Ijumaa, 24 Julai 2026

KANISA KATIKA KILA KIJIJI CHA AFRIKA

 









    Jambo kwa wote. Naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Kila mpandaji wa makanisa anajuwa maono ya VCP : "kanisa katika kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2050". Maono haya, inayojengwa juu ya Agizo kubwa ya Bwana wetu Yesu Kristo, inatowa mwelekeo kwa jumla na msingi kwa yote tunayoyafanya wakati tunatumika pamoja kwa kuzidisha wanafunzi, wasimamizi na makanisa.

Wapandaji wa makanisa, kwa mfano wa Mungu, hawapendi hata mtu apotee. Tunapenda wote wafikie toba. Tunajuwa kwamba Mungu hana upendeleo. Anapenda watu wote, popote. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtowa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. (Yohana 3:16). Tunapenda kuishi katika utakaso ; ndio maana tunachaguwa pia kupenda watu wa mataifa yote na kila mahali.

Kwa hiyo, ikifikia wakati wa kuhubiri Habari njema, mara nyingi vijiji vinazarauliwa. Wakaaji wa miji wako na fursa nyingi ya kusikia Habari Njema. Katika mikutano mikubwa, katika barabara kubwa, tunaona makanisa mengi. Lakini kupitiya hadisi, inachukuwa mda mrefu mbela ya Injili kufika katika vijiji. Waundaji wa huduma ya upandaji wa makanisa walijuwa hiyo.

Ndio maana waliweka kipaumbele upandaji wa makanisa katika vijiji.

Leo, uko miongoni wa hii vuguvugu inayosaidiwa na msemwa huu rahisi : "kanisa katika kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2050". Kila mpandaji wa makanisa VCP, kila mwanafunzi wa VCP, kila Mwalimu na Mratibu, kila kasisi, Mkurugenzi na mrahisishaji wa kuzidisha makanisa iko na kazi ya kufanya ili kubadilisha haya maono kuwa ukweli.

Mbele ya yote, tunastahili kuomba, tunapashwa kuomba Mungu ili ufalme wake uje na mapenzi yake yafanyike ndani ya kila Kijiji cha Afrika.

Tunastahili kumuomba ili kuwe kanisa katika kila Kijiji cha Afrika ifikapo mwaka wa 2050. Baadaye, tunapashwa kujumulisha maombi kwa matendo. Kwa namna ingine, tunastahili kutenda kama wafanyakazi pamoja na Kristo ili kuona maono haya yakitekelezwa.

Kila mpandaji wa makanisa anaye chukuwa maono haya kwa uaminifu atajuwa ni vijiji gani vilivyo karibu na kituo cha mafundisho tayari viko na kanisa na ni vijiji ngapi havina kanisa. Kama weye na rafiki zako wapandaji hamujuwe kama ni vijiji ngapi vilivyo kandokando ya km 10 ao 20 ya kituo chako cha  mafundisho ambavyo bado havijakuwa na kanisa, uliza habari, wende katika kila Kijiji cha kutembea kutwa mzima kutoka kwenye kituo cha mafundisho na ugunduwe kama kuko kanisa ao hakuna.

Gawanya habari hizo pamoja na mkufunzi wako na wanafunzi wenzako. Ikiwezekana, uonyeshe hiyo kwenye ramani.

Baadaye, zidisha maombi kwa ajili ya vijiji vya kandokando ambavyo bado havina kanisa. Kila mwanafunzi wa VCP anastahili kuchukuwa majukumu ya kupanda makanisa ndani ya vijiji vinavyojulikana kuwa havijafikiwa. Tembelea vijiji hivyo kwa maombi. Muombe Mungu akuonyeshe watu wa amani, wanaume na wanawake walio na kiu ya kumjuwa Mungu na wako wazi kusikia Habari Njema. Gawanya ushuhuda wako, ombea wakaaji, uwasimulie hadisi za Biblia, onyesha filamu ya Yesu kwa baadhi ya watu ao kwa Kijiji chote. Uwe mwaminifu kwa Mungu ili akutumikishe, wewe pamoja na wenzako wa huduma, ili muanze kupanda makanisa yenye afya ndani ya vijiji ambavyo havina kanisa. 

Unaweza kufikiri kwamba juhudi yako haitabadilisha Afrika. Lakini wakati itajumulishwa na yale ya wengine maelfu ya wapandaji wa makanisa katika vijiji, watafanya utafauti. Mungu atakutumikisha kama chombo kubwa cha kazi yake kwa ajili ya kuleta maisha tele ndani ya Kristo kila mahali. Sababu inchi itajaa na ujuzi wa utukufu wa Bwana, kama maji yazavyo vilindi vya bahari (Habakuki 2;14). Amini hayo!

Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis. Nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Kutumika kwa mda wa sasa. Kuomba kwa ajili ya wakati ujao

      Jambo kwa wote. Naitwa Dean Davis, na munasikiliza ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapand...