Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Umekwisha kusikia ikisemwa Siku 90 za maombi, na kifungo na upandaji wa makanisa itakayotekelezwa katika inchi 32 za Afrika kuanza tarehe 01/Agosti hadi tarehe 29/oktoba 2024? Nina furaha kwa ajili ya fursa hii kwa kujinyenyekeza na kuita Mungu kwa ajili ya neema yake, msaada wake na wokovu wake vijae vijijini ambako hakuna kanisa kupitiya Afrika nzima. Ninafuraha kubwa kwa wazo kwamba kanisa 13 000 zimeweza kupandwa na wapandaji wa makanisa wa VCP kama vile zinaweza kugeuka kuwa kanisa 26 000 kwa myezi ifuatayo.
Wakati unaposikia ikisemwa kipindi cha Siku 90 zilizotengwa juu ya upandaji wa makanisa, kuanza tarehe 01 Agosti, umeifikiria nini? Ulisikia boga? Ulichanganyikiwa? Tangazo lilikuwa pengine la kuchanganya. Sababu gani tutasimamisha majifunzo yetu ya kawaida katika vituo vyetu vya majifunzo ya VCP ili kujiusisha na maombi na kifungo ?
Sababu gani tunastahili kuifanya sote kwa mda moja? Sababu gani Siku 90? Ni kipindi kirefu! Wanatarajia kabisa nifanye kifungo cha Siku 90 za kufuatana ?
Muniruhusu kujibu kwa baadhi ya swali hizi za muhimu sana. Kasisi wa VCP, Claude Douti, alituomba kusimamisha masomo katika vituo vya majifunzo ya VCP
Mwanainchi Douti alituomba kusimamisha masomo yetu ya kawaida katika vituo vya majifunzo ya VCP ili wapandaji wote wa makanisa, waalimu, waratibu, na wa superviseurs na wa wezeshaji wa kuzidisha makanisa ya VCP ili waweze kujinyenyekeza na kuhusisha roho zao katika maombi. Tutatoa wito kwa Mungu ili kwamba kila kanisa lianze kanisa lingine mpya.
Tunafurahia makanisa yote iliyokwisha kupandwa tangia mwaka wa 2020, tarehe ambayo mfumo mpya wa VCP ulianzishwa kwa mara ya kwanza. Lakini tunatarajia sana watu ndani ya vijiji zaidi wajue upendo wa Yesu na wafanye uzoefu wa kuzaliwa upya ndani ya jamaa ya Mungu. Tunafurahia yale tuliofanya ili kupanda makanisa, lakini tunashugulikia yale bado kutekelezwa. Tunaitaji nguvu na uwezo wa Mungu. Tunaitaji milango ifunguliwe. Tunastahili kupata watu wa amani.
Tunastahili kuonyesha kupitiya kifungo siyo kwa nguvu, wala uwezo, lakini kwa Roho wa Mungu ambayo maoni ya VCP yatatimizwa.
Tunasimamisha hivo masomo yetu ya kawaida na tutarudilia kwenye vituo vyetu vya masomo kwa mwezi wanane kwa kufanya mambo yafuatayo :
Mtiani wa huduma juu shamba 1 na 2, tukiendelea na maombi, kutafuta watu wa amani na ugawaji wa Habari njema. Na tunaomba, Sisi wenyewe, kwa vikundi kidogo vidogo na vile vikubwa. Tutaandaa na ibada za maombi ndani ya kanisa zetu binafsi na ndani ya makanisa tunayoshirikiana nayo.
Na ikiwa tuna afya njema, tunafunga pamoja na maombi, tukijizuiza kula.
Mara nyingi tunafunga na wengine, Mara nyingi Sisi wenyewe.
Zaidi tena tunafunga kwa mda wa Siku nyingi. Mara nyingi, tunasimamisha ili kuanzisha kifungo inga ijayo. Hatuko chini ya sheria, lakini chini ya neema. Mufunge vile munajisikia kusukumwa kuifanya. Mujinyenyekeze mbele ya Bwana. Kama hauna afya njema, usifunge, lakini uombe.
Mwezi wa munane, tumika pamoja na Mwalimu wako ili ku orozesha vijiji ambavyo havina makanisa mahali ambako weye na rafiki zako mutakwenda kutafuta watu wa amani. Baadaye, pamoja na wapandaji wako vijana, muchukue mda mwingi uwezekanayo ndani ya vijiji hivyo kwa mwezi wa kenda na wakumi.
Mutafute watu wa amani, muombee wagonjwa, mugawanye ushuhuda wenu, mugawanye miviringo tatu. Ikiwezekana, muonyeshe filamu ya Yesu. Muwasaidiye waamini wapya kukusanyika ili kupokea Neno la Mungu na kuabudu Mwenye nguvu zote.
Na usisahau kwamba kupitiya Afrika, wapandaji wa makanisa 13 000 wanapatana ndani ya maombi pamoja nanyi.
Katika Marekani, waombaji wanapatana ndani ya maombi ili usaidiye kila kanisa ambalo utatumika nalo kuanzisha kanisa lingine mpya ambalo pamoja nalo pia mutatumika kuunda kanisa lingine mpya.
Mujae matumaini. Mujae nguvu za Kristo aliye hai. Yeye aliye waita ni mwaminifu ! Hatawaacha wenyewe!
Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis na ninawauliza; ''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni