Jumatatu, 23 Septemba 2024

Jifunze Upya Misingi Ya Upandaji Wa Kansisa - Siku 90 za Maombi na Kufunga



 Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Imenifikia mara nyingi kwenda kwenye ibada pamoja na binti wangu na kumuonyesha kuhusu ujumbe : ''ni ujumbe gani mzuri ! Ilikuwa kujazwa na injili tofauti na kingine isipokuwa tu injili''.

Yeye na mimi tunapendelea kusikia ujumbe wa kiinjili inayosema kuhusu nguvu za wokovu za Yesu-Kristo. Ni hadisi ya kimsingi ya wakristo wote.

Kwa namna hiyo, napenda kushiriki kwa mafundisho ya kimsingi ya wapandaji wa makanisa. Napenda kuona tena vipindi vya muhimu vinavyosaidia kupanda kanisa chembechembe itakayo komaa na kujizidisha. Ninaamini kwamba kwa mwezi wa nane, wapandaji wa makanisa wa Afrika nzima watakutana katika vituo vyao vya majifunzo VCP vya kawaida pamoja na wakufunzi wao ili kurudilia misingi ya upandaji wa makanisa.

Ni nini misingi ya upandaji wa makanisa ?

Ni ujuzi zinazo onyeshwa ndani ya muhula wa 1 na wa 2 ya mpango mpya wa VCP .

- pambanuwa, tafuta vijiji visivyo na kanisa 

- omba kwa ajili ya vijiji, pamoja na kuendelea katika maombi katika vijiji.

- tafuta na kupata watu wa amani 

- Gawanya Habari Njema ya Yesu pamoja na watu wa amani, jamaa zao na marafiki wao

- Fanya wanafunzi kwa kufundisha waamini wapya kutii Agizo Saba za msingi za Kristo,

Ndizo kazi za muhimu za wapandaji wa makanisa. Wakati tukienenda kwa imani na kufanya kazi hizi 5 za msingi za upandaji wa makanisa, Tunakutana na Mungu. Anatupa nguvu. Anatusaidia kujenga mawasiliano mema.

Wakati tunatekeleza kazi hizi kwa kuweka Imani yetu kwa Mungu na kwa upendo wake mukubwa kwa watu waliopotea, anatujaza upendo na nguvu.

Ni ujuzi wa msingi ambao wapandaji wote wa makanisa katika vijiji wanastahili kujifunza, kutumika na kuboresha.

Lakini kwa wengi ndani yetu, kazi hizi ziko ngumu sana. Tunapata basi zingine kazi zilizo rahisi zaidi ambazo tunahusika.

Siku zetu 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa ziko na lengo ya kubadilisha hayo yote. Mbele ya yote, tunaomba. Tunaomba ili tujazwe na upendo. Tunaomba ili madaraka ya ondoke. Tunaomba ili Mungu atuonyeshe watu wa amani na kuwavuta kwake. Tunaomba ili Mungu awavute kwake watu waliopotea. Kwa kuendelea kuomba, tunaboresha ujuzi wetu wa msingi kwa hatuwa ya upandaji wa makanisa.

Kisha tunaendelea.

Kwa mda wa mwezi wa nane, wewe, pamoja na wapandaji wa makanisa wa VCP kwa Afrika mzima, watakutayarisha kwa vitendo. Kwa maombi, utatengeneza Imani yako na kufikia nguvu za Mungu ili kuwa mashahidi wake.

Kupitiya mafundisho, utaimarisha uwezo wako kwa misingi ya upandaji wa makanisa.

Baadaye, utaondoka pamoja na washiriki wa kanisa ambao utachukuwa kama wapandaji wa makanisa mapya. Wakati utaenda pamoja nao ndani ya vijiji visivyo na kanisa, Utakutana na Mungu. Atakuwa pamoja nawe atakufanya uwe na matunda. Kumbuka ahadi ya Yesu. Alisema : ''Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni''.

(Yohana 15:16).


Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis nawauliza : ''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...