Jumatano, 25 Machi 2026

MIFANO YA KIBIBLIA KUHUSU WATU WA AMANI

 










     Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Wakati nilipoanza kupanda makanisa katika miaka ya 1980, nilikuwa bado kusikia neno  ''mtu wa amani'', hata na rafiki zangu nao pia. Tulijifunza Luka 10:1-10, pale ambapo Bwana wetu Yesu anafundisha wamitume wake 72 kutafuta watu wa amani.

Lakini, hatukuwai kusisitiza juu ya fundisho kubwa linalohusu kifungu hiki;

Kuko wanaume na wanawake, kwa eneo nyingi, waliyo tayarishwa na Mungu ili wapokee injili na kuwapokea wale wanaotangaza Habari njema. Mutafute hawa wanaume na hawa wanawake. Mukae pamoja nao wakati wote munao tangaza ufalme wa Mungu.

Moja ya hadisi za Biblia zinazovutia zaidi zinazohusu mtu wa amani, ni ile inayohadisia kukutana kwa Yesu na mwanamuke Msamaria kwenye kisima. (Yohana 4:1-43). Yesu alikutana na mwanamuke Msamaria aliyekuwa na sifa mbaya. Lakini alikuwa na kiu ya kumjuwa Mungu. Wakati aliposikia Habari njema, alitangaza habari kwa mji wote. Bwana wetu Yesu alibaki siku mbili pamoja na waamini wa Samaria mbele ya kuendelea na huduma yake Galilaya.

Baada ya ufufuko wa Yesu na ujio wa Roho Mtakatifu kwa wanaume na wanawake waliokusanyika kwenye mzunguuko wa ndani, wamitume walikawia kufanya mafundisho ya kutafuta watu wa amani. Hakika, waliendelesha kanisa lao pa Yerusalemu na wakatangaza Habari njema ya ufalme wa Mungu. Lakini wamitume hawakutafuta watu wa amani inje ya mji. Ilibidi miujiza mingi itendeke ili hiyo ifanyike.

Petro alimpata mtu wa amani aitwaye Kornelio. Hadisi ya kukutana kwao inapatikana katika Matendo ya Mitume, sura 10. Kornelio alikuwa kasisi wa jeshi la kirumi. Kupitiya ujuzi wake, petro hakupenda kabisa kushirikiana na Warumi.

Lakini Mungu alimuelewesha kiwazi katika ndoto kwamba angestahili kwenda kumuona Kornelio. Akampata mtu mwenye sifa njema, aliye na kiu ya kumjuwa Mungu. Kornelio alikusanya majirani na rafiki zake ili wasikie mafundisho ya Petro. Wakati Petro akihadisia hadisi ya Yesu na kueleza unabii wa Agano la kale kumuhusu, Roho Mtakatifu akawashukia hata na kwa wapagni ! Petro akabatiza walio amini na kubaki nao kwa mda wa siku chache.

Mumeona njia ? Mungu anatayarisha watu kupokea injili. Anawapa kiu ya kumjuwa. Waamini wanapokea ujumbe wa Yesu, ujumbe wa mpango kabambi wa Mungu ili kuokowa ulimwengu ulio vunjika. Wakati watu wa amani wanasikia Habari njema, wanaipokea. Wanakuwa na kiu ya kuijuwa zaidi. Hawachungi injili kwa ajili yao wenyewe ; wana alika rafiki zao kuisikiliza. Waamini wanao tangaza Habari njema wanabaki na waamini wapya kwa kujenga imani yao. Kuko watu wa amani ambao Mungu anataka mukutane nao. Kuko watu wanao ishi karibu yenu na wako na kiu ya kumjuwa Mungu. Muwaombee. Muwatafute. Muombe pamoja nao. Mugawe Habari njema pamoja nao. Mubakiye nao. Muwaambiye kuhusu Yesu kwa majirani na rafiki zao.

Ndiyo ! Kuko watu wa amani ambao Mungu anataka mukutane nao.

Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Jumanne, 24 Machi 2026

MTU WA AMANI NI NANI ?


 











Karibu kwenye ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji na wasimamizi wa makanisa. 

Mimi ni Brad Snowden, na leo, napendelea kuzungumzia kifungu cha maandiki cha muhimu.

Luka 10:5-6 "[5]Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; 

[6]na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu. 

Kifungu hiki kinaonyesha vizuri sana , maana ya kukutana na ''mtu wa amani'' kwa kufika kwa Kijiji kipya. Ni muhimu kukutana na watu wenye moyo mwema na walio wazi, sababu ukarimu wao unakuza  mahusiano ya kina. Wakati mtu anakupokea, ana mwelekeo zaidi wa kuwa msikivu na tayari kwa kusikia ushuhuda wako. Ufunguzi huu unaruhusu Mungu kuanza kazi yake ndani ya maisha yao, kisha ndani ya jamaa zao, na kwa mwisho kutoa fursa kwa Kijiji chote kusikia Habari njema ya Yesu -Kristo.

Baba yangu mukwe alipenda kuhadisia hadisi moja ya wakati 

Kampuni za kukata miti zilielea miti juu ya mito. Mara nyingi, gogo lilikwama kwenye mwamba au kisiki, na kuzuwia bingine byote. Alizowea kuiita ''gogo fungulo '', alikuwa akisema kwamba wachungaji, maana yake wapandaji wa makanisa, ni wale ambao wangestahili kutafuta hili ''gogo fungulo '' na kulifanyia kazi ili kulifunguwa, na kuruhusu hivo wengine wote kushuka juu ya mto bila msongamano. Kwa namna hii, mtu wa amani anaweza kuwa kama hili gogo fungulo : 

mtu ambaye ushawishi wake unaweza kubadilisha mazingira ya kijiji kizima.

Mara nyingi katika utafutaji wetu wa matokeo ya kuvutia, tunasahau mtu huyo wa muhimu anayefanya kila kitu kiwezekane. Mtu wa amani ni muhimu zaidi ili kazi ya Mungu ifanyike ;  tuombe ili Bwana atayarishe roho hizo ziweze kupokea wapandaji wa makanisa. Ni Roho Mtakatifu peke yake tu, anaweza tayarisha roho na mioyo ya wale waliochaguliwa kwa kazi hiyo, kwa nafasi nzuri na kwa mda mzuri. Mtu wa amani ni yule anayefungula mlango wa kiroho kwa Kijiji na kandokando.

Tuombe Bwana wa mavuno atufunulie ni akina nani hao ''watu wa amani'' katika kila jamii na namna gani anatarajia kuwatumikisha.

Ujumbe huu ulikuwa chimbuko la kutiya moyo wasimamizi wa upandaji wa makanisa katika vijiji 

Ni pamoja na wanani utagawanya nao leo ?

Mungu awabariki sana.

Jumatano, 11 Machi 2026

RAMANI YAKO YA MAWASILIANO

 








       Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama "ongezeka" ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Hatujuwe habari zaidi inayo muhusu Mtume wa Yesu aitwaye Nathanaeli.

Lakini kitu kimoja ni kweli : iko na deni ya kumshukuru Mtume mwengine Filipo. Sikiliza Yohana 1:44-49 :"Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. 

Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. 

Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. 

Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.

Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. 

Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli." Amini ao usiamini, Nathanaeli hakujuwa la kufanya, alikuwa na mawazo mabaya zidi ya watu wa Nazareti, siyo wanazareti tu pengine hata pia na mkowa mzima wa Galilaya. Hakufikiri kwamba mtu mwema wala mawazo mazuri yanaweza kutokea Nazareti. Lakini rafiki yake Filipo alimuona Nathanaeli na kumshuhudia Yesu. Alikazia kwamba Yesu alikuwa Masiya ambaye Musa na Manabii walisema. Na, kitu cha kushangaza, ijapokuwa mawazo yake mabaya, wakati Filipo aliposema tu : ''njoo uone'', Nathanaeli akakutana na Yesu na akamjuwa kama Mwana wa Mungu. Ni urafiki gani uliyokuwepo kati ya Filipo na Nathanaël ? Walikuwa wandugu? Walikuwa wanaungana kwa kiapo? Wala walikuwa tu marafiki wazuri? Hatujuwe. Lakini ni wazi kwamba, walikaribiana sana, sababu Nathanaeli alikuwa mtu wa kwanza miongoni mwa watu ambao Filipo alisema baada ya kukutana kwake na Yesu. Filipo alifurahia wazo ya kukutana na Masiya ambaye wangestahili kugawana Habari njema. Akamwambia Nathanaeli, rafiki wa karibu. Uko na urafiki mzuri na mtu yeyote. Uko na Habari njema ya kumwambia, unamjuwa Yesu Masiya. Unajuwa kama ni Mwokozi wa ulimwengu. Unajuwa kama anatusamea dhambi, anatupa nguvu na anatupa uzima wa milele kwa wingi.

Sasa, andika ramani ya mawasiliano.

Chora kiviringo katikati ya karatasi na uandike ndani yake jina lako. Baadaye, chora mistari inayo unganisha kiviringo chako na majina ya marafiki na watu wakaribu yako ambao unajuwa wako mbali na Mungu. Kata mistari kwenye majina yao na marafiki zao na watu wa jamaa zao ambao nao pia wako mbali na Mungu. Utapata sasa ramani ya mawasiliano. Omba kwa ajili ya kila mtu aliye kwenye ramani yako. Baadaye, tarajia kwenda kuwaona ili kugawanya nao ushuhuda na Habari njema ya Yesu. Nani anajuwa? Kwa kwenda kuwaona, marafiki zako wanaweza kukushangaza. Wanaweza kuitikia mwito wa Yesu kama imani ile ile ya Nathanaeli wakati Filipo alipo muongoza kwa Bwana imepita sasa miaka mingi.

Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Jumatano, 4 Machi 2026

Maendeleo ya Uongozi - Tabia ine za viongozi wanao jitokeza

  

      Mimi ni Chuck Rapp na ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji na waongozi wao.

Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Katika toleo langu la tarehe 23 Januari, nilielewa na kuwapa moyo viongozi kuwa waangalifu sana na watu wakaribu na kuchunguza pamoja na kufundisha viongozi wapya.

Leo, na katika vipindi vijavyo, natarajia kugawa mawazo mamoja kuhusu mwenendo ninao utafuta kwa viongozi wa baadaye. Pengine muko na tabia zingine ambazo munaendelea kutekeleza : ikiwa hivo, usisite kunijulisha. Nazingatiya pia kuonyesha kwamba ni mawazo na uchunguzi wangu binafsi. Wengine wanaweza kuwa na mawazo tofauti. Horoza hii haitoshi ; naamini kwamba kuko tabia zingine muhimu kwa viongozi wanaokuja. Ya kwanza, napata utambulisho wa kibinafsi unaopata mizizi katika Kristo. Wakolosai 3:3 inasema "Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.'' nafurahia matumizi ya neno '' kufichwa '' ya Mtume Paulo, sababu kiini cha kweli cha maisha ya mwamini iko ndani ya usalama na ulinzi wake katika Kristo.

Umenisikia pengine nikikazia katika podikasti zangu za mbele kuwa moja ya matokeo ya hatari sana ni ile ya mtu kuwa kwenye mstari wa uongozi kisha anakosa kujiamini. Kwa hatuwa tofauti, kiongozi ambaye usalama wake uko na mizizi ndani ya Kristo yuko na uaminifu ndani ya Bwana anaye muruhusu kutumikia wengine. Wafiliipi 2:4 inatufundisha kwamba ''Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.''  kwa hisia hii ya utambulisho wakibinafsi wenye mizizi ndani ya Kristo kunaongezeka unyenyekevu.

Ni tabia inayo jionyesha katika utumishi wa kutafuta faida kwa wengine.

Sikubaliani na wale wanao onyesha mwenendo wa kujinyanguwa ''kama watu maarufu''. Katika tafsiri ya J.B. Philips, tunasoma haya katika Warumi 12:3 . Mimi kama mwongozi wenu wa kiroho, ninawapa shauri hili :Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. Shauri gani kubwa namna hii! ''Msijidanganye kwa kunia makubwa, lakini mujitaidi kuwa na uhakika wa uwezo  wenu... Ni shauri gani kubwa namna hii! ''Msijidanganye kwa kunia makubwa, lakini mujitaidi kuwa na uhakika wa uwezo  wenu.'' Chuck Colson, kiongozi mkubwa katika maisha yangu, alizoeya kusema hivi : "anaye tarajia kuwa kiongozi akijizania kuwa ubinafsi wake unaenea tayari atashindwa.'' imenichukuwa miaka mingi kwa kuelewa somo hili muhimu.

Nitaendelesha mawazo yangu juu ya tabia za kutafuta kwa viongozi wabaadaye katika podikasti yangu itakayofuata.

Hii ni ujumbe wa kutiya moyo kwa wapandaji na viongozi wa makanisa katika vijiji.

WAZO Z. MPANGO WA MUNGU KWA MKOWA WANGU

 










     Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Tunajuwa kama wazo Z inamaanisha kuanzia Ku mwisho. Tunaelewa pia kuwa ''wazo Z'' inamaana kuwazia kwa upekee kwa mambo ya baadaye ambayo Mungu alitayarishia ulimwengu. Tunawazia hivo ili kujiunga kwa Mungu, kama wafanyakazi pamoja na Kristo, ili kutekeleza mipango yake duniani. Tunajuwa kwamba Mungu hapendi hata moja apotee, bali wote waifikie toba. Mungu ni mvumilivu kwetu. Ndiyo maana bado Yesu hajarudi duniani. Ni kutokana na upendo  wa uvumilivu wa Mungu, hukumu ya mwisho haijakuwa (2Petro 3:4-10). Tofauti na hayo, Mungu anaita watu wote, mahali pote, kutubu na kuamini Habari njema (Matendo ya Mitume 17:30-31). Lakini jukumu langu ni nini katika huu mpango? Najuwa kama Mungu iko na mpango kwa ajili ya dunia nzima, sasa ni mpango wake gani kwa mji, mkowa, idara langu, ao Taifa langu ? 

Wanafunzi wengi waaminifu, wanao muheshimu Kristo, walijiuliza swali hili la muhimu. Pengine nawe pia. Kaka na dada, naweza kuwaakikishia kuwa, Mungu iko na mpango mkubwa kwa ajili ya ulimwengu, na anaitekeleza polepole Ila kwa uangalifu. Lakini iko na mpango gani kwa eneo ambako naishi ? Rafiki yangu, mpango wa Mungu kwa ajili ya mkowa ambamo unaishi ndani ni ule ule mpango wa Mungu kwa dunia nzima. Mungu anapenda kuwa watu wote wa mkowa wako wasikie na kuelewa habari njema. Anapenda kwamba kila mwanaume na kila mwanamuke, kila kijana na kila binti wa mkowa wako ajuwe Habari njema, atubu na kuweka tumaini lake kwa Kristo. Anapenda kama sote tufahamu neema yake ya wokovu ya mabadiliko ndani ya kanisa.

Ni namna gani sasa tunastahili kuomba? Maombi yetu yatasaidiwa na wazo Z. Tunapashwa kuomba kama vile Kristo alivyo tuamuru: "ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama mbinguni.'' (Mathayo 6:10). Tunastahili kuomba ili wapandaji wa makanisa na waamini wa makanisa wapande kanisa katika kila Kijiji cha mkowa. Tunastahili kutembea kwa maombi na kuhimiza waombaji, tukiwasaidia kuchaguwa wazo Z. Tuombe tukichunga moyoni mwetu mpango wa Mungu. Tutatumika namna gani ? Tunapashwa kutumika tukihakikisha kwamba makanisa safi yanajizidisha kwa haraka katika mkowa wetu, ili kwamba mipango ya Mungu itekelezwe duniani, yatekelezwe karibu yetu, miongoni mwa watu wanaosema lugha yetu na wanaoishi kandokando yetu. Ni nani tutamtuma? Tunapashwa kutuma watumishi, wengi katika mkowa wetu hadi mwisho wa dunia. Tunapashwa kutuma watu wanaojuwa roho ya Mungu, watu wenye juhudi kutumika na kuomba kufuatana na wazo Z. Tunapashwa kutuma watumishi waliyo jiandaa kutangaza habari njema ya Yesu, kufanya wanafunzi na kupanda makanisa safi yanayokomaa. Kaka na dada, tuchaguwe wazo Z katika yote tunayotenda, tukiwa na uaminifu kwa Mungu kwa ajili ya utawala wake ujao na ili kwamba mapenzi yake yafanyike duniani kama mbinguni.

Ilikuwa "Ongezeka" na mimi Dean Davis.

Nawauliza : "ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

SABABU GANI KUPANDA MAKANISA ? Sehemu ya 2

 










      Jambo na karibu kwenye ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji na viongozi wa makanisa katika vijiji, wachungaji na viongozi wakikristo.

Mimi ni muhamasishaji wenu Daneille Snowden. Nafurahia kugawanaya nanyi leo, ao kukazia maono ambayo Mungu ametowa kwa One Mission Society kwa ajili ya upandaji wa makanisa katika vijiji ; kupanda kanisa katika kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2050. Ni maono makubwa sana ambayo tumepewa na Bwana wetu Yesu mwenyewe, wakati aliposema :"Enendeni, mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu... '' (Mathayo 28.19-20). Mimi na mume wangu tuligunduwa upandaji wa makanisa katika vijiji pa Mozambique.

Usomi na shuhuda tulizo zisikia zilitugusa sana. Zaidi ya mwaka moja baadaye, Mungu alituita kutumika kama wamisheni ndani ya huduma ya CMF kwenye vuguvugu hili kubwa.

Tukiwa wanafunzi wa Yesu-Kristo, tunafuata mfana wake, kama inavyosemwa katika Mathayo 9:35 :"Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.''

Yesu alikuwa akizunguka katika miji na vijiji ! Wengine watajiuliza pengine wapi wataanzia kulingana na kazi hii iliyo kubwa mno. Jibu ni rahisi : kufuata Yesu, kutafuta uwepo wake, kungojea ukiwa ndani, na zaidi, kufuata mfano wake. Kwa hiyo, tunapashwa kuwa waangalifu sana na kuelewa vizuri Agizo kubwa. Pamoja na maono, Mungu anatupa mpango ! VCP inatuonyesha mfano wa Shamba ine, mpango uliyo ndondolewa ukieleza namna gani kuingia kwenye maono haya.

Shamba la 1 ni sehemu zabiti ya  mpango ; inahusisha maombi mengi, hata na maombi ukiwa ukitembea ukiwa na ramani na Biblia ; vyombo viwili kwa ajili ya kuendelesha maono.

William Carey, Mmisheni wa karne ya XVIIIe, aliandika :"kwa kujuwa mapenzi ya Mungu, tunaitaji Biblia na ramani vilivyo funguliwa ''. Ninawaalika leo kuchunga sana maono haya iliyo rohoni mwako, na moyoni mwako na nafsini mwako.

Habakuki 2:2 inatuambia : ''BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.''

Tujulishe mapenzi ya kweli ya Mungu ya kwamba watu wote waokolewe!

Ilikuwa ''ongezeka''.

Usisahau kugawanya podikasti hii pamoja na kaka na dada ndani ya Kristo na viongozi wenu wakikristo !

Enendeni, mkawafanye wanafunzi !

WAZO Z MPANGO WA MUNGU JUU YA ULIMWENGU

 










     Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama "ongezeka", ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Watu wengi walisema :"anza ukifikiria mwisho kichwani." Wajengaji wanaanza na mwisho kichwani mwao wakati wanapojenga nyumba.

Ata mbele ya kuondowa udongo sababu ya kujenga msingi wa nyumba mpya, mjengaji hodari anajuwa urefu na upana bitakuwa namna gani.

Anajuwa hesabu ya vyumba atakuwa navyo na nyumba itakuwa na urefu gani.

Mbele ya kuweka jiwe la kwanza la msingi, iko tayari rohoni mwake na picha ya namna itakavyokuwa nyumba ikimalizika kujengwa.

Wajengaji wenye hekima wanaanza na mwisho kichwani mwao. Yote wanayojenga, kuanza msingi hadi dari, yanawekwa tayari ili kufikia lengo lao la mwisho : "nyumba nzuri."

Ninyi kama wapandaji wa makanisa, nanyi pia mungestahili kuanza na mwisho kichwani.

Mungeuliza Bwana : "kanisa hili litakuwa la namna gani? Bwana, namna gani tutakuabudu? Tutatumikisha lugha gani?

Namna gani tutatowa injili? Tutafanya namna gani ili kufundisha wanafunzi ? Bwana, ni kwa namna gani kanisa hili litaonyesha upendo wako kwa jirani zetu?"

Kama wajengaji wa nyumba, wapandaji wa makanisa wanapashwa kuwa na picha ya wazi ya namna kanisa litakuwa. Na mpango huo utatoka kwa Mungu.

Lakini haitoshi kuwa tu na mpango mzuri kwa hiyo, ni kwa neema ya Mungu, ndivyo kanisa letu litakuwa.

Tunamtumikia Mungu aliye hai. Na iko na mpango kuhusu dunia yetu. Anajuwa anachokipenda, na alituambia kile anachokipenda kuhusu ulimwengu:

Hapendi hata moja apotee, bali wote waifikie toba (2Petro 3:9).

Anasema kwamba ujuzi wa utukufu wa Bwana utaijaza inchi, kama maji iijazavyo Bahari (Habakuki 2:14)

Anatayarisha siku ambayo mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wata muabudu (Ufunuo 7:9).

Ndivyo Mungu anavyopenda, na tungestahili kupenda hivo pia.

Herufi ya mwisho ya Alfabeti ya kirumi ni Z, inayoitwa Zed _ ao, kama inavyoitwa katika inchi yangu, Zii. Wakati tunapoanza na mwisho kichwani, tunatumia wazo Z. Wazo Z inamaanisha kwamba tunatarajia mda ujao ambao Mungu anatarajia sisi tujiunge kwake ili kutumika ili kwamba malengo yake yageuke kwa matendo.

Katika upandaji wa makanisa katika vijiji, maono yetu ni kuwa na kanisa katika kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2050.

Waundaji wa VCP walikubali maono hayo sababu walipendelea kukubaliana na mpango wa Mungu kwa ajili ya uumbaji wake.

Walijuwa kama Mungu anapenda inchi ijae ujuzi wa utukufu wa Bwana, kama vile maji iijazavyo Bahari.

Walijuwa kama Mungu hapendi hata moja apotee, bali wote waifikie toba. Walijuwa kama ni mapenzi ya Mungu, ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. (Wakolosai 1:28).

Ndiyo maana walichaguwa kumjulisha Kristo kwa kupanda makanisa katika vijiji ambavyo hakuna makanisa. Walitumikisha wazo Z. Mbele ya yote, walielewa mapenzi ya Mungu kwa uumbaji wake. Baadaye, walichaguwa kujiunga kwake ili kutekeleza maono yake ya mwisho.

Wewe pia, uko miongoni mwa VCP. Nategemea kwamba utaambatana na maono haya ya kuwa na kanisa katika kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2050. Funga macho yako kwa mda mchache na ufikirie kanisa katika kila Kijiji. Fikiria hivo kwa uwazi, ili maono yageuke kuwa matendo. Kisha usimame na ufanye yanayokuhusu ili kuiweka katika vitendo!

Ilikuwa "ongezeka", na mimi ni Dean Davis, nawauliza : " ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

KWA NINI KUPANDA MAKANISA?

 









    Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Wamoja walisema : "hakuna amri ndani ya Biblia inayo tu amuru kupanda makanisa. Sababu gani kupoteza nguvu na wakati katika upandaji wa makanisa ?"

Hakikisha ambayo inasema kwa wazi hakuna amri ya Biblia : "Enendeni mukapande makanisa !" Ni kweli. Lakini hakikisho hiyo inadanganya. Wakati Mitume waliposikia amri ya Yesu inayosemwa katika Mathayo 28:19-20, iliyotolewa wakati alipopaa, mbele kidogo ya Pentekoste, waliweka neno lake katika vitendo kwa kupanda makanisa. Walipanda kanisa lao la kwanza pa Yerusalemu. Baadaye, kuanza hapo, waliendelea na upandaji wa makanisa katika Uyahudi, Samaria na mwisho wa dunia, vile vile kama alivyo amuri.

Wakati tunapopanda makanisa, tunafuata mfano wa Mitume wa Yesu.

Amri kubwa inapata msingi wake katika Agizo kuu : mpende Mungu na umpende jirani yako. Wito wa Yesu wa kumpenda jirani yako kama nafsi yako mwenyewe ni msingi wa mafundisho ya wanafunzi kupitiya upandaji wa makanisa. Roho ya wapandaji wengi wa makanisa inajaa upendo kwa wale wasio bado kumjuwa Kristo. Mfano wako uko je?

Tunapanda makanisa sababu upendo wa Mungu unatushurutisha. Tunapendelea wengi, siyo wachache, wapatane na Mungu. Wawe na uzoefu wa maisha tele ndani ya Kristo, wajuwe Mchungaji Mwema, waishi na uhakikisho na tumaini tele. Ndiyo sababu tunapanda makanisa.

Tunatarajia pia kwa mabadiliko, kwa ukombozi, kwa amani na maelewano. Tunajuwa kama Mungu pekee anaweza leta ukombozi.

Tunajuwa kama Yesu peke yake anaweza kujibu maitaji makubwa ya jirani zetu. Lakini tunajuwa pia kwamba jamii ni wazo kutoka kwa Mungu na iko miongoni mwa mpango wake mkubwa wa kubariki dunia. Alimuongoza Adamu kwenye baraka wakati aliposema : "si vema huyu mtu awe peke yake." Hiyo inaambatana bila shaka na ndoa, lakini pia kwa mitindo mingine ya jamii, kama kanisa.

Tunapanda makanisa sababu tunapenda baraka, wakati wanafunzi wa Yesu wanajiunga pamoja kwa imani, wakati wanapo kusanyika kwa wazo moja, wakati wanajinyenyekesha pamoja kwa Uungu wa Kristo. Watu wengi katika Bara la Afrika, Esia, Ulaya na Marekani, wanao onja ushirika wa ndugu na itaji la kuwa ndani ya kanisa takatifu, wanasela : "sijawai bado kuona upendo kama huu ndani ya jamaa yangu. Kanisa hili ni baraka za ajabu kwangu!" Kwa hiyo, tunapanda makanisa sababu tunapenda watu wawe na uzoefu wa jamii la kweli, mahali ambako wanatembea nuruni, kama Yesu alivyo nuruni, na mahali wanapoishi ushirika uletao uzima.

Sababu gani tunapanda makanisa ? Haya yote ni swali la upendo. Tunafuata mfano wa Yesu, aliyetupenda na kujitowa mwenyewe kwa ajili yetu. Unapoanza kupanda makanisa, usiache. Hata kama ulisha panda makanisa mingi, usiache. Upandaji wa makanisa, ni upendo katika vitendo.

Ilikuwa "Ongezeka" na mimi Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao neno hili la kutiya moyo ?


Maendeleo ya Uongozi - Tunatarajia kusema nini kuhusu neno ''Uongozi''?

 










   Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Leo natarajia kuanza kwa kuzungumzia mafundisho mamoja ya msingi kuhusu uongozi... Ambayo nawaza ni ya muhimu zaidi wala isiwe ya muhimu.

Kwa miaka 33 iliyopita, nilichaguwa tafsiri ya Uongozi ifuatayo, ambayo nilichangiya na Mwalimu wa shule la juma pili ambaye nilikutana naye kwa miaka yetu iliyopita katika inchi ya Ubeljiji. Alikuwa akionyesha mtazamo wa kijeshi na wa Biblia ya Kikristo wakati alipokuwa akitufundisha juu ya Uongozi.

Uongozi ni uwezo wa kushawishi watu juu ya uaminifu usiogeuka kuhusu amri za Mungu.

_ Jemadari Kanali Gene Klann, OTAN, wa 1993 nafurahia uwazi na upole wa tafsiri hii.

_ uongozi unahusu zaidi ushawishi zidi ya nguvu ao mamlaka.

_ Viongozi wachaMungu hawapashwi kugeuka katika uaminifu wao kwa Mungu. Watu watachaguwa kutokufuata wale walio wanafiki.

_ Msingi wa uongozi wetu unastahili kuwa uwaminifu kwa Neno la Mungu na kwa mafundisho ya Roho - Mtakatifu.

Angalia mtazamo mwengine unaoshikamana vizuri kwa viongozi wanao muheshimu Kristo. Unatokana na Daktari Robert Clinton.

Kiongozi ni mtu aliye na :

Majukumu aliyopewa na Mungu ya kushawishi kundi fulani la watu wa Mungu kwa kusudi ya kutekeleza mipango ya Mungu kwa lile kundi.

Nafurahia uwazi wake.

- uwezo wa kiongozi unatoka kwa Mungu (tutairudilia baadaye kidogo)

- Uongozi ni majukumu tuliyopewa na Bwana Mungu (tutairudilia pia baadaye)

- Uongozi unahusu ushawishi bali siyo woga

- Viongozi wanaongoza makundi za watu kwa lengo ya kufikia mipango ya Mungu , hii inaambatana na mtazamo wetu wa mwaka jana kuhusu kiongozi muwakili kama ''mtu anayeongoza raslimali zilizo za mtu mwengine kwa kusudi ya kufikia malengo ya mwenye mali ''.

Bado ningali na maoni ya kugawanya nanyi leo.

Uongozi ni karama ya kiroho. Katika warumi 12 :8, Paulo anaandika kuhusu karama za kiroho na anadai ya kwamba :''mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.''

Uongozi pia ni wito. Matendo ya Mitime 13:2 inaonyesha uzoefu wa Sauli kwa Barnaba :

''Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.''

Watu hawa wawili waliitwa kuwa viongozi ndani ya kanisa la kwanza, na Mungu anaendelea hata leo kuita na kuomba viongozi.

Je! Tunaweza kuwa wazi na kupokea wito kwa karama za Mungu ndani ya maisha yetu.

Je! Tunaweza kuwa waangalifu kwa wale wanaotuzunguka, kwa kuwa waangalifu ili kuchunguza na kufundisha viongozi wapya.


Hii ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakristo katika vijiji.

Maendeleo ya Uongozi - Utangulizi wa Mtiririko wetu wa 2026


     Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wa kikristo katika vijiji.

Mada yetu katika mwaka wa 2025 ilikuwa uwakili wa uongozi, na leo tumeanza mwaka mpya wa 2026 na mtiririko unaohusu maendeleo ya Uongozi. Mada ya mwaka huu inatokana na maongezi niliyokuwa nayo kwa mwanzo wa Disemba wakati wa shauri la ''coalition of the willing'' pa mji wa Lomé.

J.J, kiongozi wa kazi za ''coalition of the willing'' aliniuliza swali lifuatalo :

''Tufanye nini ili VCP izidishe maradufu kwa miaka mitano ijayo?''

Lilikuwa swali nzuri, ambalo nilifikiria kwa mda mchache.

Nawaza kwamba ni Bwana aliyenileta kwa haraka kwa kutekeleza kwamba tayari imezidisha maradufu kwa miaka mitano ya nyuma. Mbele ya COVID, VCP ilikuwa na vituo vya mafundisho 350 ndani ya inchi 19 ; leo , tunatumika ndani ya inchi 36 tukiwa karibu na vituo 900 vya mafundisho. Tunashukuru Mungu kwa ukuaji huo.

Kwa kurudilia swali la J.J, Bwana amenionyesha kuwa mipaka yetu siyo pesa. Bwana ameonyesha kwa mara nyingi akiba yake kwetu.

Naamini kwamba mipaka yetu kwa Sasa kwa ukuaji mkubwa zaidi unatokana na umuhimu wa kuchunguza, kusisimuwa, kuandaa na kuwaachilia viongozi.

Tuko na haja ya wakufunzi wengi, waratibu wengi, makasisi wengi wa VCP.

Tuko na haja ya warahisishaji wengi wa kuzidisha makanisa na watumishi wafazili katika inchi ya Marekani. Tuko na haja na wafundi wenye uzoefu katika Bara la Afrika, pamoja pia na wasimamizi wa miradi katika Afrika na Ulaya. Na kwa misingi ya hayo yote, tuko na haja zaidi  ya watu wenye kujitolea katika maombi.

Kutokana na hayo, katika mwaka wa 2026, mtiririko huu wa podikasti utahusika zaidi na Maendeleo ya Uongozi. Makasisi na waratibu, najielekeza kwenu kwa mda huu. Ninaitaji msaada wenu kwa kutafsiri na kugawa vipindi hivi kwa wale mnao waongoza.

Nawaomba pia kuwa waangalifu katika juhudi yenu kwa kuchunguza, kuandaa, kufundisha, kuachilia na kuacha huru viongozi wanaopanda viwango. Tazama kanuni moja muhimu ya kuzingatiya :

Wasimamizi, wakati bado hamujatayarisha mtu wa kukugombowa, hauwezi kulinganishwa kwa kupanda cheo. Narudilia : wasimamizi, wakati bado hamujatayarisha na kuchunguza mtu wa kukugombowa, hauwezi kupandishwa cheo ; ungali peke yako tu mwenye uzoefu wa kutumika kwa wazifa wako wa sasa.

Nitahitimisha kipindi hiki kwa maono ya Yesu kuhusu uongozi, ambayo inatokana na Mathayo 20:25-28. Kulingana na Mungu, viongozi wameitwa kutumikia wale mnao waongoza.

Yesu akawaita nakusema :

''Mathayo 20:25-28

[25]Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. 

[26]Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 

[27]na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; 

[28]kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.''

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wa kikristo katika vijiji

UONGOZI WA MUWAKILI - Thamani ya kasisi wa VCP, Claude


       Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wa kikristo katika vijiji.

Tunatoka kuitimisha mtiririkl wetu kuhusu uongozi wa uwakili (Steward Leader).

Leo, ningependelea kurudiliya podikasti moja imepita miaka 4 ambamo ndani yake nilizungumzia kuhusu thamani ya kasisi wa VCP, Claude.


1. Claude kwa kulinganisha maoni ya kila mutu.

Hafanyi tu yale anayo kusudia; kama kiongozi, anajuwa kama kila m'moja anahaja ya kusikilizwa na maoni yake yanastahili kuchukuliwa. Hiyo inanikumbusha Wafilipi 2:3-4

''Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. 

Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.''

viongozi bora, wanao ongozwa na Mungu, wanatafuta mchango wa watu wote na wanamuuliza Bwana wakati wanapokamata maamuzi.

Hatuwezi kumfurahisha kila mutu kwa kila maamuzi, lakini viongozi bora watahakikisha kama kila mtu alisikilizwa.


2. Claude yuko tayari kusaidia.

Thamani hiyo inajionyesha kwa hatuwa mbali mbali : kutowa mafundisho, shauri wala msaada kwa jukumu fulani. Alipangililia pia pesa ndani ya bajeti ya VCP kwa kusaidiya viongozi wamoja maarufu wakati wa shida ya kiafya wala msaada wa zarura. Claude anasaidiya wale anao waongoza kwa kuwakaribia mara kwa mara katika utumishi wao wa kihuduma na katika maitaji yao kazini. Viongozi bora, kulingana na Mungu, wanaitaji kusaidia wale anao waongoza.


3. Claude anajizoweza katika tabia zake. 

Wakati anatakiwa kujiheshimu na kutumika, Claude anakuwa wa kwanza kufika.

Kama ni mda wa kujifurahisha na kujipumzisha, anajuwa kuchukuwa mda huo pamoja na watu wote.

Kwa mfano anaongoza na kusaidia wengine kuelewa kile kinacho subiriwa katika kila tukio. Hiyo inanikumbusha maneno ya Mtume Paulo :

''Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.

(1Wakorintho 11:1). Hiyo inakazia pia umuhimu wa kushikilia usawa bora kati ya kazi na maisha ya kibinafsi.

Kama viongozi wanatumika bila kukoma, wanaweza kuchoka.


4. Kwa mwisho, Claude anapenda kuwapa wengine kile anacho kijuwa.

Hiyo inaweza kutendaka kupitiya mafundisho, ushauri ao kwa majadiliano. Anajadiliana na wengine ili kukuza uwezo wao ndani ya Uongozi kwa kiwango cha juu. Kristo alifuata mkondo huo : alichukuwa mda pamoja na wanafunzi na kuwaonyesha maisha yake na mafundisho yake. Mtindo huo ulitumika vizuri kwa Yesu, na unatumika hata leo kwa viongozi wachaMungu :Matendo ya Mitume 4:13 unasema :

''Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.''


Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...