Jumatatu, 23 Septemba 2024

Hamasisha Waombaji - Siku 90 za Maombi na Kufunga



 

Hamjambo nyote !

Hamjambo wapandaji wapendwa. Tazama ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wote wa makanisa katika vijiji.

Mimi ni Mchungaji Douti Claude Kasisi wa VCP.

Turu ya mwisho, niliongelea kuhusu unyenyekevu ndani ya upandaji wa makanisa.

Tangia mda uliyopita, maneno yetu yote ya kutiya moyo yanahusika na siku 90 za kifungo, maombi na upandaji wa makanisa.

Asubui hii, nitaongelea kuhusu maombezi. Ninaipa jina la ''kuhamasisha waombaji''.

Kwa kipindi hiki cha siku 90 za kifungo, maombi na upandaji wa makanisa. Nitawapa moyo, Kaka na dada wapendwa kwa kuhamasisha waombaji wote.

Muombaji ni nani ?

Muombaji ni yule anayekuwa katikati ya Mungu na wanadamu ili kutetea itaji za watu. Ukiwa muombaji, uko msaada unayejiweka karibu na mtu.

Tunastahili kuonyesha maono ya VCP kwa makanisa shirika, kwa ndugu zetu, ndani ya kila kanisa, katika Afrika nzima. Kwenye Tik tok, Facebook ....

Tuongelee kuhusu maombi. Ni maombi ndiyo inayoweza kuokowa Afrika.

Kuanza leo, viongozi wa inchi zetu za Afrika wanaonyesha uzaifu mwingi usio weza kusaidiya makanisa, isipokuwa kuyasumbuwa.

Nguvu yetu kwa kipindi hiki ingekuwa maombezi, maombi tu ili kubaki kwenye uwepo wa Mungu na Mungu atagusa roho za viongozi.

Alibadilisha viongozi wote ili kwamba watu watoe maisha yao yote kwa Yesu ili kwamba Afrika iokolewe. Maombezi yako na nguvu.

Mtume mkubwa Paulo aliomba maombezi kwa makanisa. Akatuma baruwa kwa kanisa la Efeso katika kitabu cha Waefeso 6 :18-19 

''kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; 

[19]pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili.''

Kaka na dada, nawapa moyo kupitiya maneno haya kuhamasisha hesabu kubwa ya waombaji hata kama wengine miongoni mwao hawawezi kufunga, washirikiane wote kwa maombi kwa mda huu wa siku 90 kwa ajili ya Afrika. Ni kwa ajili ya wokovu wa Afrika. Pandeni makanisa mengi inamaanisha kuleta suluhusho kwa wa Afrika wengi.

Ninawapa moyo kuifanya kwa moyo wa kuchangamka na upendo mkubwa.

Hamasisha waombaji kwa ajili ya vijiji vyenu, nyumba zenu, kwa marafiki zenu.  Sababu gani kuangalia podikasti za mambo ambayo hayakuletei faida yoyote kwenye Tik tok mahali wanaongelea tu siasa, ununuzi wa vifaa vya vita, mahali ambako tunaona tu vita, lakini mahali ambako tunaweza simamisha vita kuipa tena Afrika amani kupitiya maombi, kifungo, kupitiya nguvu ya kanisa. Ninawapa moyo, Kaka na dada, kwakujiweka sawasawa kwa ajili ya maombi.

Acha Mungu awabariki, awape nguvu kwa mda huu wa siku 90 za kifungo, maombi na upandaji wa makanisa ili kuona matokeo ya maombezi.

Amani kwenu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...