kutafuta upandaji wa makanisa yenye afya ambazo zitajizidisha, kwa kipekee kwa maeneo ambako hakuna kanisa (Warumi 15:20-21).

- kuwa tayari kuteseka kwa ajili ya Kristo (2Timotheo 2:3).

- kufuata mashauri ya mukufunzi na kutekeleza kwa uaminifu majukumu zangu zote kwa kazi na mafunzo.

Ni alama gani kati ya hizi iliyo ya muhimu zaidi kwako leo ? Kwangu mimi, ni alama ya kwanza. ''kupenda Yesu-Kristo na kuweka kipaombele utii kwa amri zake zote ''. Alama hii inanipa mafasiriyo makubwa ya namna inavyonipasa kuishi maisha yangu. Inanikinga na majaribu na kunijulisha ni wakati gani napashwa kuungama na kutubu.

Naipenda sababu inaniongoza mimi kama mwanafunzi wa Yesu. Ni maamuzi gani iliyo ngumu kutekeleza kwako? Kwangu mimi, iliyo nguvu ni ''kukubali kuteseka kwa ajili ya Kristo ''. Sipendi kuteseka. Ninajaribu kuepuka mateso.

Lakini najuwa mimi kama mwanafunzi wa yule aliye vumilia msalaba kwa ajili yangu, nimeitwa pia kuteseka. Japo hiyo, wito huo unanihusu kwa sehemu kubwa. Kwa sasa vile munavyojitolea kufundisha wanafunzi ili kupanda makanisa mapya, muniruhusu niwape moyo kuwaonyesha kujitolea huku.

Muwaulize wanafunzi wenu wajiulize kwa ndani zaidi kujitolea kwa imani. Mungu anafurahi wakati watoto wake wanajitolea kumtii, kutangaza Habari njema na ''kutafuta upandaji wa makanisa yenye afya ambazo zitajizidisha, kwa kipekee kwa inchi maskini'', makanisa mapya yenye afya ambazo zitajizidisha kwa kipekee kwa maeneo ambako hakuna kanisa ''.

Mimi ni Dean Davis : ''ninawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Jumapili, 6 Aprili 2025

Mkutano Mkubwa


     Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Siku kubwa inafika. Siku ya ajabu iko mbele yetu. Ni siku iliyo andaliwa na Yesu imepita miaka 1900. Ni siku ya furaha kubwa ! Sikia maneno ambayo Mtume Yohana alitumikisha kwa kuonyesha siku hii kubwa inayokuja: "Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; 

wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo. 

Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu, 

wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele  Amina !" (Ufunuo 7:9-12)

Ni siku ya ajabu ! Kundi kubwa. Ni mkutano mkubwa ambao hakuna mtu awezaye kuuhesabu. Na sio mkutano wa kawaida ; ni mkutano mkubwa wa watu ambao wamepata msamaha ndani ya Yesu-Kristo, Mwana Kondoo wa Mungu, mbaye kwa damu yake iliyomwangika () na kwa ufufuko wake wa ushindi zidi ya kifo, unatowa msamaha wa dhambi na wokovu kwa wote wanao mtumainia.

Watu walio ndani ya mkutano huo hawasemi lugha moja wala mbili, wanasema lugha za dunia mzima. Wanawakilisha mataifa ya kila kabila na kila taifa.

Wametoka wapi na wanafanya kazi gani? Wanatokea kila sehemu. Lakini zaidi, wanakuja kwa Kristo na wamesimama mbele ya kiti chake cha enzi kwa kumsifu sababu wanafunzi wa Yesu, ndani ya vizazi vyote, walitoka na walitangaza Habari njema. Mkutano umesimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kwa sababu mbili :

1) sababu Yesu alilipa deni zote ili waokolewe.

2) sababu wanafunzi wake walizidisha wainjilisti, wafanya wanafunzi na watumishi kutoka kila asilia ili kupeleka Habari njema kwa kila taifa, Kabila na Lugha.

Tukio hili la mkutano mkubwa mbele ya kiti cha enzi ni jambo litakalo kuja. Lilionyeshwa kwa Yohana katika maono imepita sasa miaka 1930. Tukio hili haliwezi kutokea  kufuatana na mazingira tuliyo nayo leo, sababu bado kungali kabila nyingi na taifa ambazo hawana hata mtu moja aliye na kanzu nyeupe iliyo safishwa katika damu ya Mwana Kondoo. Jukumu letu ni kuzidisha wafanya wanafunzi ili tukio la Ufunuo 7 mbele ya kiti cha enzi iwe kweli kwa haraka iwezekanayo.

Sasa, kaka na dada zangu, muendelee kuvuka vizuwizi vya asilia ajili ya kumtambulisha Kristo.

Ilikuwa Ongezeka ! Na mimi Dean Davis nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Kuomba na kutegemea Roho Mtakatifu



 Jambo, Tazama ''ongezeka''ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wakikristo katika vijiji.

Mimi ni Brad Snowden.

Kaka na dada, ni furaha kubwa ya namna gani kumtumikia Bwana na ni wito gani muzuri wa kupanda makanisa. Tuko na bahati ya kuona namna vijiji vinavyobadilishwa pamoja na kuwa na tumaini wakati Yesu anagusa maisha ya wengi.

Wito huo unaweza pia kupatwa na vipindi vya magumu mengi kwa utu wetu wa inje.

Tunapenda kufaulu na kuona kile kilicho ndani ya roho zetu kuwa yanatendeka.

Ni kipindi chetu kizuri cha kutembea pamoja na Kristo wakati anapoweka ndani ya roho zetu kile anachotaka kutekeleza. Ni kipindi kizuri sana kwa wapandaji wa makanisa, sababu ni kama vile tunaweza kuona ni kwa namna gani haya yanafananishwa  hata mbele ya hayo kuanza. Ni kipindi cha muhimu cha mpango wa Mungu kwa wale munao watumikia.

Mda huu unaweza pia kuwa moja ya magumu makubwa.

Nikigunduwa mimi kama Mchungaji, vipindi hivi vilinileta kwenye uwanja wa mapambano, nilijuwa kile Bwana alizalisha ndani ya roho yangu, na ningeweza kuyatarajia yote. Lakini hapo ndipo penye tatizo : sikujuwa ninani angeweza kupokea maono ambayo Mungu amenipa.

Sikujuwa namna gani ingezaa matunda, wala pia ni kwa namna gani tungeweza kupata pesa za kuiendelesha.

Vita haikukuwa juu ya uzoefu ao kwa yale ambayo nimejifunza kupitiya mafundisho niliyopokea. Hakuna kibaya kwa kuishi yale ambayo tuliyo fundishwa wala pia yale tuliyoyapitiya hapo nyuma. Shida ilitokea pale nilipotegemea katika vipindi vinavyo nihusu  siyo kwa maono mapya ya Mungu.

Ushindi mkubwa ambayo Mungu hajawai kuniruhusu kuishi ilifanyika wakati niliposema; ''sijue ni kwa namna gani utaichukuliya. Sijue ninani atatembea pamoja nami ili nione ginsi kazi yako itatendeka. Oh Bwana, naitaji unisaidiye kuelewa na kutekeleza kazi hii uliyoniitiya kutenda.

Yakobo 1;5 anasema; ''Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.''  Bwana hatuangalii kwa juu wakati tusemapo : ''sijue chakufanya'' ao ''sielewi kabisa kila napashwa kufanya''. Neno la Mungu linasema tuombe tu kwa unyenyekevu, sababu tuko na mtoaji mwenye huruma anayeweza kufunguwa macho yetu ili kuona. Tunaweza kutegemea sauti ndogo ya ukimya ya Roho Mtakatifu itakayo tupatiya uelewa mpya wa namna Mungu anataka kutenda ndani yetu na kupitiya sisi. Oh, Mpandaji wa kanisa, ushindi wetu unatokea wakati tunapoomba Roho Mtakatifu afanye kazi na ginsi tunavyojitolea kwake.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa.

Ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Mungu awabariki.

Jumamosi, 5 Aprili 2025

Je! Wewe ni Mwaminifu ?



 

Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Uaminifu ni moja ya tabia kubwa za kila mwanaume ao mwanamuke anaye mufuata Kristo. Mtu mwaminifu ni mkamilifu na mwenye  haki. Copy iliyo nzuri ni ile inayofanana na ile ya asilia.

Moyo wangu unajaa furaha na tumaini wakati ninapokutana na wanaume na wanawake wanao mtumikia Kristo tangu zamani bila kuchoka.

Petro alitowa maelekezo yafuatayo kwa wanafunzi wake :  ''kila moja wenu anastahili kutumikisha karama aliyo ipokea ili kuwahudumia wengine, kama vile Mwakili mwaminifu wa neema ya Mungu kwa hali zake zote.

Je! Wewe ni Mwaminifu ?

Mwanafunzi mwaminifu anawapa wengine kile alichopokea kwa bwana wake. 

Na anatowa kwa uaminifu. Mwanafunzi mwaminifu habadilishi kile alichopewa.

Mtume Paulo kwa mwanafunzi wake Timotheo katika 2Timotheo 2:2 ni kifungu cha pili cha maandiko inayotajwa zaidi ndani ya VCP kisha Agizo kubwa.

Maneno hayo ni shurti yetu ya kutembea wakati tunapotumika kwa imani kwa kupanda kanisa ndani ya kila Kijiji cha Afika ifikapo mwaka wa 2050.

Paulo alimwambia mwanafunzi wake Timotheo : ''Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.'' Watu waaminifu, watu wanaofaa, watu wenye kujaa uaminifu. Watu watakao tumika kama Mawakili wema wa ujumbe wa tumaini watakao ipokea.

Je! Wewe ni Mwaminifu ? Wewe ni mfano wa watu ambao Petro alisema wakati alionyesha Mawakili waaminifu wanao tumikisha ujumbe wa tumaini kwa kufundisha wengine? Ao wewe ni Mwakili asiye mwaminifu, mtu anayepokea vizuri kwa mda lakini anagawanya pole pole? Siyo rahisi kwangu kuuliza swali hili, sababu najuwa wengi miongoni mwenu wanaotumika kwa bidii ili kuwasilisha yale waliofundishwa kwa ajili ya Kristo na kwa namna ya kutumikisha huduma yao ndani ya uwezo wa Roho Mtakatifu. Naona uaminifu wako. Japo hivo, nauliza swali : ''je! Wewe ni Mwaminifu ?'' sababu tunastahili kujiuliza mara kwa mara kuhusu Neno la Mungu.

Mwakili mwaminifu anasikia neno la Mwalimu wake, Mwakili mwaminifu anawasiliana na Mwalimu wake, anatumika, anapambana na kuomba ili kuelewa Neno. Mwakili mwaminifu anaweka mafundisho katika vitendo ndani ya maisha yake na katika huduma yake.

Mwanafunzi mwaminifu anafundisha wengine.

Je! Wewe ni Mwaminifu ? Mimi ni Mwaminifu ? Tafazali tuweke katika vitendo na kuwasilisha bila kukawia yale tuliyo fundishwa kutoka waalimu wetu waaminifu, ili wanafunzi wetu pia waweze kufundisha wengine.

Mimi ni Dean Davis nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

UONGOZI WA MUWAKILI - Mfano wa Muwakili Mwaminifu na mMwenye busara Sehemu 1


 Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Kama ilivyo mwaka mpya, nilianzisha mtiririko mpya kuhusu Mada ya uongozi wa muwakili.

Mwandishi moja anatafsiria Mwakili kama ''mtu anaye ongoza rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali ''

Leo tunaendelea na somo letu juu ya mfano wa Mwakili mwaminifu na mwenye busara ambaye tunamukuta katika kitabu cha Mathayo 24:45-51 na katika Luka 12:42-48.

Kwa kifupi, Yesu alihadisia hadisi hii ili kufundisha wanafunzi wake kwamba matendo yetu yanaonyesha yale tunayo yaamini kweli. Wanaomtii Mungu watalipwa, lakini Wale wasiomtii wanaonekana kuwa siyo waaminifu na wanafiki kupitiya matendo yao.

Mfano huo unafundisha vile vile kwamba Mitume wa Yesu wanastahili kuishi wakiwa kila Siku tayari kwa kugonja kurudi kwake.

Yesu anauliza swali hili kwa vesi ya 45 kwa kitabu cha Mathayo :Ni mwanafunzi gani mwaminifu na mwenye busara (kwa kitabu cha Luka, neno hili linatafsiriwa ''Mwakili''), ambaye bwana wake amemuwaka juu ya watumishi wa nyumba yake ili kuwapa chakula kwa mda mwafaka?

Ningependekeza tuangalie hapa kwamba:

- watumishi waaminifu, wala Mawakili, waliwekwa juu ya watu wengine. Mwelekeo, wala uangalizi wa watu ao wa kazi za huduma, ni kipendeleo na wito wa Bwana wetu. Mwakili hakujichaguwa mwenyewe kwa kazi hiyo, ni Bwana ndiye aliyefanya hivo.

- watumishi waaminifu, ao Mawakili, wanawapa watumishi wengine ''chakula chao kwa mda mwafaka''. (Kifungo cha Luka kinasema anagawanya chakula chao'').

Sisi kama viongozi, ni majukumu yetu kujibu kwa maitaji ya wale tunao waongoza.

Katika VCP, ''chakula chao'' inaweza kuwa maono, kutiya moyo, motisha, mafundisho na mafunzo, marudilio ya somo wala mambo mengine. Viongozi bora na wachaMungu wanastahili pia kutowa vitu hivyo ''kwa mda mwafaka''.

Mfano unaendelea kwa vesi 46 na 47. Mtumishi ambaye wakati bwana wake aliporudi, atamkuta akitenda hivi atafurahi.  Nawaambia hakika, atamukabizi Mali zake zote.'' Yesu anafundisha - kama kwa mfano wa Talanta - kwamba Wale walio waaminifu watalipwa. Katika kipindi cha utangulizi wa huu mtiririko, niliongelea Mada Tano za mifano ya Yesu juu ya Uwakili.

Moja ya Mada hizi ni kwamba Mawakili waaminifu wanaendelea, ndivyo ilivyo onyeshwa hapa.

Kwa hatuwa hii, nitarejelea kwa tafsiri ya Luka, mahali ambapo tunasoma kwa vesi ya 45.

Lakini tuseme hivi kwamba Mtumishi atajiuliza : ''bwana wangu anakawia kurudi'', na akianza kuwanyima watumishi wenzake, wanaume na wanawake, chakula, kinywaji na kuanza kulewa pombe.

Mfano huo mbaya unatuonyesha kama Mawakili waaminifu wanastahili kuepuka kurizika na kushikilia heshima.

Kwenye kipindi chetu cha kufuata, tutaendelea na somo letu kuhusu Mwakili mwaminifu na mwenye busara.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Wote wamesikia Neno la Mungu




 Jambo kwa wote naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Mwanzilishi wa ''One Mission society'' ni mtu anayejulikana kwa jina la Charles Cowman, alipata wito wa kumtangaza Kristo. Alipata msukumo kutokana na kifungu cha Marko 16:15, mahali ambapo Yesu anawaomba Mitume wake kwenda ulimwenguni kote na kuihubiri Habari njema kwa kila kiumbe.

Cowman alipendelea kwamba kila mtu asikie Habari njema. Moja ya yale aliyoyafanya huyu mwanzilishi wa ''O.M.S.'' ilikuwa utekelezaji wa Kampeni kubwa ya Kijiji '' iliyo ruhusu kuleta injili kwa kila jamaa ya Japani mnamo miaka ya 1912 hadi 1918.

Cowman alitambuwa upendo wa Mungu kwa kila mtu na ndipo sasa akafanya nguvu ili kwamba kila mtu apate kusikia Habari njema ya wokovu ndani ya Krsto.

Kwa bahati mbaya, hata leo, pamoja na teknolojia tuliyo nayo, si vyepesi kwamba kila mtu kutoka  katika kila mkowa, jimbo wala inchi awe tayari amesikia Habari njema ya wokovu ndani ya Kristo.

Lakini kitabu cha Matendo ya Mitume kinatueleza kuhusu kipindi kikubwa cha miaka mbili mda ambao mkowa wote mzima ulisikia Neno la Bwana.

Paulo alikuwa Efeso, fasi ambayo kwa leo ni Uturuki. Matendo 19 inatufundisha kwamba Paulo alifundisha ndani ya Sinagogi kuhusu Ufalme wa Mungu.

Sikiliza Matendo 19:9,10 :''Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tirano. 

[10]Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hata watu wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani. 

Nini? Paulo anafundisha ndani ya ukumbi mkubwa kwa mda wa miaka mbili na wakaaji wote wa mkowa mkubwa wa Kirumi wanaisikia Neno la Bwana ? Hiyo ilitendeka namna gani? Kifungo kinatupatiya alama tatu.

Alama ya 1: Mungu alifanya miujiza ya ajabu kupitiya Paulo. Na hiyo ilileta msukumo mkubwa kwa watu wengi ambao hawangeweza kusikia Injili kwa namna ingine.

Alama ya 2: Paulo alikuwa na wanafunzi pamoja naye wakati alikuwa akifundisha na kufanya huduma yake ndani ya huo ukumbi mkubwa.

Wanafunzi wanafanya kila ambacho Mwalimu wao anafanya. Paulo aliongea kwa namna ya kushawishi kuhusu Ufalme wa Mungu, na wanafunzi walifanya namna hiyo. Paulo alikuwa akibishana kila Siku ndani ya ukumbi mkubwa wa Tirano, na hakuna Shaka kwamba wanafunzi wake, walifanya nao Pia mabishano kuhusu Yesu katika sehemu zingine za mikowa ya Asia.

Alama ya 3 inatusaidia kuelewa ginsi wakaaji wote wa mkowa walivyosikia Neno la Mungu. Wanafunzi, kama vile Paulo, walijazwa Roho Mtakatifu.

Vipi sasa kwako pia?

Utashinda tatizo la kumusaidia kila mtu wa kamati yako, Jimbo lako, mkowa wako kusikia Habari njema ?

Unafuata mfano wa Mtume Paulo na wa Charles Cowman ? Kama unatarajia kwa kweli majirani wako wote wasikie na kuelewa Habari njema, tafakari kuhusu Matendo 19:1-11 itakupa fursa nzuri ya kuanza. Ujazwe na Roho Mtakatifu, uombee wagonjwa, andaa na kuruhusu wanafunzi kwenda.

Uwe mwaminifu kwa Mungu ili huduma yako ya injili ipate kuenea na kuwa na matokeo makubwa.

Mimi ni Dean Davis nawauliza, ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

UONGOZI WA MUWAKILI - Mfano wa Talanta sehemu 2


 Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Kama ilivyo mwaka mpya, nilianzisha mtiririko mpya kuhusu Mada ya uongozi wa muwakili kama ''mtu anaye ongoza rasilimali za mtu mtu mwengine ili kufikia malengo za mwenye mali''.

Leo, tunaendelea na somo letu la mfano wa talanta unaopatikana katika Mathayo 25:14-30.

Katika toleo langu la nyuma, tulijifunza kanuni tatu ambazo zimetolewa ndani ya hadisi; leo, tutajadiliana kanuni zingine ine.

- kila mfanyakazi (wala mwakilishi) atatowa ripoti ya yale aliyofanya kwa ile mifuko ya dhahabu aliyoipokea. 2wakorintho 5.10 inatuambia ''Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.'' kwa vesi ya 21 ya kifungu chetu, bwana anamsifu Mtumishi wa kwanza kwa kusema : ''ni vema, Mtumishi mwema na mwaminifu ! Ni ripoti gani tutaitowa mbele za Mungu kwa yote aliyotupatiya?

- kuko malipo kwa uongozi bora wa rasilimali. Angalia vile vesi ya 21 na 23 zinavyo fanana. bwana wake akamjibu : ''ni vema, Mtumishi mwema na mwaminifu ! Ulikuwa mwaminifu kwa mambo madogo ; nitakupa vitu vingi. Njoo tuchangia mema ya bwanawako. Mtumishi aliyepokea mifuko tano na ule aliyepokea mbili walizipokea sifa zilezile kutoka kwa bwana wao. Katika toleo langu la nyuma, nilitowa tahazari zidi ya mtego wa kulinganisha watu na wengine. Ndani ya VCP, wamoja wanatumika katika eneo ambao udongo wa kiroho uko na rutuba zaidi na ni mahali ambako mavuno ni mengi sana, na wengine wanatumika mahali pa nguvu sana. Matarajio ya bwana yanatokana na mazingira ya mahali ambako kila moja anatumikia.

- Mawakili wabaya watahamakiwa na kuhazibiwa. Ndivyo tuonavyo katika vesi za 24-30. Mtumishi ambaye hakufanya lolote na mfuko wake moja alio upokea aliambiwa Mtumishi ''mbaya'' pia ''mvivu''. Mfuko aliokuwa nao ulinyanganywa. Ndani ya utamaduni wangu, tuko na msemwa usio nanizamu usemao : ''unaitumikisha wala unaipoteza''. Baba yangu, leo tayari amekufa, alinirudilia msemwa huu mara nyingi kipindi cha mafundisho yangu. Je! Muko na msemwa unaofanana na huu? Hadisi hii inatowa ukweli ulio ndani yake.

- kwa mwisho, Mawakili wazuri watajikuta wamepewa zaidi. Kwenye vesi ya 28, tunaona kwamba mfuko ule ulionyanganywa kwa Mtumishi mvivu, ulipewa kwa yule Mtumishi ambaye alikuwa sasa na mifuko 10. Kanuni hapa katika VCP, na katika kila shirika, wale wanaoongoza vizuri rasilimali walizopewa watajikuta kwa mda fulani wamepewa zaidi... Zaidi ya majukumu, zaidi ya madaraka, na pengine zaidi ya mali.

Katika kipindi chetu chakufuata, tutaendelea somo letu juu ya uongozi wa Mawakili.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Neno la Mungu linatawanyika


 Jambo kwa wote naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Moja ya madai za ajabu sana kuhusu kanisa la kwanza, kanisa lililoanzishwa na mitume pa Yerusalemu Siku ya pentekoste, inapatikana katika Matendo 5:42 :

''Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.''

Hata kama wakati maisha inaendelea vizuri na matatizo ni machache, ni vigumu kufuata huduma ya muhimu bila usumbufu. Kwa mfano, niliwazia kama muundo mpya wa vitabu vya VCP ilikuwa jukumu langu la muhimu ndani ya huduma kuanzia mwaka wa 2019.

lakini kadiri nilivyojaribu kukaza fikira, nilizubaa na kushangazwa na muundo wa somo.

Kwa mwisho, kwa mwezi wa Disemba, nilimaliza sehemu yangu ya mradi huu kwa kuwasilisha somo za muhula wa 8.

Ni vigumu kufuata huduma ya muhimu bila usumbufu. Lakini kanisa la Yerusalemu ''halikuacha kufundisha na kutangaza Habari njema ya kwamba Yesu ni Masiya''.

Kama mulivyojifunza kwa kusoma huduma kenda za kanisa lenye afya, uinjilisti ni muhimu. Kanisa la Yerusalemu lilielewa hivo. Halikuacha kutangaza Habari njema ya Yesu.

Mateso hayakuwaziwia. Matendo 5:40 inatuambia kama viongozi wayahudi waliwapiga fimbo Mitume na kuwakataza wasitamke jina la Yesu. Lakini walipata fursa ndani ya ukumbi wa hekalu na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha.

Magomvi ya wao kwa wao ndani ya kanisa hayakuwaziwia Mitume wa Yerusalemu kutangaza Neno la Mungu. Wakati ulipotokea mgawanyiko kati ya waamini wa lugha ya kiyunani na wale wa lugha ya kiebrania kuhusu ugawaji wa chakula kwa wajane, kanisa, lililoongozwa na m

Mitume, lilipata haraka suluhisho.

Katika Matendo 7:7 inatuhadisia yaliyotendeka baada ya suluhisho ya tatizo ya ugawaji wa chakula. Imeandikwa ''Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.'' Hakuna kitu, hakuna kilicho zuwia kanisa la Yerusalemu kutangaza Habari njema ya Yesu.

Na hakuna chochote kingeweza Pia kuzuwia kanisa zetu. Kama kuko huduma ambayo tunastahili kuendelea kuifanya, ni vizuri kutangaza injili.

Muendelee basi kufundisha na kuandaa washiriki wenu ili watumikishe zana ine za Mpandaji na kutowa injili kwa mtindo wa miviringo tatu.

Fundisho moja halitoshi. Muendelee kuwatuma katika kijiji chenu na vijiji vilivyo kandokando.

Muendelee kuonyesha filamu ya Yesu.

Mufanye mupangilio wa kutumikia vionyesheo ili visibaki kwa mtu bila kutumikishwa na hapo vingeweza kutangaza Habari njema ndani ya Kijiji ambacho hakija sikia injili.

Kama kanisa lako, mfano wa lile la Yerusalemu, ''usiache kamwe kufundisha na kutangaza Habari njema ya kwamba Yesu ni Masiya'', kanisa lako nalo pia litakomaa na kupanuka.

Mimi ni Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Kuwa mfano wa kuongezeka



 Tazama Daneille Snowden na Ongezeka.

Karibu kwenye Ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji, wachungaji na kwa viongozi wakikristo.

Leo, tutazungumzia namna ya kuwa mfano wa kuongezeka.

Kuwa kielelezo kwa mtu, inamaanisha kuwa mfano wa kuigwa (kufuatwa). Hii inamaanisha pia kujenga wala kuunda picha wala sura. Zaidi pia tendo kuongeza inamaana ya kuzidisha kwa hesabu, zaidi kwa namna iliyo juu. Mtume Paulo aliandika :  

''Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.''

1Wakorintho 11:1

Wengine wanaweza kujiuliza hii inatumika namna gani. Namna gani naweza kuongeza na hata kuzidisha ?

Kwa Siku hizi za nyuma, Andiko la Ahadi yangu ni vesi ya Agano la kale, Zekaria 4:6b inayosema :''... Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.''

Tunamaliza kazi hii kwa kutangaza ukweli wa Neno la Mungu. Neno la Mungu halistahili tu kukaa ndani yetu, lakini litumikishwe sabau ya kupanda mbegu nyingi ndani ya roho za watu.

Ni muhimu kutukumbusha kwamba udongo wa roho wa mwanadamu unastahili kutayarishwa na kulimwa ili kupokea mbegu hiyo.

Kwa kufanya hivo, upako mkubwa wa Roho Mtakatifu utawaka ndani ya moyo na kuzaa matunda mengi. Hiyo inafanana kuwa rahisi, sivyo? Ugumu wa jukumu hilo liko kwa ngambo yetu kwa kuacha na kutii.

Inatupasa pia kuendelea mbele na kutokuacha.

Katika Marko 8:34, Yesu anasema :''...Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate'' ni kwake tunapata mwelekeo na namna gani tunaifanya ! Kwa hiyo, inapashwa kumfuata Kristo kwa karibu sana, kukaa ndani yake na ndani ya uwepo wake. Tunafikilia kuachana na matakwa yetu (sababu kila Siku tunatumaini kwamba Bwana atajishugulisha nasi na maitaji yetu), na kwa mwisho, tunastahili KUCHUKUWA Msalaba wetu na kufuata mwelekeo na mfano wake.

Nafikiria maisha yangu ndani ya huduma na ninatambuwa kwamba vile miaka inavyo enenda, niliona mtu moja wa kawaida akiishi tu kwa kawaida maisha ya utii na ya kujitolea.

Je! Nimekwisha kila siku kutimiza yale Bwana aliniitiya kufanya? Apana hata kidogo.

Je! Nimeacha? Ebu kwa kuwa mkamilifu, kulikuwa wakati ambao niliitarajia. Lakini Yesu pamoja na upendo wake walisukuma moyo wangu na wakanipa Roho yake kwa ajili ya mioyo iliyopotea katika dunia hii.

Ninaweza kuwaambia kama, mara na mara, Yesu ananishika mkono, ananihakikishia nguvu yake na, kwa pamoja, tunaendelea kupenda wengine katika Ufalme wa Mungu!

Utafanya namna hii?

Mnifuate, kama ninavyo mfuata Kristo ! Na tutageuka sote kuwa wavuvi wa watu!

Ilikuwa Ongezeka, tunatarajia kwamba utabarikiwa na neno hili la leo ! Usikose kuligawanya pamoja na wengine na kutupata kwenye mtandao vcpencouragement.org

Punje ya ngano



 Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka''ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

 Maisha ya Yesu ni mfano mzuri kwetu sote. Petro na wanafunzi wengine walipoelewa Yesu alikuwa nani, mafundisho yake yalianza kubadilika. Alielekeza juhudi zake Yerusalemu, mahali ambapo alijua kwamba angesalitiwa, kuhukumiwa vibaya, kuhukumiwa na kusulubiwa. Kwa makusudi alielekea Yerusalemu na msalabani. Na njiani, aliwafundisha wanafunzi wake gharama ya ufuasi. Yesu hakugeuza maneno yake. Alisema waziwazi. Alituita tuchukue msalaba wetu kila siku na kumfuata.

 Yesu alisema katika Yohana 12:23-28, "Yesu akawajibu, "Saa imefika ambayo Mwana wa Adamu hana budi kutukuzwa. Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa matunda mengi. Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; na yeye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu, ataiokowa kwa maisha ya milele. Mtu akinitumikia na anifuate; na nilipo, ndipo atakapokuwa na mtumishi wangu, mtu akinitumikia, Baba atamheshimu?... Baba, uniokoe na saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hiyo ndiyo maana nilikuja, Baba litukuje jina lako!

Unapopanda mbegu ya ngano au mahindi, au nafaka nyingine yoyote, mambo hubadilika.

Mbegu iliyopandwa haifai tena kuliwa. Chini ya udongo,  inakuwa haina maana kula. Umbo lake hubadilika kadiri inavyovimba na kibaridi. Maganda yake hutengana na mbengu. Hakuna mtu anayeiita "mbegu" tena. Kimsingi imekufa na haiwezi kutumika kwa chakula. Lakini ubora zaidi bado unakuja. Kwa sababu mbegu hii isiyo na maana inakuwa mmea mdogo hai, unaokua na mzuri sana. Haionyeshe sura ya chochote, lakini amejaa uwezo! Inapokua na kukomaa, mmea huu mdogo unakuwa mkubwa na wenye nguvu. Kisha hutoa matunda: matunda mengi sana za mbegu. Na huleta furaha kwa mkulima wakati wa mavuno.

 Hakuna hata moja kati ya haya ambayo yangetukia kama ile punje ndogo ya ngano isingeanguka chini, kufunikwa na udongo, na kufa kama punje. Kama Yesu alivyosema, "Chembe ya ngano isipoanguka katika udongo, ikafa, hubakia mbegu moja tu; lakini ikifa, hutoa mbegu nyingi." 

Maisha yako na yangu ni kama punje hii ya ngano: iliyojaa uwezo usioweza kufikiwa. Hatujui ni maisha ngapi tunaweza kuathiri kwa wema ikiwa tutakufa kwa nafsi na kujitoa kabisa kwa Yesu. Lakini tunajua kwa uhakika kwamba ikiwa hatutakufa kwa malengo yetu ya ubinafsi na maono ya kibinafsi ya kumfanya Yesu kuwa mfalme wa maisha yetu, hatutafanya kitu kikubwa cha wema mwingi kwa ajili yetu au wengine katika ulimwengu huu.

Tunakufa kwa ubinafsi kwa kuacha malengo yetu ya ubinafsi kwenda mahali Yesu anataka twende, kufanya kile ambacho Yesu anataka tufanye. Yesu anatutaka twende, tufanye kile ambacho Yesu anataka tufanye, na kusema kile ambacho Yesu anataka tuseme. Hata kama inatugharimu kila kitu. Hapo ndipo ahadi ya Yesu inaanza kutimia. Akasema, “Mmea ukifa, hutoa mbegu nyingi.” Wakristo wanapokufa kwa ajili ya nafsi zao na kuishi kwa ajili ya Mungu, baraka zinazotiririka hazina mwisho. Hii pia ni nguvu ya kuongezeka. 

Mimi ni Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

UZAE MATUNDA MENGI


 Hujambo, uko kwenye Ongezeka, ni podikasti inayokusudiwa kuwahimiza wapandaji na viongozi wa makanisa katika vijiji. Jina langu ni Brad Snowden na ningependa kusoma Yohana 15:4-5 ambayo inasema: "Kaeni ndani yangu, nami nitakaa ndani yenu. Tawi haliwezi kuzaa peke yake, bila kubaki kwenye mzabibu. Ni vivyo hivyo kwenu: msipokaa ndani yangu, hamwezi kuzaa matunda yoyote. 

V5 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, ninyi mkaa ndani yangu. Mtazaa matunda kwa wingi; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” Ninatambua mawazo mawili muhimu katika maandiko ya Yohana 15 ambayo yanatuonyesha moyo wa Kristo. Inahusu uhusiano wetu naye na matokeo ya uhusiano huo wa karibu, ambao ni kuzaa matunda. Yesu alikuwa anakaribia mwisho wa maisha yake duniani, alikuwa amewafundisha wanafunzi wake na kuwaonyesha moyo wake. Katika kifungu hiki anaifafanua kwa kuunganisha tu vipengele viwili vinavyoleta uhai na uwezo wa kuzaa matunda. Inahusu tu kuunganishwa na Yesu na kumruhusu kufanya kazi kupitia sisi. Nimeona katika maisha yangu kwamba ninaweza kusema wakati mambo yamebadilika, kama vile kulikuwa na wakati ambapo sikuona mengi yakifanyika, wakati sikuhisi kuwa muhimu au kipingamizi kama ningependa. Ni kana kwamba maji yamekatika ghafla na maisha yamekuwa makavu. Haikuchukua muda mrefu kugundua kuwa sikuzungumza ya Mungu mbele zake kama nilivyofanya hapo awali. Niliona kwamba shangwe yangu haikuwa kubwa jinsi inavyopaswa kuwa katika kumtumikia. Sikuwa na amani niliyohitaji na hii ilisababisha matatizo mengine ambayo hayakuongeza maisha yangu na ushuhuda wa Yesu katika maisha yangu. Sikuwa mkarimu kama wengine walivyohitaji niwe. Matunda ya uhusiano wangu, au ukosefu wake, yalionekana na wengine. Mbali na Yesu, hatuwezi kufanya lolote. Kando na uhusiano wa karibu na Yesu Kristo, hatutabeba mema. Tunazaa matunda kwa ajili yake tu na tuna furaha na amani, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Ni matunda haya ambayo yataonekana na wengine 

- ndipo tunaweza kushiriki jinsi Yesu amebadilisha maisha yetu. 

Baba mkwe wangu alinishirikisha umuhimu wa kuwa mkaguzi wa matunda. Ninaukagua moyo wangu mwenyewe ili kuona ikiwa matunda ya uhusiano wangu ni vile inavyopaswa kuwa au vile Mungu anataka yawe. Ni lazima tuwe na nia ya kuchunguza maisha yetu ya kiroho ili kulenga kuzaa matunda ili wengine wamwone Yesu. Hili linaweza tu kufanywa kupitia uhusiano wa karibu, kumruhusu Roho Mtakatifu kutulisha na kutuwezesha kuwa zaidi kama Kristo. Kwa kuzaa matunda, tunapanda mbegu kwa mavuno ya milele. Ni zawadi inayoendelea kutoa, na wale wanaoipokea wataweza kujitayarisha wenyewe Habari za matunda wanapokua katika uhusiano wao na Kristo Yesu. Ni lazima tutiwe moyo na neno la Mungu: tunaweza kuzaa matunda mengi, lakini ni kwa Yesu Kristo tu tunaweza kufanya hivyo ikiwa tunatembea naye kwa ukaribu.

 ilikuwa neno la kutia moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. 

Je, ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Bwana akubariki.

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...