Tazama ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji, wachungaji na viongozi wa Kikristo. Mimi ni mgeni wenu wa leo, Danielle Snowden.
Zaidi ya 10 000 ya wapandaji wa makanisa katika vijiji walihamasishwa katika inchi 32 tangia mwaka wa 2020. Tunaamini kuwa Mungu alitayarisha wanaume na wanawake wa amani kwa vijiji hivi vyote, ili wapokee Habari Njema.
Wapandaji wetu wa makanisa katika vijiji wanakabiliana na matatizo mbali mbali wakati wanapoitikia wito wa kupeleka injili ndani ya maeneo haya yaliyo mbali na miji.
Ni muhimu kwamba wote miongoni mwetu wanaogawanya maono mamoja ya upandaji wa makanisa waunganishwe ndani ya maombi, kwa makubaliano yenye nguvu (wakati Sisi tunaomba).
Kwa hiyo, mwongozo wa maombi iliyo andikwa kwa udondozi kwa ajili ya siku 90 za maombi, inayoitwa : Siku 90 za maombi, kifungo na za upandaji wa makanisa, ni kitabu kinacho tusaidiya sote kuomba.
Wakati tunapokuwa katika kifungo, tunajihusisha kwa ajili ya kila siku na ya maombi inayo onyweshwa, angalieni kwamba inashindikizwa na kifungu cha Biblia.
Ninataka kuwapa moyo kuomba na kujuwa kwamba watu wengine wanaomba maombi haya kila siku na kukariri maandiko ya ahadi juu ya mwongozo wa maombi.
Chukuwa kila ombi, ikariri, iangalie vesi inayo ambatana na maombi. Ngojea Bwana, baadaye omba kwa ajili ya kazi yako, ya wapandaji wako wa makanisa, viongozi wako, makanisa yako, wachungaji wako na wewe mwenyewe. Tunakutiya moyo kuifanya mara mbili kwa siku, wewe mwenyewe na baadaye na vituo vyako vya majifunzo wakati munapo kusanyika, na hivo pia pamoja na makanisa yenu. Omba tafazali, tafakari, na ngojea Bwana Ili kusikia. Ingestahili kuwa mda ambao Mungu atakupa ahadi, maono na mwelekeo.
Muwe waaminifu na kubaki ukitafakari, sababu maandiko yanasema :
''Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya.'' (Isaya 50:7).
Uwe mwaminifu kwa Mungu na utangaze kwamba hautarudia nyuma mbele ya wajibu wako ambao Mungu amekupangia !
Asante kwa kutusikiliza leo!
Je! Unajuwa kwamba tuko na mtandao : vcpencourangement.org ?
Tuko pia kwenye mitandao mingi ya podikasti, na unaweza kutupata kwenye Facebook : na You tube, kwa anwani hii :
''Encouragement pour les planteurs d'églises de village/Multiplier ''.
Ilikuwa ongezeka, asante na Mungu awabariki !

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni