Jumatatu, 23 Septemba 2024

Gawanya Ushuhuda Wako Wa Sekundi 15 - Siku 90 za Maombi na Kufunga




 

Hamjambo wandugu wapenzi Kaka na dada wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Nawasalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu-Kristo. Napendelea kuwaambia asubui ya leo kuhusu ushuhuda wa sekundi 15.

Tunaweza kupata Mada hii ndani ya kitabu cha VCP Fundisha na ongezeka muhula wa 1 katika ukurasa wa 66-18 hadi 66-27.

Wandugu wapenzi Kaka na dada, wakristo wengi hawajuwe namna ya kutangaza injili. Namna gani kuwakaribia watu ?

Wakristo wamoja wanasema kama watu hawatajiamini wenyewe, wengine wanasema hawajuwe nini watasema, wengine wakristo wako na haya na mtindo huu wa tabia unapunguza mwendo wa kazi ya Mungu.

Muniruhusu niwakumbushe, wapandaji wapenzi kwamba ushuhuda wenu wa sekundi 15 unaweza kuleta msisimuko wa mawazo, kufunguwa vifungo vya roho zilizo ngumu.

Ushuhuda wa sekundi 15 ni nini ?

Wakati unapenda kutumikisha ushuhuda wa sekundi 15, Utakutana kwanza na mtu, unakutana na msikilizaji wako baadaye unamusalimia, na unamwambia : tafazali, naweza kugawanya nawe hadisi ndogo ? Watu wote wanapenda hadisi, sherti watakubali kukusikiliza kwa makini na baadaye utawaambia ''kwa wakati mwengine ilifikia kwa maisha''.

Kila ushuhuda wa sekundi 15 unaanza na msemwa huu ''ilifikia wakati mwengine ndani ya maisha yangu''. Baadaye utawaambia kuhusu maisha Yako kabla haujampokea Yesu, kisha utasema namna gani rafiki ao ndugu yako alikueleza kuhusu Yesu na ukampokea kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako binafsi, baadaye utamuhadisia namna gani Yesu alibadilisha maisha yako.

Usisahau kumuuliza swali hili:

Je! Unaweza kuwa na hadisi kama hii ya kugawanya nami ?


Akisema ''ndiyo'' utajuwa kama ni ndugu katika Kristo na hapo utaweza kusherekea na kumsifu Mungu pamoja naye.

Akisema ''hapana'', endelea maongezi naye ukimuuliza ''unaweza kuniruhusu nigawanye nawe uzoefu mzuri niliopata ndani ya Yesu? Akijibu ''ndiyo'', unapata tena fursa ya kumwambia kuhusu Yesu kama Bwana na Mwokozi. Akisema ''hapana'', usimukaze. Kubali maamuzi yake. Baadaye, munaweza kubadilishana namba za simu na kuendelea kumuombea.

Hiyo ndiyo ushuhuda wa sekundi 15. Chombo hiki kinanguvu sana, usichoke.

Uko na hatuwa ine za kutenda wakati unaendelea kuongea kuhusu ushuhuda wa sekundi 15.

- kipindi cha 1: ilifikia wakati mwengine katika maisha yangu wakati niliteseka mbele ya kumjuwa Yesu-Kristo .

- kipindi cha 2: rafiki ao ndugu yangu alinieleza kuhusu Yesu.

- kipindi cha 3: nilimukubali kuwa Bwana na Mwokozi wangu binafsi, ni mageuzi yaliyo tendeka ndani ya maisha yangu. Leo, nina amani rohoni mwangu.

- kipindi cha 4: swali la muhimu : je! Unayo hadisi kama hii ya kuhadisia ?

. Mungu awabariki, wapenzi wapandaji wa makanisa.

. Nafurahia kazi yenu ngumu kwenye vijiji ili kuwapata watu wa amani na kugawanya ushuhuda wa sekundi 15.

Amani ya Mungu iwe pamoja nanyi. Mimi ni Mtumishi wenu, Mchungaji Douti Claude, Kasisi wa VCP.

Ulikuwa ongezeka.

Shalom.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...