Jambo kwa wote ! Wapendwa wapandaji wa makanisa.
Nawasalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Ni mimi Mtumishi wenu, Mchungaji Douti Claude Kasisi wa VCP.
Hii ni ongezeka, Neno letu la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa. Imepita mda mchache, tuliongelea kuhusu Siku 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa.
Mumepokea ujumbe nyingi kwa kipindi hiki.
Kwa hiyo, asubui ya leo, napenda kuwaambia kuhusu ''maombi ya imani''. Kuomba kwa imani. Muniruhusu kwanza nisome kifungu cha Waebrania 11:1-6 inayosema :''Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
[2]Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa.
[3]Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.
[4]Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.
[5]Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.
[6]Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao''.
Tazama, wandugu wapendwa, Neno hili, muniruhusu ni anze kwa vesi ya mwisho. kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko.
Muwajulishe kwamba maombi munayo elekeza kwa Mungu, Mungu ataitekeleza. Nawapa moyo kupitiya vesi hii kuomba kwa imani. Muwe na Imani ndani yenu. Uhakikisho. Imani ni hakikisho ya mambo yatarajiwayo. Tunatarajia nini ?
Tunatarajia kupata makanisa mengi yaliyopandwa, mioyo mingi iokolewe katika Bara la Afrika katika mda wa miezi tatu ambayo tumeitowa kwa Mungu wakati tunapo enenda mbele zake.
Ndugu wapendwa, Imani ni ya muhimu sana, Mtume Yakobo anasema haina maana kuomba wakati tunakuwa na mashaka.
Nina Imani kwenu pia, wapandaji wa makanisa, tumepitiya mambo mengi, tuko na ushuhuda zinazoleta nguvu kwa imani yetu.
Ninajuwa kwamba baada ya miezi hii mitatu za maombi tutapata matokeo mazuri kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Munastahili kuwa na imani, kuomba kwa imani. Ombeni kwa kujitolea.
Amini kwamba maombi yenu yatakuwa na matokeo makubwa na kwamba jina la Mungu litatukuzwa.
Ilikuwa ongezeka, podikasti yetu ya kutiya moyo kila Siku.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni