Tayari umekwisha kusikia ikisemwa Siku 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa, ambazo Kasisi wetu Mchungaji Claude, alitangaza kwa mwezi wa nane hadi wa kumi wa mwaka huu.
Maombi, kifungo na upandaji wa makanisa ni kazi tatu zinazo muheshimu Mungu na tunatumika pamoja.
Siyo kazi za uchawi. Hazimushurutishi Mungu kutenda. Lakini ziko na nguvu.
Mbele ya yote, kwa kuomba, kwa kufanya kifungo na kwa kwenda kupanda makanisa katika vijiji ambako hakuna kanisa, tunatangaza tegemeo yetu yote kwa Mungu mwenye nguvu zote. Tunajuwa kwamba ni kazi yake, bali siyo yetu. Yeye ni kiongozi wetu, sisi ni wasaidizi wake. Tunatumika pamoja na Kristo na tunamtegemea yeye. Sisi tuko zaifu lakini yeye ni mwenye nguvu. Tunaomba sasa. Tunajikumbusha ahadi za Mungu. Tunaunguma mazaifu yetu. Tunakumbuka namna gani aliwapa Mitume Agano jipya. Tunamwaminia ili kwamba atupe nasi uwezo huo huo.
Lakini siku zetu 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa siyo tu siku za maombi kwa ajili ya nguvu za Mungu.
Zinajionyesha siku zilizo andikwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 1 na 2, ambazo Mitume waliingia ndani ya chumba cha juu wakati wa kula karamu ya mwisho mbele ya siku ya Pentekoste. Waliomba kwanza, baadaye wakajazwa na Roho Mtakatifu.
Walitoka na kutangaza maajabu ya Mungu kwa watu ambao walikuwa bado kuamini Habari Njema.
Kwa mwisho, Bwana aliongeza kila siku hesabu ya wale waliokoka.
Sasa kwa nini kuongeza kifungo kwa maombi yetu ? Kifungo siyo uchawi. Haishurutishi Mungu kutenda.
Lakini ni ya muhimu ? Kama ni ndiyo, kwa namna gani ?
Kifungo ni cha muhimu, ni vema kujizuwiya kula wakati wa Siku moja wala Siku nyingi ili kumtafuta Mungu. Lakini tunajuwa kwamba tunakutana na Mungu wakati tunapo acha kiburi chetu na tukimtafuta kwa unyenyekevu.
Anapingana na wenye kiburi, lakini anawapa wanyenyekevu neema.
Yesu alitarajia kifungo kwa wanafunzi wake, lakini mwelekeo maalmu aliyowapa kuhusu kifungo ni kuepuka kifungo kinacho sababisha kuleta maabudu kwa wanadamu.
Hatufanyi kifungo ajili ya kupata ukubalifu kwa wengine. Tunafanya kifungo ajili ya kujiweka kwa Mungu, ili kusikia sauti yake na kukubali atuongoze maishani mwetu.
Kwa mda wa siku 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa, hakuna mtu atakaye tushurutisha kufanya kifungo. Kifungo ni tendo la kujitolea.
Lakini kama ni turu ya kwanza unafanya kifungo na ukiwa mwenye afya njema, nakupa moyo kujaribu kifungo.
Mtafute Bwana kwa moyo wako wote. Onyesha upendo wako kwa Mungu kwa nafsi yako yote. Ukionyesha kwa maneno tegemeo lako kwa Mungu, uionyeshe kwa wakati wa mda fulani, kwa kumtafuta Mungu ukijizuwiya kula.
Wakati wa kifungo chako na zaidi baada ya kifungo chako, Utakutana na Mungu. Atakuongoza, atakupa uwezo. Na nguvu za Mungu ni kila Siku kitu cha ajabu !
Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi ni Dean Davis nawauliza : ''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni