Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Yesu alimwambia Petro na marafiki zake: ''munifuate na nitawafanya kuwa wavuvi wa watu''. Pengine uliwai kama mimi kusikia hadisi na kujibu ''napenda kuwa muvuvi wa watu. Nifanye na mimi kuwa muvuvi wa watu. Kuvuwa watu siyo rahisi. Kuita wanaume na wanawake, wavulana na wasichana kutubu na kuamini Habari Njema mara nyingi ni kazi ngumu.
Najuwa ilinifikia kutumika nguvu kwa kujitayarisha kwenda kutangaza injili. Nilitayarisha vizuri sana ujumbe wangu. Niliomba sana. Na baadaye, nilipofika kwenye mahali, nikahubiri na sikuona matokeo yoyote. Umekwisha wai kuishi tokeo hili?
Inavunja moyo. Lakini baada ya miaka 30 tangia nilipoanza kuhubiri Habari Njema, nilijifunza kuwajuwa wa amani. Luka 10:1-12 inatufundisha kuwa Mungu anatusaidia kupata wanaume na wanawake walio na kiu ya kumjuwa. Wakati tunagawanya Habari Njema, wanasikia. Wakati tunapo wapendekeza kuomba, wanafurahia Sisi kuifanya. Wakati wanapokuwa na maswali juu ya Biblia, wanayauliza... na wanasikia baadaye kila neno tunalotamka kama jibu. Wakati tunapowafundisha kutii Yesu wanafanya hivo. Watu hawa wanaitwa ''watu wa amani ''.
Wakati naenda kuvuwa watu na kama nawapata watu wa amani, ni kama vile sikuweza kutupa wavu na kuikokota. ''samaki'' hawa wanafanana kurukia ndani ya mtumbu wangu ! Ni sababu Mungu kwa neema yake, alitayarisha watu wa amani kujibu kwa Habari Njema.
Wakati wa mwezi wamunane, wakenda na wakumi, mutatumika kwa upandaji wa makanisa mapya. Lakini Mungu hakungojea mwezi wa munane ili kuanzisha huu mradi. Mbele ya mwezi wa munane, alitumika katika roho za wanaume na wanawake walio na njaa ya kumjuwa Mungu. Ni kwenu kuwapata.
Kupata watu wa amani ni fungulo kwa kupanda makanisa mapya katika vijiji visivyo na kanisa.
Lakini muliwafundisha wanafunzi wenu kutafuta watu wa ?
Muliwahafisia hadisi ya mwanamuke kwenye kisima. Alikuwa akiisha kwa ukahaba, lakini alipokutana na Yesu, roho yake ilibadilishwa na, kupitiya yeye, kijiji chake kilibadilishwa pia (Yohana 4).
Muliwaambia wanafunzi wenu kuhusu Kornelio, askari wa kirumi aliye muita Petro kufika nyumbani kwake?
Kupitiya Kornelio, jamaa yake yote ilipokea Habari Njema na Roho Mtakatifu akawashuka kwao wote. (Matendo 10). Muliwafundisha wanafunzi wenu kutafuta watu wa amani kwa kugawanya ushuhuda wa sekundi 15 ? Muliwaonyesha namna ya kuwapendekezea kuombea wagonjwa na maitaji mengine ya watu walio mbali na Mungu ? Mulikwenda pamoja na wanafunzi wako wakati ulipo muuliza mtu moja ''naweza kukuhadisia hadisi ya Biblia ambayo imenigusa sana ?
Umekwisha kuwaonyesha tu namna ya kuhadisia hadisi ya Biblia na baadaye kuwaambia maana kwa kuuliza maswali sita rahisi ?
Wanafunzi wako wanajuwa kutafuta watu wa amani ? Ni mda wakuwafundisha. Ni mda wakuwasaidiya wa kujaribu tendo la Mungu kwa kutafuta na kupata watu wa amani ! Tuko katika mwezi wa kwanza wa Siku 90 za kifungo na maombi kanisani. Ni wakati wa kufundisha wanafunzi wako ginsi ya kupata watu wa amani. Ni wakati wa kwenda pamoja nao katika vijiji ambako hakuna kanisa ili waweze pamoja nawe, kuvuwa watu. Ni kwa mda huu unastahili kufurahi pamoja wakati wewe pamoja na wanafunzi munawapata watu wa amani.
Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis nawauliza ''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni