Alhamisi, 13 Agosti 2026

Sababu gani kufundisha amri 7 za msingi za Kristo ?

 










Karibu kwenye ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, wachungaji na viongozi wakikristo.

Mimi ni muhamasishaji wenu Daneille Snowden kwa siku ya leo.

Mathayo 28:18-20 inasema : 

''Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 

[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 

[20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.''

Mada maalum ya mfikiri yetu ya leo ni kufundisha utii kwa amri za Kristo. Neno la Mungu linatafsiri utii kama tendo la kusikiliza kwa makini Mungu, kumtegemea na kunyenyekea chini ya mapenzi yake. Kwa kutii amri za Yesu, mwamini anaonyesha uaminifu wake kwake na kujitolea kwake.

Tusisahau kamwe mfano kamili wa utii ambao Yesu alituonyesha, kama tunavyosoma katika Wafilipi 2:8 :

''tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.''

Shabaa ya Mchungaji wa kanisa, Mchungaji wala kiongozi wowote ule wakikristo ni kufundisha utii. Kwa kutii amri za Yesu, tunakuwa pia mashahidi wa namna anavyobadilisha maisha na vizazi vyote, ndio maana ya kufanya wanafunzi !

Wakati Yesu alipowaita kila moja wa wanafunzi wake, alikuwa akisema ''nifuate.'' kwa kumufuata, tunapendelea kumpendeza na kumtii.

Tufanye kifupi cha amri saba za msingi za Kristo :

1. Tubuni na muamini (Marko 1:15)

2. Mubatize waamini wapya (Mathayo 28:19)

3. Mpende Jirani yako (Mathayo 22:37-39)

4. Shiriki Meza ya Bwana (Luka 22:19-22)

5. Ombeni na kutafakari Neno la Mungu (Mathayo 6:9-13)

6. Towa (Luka 6:38)

7. Fanya wanafunzi (Mathayo 28:19-20)

Wakati nilipokuwa shuleni ndani ya shuke letu la Biblia na wakati walipotufundisha amri za Kristo, moyo wangu ulijaa na huruma mwingi : jambo la kwenda tu na kuzingatiya amri hizo, maisha yangu yote !

Nikiwa bado binti kwa mda ule, na leo nakuwa mwanamuke mwenye uzoefu, naweza kushuhudia kwamba amri 7 za msingi za Kristo bado zingali muhimu sana ninapo shuhidia maisha ya wengi yakibadilishwa kwa utukufu wa Mungu. Ninapo fundisha amri hizo, tunaleta TUMAINI duniani mzima kwa utii wetu.

Ilikuwa Ongezeka.

Usikose kugawanya podikasti hii pamoja na wengine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Usikawize ubatizo

  Karibu kwenye ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, kwa wachungaji na viongozi wa Kikristo. Mimi...