Alhamisi, 31 Julai 2025

Kufundisha kwa ajili ya mavuno mengi


 Jambo, munasikiliza, Ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji. Mimi ni Brad Snowden.

Yohana 4:35-38

: ''Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno. 

Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate kufurahi pamoja.   Kwa maana hapo neno hilo huwa kweli, Mmoja hupanda akavuna mwingine. 

 Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.''

Yesu, katika huduma pamoja na wamitume wake, alikuwa akiwafundisha kwa namna ya kuzuwa maswali mengi ndani ya roho zao. Katika kifungu hiki, swali nyingi zingeumiza mioyo yao : ni nani ninastahili kutafuta? Nani anaendelea kuvuna, na anavuna nini? Namna gani walipata tunda hili ? Mawazo na swali hizi zinaweza kuongezeka.

Yesu alitupatiya mifano mingi ya Mitume waliofunzwa kwa maswali yaliyo wazi, yanayoleta mabishano ya nguvu na kwa maelezo bora.

Huduma yake ilivizia kuongezeka kwa mitume na faida yake katika dunia hii. Umaarufu ambao kila mmoja wao angekuwa nao, na maisha mengi ambayo yangebadilishwa.

Siyo tofauti kwetu Sisi pia. Bwana anapenda kujionyesha kwetu ili tukomae katika ujuzi wa vile alivyo na hata zaidi tena. Anapenda pia kututumikisha ili kuongoza watu wengine na kuwasaidia kukomaa katika huduma yao yakipekee.

Namna gani tunaweza kuwa chanzo cha kuwatiya moyo ndani ya maisha yao?

Namna gani tunaweza kuwahimiza wengine kuamini kwamba Mungu anataka kutumika zaidi pamoja nao ?

Namna gani ya kugawanya maneno ya haki yanayozuwa maono mapya ?

Ni nani Bwana anaweka rohoni mwako ili kumwendea, kutembea karibu yake na kumusaidia kugeuka kuwa mvunaji mukubwa ?

Ni maongezi gani yaliyo ya muhimu ili wachukuwe maamuzi mazuri na kuwakilisha mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yao na kwa wale wanaoitaji tumaini ?

Wapandaji wa makanisa, viongozi, ni furaha gani kuona wanafunzi wenu kugeuka kuwa wenye hekima !

Mithali 11:30 :"Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; 

Na mwenye hekima huvuta roho za watu.''

Yote tunaweza kufanya ili kutiya moyo, kufundisha, kutowa mfano, kutembea karibu na wengine na kuwatolea yale Mungu alitupatiya ili wageuke kuwa na hekima kwa yale yanayofurahisha roho ya Mungu na kazi bora.

Endelea, sababu kwa mda uliyopangwa, utavuna matunda ya kazi yako yote.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Ni pamoja na wanani utagawanya nao leo hayo ?

Hakikisho la wokovu


    Jambo kwa wote naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Leo, niliongea na ndugu moja anaye mtumikia Kristo katika inchi ya Afriki ya Mangaribi. Aliniambia kama aliuliza zaidi ya watu 1000 kama wanajuwa ni wapi watakaa milele baada ya kifo chao.

Juu ya watu 1000 walioulizwa, ambao wengi miongoni mwao walikuwa wafuasi na wanashiriki kanisa kila siku ya Mungu, ni watu Saba tu miongoni mwao ambao walitambuwa kama wataishi milele pamoja na Kristo sababu ya kile Yesu aliwatendea. Wengine walijibia kwamba hawana uwakika na mahali ambapo wataishi milele, wala wanajuwa kama wataishi milele katika jehanamu. Ndugu yangu aliguswa sana na vile wengi wanaoingia kanisa hawakuwa na uhakika wa wokovu ndani ya Kristo.

Neno langu la kutiya moyo ni hili hapa : tunaweza kuishi ndani ya dunia hii iliyovunjika na kuwa na uhakika kwamba tuko wana wa Mungu, warithi pamoja na Kristo, waliosamehewa, walio okolewa, waaminifu wenye maisha mapya na ya milele ndani ya Kristo.

Hatuna cha kuogopa kifo wala jehanamu.

Nilipata hakikisho la wokovu wakati nilikuwa na umri wa miaka 13. Na ninahishi na uhakika huo tokea sasa miaka 55. Ona namna hayo yalitendeka.

Niliambia ndugu moja katika Kristo kama sikuwa na uhakika wa kuwa Mkristo. Alifunguwa Biblia yake katika kitabu cha 1Yohana 5:10 na akanisomea haya maneno :

''Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.''

Kisha ndugu akaniuliza : ''Dean, je! Uko na Mwana wa Mungu ndani ya maisha yako ?''

Nilijiwaza kwa mda mchache, baadaye nilisema : ''ndiyo. Niliweka tumaini langu ndani ya Yesu kuwa Mwokozi wangu. Anaishi ndani yangu.''

Kisha ndugu alisoma tena 1Yohana 5:11-12 :

''Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. 

Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.''

Kisha akaniuliza : ''uko na uzima wa milele? Nilijibu : ''ndiyo, niko na Yesu : niko na uzima wa milele.''

Sasa, ndugu akaniahakikishia : ''Dean, unaweza kuondoka hapa bila kuwa na mashaka ya kwamba uko Mwana wa Mungu, Mkristo aliye na uzima wa milele.''

Je! Unajuwa nini? Niliondoka mahali pale nikiwa na uhakikisho kama mimi ni Mwana wa Mungu na kwamba Niko na uzima wa milele.

Tokea hapo, niliona woga wa kila namna. Lakini sijasikia woga wa kwenda jehanamu wala wa kutengwa na Yesu.

Ninao.

Je! Uko na uhakikisho wa wokovu ndani ya Yesu-Kristo ? Unaweza kuwa nao. Wafuasi wako wanao  huo uhakikisho ? Wanaweza kuwa nao. Tafazali, bila kungoja, wagawia huo uhakika wa ajabu kuhusu uhakikisho wa wokovu kutokana na Neno la Mungu, ndani ya 1Yohana 5:10-12

Mimi ni Dean Davis, naomba ili kuwe kanisa katika kila kijiji cha Afrika, na kila mtu katika hizi kanisa aishi kila siku na uhakikisho mukubwa wa wokovu wa Kristo ndani yake, tumaini la utukufu.

Karama za unabii kwa ajili ya kuongezeka


     Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Katika kipindi changu cha nyuma, nilionyesha kwamba neno ''Mtume'' mara nyingi linaeleweka vibaya, sababu liko na tafsiri nyingi kulingana na makanisa tofauti. Japo hiyo, tunastahili kungojea kwa Kristo atoe Mitume kwa kanisa zetu, kama alivyo ahidia ndani ya kitabu cha Waefeso 4. Tunaitaji watu, waliyotolewa na Mungu, kutumwa ili kufunguwa makanisa mapya pale ambako hayajakuwa bado. Ndivyo ilivyo, kazi ya Mtume !

Waefeso 4 : 11-12 inatuambia : 

''Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 

[12]kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe''.

Oh ! Neno la kwanza katika hii oroza, ''Mtume'', mara nyingi inaeleweka vibaya na la pili : ''Nabii''. Ijapokuwa, Kristo anataka kutowa Manabii kwa kanisa zake ili mwili wa Kristo ujengwe. Lakini kwa kanisa Nabii ni nani ?

Nabii anapokea kwa Mungu uwezo binafsi wa kuwapa moyo kanisa na kuonyesha matukio ndani ya dunia yanayo mchukiza Bwana. Nabii anatangaza ukweli kutoka kwa Mungu na anawaita wakristo kwa utii.

Manabii wanategemea sana maombi na karama za kiroho ili kutimiza huduma yao.

Lakini kama Nabii hatembei kwa Roho, alama mbaya zinaweza kutokea.

Nabii ambaye ambaye hayuko chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu anaweza kuchukuwa mwenendo wa hukumu wala kugeuka kuwa mwenye kiburi kwa sababu ya hali yake ya kiroho.

Anaweza kuzania kutowa unabii bila kusikia sauti ya Bwana Mungu wala kuelewa Neno lake ndani ya Biblia. Anaweza ata kuwaziwia wengine kusema ili kutamka maneno yasiyofaa.

Kanisa zenu zinaitaji Manabii, kama vile zilivyo pia na itaji ya Mitume, Wainjilisti, Wachungaji na Waalimu.

Zinaitaji pia kupewa moyo na sahisho. Zinaitaji viongozi wanaochukuwa mda mwingi katika maombi na walio tayari kutowa ujume wa Mungu.

Manabii wanahimiza huduma ya injili na upandaji wa makanisa wakiwaita washiriki kwa vitendo na kuwapa moyo waliyo watiifu.

Lakini uko mwangalifu kwa wale walio na karama ya unabii katikatika yenu? Yesu alisema kwamba atatowa Manabii kwa kanisa zetu. Kama tunapendelea kuwa Mawakili wazuri, tunastahili kuchunguza kuongezeka kwa Manabii, kukubali na kuhimiza huduma yao kuwasahihisha wakati wakienenda pembeni ya Roho Mtakatifu, na kuwapa nafasi ya kutangaza ujumbe wa Bwana. 

Kama vile Mtume Paulo alivyosema katika 1Watesalonike 5:19-22 : ''Msimzimishe Roho; 

msitweze unabii;  jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;  jitengeni na ubaya wa kila namna''.

Maombi yangu kwa kanisa zenu, Mungu awape wanaume na wanawake wenye nguvu ambao munaitaji ili kutimiza mapenzi yake, ili kukomaa na kuongezeka!

likuwa Ongezeka, na mimi ni Dean Davis nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Karama za kiuchungaji kwa ajili ya kuzidisha


     Jambo kwa wote! Karibu kwenye Ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, wachungaji na wasimamizi wa kikristo.

Mimi ni mwenyeji wenu leo, Daneille Snowden.

Leo nitajiunga na kifungu cha Waefeso 4:11-15. Fuatana nami :

''Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 

[12]kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

[13]hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 

[14]ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 

[15]Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo''.

Wakati tunapo fundisha wapandaji wetu wa makanisa, na kuongeza idadi ya wasimamizi wa mikutano yetu, karama ambazo Bwana alitowa kwa kanisa ni za muhimu na zinastahili kuwa sehemu ya mafunzo yetu.

Vesi 14 ya Waefeso inafasiriya wazi sababu gani ni ya muhimu. Hii inaonyesha kwamba Sisi - nitaongeza : kwamba kanisa - tusipelekwe kwa urahisi kuingizwa ndani ya elimu potevu.

Imesemekana : ''...ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu''.

Sisi kama viongozi, ni muhimu tufundishe na kuandaa waamini juu ya karama ambazo Mungu alitowa kwa kujenga kanisa.

Nilisikia pia ikisemwa kama ni karama ya binafsi ambayo Mungu anaeneza kwa neema juu ya kanisa na juu ya dunia.

Soma : vesi 12 - ''kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma, hata mwili wa Kristo ujengwe;''.

Moja ya karama ni ile ya Uchungaji (Mlinzi wa Kondoo). Karama hii ya Uchungaji inajionyesha kupitiya huruma na kulinda, kwa kulinda Kondoo, inamaanisha kulinda watu ambao Mungu amempa mtu. Mchungaji anafundisha, akijuwa kwamba mafundisho yake yanalisha kanisa na kuiandaa, kwa mwisho, juu ya kutekeleza mpango ambao Mungu aliandaa kwa kila mmoja. Mchungaji ni Mlinzi mkubwa zidi ya kusanyiko lake. Anakesha juu ya usalama, kwa upekee juu ya mpango wa kiroho. Wachungaji wanapenda tu taifa lao na kutamani kuwa pamoja nao.

Anapenda kujiusisha na maisha ya kanisa lake na kuonyesha msaada wake kwa maombi, mafundisho hata kwa kusaidia kwa namna mbali mbali kulingana na maitaji.

Mchungaji yuko tayari wakati taifa lake linafuraha, hata wakati wanapitiya kipindi cha mateso.

Nilikomaa ndani ya familia ya kiuchungaji, na baadaye, mimi na mume wangu tulifanya kazi ya Uchungaji kwa mda wa miaka 27. Niliona baba na mama yangu wakiwatunza washiriki wa kanisa letu kwa upendo.

Nilisikia joto ya upendo wa Mungu ukitawanyika kutoka kwa wazazi wangu hadi kwa kila mtu.

Nilijifunza, kupitiya mfano wao, ni kwa namna gani jamaa la Mungu liko bora. Niliona wazazi wangu wakilia pamoja na washiriki wao, wakiwatiya moyo kupitiya Neno la Mungu, na kuwaombea. Mimi na mume wangu tulifanya pia hivo, kwa kuwaletea chakula ao kuwasaidia nyumbani kwao kama ikiitajika.

Uchungaji ni kujitolea saa 24 juu ya 24, Siku 7 juu ya 7, kwa wale ambao Mungu alitupatiya. Hii ikiongezwa na ulinzi juu ya mashambulizi ya adui anayetafuta kunyanganya moja ya Kondoo, na kuwa tayari na haraka kumzuiya. Tumeshukuru Mungu kwa karama za wachungaji, karama itokayo rohoni hata pia kwa Mungu. Tuwe waangalifu kwetu wenyewe na kwa wengine kama tukiwa na karama hii, na tujuwe kwamba ni kupitiya Roho wake Mtakatifu ndipo tunaweza kuendelea kupenda na kutumikia taifa ambalo Mungu alitupatiya.

Ilikuwa Ongezeka, asante kwa kugawanya podikasti hii kwa wengine.

Karama za kiutume kwa ajili ya kuzidisha


  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Bwana na Mwokozi wetu Yesu-Kristo alitowa neema kwa mwili wake, ambalo ni kanisa, ili sote tubarikiwe pamoja, ili kwamba tuishi kwa umoja na kutembea kwa imani. Neema, upendeleo na nguvu anazozitowa kwa kanisa zinaonyeshwa kwa njia mbali mbali. Lakini moja ya mambo muhimu na yenye kuvutiya ni kwamba Kristo alitowa neema yake kupitiya watu. 

Hata kama sote tunakuwa viungo vya mwili moja, kila moja wetu anachangiya kwa namna yake.

Waefeso 4:7 inasema:

''Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.''

Mtume Paulo anaongeza kwa kueleza namna gani Kristo anatowa neema hiyo kwa kanisa.

Anasema katika Waefeso 4.11-13 :

''[11]Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 

[12]kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 

[13]hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;''

Ni ukweli unao onekana vile Paulo anatangaza kwa kanisa la mpya la Efeso. Kristo alitowa aina tano ya watu ili kujenga mwili wa Kristo. Anatowa aina hizi tano za huduma ili kwamba mwili wa Kristo ukomae na kuwa na nguvu : Manabii, Mitume, wainjilisti, wachungaji na waalimu.

Sasa, kama Yesu anawapa watu hawa kwa ujenzi wa mwili wake, je! Hatutawatafutiya miongoni mwa washiriki wa kanisa zetu?

Hatuwezi kujiuliza swali hili :

'' ni nani miongoni mwa washiriki wetu ni Mtume ambaye Mungu alitupatiya? Ni wanani Manabii? Na wachungaji na waalimu ?

Kwa kujibu kwa swali hizi, mara nyingi tunasubiri mshiriki moja wa kanisa asimame na kuchukuwa nafasi muhimu ya uongozi mbele ya kusema :

''Ah, huyu ni mwinjilisti'' , ao ''yule dada pale ni Nabii'' ao tena ''dada huyu ni Mwalimu''. Na wengi wanasita kuhakikisha kwamba mshiriki anaweza kuwa na karama za Utume. Neno ''Mtume'' liko na tafsiri nyingi. Kufuatana na asili za kanisa, neno hili limewekwa kwa ajili ya aina ya watu fulani.

Lakini ndani ya Agano Jipya, neno ''Mtume'' linamaanisha tu ''anayetumwa'' ao ''mwenye kupeleka ujumbe'' wamitume ni wenye kutumwa na Bwana na kanisa ili kueneza ujumbe wa wokovu na kupanda makanisa mapya.

Kwa mjibu wa Waefeso 4, Mtume ni mtu ambaye Yesu-Kristo alimpa neema, upendeleo, hekima na nguvu, ambaye matunda ni kutangaza ujumbe wa Kristo, upandaji na kuongezeka kwa makanisa katika maeneo mapya.

Ni akina nani ndani ya kanisa lako, walio na mwelekeo, maono na uwezo wa kuanzisha na kuongeza makanisa pale ambapo hayajakuwepo?

Ni vizuri kutambuwa hayo maoneo, kuomba kwa ajili yao, kuwapa moyo na kuwafundisha kwa ajili ya mavuno mengi.

Nani anajuwa? Unaweza fanya kwa watu hawa kile ambacho Barnaba alifanya kwa Mtume Paulo.

Alimbariki mbele ya wengine ambao walikuwa bado kutambuwa wito wake wa kiutume.

Kwa kufanya hivo, Barnaba alifata mfano wa Yesu katika ujenzi wa kanisa - tendo ambalo mpaka leo tunaona faida yake.

Mimi ni Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

UONGOZI WA MUWAKILI - Tabia inahusika


    Jambo nyote, tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi katika vijiji.

Tunaendelea na mfululizo wetu juu ya uongozi wa Muwakili. Leo na katika vipindi vinavyokuja, nitajihusisha kuhusu baadhi ya mada kubwa zinazoshikamana na kuongoza. Tunaanza na ukweli huu: tabia inahusika.

Kwa ukumbusho, muongozi wa rasilimali (ao Muwakili) anatafsiriwa kama ''mtu anayesimamia rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali''. Katika mazingira yetu, tunaongoza rasilimali tulizopewa na Bwana kwa ajili ya kazi ya upandaji wa makanisa katika vijiji.

Mutakumbuka pengine kwamba tabia ilikuwa Mada yangu maalm mnamo mwaka wa 2024, wakati tulikuwa tukijifunza tabia za uongozi wa Nehemia. Katika kipindi changu kinachoitwa ''kuwa mwaminifu juu ya mda, niliongea kama Danieli alitumika yapata miaka 66 chini ya uongozi wa wafalme watatu wa Babiloni! Tunagunduwa namna alivyotekeleza hayo katika sura ya 6, vesi ya 4.

[4]Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake''.

Ni ushuhuda wa namna gani ! Ni urizi wa namna gani ! Hakuna yeyote yule, hata wapinzani wake hawakupata hata kidogo ya rushwa ndani yake.Alikuwa mwaminifu akiwa Muwakili chini ya uongozi wa wafalme watatu wa Babiloni, na hakuwa na zarau katika utendaji kazi wake. Tujikaze, pamoja na nguvu, upako na kuvikwa Roho Mtakatifu, kuwa kama Danieli.

Kwa mwanzo wa mwaka, tumeanza mtiririko huu kwa mfano wa Talanta katika Mathayo 25.

Mtumishi ambaye alipewa mifuko tano ya feza ''alienda kuchuuza pesa hizo'' (vesi 16).

Mawakili waaminifu wanaonyesha utayari na wanatumika kwa uaminifu kwa kusudi ya kutekeleza kurudi bora kwa Bwana. Mwenendo huu wa unyenyekevu na uaminifu kwa Bwana ni mfano wa kufuatwa.

Tukumbushe pia kwamba mfano wa Mtumishi mwaminifu na hodari, katika Mathayo 24. Kwenye vesi za 46 na 47,

Yesu anafundisha :

[46]Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.''

[47]Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote''.Yesu anafundisha ndani ya mfano wa Talanta kuwa wale wanaomtii Mungu watalipwa. Utii wetu, ambao uko na mizizi ndani ya tabia yetu, ni vya muhimu sana.

Ninamaliza na baadhi ya vesi na maneno juu ya tabia:

Mithali 10.9 :

[9]Aendaye kwa unyofu huenda salama; 

Bali apotoshaye njia zake atajulikana''.

Billy Graham : ''uaminifu inamaanisha kwamba tuko waaminifu, wakuigwa, na usio laumika.''

Mithali. 11.3 : ''Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza 

Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.''

Ndiyo, tabia inahusika!

Wakati mwengine, tutaendelea somo letu kuhusu uongozi wa Muwakili.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji na viongozi.

Hakikisho la wokovu


     Wengine walisema kama wanajuwa kama wataishi milele jahanamu. Ndugu yangu alijihusisha sana kwa vile wengi wa wale wanaoshiriki ibada hawakuwa na uhakika wa wokovu wao ndani ya Kristo.

Neno langu la kutiya moyo leo ni kwamba tunaweza kuishi ndani ya dunia hii inayovunjika tukiwa na uhakika kwamba tu wana wa Mungu, warithi pamoja na Kristo, walio samehewa dhambi, wakiwa na uhakika kwamba wako na maisha mapya na ya milele ndani ya Kristo. Hatuna cha kuogopa kifo ao jehanamu.

Nilipata uhakikisho wa wokovu nikiwa na umri wa miaka 13. Nimeishi katika uhakikisho huo tokea sasa miaka 55. Tazama namna gani nilivyo upata.

Niliambia ndugu moja katika Kristo kama sikuwa na uhakika wakuwa mukristo. Alifunguwa Biblia yake kwa kitabu cha 1Yohana 5:10 na akanisomea maneno haya:

1 Yohana 5:10

[10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. Na tazama ushuhuda huo, ni kwamba Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huo uko ndani ya Mwana wake. Yeye aliye na Mwana yuko na uzima; yeye asiye na Mwana wa Mungu hana uzima.

Ndugu akaniuliza sasa : ''Dean, uko na Mwana wa Mungu ndani ya maisha Yako?''

Nilifikiri kiasi kidogo, kisha nikajibu : ''ndiyo, nilitumainia Yesu kama Mwokozi wangu. Anaishi ndani yangu.''

Kisha ndugu akasoma tena 1Yohana 5:11,12 : ''Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. 

Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.'' baadaye akauliza, Dean, watu walio na Mwana wa Mungu ndani ya maisha yao wako na uzima wa milele? Nilikubali, ''ndiyo.'' kisha akaniuliza : ''uko na uzima wa milele ?'' nilijibu : ''ndiyo'' niko na Yesu; niko na uzima wa milele ''. Ndugu huyo ananiambia akiwa na uhakikisho : ''Dean, unaweza kwenda na usiwe na shaka ya kwamba wewe ni Mwana wa Mungu, mkristo aliye na uzima wa milele ''. Je! Munajuwa ? Nilitoka mahali hapo nikijaa uhakika kwamba niko Mwana wa Mungu na kwamba niko na uzima wa milele.

Tokea hapo, nilikwisha kuona woga mara nyingi. Lakini sijawai kupata woga wa kuingia jehanamu ao kutengwa na Yesu. Niko naye.

Uko na uhakika wa kuokolewa ndani ya Kristo ? Unaweza kuokolewa. Wanafunzi wako wanao uhakika wa kuokolewa ndani ya Yesu-Kristo ?

Wanaweza kuokolewa pia. Tafazali, bila kukawia, gawanya nao ukweli wa ajabu wa wokovu, uliotolewa ndani ya Neno la Mungu 1Yohana 5:10-12.

Mimi ni Dean Davis na ninaomba ili kuwe kanisa katika kila Kijiji cha Afika, na kila mtu ndani ya kanisa hizi aishi kila siku akiwa na uhakika ya uwepo wa wokovu wa Kristo ndani yao, na tumaini ya utukufu na upendo wa Mungu.

UNAWEZA KUIFANYA


   Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Miongoni mwa maneno ya ajabu zaidi yaliyo tamkwa na Yesu, mamoja yanaelekezwa kwa wanafunzi wake kwa nyakati za kutatanisha. 

Karibu ya miaka tatu ya mafundisho ya kuendelea, hapa duniani, wanafunzi wa Yesu walikuwa bado kuelewa Yesu alikuwa nani.

Yohana 14 inatuambia juu ya kuchanganyikiwa kwa Tomaso kuhusu utu wa Yesu. Vesi ya 8 inazungumzia kuchanganyikiwa kwa Filipo kuhusu mawasiliano ya Yesu na Mungu Baba.

Ni katika hali hii ya kuchanganyikiwa, ya uzaifu na upungufu wa wanafunzi wake, kwa kuelekea mwisho wa maisha ya Mwokozi wao hapa dunuiani, ndipo Yesu alisema: Amin, Amin, nawaambia, yeye aniaminiye mimi atafanya naye pia yote nifanyayo, hata makubwa kuliko haya, sababu naenda kwa Baba. Na yote mutakayoomba kwa Jina langu, nitalifanya ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.''

Ajabu! Yesu aliwaambia wanafunzi wake, wakiwa wakichanganyikiwa, wangetekeleza mambo makubwa zaidi kuliko yake kama tu wangeamini.

Tunajuwa kazi za Kristo : Aliponya wagonjwa, alifufuwa wafu, kuwafunguwa walioonewa na shetani, kupambana na viongozi wa kidini wanafiki, na kutangaza Ufalme wa Mungu kwa maelfu ya watu katika Palestine. Hayo ndiyo matendo makubwa. Ijapokuwa Yesu anasema kwamba wanafunzi wake watafanya makubwa zaidi kuliko yake, Ila kwa shurti tu ya kuamini.

Maneno ya Bwana wao yalisikilika kuwa hayawezekani machoni pa wanafunzi wake.

Walijuwa kwamba ni namna gani walivyo: wafuasi wakuchanganyikiwa wenye woga wa Rabbi ambaye hawakumuelewa vizuri. Ni kwa namna gani wangeweza kufanya matendo makubwa zaidi yake?

Ijapokuwa, Yesu aliwapa moyo. Kwa kila tukio lolote lile aliwapa moyo.

Kwa mda ambao kila kitu kingekuwa giza, aliwaamini. Kwa Imani, Yesu aliona kile wangeweza kutimiza. Aliwahimiza kwa kusema:

''amini, amin, nawaambia , yeye aniaminiye mimi, atafanya naye pia yote nifanyayo hata makubwa kuliko haya, sababu naenda kwa Baba.''

Nina uhakika kwamba ninyi ndugu na dada zangu, kwa kuangalia wanafunzi wenu, mutaona pia uko kuchanganyikiwa na huo woga ambao Yesu aliusikia kwa Tomaso na Filipo.

Inakufikia pengine kujiuliza: ''ni nini kabisa watatekeleza?''

Fanya anagalisho kwa mda huo. Usivunjike moyo kwa vitisho. Badala yake, tamka neno la imani na la kutiya moyo. Ambia wanafunzi wako, kwa wakati wao wa mashaka : ''unaweza kuifanya. Mungu yu pamoja nawe. Usiache. Endelea kuwa na tumaini kwa Yesu. Utatimiza mambo makubwa''.

Nakumbuka, nilikuwa karibu na miaka 23. Nilikuwa mwanafunzi kwenye chuo cha Biblia. Sikuwa kabisa mwenye ujuzi zaidi wala mwenye busara zaidi.

Nilikuwa nikijiuliza namna gani nitakavyokuwa Siku za usoni.

Lakini wanaume wamoja waaminifu katika kanisa langu, waliniambia kama waliamini kuwa nitafanya mambo makubwa. Sikuamini maneno yao, lakini yalinitiya moyo. Na leo, ni zaidi ya miaka 50 iliyopita, wakati ninapofikiria maneno yao, ninakubali kwamba Mungu alifanya mambo makubwa ya ajabu ndani ya maisha yangu kupitiya hayo.

Si sababu niko mkubwa, lakini sababu yeye ni mkubwa, na ni mwema.

Sasa, watiye moyo wanafunzi wako. Waambie kama wakiamini, watatenda mambo makubwa ambayo hawangefikiria.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Na mimi Dean Davis nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

WAOMBEE WALE UNAOWAFUNDISHA


Jambo nyote ! Tazama Ongezeka , ni podikasti ya kuwahimiza wapandaji na viongozi wa makanisa. Mimi ni Brad Snowden, na leo ningependa kujadili kipengele cha maisha ya Yesu. Bwana alikuwa na uhusiano maalum na wanafunzi Wake. Aliwafundisha, kuwatia moyo, na kuwawezesha kutumia kile alichowapa kutimiza mipango na malengo ya Baba wa Mbinguni. Kuwa tu mfuasi wa Kristo ni chanzo kikuu cha unyenyekevu, lakini tunaposikia maombi yake kwa ajili yetu katika Yohana 17, inatufanya kuwa wanyenyekevu zaidi. Kristo alituonyesha njia ya kufuata, mfano sio tu kwa maisha yetu wenyewe, bali pia jinsi tunapaswa kuwatendea na kuwaheshimu ndugu na dada zetu katika Kristo. Katika Yohana 17, katika dakika za mwisho kabisa za maisha ya Yesu duniani, tunagundua mtazamo wa maombi, uliojaa hamu kwamba Baba wa Mbinguni angeweka ndani yetu yote ambayo Yesu alikuwa nayo. Yesu alichotaka kwa wanafunzi wake kumi na wawili—na anachotaka kwetu leo—ni kwamba tujazwe na Roho wake Mtakatifu, ili tuwe mashahidi wake. Tupo hapa duniani ili kutiana moyo na kuombeana. Tena na tena, katika Yohana 17, tunamwona Yesu akiwaombea wanafunzi wake,  wakijua jinsi ambavyo wangetumiwa kwa ajili ya Ufalme wa Mungu baada ya kuondoka kwake. Hakuwaombea tu wanafunzi wake, bali pia wale ambao wangeguswa na Habari Njema wangehubiri na kuishi mbele yao. 

Oh, kama tungeweza kufahamu uwezo wa kuwaombea wanafunzi wetu na kwa vizazi ambavyo maombi hayo yanaweza kufikia! Ninashangaa, hata katika maisha yangu mwenyewe, ni mara ngapi ninafikiria juu ya faidi hii ya kizazi. Wanafunzi ambao Bwana amenipa neema ya kusaidia, kutia moyo, na kuandamana… ni wangapi wataguswa nao kupitia nguvu za Roho Mtakatifu? Ni ajabu kufikiria juu ya suala la vizazi. Kadiri tunavyozeeka, ndivyo vizazi vingi tunavyoweza kugusa, au angalau, ambavyo vinaweza kuwa sala yetu. Yesu aliwaombea wanafunzi wake. Ushindi wa namna gani! Ombi lake lilikuwa kwamba sote tuunganishwe katika moyo mmoja na akili moja na Kristo. Kuunganishwa na wanafunzi wetu, tunaposhiriki, kuwatia moyo, kugusa maisha yao, na kumruhusu Mungu awaumbe wao wenyewe wawe wafanya-wanafunzi… na kuzidisha kunaendelea na kuendelea. Katika Yohana 17, moyo wa Kristo uliwekwa katika kuwaombea wanafunzi wake. Kuna nguvu iliyoje katika maombi!Tusijiepushe na fursa hii ya kuwaombea wanafunzi wetu. Tuombeane, tuombe Mungu atimize mapenzi yake, hata baada ya muda mrefu tutakapo toweka. 

Na mfano huu uendelee kubeba ujumbe wa Habari Njema ya Yesu Kristo. Oh, kama tungeweza kuwa na moyo huu! Ikiwa tungeweza kubarikiwa kujua kwamba Bwana husikia maombi yetu na kwamba wanafunzi wetu wanabadilishwa kwa hiyo. Ni baraka ya namna gani, ni fursa ya namna gani, kwamba Kristo alitupa mfano huu katika Yohana 17 kwa huduma yenye matunda: kuwekeza kwa wanafunzi wetu, na huanza na maombi. 

Ilikuwa neno la kutia moyo kwa wapandaji wa makanisa. 

Bwana akubariki unapowaombea wanafunzi wako. Je, ni pamoja na wanani, utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Uwe mwema kwa wanafunzi wako


      Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama''ongezeka'' ni podikasti inayoleta  neno la kutia moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Tunapowatazama viongozi, mara nyingi tunaona aina mbili: wale wanaowatumia wengine kuendeleza kazi zao, mamlaka, na madaraka, na wale wanaowatia moyo wengine kwa kufanya kazi pamoja kufikia malengo. Ulimwenguni, tunatarajia kupata viongozi wanaotumia fursa ya walio chini yao. 

Lakini daima ni uzuni kugundua viongozi wanyanyasaji ndani ya kanisa. Hata hivyo, ni lazima tutambue kwamba baadhi ya viongozi wa Kikristo hutumia watu kujiendeleza badala ya kutumikia na kuunga mkono ukuaji wao. Yesu alituonya kuhusu viongozi hao. Siku moja, alipowaona wanafunzi wake wakigombania mamlaka, aliwaambia, “Mnajua ya kuwa watawala wa mataifa hutenda kwa mamlaka, na wakubwa wao huwatumikisha; haitakuwa hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkubwa kati yenu lazima awe mtumishi wa wengine, na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza lazima awe mtumwa wenu, kama Mwana wa Adamu, ambaye hakuja kutumikiwa bali kutumikia na kutoa uhai wake uwe fidia ya wengi.” Ni nini kinachoweza kuwa wazi zaidi? Yesu anatarajia wanafunzi wake wawaongoze wengine, kama vile yeye alivyowaongoza.

Yesu alikuwa mwalimu mkuu; alitumia muda mwingi kuwafundisha wanafunzi wake. Yesu alikuwa mpangaji mkuu. Alipanga huduma yake na ya wanafunzi wake. Yesu alionyesha nguvu za kiroho kwa kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Lakini yote haya yalifanyika kwa wema. Kumbuka maneno ya Yesu: Aliwaambia wanafunzi wake, kwa maneno yenye kujaa upole zaidi, "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi." 

Kama wafanya wanafunzi, tunawaita wanafunzi wetu kuishi kwa viwango vya juu. Tunawatarajia kwao watubu njia zao potovu. Tunawatarajia wafanye kazi kwa bidii katika huduma yao kwa Kristo na kanisa lake. Tunatarajia wasamehe wengine wanapokosewa. Tunatazamia wanafunzi wetu watoe wakati kwa maombi, kufunga, na kujifunza Neno la Mungu. Tunawaita wanafunzi wetu kuishi kwa viwango vya juu. Lakini hii haimaanishi kwamba tunapaswa kuwa wakali kwao. Yesu alisema, “Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo'' Yesu anatoa pumziko kwa ajili ya roho za wafuasi wake. Vipi kuhusu wewe? Je, wafuasi wako wanakujua kama mwanamume au mwanamke mkarimu au mkali? Unapowaita wafuasi wako kufanya kazi kwa bidii, je, unahakikisha pia kuwapa muda wa kupumzika na kuongeza nguvu? Wakati tabia zao zinahitaji kurekebishwa, je, unakumbuka pia kuwapa maneno ya kutia moyo na matumaini? Unaweza kuwa mkarimu na bado ukawa kiongozi hodari. Unaweza kuwa mkarimu na bado ukatimiza mambo makubwa. Roho Mtakatifu anataka kukusaidia. Kwa hivyo, neno langu la kutia moyo leo ni: “Enendeni katika Roho ; dhihirisha matunda ya wema. Usiwatawale wanafunzi wako, bali watumikie kwa wema. Kwa kufanya hivyo, Mungu atatukuzwa, wanafunzi wako watatiwa nguvu, na kwa pamoja mtatimiza mambo makuu.


Ilikuwa ''Ongezeka''na mimi ni Dean Davis nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...