Jumatatu, 31 Agosti 2026

Maendeleo ya Uongozi - Uchaguzi wa Yesu katika maombi na wito wake kupitiya kura

 









             Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti iliyo na shabaha ya kuleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi katika vijiji.

Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi.

Katika podikasti zangu zilizopita, niligawanya mawazo juu ya maendeleo ya Uongozi kupitiya maneno ya Claude, Kasisi wa upandaji wa makanisa katika vijiji (VCP), Peter Kasisi makamo wa VCP na Fidélité, Mkurugenzi wetu wa Dynamic women katika Bara la Afrika.

Leo, na katika mtiririko wa podikasti zinazokuja, napendelea kupekuwa kwa ndani mafundisho ya Yesu kulingana na maendeleo ya Uongozi. Tunaanza na Kutambuwa kwamba, wakati ilipofikia kipindi cha kuchaguwa wa Mitume wake kumi na mbili, Yesu aliifanya akiwa katika maombi. Kwa kulinganisha na hayo, wito wake ulikuwa wa kuchagua.

Katika Luka 6:12-13, tunasoma : "Luka 6:12-13

[12]Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. 

[13]Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume"

Yesu kuchaguwa Mitume kumi na mbili, ilikuwa azimio kubwa ya muhimu kwa Kristo.

Walikuwa watu ambao pamoja nao atakuwa nawao miaka tatu ijayo, watu atakabizi kuendelea na kazi yake baada ya kurudi kwake mbinguni. Ni muhimu kuonyesha kwamba Yesu alikuwa Mungu pia Mwanadamu katika maisha yake yote hapa duniani. Na mbele ya kuchaguwa viongozi hawa, maandiko yanatuonyesha kwamba alikesha katika maombi usiku mzima.

Shurti ambalo tunaweza kuchukuwa hapa ni kwamba, tukiwa viongozi, tunapashwa kuomba wakati tunachaguwa viongozi wanaojitokeza 

watakao alikwa kujiunga kwa kazi.

Vile miaka inavyopita, niligunduwa mara nyingi kama azimio hizi zilichukuliwa kwa urahisi sana ndani ya kanisa. Ni muhimu mtu kutekeleza kazi ndani ya huduma, na apatikane "mtu aliye tayari ", msemwa unaomaanisha mtu anayejikuta kuwa tayari kwa mda huo na kumuweka katika kazi bila kuchukuwa mda wa kuomba na kufikiria vizuri uchaguzi wake. Mchakato kama huu wa uchaguzi mara nyingi unaleta matokeo mabaya.

Kwa kuunganisha na uchaguzi wa maombi, tunapata shurti la pili : Yesu alitangaza wito wa uchaguzi. Maelezo ya vesi ya 13 inatuonyesha kama Yesu alikuwa pamoja na kundi ya wanafunzi wake, inamaanisha wale walio mfuata. Kupitiya kwa kundi hili kubwa zaidi, Yesu alichaguwa ndani yao kumi na mbili ili wawe Mitume wake.Shurti ya maendeleo ya Uongozi ninayo chunguza hapa ni kwamba : wakati tunatarajia kuchaguwa viongozi wanaojitokeza, tunastahili kuwapitisha kwa kura.

Ninawatuma katika podikasti yangu ya tarehe 24 Aprili, ambamo ndani yake nilionyesha kwa kifupi baadhi ya tabia ninazo zitafuta kwa viongozi waliyo tayari. Pengine unawezakuwa na horoza yenye utofauti mdogo.

Ya muhimu ni kwamba tufanye kura, tukizingatiya juu ya tabia za muhimu ambazo tunatarajia kuona kwa viongozi wanaokuja.

utambulisho wenye mizizi ndani ya Kristo 

 mnyenyekevu  kazi zao walizofanya Siku za nyuma na uchuzi wao uliopita

 ushupavu wao katika kazi mbali mbali

 uwezo wao wakuchukuwa uwamuzi

- wito mkubwa wa kujifunza na kukomaa

- moyo uliyo tayari kupokea mafundisho 

- mtu mwema

- sifa yao, ndani ya kanisa hata karibu na watu walio inje na kanisa

- ndoa iliyo nguvu na yenye msingi juu ya Kristo 

Ni neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi katika vijiji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Usikawize ubatizo

  Karibu kwenye ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, kwa wachungaji na viongozi wa Kikristo. Mimi...