Jambo kwa wote ! Naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Injili ya Marko ni mfupi kuliko hadisi ine za maisha ya Yesu ambayo tunaita '' Injili ''. Marko anaingia moja kwa moja ndani ya hadisi ya Yesu kwa sura 1, vesi 14, akisema :
'Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akihubiri Habari Njema ya Mungu,'' alikuwa akisema : '' mda umefika. Ufalme wa Mungu umekaribiya. Tubuni na kuamini Habari njema !"
Agizo la kutubu na kuamini Habari Njema, ndiyo ya kwanza miongoni mwa zile tunazoita leo Agizo saba za msingi za Kristo.
Tunafundisha Agizo hizi saba za msingi ili kusaidia watu kuishi kama wanafunzi wa Yesu.
Sisi kama wapandaji wa makanisa, tunajuwa kama maisha ya watu yatabadilishwa kama wakiweka tumaini lao kwa Kristo na kumtii. Tunaelewa kama ''Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. (Yohana 10:10)
Na tunajuwa kwamba watu wa kila aina wanapenda maisha bora : maisha ya amani, ya tumaini na yenye mwelekeo, maisha yanayojaa upendo.
Kwa hiyo, sababu gani inakuwa vigumu kwa baadhi ya watu wanao sikia hadisi kubwa ya Mungu, pamoja pia na hadisi ya Yesu na upendo wake, kutubu na kuamini Habari Njema ?
Pengine ni sababu hawaamini kabisa kama Ufalme wa Mungu umekaribia.
Watu wanao shiriki madhehebu ya kiasili wanaamini Mungu, lakini wanazania kama iko mbali nao. Watu wanaoshiriki dini ya Uislamu wanakazia sana juu ya ukoo wa Mungu, yaani yeye yuko juu sana na ulimwengu ulio umbwa Wala hahusiki nayo. Wakristo wengi wa jina wanazania kama Mungu anashugulikia sana maswala makubwa ya muhimu kwa hiyo hausike kabisa nawao. Lakini Yesu alisema kama Ufalme wa Mungu umekaribiya.
Kama watu wanaweza kuamini kwamba ufalme wa Mungu umekaribiya, itakuwa kwao rahisi sana kutubu na kuamini Habari Njema.
Kwa hiyo, sehemu kubwa ya kazi yetu sisi kama Wainjilisti walio jitolea na upandaji wa makanisa unahusu kusaidia watu kuelewa kama Ufalme wa Mungu umekaribiya.
Kazi yetu ya uinjilisti inahusu kutangaza kama Mfalme mwenye nguvu na mwenye upendo, Yesu, yuko hapa pamoja nasi sasa : ili kusamea na kuponya, ili kununuwa na kuokowa.
Kama watu wanaweza kuamini tu ya kwamba Ufalme wa Mungu umekaribiya, itakuwa kwao rahisi sana kutubu na kuamini Habari Njema.
Kuko hatuwa tatu maalum kupitiya hizo tunawasaidia watu kuamini kwamba ufalme wa Mungu umekaribiya : tunagawanya ushuhuda wetu, tunasimulia hadisi ya Yesu na tunaomba. Tunahadisia yale ambayo Yesu alifanya kwetu.
Tutasema kwa wazi kuhusu uwezo na upendo wake ukitenda kazi ndani ya maisha yetu.
Tunahadisia pia matendo yake yenye nguvu na upendo wake wa ajabu wakati aliposhinda mwili hapa duniani, imepita miaka 2000.
Na tunaomba pamoja na watu na kuombea watu, ili waone uwezo wa Mungu ukionekana kupitiya maombi yaliyojibiwa.
Wakati watu wanasikia ushuhuda wetu na hadisi ya Yesu, wakati wanaona Mungu akijibu maombi, imani inaanza kukomaa ndani yao.Wanaanza sasa kusemezana :
Pengine ni kweli Ufalme wa Mungu umekaribiya. Pengine Yesu anaweza hakika kunipa maisha tele, yenye kujaa tumaini, ya furaha, ya upendo na mwelekeo."
Ndipo kwa wakati huo tunaweza kuwaalika wazi wazi, lakini kwa upole, kutubu na kuamini Habari Njema kuhusu maisha, kifo na ufufuko wa Yesu.
Wakati rafiki zetu wanajuwa kama Ufalme wa Mungu umekaribiya, nawao pia watatubu, wataamini na watabadilishwa kupitiya uwezo wa Mungu.
Ilikuwa " Ongezeka."
Na mimi, Dean Davis, nawauliza swali hili :
Ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni