Jambo kwa wote. Naitwa Dean Davis, na munasikiliza ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Wakulima na wapandaji wa makanisa wanakuwa na vitu vingi vya kufanana.
Wote wawili wanatumika kwa imani. Moja kama mwengine hakuna anayejuwa kwa uhakika kama kazi wanayoifanya leo itazaa mavuno kwa myezi inayokuja.
Ijapokuwa, wote wawili wanatumika kwa bidii leo kwa matumaini yakupata mavuno mengi kwa Siku chache baadaye.
Wakulima wanalima udongo siku baada ya siku ili kuitayarisha kwa kupanda mbegu. Wanapanda kwa makini sababu mbegu zipate kukomaa na kutowa mavuno. Wanaboresha ukulima ili kuondowa majani mabaya, na wakati wamavuno inapofika, wanatumika kwa bidii ili kuvuna kila mbegu.
Ni kwa namna hiyo, wapandaji wa makanisa wanatumika kwa juhudi leo kwa matumaini yakupata mavuno mengi kwa myezi inayokuja. Wanatayarisha eneo wakiomba ili kwamba Mungu awakutanishe na watu wa amani. Wanapanda kwa hekima na kwa uhakika mbegu njema ya Injili kwa namna iweze kuzaa matunda. Wakati mbegu inapo pokelewa, inalinda mioyo ya waamini wapya kwa kuwafundisha kumtii Kristo. Wanawasaidia pia kuondowa majani mabaya ya shaka na kutokutii wale wanaotafuta kuzimisha imani yao kabla haijazaa matunda.
Wakulima wanatumainia mavuno mengi yatakayoleta chakula cha kutosha. Wanatarajia kwamba yote yatatendeka vizuri. Wanapendelea mvuwa inyeshe kwa mda muhafaka na kiwango cha kutosha. Wanatarajia mavuno mazuri ili waweze kufurahi pamoja na jamaa zao wakati mavuno yatakuwa yamekusanywa.
Kwa namna hiyo, wapandaji wa makanisa wanapendelea kuona makanisa yenye afya yanapandwa, yakikomaa, kwa hesabu ya kila Siku watu wengi wanamjuwa Yesu na wanajifunza kuishi kama wanafunzi waaminifu. Wakipendelea hivo kwa siku zijazo, tunaomba. Tunaomba kwa ajili ya mavuno yajayo, tukimsihi Mungu kwa makini abariki, kwa kurizisha maitaji na kukingia kazi yake.
Kwa hiyo, wapandaji wamoja wanachukuwa mda mwingi wakifikiria siku zijazo, kwa kupangilia na kuomba juu ya baraka zijazo wakizarau kazi itakayotekelezwa leo. Wengine, kwa kinyume, wanamezwa na majukumu ya sasa hadi kusahau kupangilia na kuomba kwa kile kinastahili kutendeka kwa majuma wala kwa myezi michache ijayo.
Tunastahili kupata usawa kati ya hizi hatuwa. Lakini ni kwa namna gani tutaifikilia ?
Namna gani wapandaji wapya wa makanisa wanaweza kupata usawa kati ya kazi inayotekelezwa leo na mpangilio pamoja na maombi ya siku zijazo ?
Mfano wa mashamba ine unaweza kukusaidia kuifikilia.
Wapandaji wanaofuata mfano wa mashamba ine wanajuwa kwa uhakikisho yake wanastahili kufanya leo. Wanatambuwa ''eneo'' ambako wanatumikia na kutekeleza majukumu yanayowastahili. Kwa wakati huo, wanatazamia kwa wasimamizi wanaowangoja kwa shamba mpya. Kwa hiyo, wanaweza kuomba ili Mungu atende, afunguwe milango na kuwabariki, ili wawe tayari kutekeleza haya majukumu mapya wakati mda utaruhusu.
Mtindo wa mashamba ine ni mwongozo wetu. Unatusaidia kukusanya nguvu zetu juu ya kazi ya leo pamoja na kupangilia na kuomba juu siku zijazo. Sasa, fuata mtindo wa mashamba ine katika kazi yako na katika maombi yako. Itakuongoza kwenye huduma ya upandaji wa makanisa ya kina zaidi.
Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis. Nawaacha na hili swali :
''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?''

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni