Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji
Mkutano wa Siku 90 za maombi, kifungo na upandaji wa makanisa ! Ni bora zaidi !
Ni nini Mungu angefanya kwa kujibu maombi yetu ?
Ni milango gani itafunguliwa wakati tutajielekeza kwenye vijiji visivyo na kanisa ?
Ni roho gani ngumu zitatulizwa ? Ni nani ataokolewa wala kuponywa ?
Siku 90 za maombi, za kifungo na upandaji wa makanisa zitaanza tarehe 01/08/2024.
Wapandaji wa makanisa na washirika wao katika inchi 32 za Afrika wataomba hawa wakiombea wengine.
Kipindi cha kwanza kinahusu kuhamasisha waombaji kuanza sasa. Waambie kuanza hivi sasa washiriki wa kanisa lako na kwa wasimamizi wa makanisa jirani kuhusu kuzingatia kwa kujitowa juu ya maombi kuanza, tarehe 01 Agosti 24. Tunapendelea kuleta Habari Njema ya Yesu na uwezo wake wa wokovu kwa maelfu ya vijiji vya Afrika visivyo na kanisa.
Waombe washiriki wa kanisa lako na wachungaji wa makanisa mengine wajiunge nanyi kwa maombi.
Soma mwongozo wa maombi inayotumwa na hii podikasti.
Baadaye gawanya kupitiya WhatsApp kwa waombaji wengi. Waambie waombe mara tatu kwa hizi itaji 30 za siku 90 kuanza tarehe 01 Agosti 24.
Ndani ya mukutano yenu ya maombi, waombe washiriki wenu wajihusishe juu ya maombi kwa ajili ya waliopotea na kwa ajili ya wapandaji wa makanisa mapya ya kizazi cha kwanza, cha pili na cha tatu watakao kwenda kwenye vijiji visivyo na kanisa ili kuenenda kwa maombi na kupata watu wa amani. Sema kwa wanaume na wanawake hawa kuanza leo.
Gawanya maoni !
Usisahau kwamba lengo letu ni kila kanisa la VCP lianze kanisa lingine mpya katika Kijiji kisicho na kanisa.
Tunapenda kufikia lengo hili ifikapo tarehe 29 oktoba 24. Makanisa mpya yatakayopandwa yatendelea kukomaa na kuendelea baada ya mwezi wa Oktoba. Lakini lengo letu ni kuanzisha maelfu ya makanisa mapya katika kipindi hiki cha Siku 90.
Ndani ya mwezi wa Agosti, fuata maelekezo ya Mkufunzi wako wa VCP. Mukutanane na marafiki wenzenu wapandaji wa makanisa katika vituo vya majifunzo. Kama uko na afya njema, fanya kifungo. Watu wote wataomba. Nyenyekeeni mbele za Mungu. Mungu anapingana na wenye kiburi, lakini anawapa wanyenyekevu neema. (Yakobo 4 :6). Kama uko na dhambi maishani mwako, uihungame. Fanya uzoefu wa utakaso wa Mungu.
Baadaye, waite kwa ajili ya vijiji vilivyo karibu na kituo chako cha majifunzo, visivyo na kanisa.
Baada ya kipindi cha maombi, Mkufunzi wako atakuongoza kwenye mtiani wa kanuni za msingi za upandaji wa makanisa.
Wakati unapo rudilia mfano wa shamba ine kwa kujihusisha juu ya shamba la kwanza na la pili, acha moyo wako ujae na imani kwa kugunduwa watu wa amani na uanzishaji wa makanisa mapya. Kila Juma ya mwezi wa munane, mutakutana ndani ya kituo cha majifunzo ili kuomba na kupata misingi ya upandaji wa makanisa.
Ndani ya mwezi wa munane na wa kenda, wewe na wapandaji wa makanisa mapya mutatembea ndani ya maombi kwenye vijiji visivyo na kanisa. Mutaomba kwa ajili ya maitaji ya watu, mutahadisia hadisi za Biblia, mutagawanya filamu ya Yesu na kutumikisha miviringo tatu ili kuita watu kwa toba na kwa imani ya Kristo. Hapa Mwezi wa Oktoba, kila Mpandaji wa kanisa ataombwa kutafuta mahali ambako waamini wapya wataweza kukutanana kwa ajili ya ibada na kujifunza namna ya kumtii Mungu na Agizo Saba za msingi za Kristo.
Na usisahau kama wapandaji wa makanisa 13 000 wanakusaidia katika maombi, kama vile naweye unavyo wasaidia !
Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi ni Dean Davis nikiwauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni