Alhamisi, 10 Oktoba 2024

MWAMINI MUNGU KWA AJILI YA UPANDAJI WA MAKANISA MAPYA - Siku 90 za Maombi na Kufunga


 

Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Katika upandaji wa makanisa katika vijiji, tunakazia juu ya umuhimu wa makanisa yanayo panda makanisa mengine.

Kwa hiyo, kama huduma yetu haiitwe ''vijiji vya upandaji wa makanisa '', ingeitwa tu kwa urahisi ''upandaji wa makanisa mapya''. Lakini sehemu kubwa ya makanisa duniani leo wako na shida kubwa ya kupanda makanisa mapya. Makanisa mamoja yangefikia kusema kwamba haiwezekani kwao kuunda makanisa mapya kwa maeneo mapya. Lakini ni kwa nini ? Sababu gani ni vigumu zaidi kupanda makanisa mapya ? Ni vigumu sababu watu wanajiusisha zaidi na jamaa zao binafsi zidi ya mengine yote, majirani zao binafsi na vijiji vyao binafsi tofauti na watu wengine wanaoishi ndani ya vijiji vingine.

Upandaji wa makanisa mapya ni mgumu sababu watu wanapendelea kupanda makanisa yao binafsi pahali ya kuunda makanisa mapya.

Mara nyingi haja hii nzuri ya kupanda kanisa inatokana na sababu za ubinafsi.

Viongozi wanasema wanasema wao kwa wao : ''ninapenda zehebu langu liwe nguvu ili namimi niwe mwenye nguvu n'a mwenye usalama.'' umekwisha wai kutamka neno kama hilo?

Oh ndugu na dada yangu, Mungu atafanya, uwe hodari. Atakulinda hata itokee nguvu ya kanisa lako la mahali.

Upandaji wa makanisa mapya ni mgumu sababu inatahazari. Siyo wote watakaopanda makanisa yatakayoongoka wakati watakapojaribu. Kwa bahati mbaya, baazi ya watu wako na woga wakushindwa hadi wanashindwa kuchukuwa tahazari na hawajaribu kupanda kanisa mpya. Upandaji wa makanisa mapya ni mgumu sababu unagarama kubwa.

Inalomba pesa kwa ajili ya kusafiri kuelekea katika eneo mpya na kuanza kazi mpya. Inaitaji mda mwafaka kwa kwenda huko kwa Kijiji kingine ili kufundisha watu kutii yote aliyo yaamuru Bwana Yesu ; mda ambao ungetumikishwa kwa kuangalia mifugo, kufanya mambo mengine pamoja na jamaa zetu binafsi.Gharama ya fedha na gharama ya muda ya upandaji makanisa ni kubwa. Na upandaji kanisa hutuweka wazi kwa kukosolewa na wengine. Watu wengine hawawezi kustahimili kukosolewa. Kwa hiyo wakati kutaniko linapofikiri kuhusu matatizo na changamoto zote zinazohusiana na upandaji makanisa binti, mara nyingi wanajaribiwa kukata tamaa, kukaa nyumbani na kutumaini mema. Mawazo haya yenye sumu yanawezaje kushindwa? Je, ni dawa gani ya mawazo haya yote hasi? Njia pekee ya kupunguza sumu hii ni kutumia imani. Je, ni ghali kupanda makanisa? Ndiyo ni. Lakini Mungu atatoa. “Kumbuka hili: Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mmoja wenu atoe kile ambacho moyo wake umeamua kutoa, bila kusita wala kulazimishwa, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwabariki sana, ili katika mambo yote siku zote, mkiwa na kila kitu mnachohitaji, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema. ( 2 Wakorintho 9:6-8 ). Je, ni hatari kupanda makanisa? Ndiyo ni. Hakuna uhakika kwamba utaifanikisha. Lakini Mungu atakuwa pamoja nawe, atakomboa juhudi zako zote. Kwa hivyo chochea imani yako. Changamsha imani ya wanafunzi wako na kanisa lako zima. Huwasaidia kutazama tu changamoto lakini kuzingatia wema wa Mungu Baba yetu wa Mbinguni. Aliahidi kutotuacha wala kutuacha kamwe.

Wasaidie kumtazamia Bwana ambaye ameahidi kufanya bila kikomo, kwa wingi, zaidi ya yote unayoweza kuuliza au kutafakari. Jenga imani ya watu wako; mwamini Mungu kwa ajili ya makanisa mapya

 ilikuwa "ongezeka" na mimi ni Dean Davis nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

CHUKUA MWANAFUNZI MMOJA PAMOJA NAWE - Siku 90 za Maombi na Kufunga



  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Upandaji wa makanisa ni huduma inayotokana na mafundisho ya nguvu kwa mda mrefu.

Kwa mda wa miaka ine, wapandaji wa makanisa wa kizazi cha kwanza wanafuata masomo ndani ya kituo cha mafunzo cha VCP. Ndani ya kituo hicho, wanasoma na kujifunza Biblia, wanazingatia na kuweka katika vitendo ujuzi mpya za kihuduma na wanaweka kipao mbele kutangaza Habari Njema, kufanya wanafunzi na kupanda makanisa mapya. Lakini hata iwe bora mafundisho kwenye kituo cha mafunzo kwa ajili ya upandaji wa makanisa katika vijiji, haitoshi. Usinielewe vibaya.

Napenda wakufunzi wa VCP na majifunzo yanayo fanyika kwenye vituo vya majifunzo. Lakini haitosheleze kabisa. Kwa kujifunza kupanda makanisa, unastahili kuchunguza wapandaji wa makanisa wakiwa kazini. Acha nirudilie kwamba : ''kwa kujifunza kupanda makanisa, unastahili kuchunguza wapandaji wa makanisa wakiwa kazini.'' kwa hiyo, wakati unapokwenda kufanya kazi ya upandaji wa makanisa, kamata mwanafunzi moja pamoja nawe. Wakati unapofanya huduma  ya maombi, chukuwa mwanafunzi moja pamoja nawe. Wakati unaongea na kiongozi wa mji, kamata mwanafunzi moja pamoja nawe. Wakati unapo hadisia hadisi za Biblia, chukuwa mwanafunzi moja pamoja nawe.

Wakati unapo ombea wagonjwa, kamata mwanafunzi moja pamoja nawe. Wakati unapofundisha moja ya agizo Saba za msingi za Yesu-Kristo, chukuwa mwanafunzi moja pamoja nawe.

Yesu alifundisha kwa wamitume kutoka kwenda wawili wawili (Marko 6:7).

Aliwaambia wanafunzi 72 kwenda wawili wawili (Luka 10:1).

Lakini ni sababu gani Yesu alisisitiza kuhusu huduma kwa kikundi ?

Sababu gani alifundisha kila Siku wanafunzi wake kutoka wawili wawili wakati wanapokwenda kwenye huduma na kutangaza Habari Njema ? Nawaza kwamba kuko sababu nyingi. Ilikuwa hatuwa ya usalama. Watu wawili wanao safiri pamoja wako Salama zaidi ya mmoja. Wako Salama zaidi zidi ya mashambulizi na wanaepuka ajali nyingi na magonjwa. Watu wawili  wanaofanya huduma yao pamoja, tunakuwa na imani zaidi ya mtu moja anayefanya huduma yake binafsi.

Kwa pamoja wanapatana kwa maombi, na makubaliano haya yanaleta baraka. Yesu alisema; Mathayo 18:19):''Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani kuomba neno lo lote duniani, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.''

Kwa hiyo, kwa kukamata mwanafunzi moja pamoja nawe, usalama wako unaongezeka na nguvu zako za kiroho kwa imani ndani ya Kristo zinaongezeka. Hizo ni sababu zakutosha ili kuchukuwa kila Siku mwanafunzi moja pamoja nawe wakati unapofanya huduma.

Lakini ziko nyingi ! Wakati unapokamata mwanafunzi moja pamoja nawe unapofanya huduma, unatekeleza shabaha mbili kwa wakati moja. Unasaidia wengine na kufundisha mwanafunzi wako.

Yeye atakuchunguza wakati unapojitayarisha kwa huduma. Mwanafunzi wako anakuchunguza, anakusikiliza na kuona namna unavyofanya kazi yako. Anaweza pengine kukuuliza maswali ili kugunduwa sababu gani unafanya yale unayofanya katika huduma.

Uchunguzi huo na mazungumuzo yanaleta faida kwa mwanafunzi na kwako.

Ni hapo majifunzo ya kweli yanafanyika.

Wakati mwanafunzi wako anakuchunguza unapofanya huduma ya Roho Mtakatifu, mawazo, masomo na habari zilizo jadiliwa ndani ya kituo cha mafunzo yanakuwa ya kweli ndani ya roho na mioyo yao. Kwa hiyo, kuchukuwa mwanafunzi moja pamoja nawe wakati unapofanya huduma.

Wafanyishe wanafunzi wako mazoezi ili nawao pia wachukuwe wanafunzi wao pamoja nao wakati wanapofanya huduma.

Kwa kufanya hivo, huduma yako itaimarika na kizazi kipya cha watumishi wakristo kitaendelea.

Ilikuwa ''ongezeka'' na mimi Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Kuwaombea Watumishi - Siku 90 za Maombi na Kufunga


 

Jambo, tazama ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, wachungaji na viongozi wa Kikristo. Mimi ni mgeni wenu Daneille Snowden.


Andiko linatuimiza kuombeana, Sisi kama viongozi wa Kikristo wa kanisa la Yesu-Kristo, ni muhimu sana kuombea wale wanaotumika kwa ajili ya ufalme wa Mungu.


Ninapenda hii andiko : Wakolosai 4:2 : lisemalo ''Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; 

mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,''


Kuomba kuko na tafsiri ya kushangaza kwa kutenda kwa kila hatuwa ya maisha yetu.

Kwa kuomba, tunastahili kuwa wanyenyekevu ndani ya roho yetu, tukimwomba Mungu kwa utaratibu mkubwa.

Hiyo inaungana na tendo lakuendelea, kwa hiyo, ''kuomba'' na kuendelea kuomba ! Kwa mwisho tunaomba bila kukoma.


Sisi kama wapandaji wa makanisa na viongozi wa makanisa, wakati tunapo omba kwa ajili ya watumishi wetu wote, tunaomba kama vile Paulo alivyofundisha katika Wakolosai :''... Ili kwamba Mungu afungue mlango kwa ujumbe wetu, ili kwamba tutangaze maajabu ya Kristo...''


Tuendelee kuombea watumishi na sisi wenyewe ili kwamba'' ...Injili hii ya Ufalme itangazwe duniani mzima kama ushuhuda kwa mataifa yote, na baadaye mwisho utatokea ! Mathayo 24:14


Hiyo ilikuwa ongezeka, munaweza tafazali kuigawanya na wengine?

Asante na Mungu awabariki.

Watiye Moyo Waombezi Wako - Siku 90 za Maombi na Kufunga


 Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Sote tunaitaji waombaji. Tunaitaji sote watu wanaokuwa kati yetu na Mungu na wanaotuombea. Maombezi, ni kuingilia kati kwa niaba ya mtu mwingine. Maombi ya maombezi ni maombi yanayoelekezwa kwa Mungu kwa faida ya watu wengine. Kama wapandaji wa makanisa, munaitaji maombi kwa mda wa siku 90, ao zaidi ya mda mwengine wote tangia pale ulipo anza kupanda makanisa.

Unaitaji kuomba ili mbingu zifunguke. Unaitaji waombaji ili kumsihi Mungu kueneza Roho wake kwa kuwavuta wanaume na wanawake kwake,  wakati wewe na wanafunzi wako munagawanya Habari Njema.

Unaitaji maombi ili milango ifunguke,  wakati wewe unawatafuta wanaume na wanawake wa amani katika vijiji ambako bado hakujakuwa makanisa. Na unaitaji maombi kwa ajili ya ukingo wa kimwili na kiroho wakati wewe pamoja na wanafunzi wako munatangaza Habari Njema.

Kama mujuavyo kupitiya maombi yenu na kifungo, maombezi ni kazi ngumu.

Kwanza, unaitaji kuwa na mda.

Na ni kweli, inaitaji imani.

Waombezi wanastahili ku amini kwamba  Mungu iko na anawalipa wale wanaomtafuta kwa bidii (Waebrania 11:6).  Lakini kuko mtindo mwengine wa maombezi unaotuchokesha. Maombezi ni kazi ngumu sababu tunapambana ndani ya maombi. Tunapambana zidi ya adui anayeonekana kushinda mapambano kwa maeneo mengi. Na tunapambana zidi ya mashaka yetu.

Inachokesha. Kwa hiyo, hata waombezi wenye uzoefu wanajaribiwa kutokuomba zaidi. Waombezi wote wanaitaji kutiwa moyo.

Kwa hiyo, ni namna gani kuwatiya waombezi moyo ? Mbele ya yote, tunawakumbusha wema wa Mungu. Tunagawanya ushuhuda wa maombi yaliyo jibiwa. Kusikia namna gani Mungu mwema na mwenye upendo alivyo jibia maombi yao na yetu inasisimuwa imani kwa ajili ya maombi mengi.

Ya pili, tunawakumbusha ahadi za Mungu kwa kusikia na kutekeleza maombi yetu. Kuko ahadi nyingi katika Agano la kale na jipya.

Lakini moja ya ahadi hizo inayo nijenga katika maombi yangu inapatikana katika 1Yohana 5:14;15 :

''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 

Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.''

Wakati tunapo omba kwa ajili ya waliopotea na kwa ajili ya makanisa mapya, tunajuwa kwamba tunaomba kulingana na mapenzi ya Mungu.

Kutiwa moyo kwa namna gani !

Namna ya tatu ya kuwatiya moyo waombezi ni kugawanya pamoja nao maitaji mapya ya maombi maalmu.

Na namna ya ine ni kuwashukuru tu kwa ajili ya kazi kubwa ya maombi ambayo wamejitolea.

Mpandaji mpenzi wa makanisa, unaitaji waombezi na waombezi wako wanaitaji kutiwa moyo, zaidi kwa mda wa Siku 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa. Unapendelea kuimarisha imani yao kwa Neno la kutiya moyo leo ?

Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis nawashukuru kwa ajili ya uaminifu wa maombezi yenu kwangu zaidi ya wapandaji wa makanisa katika vijiji 13 000 kwa Afrika .

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...