Karibu kwenye ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, wachungaji na viongozi wa Kikristo, na mimi ni muhamasishaji wenu, Daneille Snowden.
Moja ya Mada zangu ninazopenda kufundisha na kukazia zaidi kwa mambo ya kutangaza injili ni ile ya ''watu wa amani''. Ni namna bora ambayo Roho Mtakatifu anatenda ili kuongoza wapandaji wa makanisa na wa injilisti kuelekea kwa watu, na kuwaruhusu kushuhudia namna gani Roho Mtakatifu anavyotayarisha mioyo yao kupokea ujumbe.
Ndiyo maana, katika matayarisho, tunachukuwa mda mwingi katika maombi, baadaye tunaendelea na vipindi vya maombi katika vijiji, tukiingia ndani ya jamii pale ambapo tunajisikia kwamba Bwana anatuongoza.
Wakati tunapo jifunza vifungu vya Biblia kama vile Luka 10:1, 12 na Marko 4:26, 29, tunakutana mtindo huu kupitiya Yesu mwenyewe. Akawatuma wale 72 na akawaambia na kwenda ! Kwenye vesi ya 5 na 6, anasema ''Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, amani iwemo nyumbani humu;
[6]na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu''. Katika vesi hii, tunaona kama Bwana Yesu anashauri kujenga mawasiliano pamoja na mtu huyo. Ufanyapo hivo, amani inatangazwa. Kupitiya ushirika wa ndugu, maongezi yanaendelea. Mtu wa amani anafurahia kufunguwa nyumba na moyo wake kwa wote waletao Habari njema ya injili.
Mtu wa amani ni mwenye kupokea, anaye pokea wageni, anayegawanya kwa moyo mkunjufu kile alicho nacho, anawasiliana vizuri na wengine, na anahakikisha amani hiyo ya Mungu kuwa kama kitu ambacho alikuwa anatafuta. Kuendelesha mawasiliano ya namna hii katika injili inaruhusu kufunguwa mlango ili kwamba injili ifikie kundi la jamii, jamaa na watu wengi.
Tunapashwa kuwa waangalifu, wenye kuongozwa na Roho Mtakatifu na kujawa na uhakika ili tu kuongea na watu hawa. Ni kupitiya Roho Mtakatifu ndipo macho ya mioyo yao inafunguliwa.
Tunayatekeleza yote haya kupitiya uwezo wa maombi na mwongozo wa Roho.
Mume wangu na mimi tulikuwa na tabia ya kutangaza injili katika mitaa ya Indianapolis, katika mkowa wa Indiana. Mungu alituongoza kuelekea watu wasio na makao ambao walikuwa walevi. Tulikuja na upendo ndani ya mioyo yetu ili kuwaambia kuhusu Yesu.
Matokeo yao ya kwanza wakitoa machozi, ilikuwa kusema kwamba hakuna mtu aliye chukuwa mda, kuwaambia kwamba Yesu aliwapenda. Walitoa maisha yao kwa Yesu na kuanza kumzungumzia kwa wengine ndani ya jamii zao za watu wasio na makao. Waligeuka kuwa sasa watu wetu wa amani, wakiwaongoza ma mia ya watu kwa Kristo. Kuko mifano mengi katika maandiko, kama vile Yona na Mfalme wa Ninawi, mtu mwenye pepo katika kitabu cha Marko 5, mlinzi wa gereza, mwanamuke Msamaria, na wengine wengi.
Unaweza kukumbuka mtu wa amani ambaye Mungu alikuongoza kwake ? Wapandaji wa makanisa walipenda kusikia hadisi na shuhuda hizi, sasa nawapa moyo kuzigawanya pamoja na viongozi wenu, ili kwamba wao pia wazitangaze kwa wengine. Ndipo dunia yote itatambuwa na kujuwa matendo makubwa ambayo Mungu ametenda kupitiya mataifa, ni sababu tu ya mawasiliano na WATU WA AMANI !
Ilikuwa ongezeka. Usishite kugawanya podikasti hii kwa wengine.
.jpeg)