Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo.
Leo, tunaendelea na mfululizo wetu juu ya uongozi wa Muwakili, na tunamaliza somo letu la mfano wa Muwakili dhalimu.
Muwakali anatafsiriwa kama ''mtu anayesimamia rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali''. Katika mazingira yetu, tunaongoza rasilimali tulizopewa na Bwana kwa ajili ya kazi yetu ya upandaji wa makanisa katika vijiji.
Katika podikasti zangu za nyuma. Nilionyesha Mada tatu za msingi za mfano huu:
Mawakili wanastahili kutowa ripoti.
Ujanja wa Muwakili na sifa alizopokea kwa bwana wake.
Umuhimu mkubwa wa uaminifu katika mambo madogo kama vile ndani ya rasilimali.
Shurti muhimu ambayo Yesu anajaribu kututolea hapa ni kwamba inafaa kuwa Muwakili mwaminifu. Usizoofike na sifa anazozipokea Muwakili dhalimu - tulijadili swali hili katika kipindi cha nyuma. Muwakili dhalimu alichukuwa rasilimali za bwana wake kama njia ya kujibia maitaji yake na kujiendelesha mwenyewe. Yesu, kwake yeye, anapendelea wafuasi wake wawe waaminifu na wenye haki katika usimamizi wao wa rasilimali.
Yesu anaeleza katika vesi 10 na 11 :
''Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli?''
Hii inanikumbusha somo letu la mfano wa Talanta katika Mathayo 25.
Tukiwa waaminifu katika mambo madogo, kwa hiyo tunaweza kukabiziwa mengi. Na kama hatuwezi kuwa waaminifu katika mambo ya dunia - yasiyo yetu hata kwa mwanzo, namna gani Mungu anaweza tukabizi ''utajiri wa kweli'' wa Ufalme wake?
Neno kubwa ya utashi wa Yesu uko kwenye vesi ya 13 :
''Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.''
(Angalia pia Mathayo 6:24)
Kama Mungu ndiye Bwana wetu, kwa hiyo sasa, rasilimali zetu, mda wetu, vipaji vyetu na pesa zetu vitakuwa kwa ajili yake.
Muwakali mwaminifu na mwenye haki, ambaye Bwana wake ni Mungu, ataweka vyote alivyo, na vyote anavyofanya kwa kazi ya kujenga Ufalme wa Mungu.
Kwa mwisho, wanaopenda pesa kuliko Mungu, ambao wanatafuta tu kulipwa ao kutajirika, hawaweki Ufalme wa Mungu katikati ya vipaumbele vyao.
Katika podikasti yetu ijayo, tutaendelea na somo letu kuhusu uongozi wa Muwakili.
Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni