Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis. Na munasikiliza ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Imewai kukufikia kuuliza kwa mwana muziki maarufu ''ni kwa namna gani unafanya ili kucheza namna hii?'' kama ni ndio, pengine alikujibu kwa swali lingine : ''namna gani ninafanya nini ?'' unamaanisha sasa : ''namna gani unajuwa ni kwa sauti gani utaimba ? Kufata mtindo gani ? Ni kwa namna gani unafikia kutunga muziki muzuri kwa kutumia chombo hiki ?
Wasaani wamoja watakujibu : '' hakika sijue. Niliangalia tu watu wengine wakicheza. Baadaye nikanunuwa chombo, nikaanza kujifunza, na sasa ninacheza tu.''
Mtindo huu unastahili kwa watu ambao kwa asilia ni wazoefu wa muziki, lakini siyo hivo kwa watu wengi. Baadhi ya watu wengi wanaitaji kufunzwa kwa mtindo maalum kama wangependa kucheza na chombo.
Ni hivo pia kwa wapandaji wa makanisa. Kuko wapandaji wa makanisa wenye uzoefu ambao walianza tu kuhubiri na kuwakusanya watu ili kuabudu Mungu. Waliangalia tu wachungaji katika huduma yao na wakaanza tu kupitiya hisia zao namna gani ya kupanda makanisa mapya, bila kupata mafundisho mengi. Lakini haina ya hawa wapandaji wa makanisa wako nadra, na, mara nyingi, hawajue ginsi ya kufundisha watu wengine kupanda makanisa. Kama vile wengi miongoni mwa wasaani wako na haja ya kujifunza kuchezesha chombo. Wapandaji wengi wa makanisa wanaitaji kufundishwa ili wajue kupanda kanisa.
Haina ya mashamba ine inahusu mafundisho ya msingi ambayo wakristo wakawaida wanaitaji ili kupanda na kuzidisha makanisa. Ni mtindo bora, sababu iko rahisi kuelewa na kurahisisha kuzalisha. Wote wanaoitaji kupanda makanisa watazidishwa nguvu kama wakichukuwa kila mara mtindo wa mashamba ine. Ndio kwa maana imechapishwa nyuma ya vitabu vya VCP kwa kila muhula. Imetengenezwa ili ichukuliwe kila mara na kugawanywa pamoja na wanafunzi.
Mtindo wa mashamba ine inajibu swali la ''ni wapi kwa kuanzia ?''
Utaanza na kuomba ili Mungu akusaidiye kupata watu wa amani ndani ya Kijiji ambako hakuna kanisa. Utaanza na hatuwa ya maombi. Hiyo inamaanisha kama utatembea Kijiji chote, macho yakiwa wazi na moyo mwangalifu, katika kuomba ndani ya Kijiji kilicho na itaji ya kanisa. Utaomba kwa Mungu akuongoze kuelekea watu wa amani : watu wasikivu, wakaribishaji na wenye haja ya kumjuwa Mungu.
Mtindo wa mashamba ine inakuonyesha pia kile unastahili kufanya wakati unapata watu wa amani : msaidie kuweka tumaini lake kwa Yesu Kristo kama Mwokozi wake. Mufundishe Ku alika jamaa lake na maraflki kuja kusikia Habari Njema ya Yesu. Saidia kikundi hiki kujifunza kutii kwa yote Yesu aliyo amuru.
Kwa mwisho, mtindo wa mashamba ine inakufundisha kuandaa viongozi kwa ajili ya kanisa lako mpya na kuwatuma kwa vijiji vingine ambavyo havina kanisa ili waanze mchakato wote wakiomba na kutafuta watu wengine wa amani.
Kwa hiyo, mtindo wa mashamba ine ni mwongozo lakini pia ni mwongozo wa maombi. Tunastahili kumuomba Roho Mtakatifu atende kazi ndani ya kila moja ya shamba hizi ine. Tunaitaji msaada wa Mungu ili kupata watu wa amani. Tunaitaji msaada wake ili kutangaza waziwazi na nguvu Habari njema. Tunaitaji hekima ya juu ili kufanya wanafunzi na kufundisha na kuunda vikundi vipya vya maabudu. Na tunaitaji hakika msaada wa Mungu ili kuandaa na kutuma viongozi ili watumike ndani ya kanisa letu Jipya na wanapanda makanisa mengine ndani ya vijiji vingine.
Wakati unaendelesha kazi yako ya upandaji wa makanisa, acha mtindo wa mashamba ine ukuongoze. Pengine unajisikia kama hauna uzoefu, lakini Mungu atakusaidia kama ukiwa mwaminifu kwake na kutumikisha kwa mwisho mtindo wa mashamba ine kwa upendo mkubwa kwa watu wanaopotea.
Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Mimi ni Dean Davis, nawaacha na hili swali, ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni