Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.
Katika mwaka huu mpya, nilianzisha mtiririko mpya kuhusu Mada ya uongozi wa Mawakili. Mwandishi moja anatafsiri Mwakili ''kama ni mtu anayeongoza rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali'' katika mazingira yetu, tunaongoza rasilimali tulizopewa na Bwana kwa ajili ya kazi yetu ya upandaji wa makanisa katika vijiji.
Kifungu chetu katika podikasti ya leo ni Luka 13:6-9.
Yesu akahadisia hadisi hii: ''Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.
Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?
Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi;
nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate''.
Kwa kuanza kujifunza mfano huu, kitu cha kwanza nilicho jiuliza, ni '' ni myaka ngapi inayo chukuwa Mtini ili kuzaa matunda?''. Hii inaonekana kuwa swali lenye busara, kwa sasa, nimefanya utafiti wa haraka kwenye mtandao na nilipata mitandao mingi iliyoonyesha kwamba Mtini unazaa matunda baada ya myaka 3 ao 4.
Ni kweli! Muumba wa ulimwengu haijui hayo? (Tuone wakolosai 1:16)
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, ''mtu'' wa mfano wetu - anaye wakilisha Mungu - anangojea kwetu sisi kuzaa matunda kwa mda uliyopangwa. Na kwetu pia ni hivo ; anasubiri kwetu pamoja na huduma yetu - tuzae matunda wakati tunapofikia kiwango cha kukomaa wakati matunda yanasubiriwa.
Tulinganishe mazingira ambayo Mtini uliishi. Ulikuwa umepandwa kwenye udongo mzuri wa mzabibu. Jua na mvua vilikueko. Baada ya mwaka wa tatu, mtengenezaji wa divai alichimba Shimo kandokando ya mti na kuweka mbolea. Mti ulifaidika na mazingira yote yanayostahili kwa kuzaa matunda. Tazama mafundisho maalm ya huu mfano.
- Mungu anangojea matunda kwa mda unaotakika ; alitowa yote yafaayo ili kwamba matunda yazaliwe.
- uvumilivu na neema yake vinatoa mda zaidi kwa kuzaa, na anatutendea sote kwa namna moja
- kwa mwisho, kuko kuwajibika kwa ukosefu wa matunda.
Namaliza kwa ukumbusho wa 2Petro 1:3. ''Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe''.
Katika kipindi chetu cha kufuata, tutaendelea na somo letu juu ya uongozi wa Mawakili.
Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wakikristo katika vijiji.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni