Jambo kwa wote. Naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Moja ya bahati ya kipekee kwa Mchungaji wa kanisa ni kuwa mwakili wa Kristo. Wewe kama Mwakili wa Mungu, tunaenda katika mahali pasipo julikana na tunatangaza Habari Njema. Ni bahati kubwa ya kipekee kutangaza Habari njema. Mungu alituona tukipambana ndani ya dunia iliyo vunjika, tukijaribu kujiokowa kwa namna yetu. Alituma Mwana wake Yesu kuja kujenga ufalme mpya wa haki, wa amani na furaha. Yesu alimshinda Shetani kwa nguvu za maisha yake bila dhambi na kwa ufufuko wake wa mwili.
Ndiyo Habari njema tunayo tangaza sisi kama mawakili wa Kristo.
Kwa hiyo, shetani, mpinzani aliye shindwa na Mungu, anaendelea kutenda kazi kwa kuiba, kuuwa na kuharibu. (Yohana 10:10), anatafuta kutuzuwia kupatanishwa na Mungu. Kila moja wetu, kwa kuja duniani, alikuwa mwenye kufa kwa ajili ya makosa na dhambi zake. Tunafuata njia za dunia hii na kanuni za nguvu za anga, roho itendayo kazi kwa sasa ndani ya wana wa kuasi. Sisi nasi, tuliishi zamani pamoja nao, tukitimiza tamaa za utu wetu wenye dhambi na kufuata mapenzi na mawazo yake. Kama wengine, tulistahili kupata ghazabu ya Mungu. Lakini Mungu, aliye mwenye rehema nyingi, kwa sababu ya upendo mkuu ambao aliotupenda, alitufufuwa pamoja na Kristo wakati tulikuwa wafu ndani ya makosa yetu.
Ni kwa neema uliokolewa. Alitufufuwa pamoja na Kristo na akatuketisha pamoja naye mahali pa mbingu katika Yesu-Kristo, ili kuonyesha katika miaka ijayo utajiri usio na mipaka wa neema yake, unao onekana kupitiya wema wake kwetu katika Yesu-Kristo. Kwa hiyo, mumeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani. (Waefeso 2:1-8).
Sasa, sisi kama wapandaji wa makanisa, tulio okolewa kwa neema ya Mungu kupitiya tendo la Kristo, tunaenda pale ambapo Kristo hajulikane. Tunaalika waliokufa katika makosa na dhambi zao ili wazaliwe upya kama watoto wa Mungu.
Hiyo, kwa hakika, ni tendo la vita vya kiroho.
Wakati wote tunapo tangaza Kristo, wakati wote unapo onyesha upendo wake, wakati wote unapo inuwa juu Jina la Yesu, unashindana na adui. Wakati wote unapo tangaza kwa wazi na kwa uaminifu Neno la Mungu, unaendelesha ufalme wa Mungu. Wakati wote mtu aliye potea anapotubu dhambi zake na kuweka tumaini lake kwa Kristo, ufalme wa Mungu unaendelea zidi ya ufalme wa mpinzani wetu.
Na shetani hafurahie wakati ufalme wa Mungu unaendelea zidi yake.
Analipiza kisasi kama simba mwenye hasira, akitafuta nani atameza. Lakini hatuko miongoni mwa wenye woga wanao rudi nyuma. Tukiwa wapandaji wa makanisa wenye hekima, tutavaa silaha zote za Mungu (waefeso 6:10-18).
Kwa kujilinda, tuchukuwe upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu. Tuhamasishe taifa la Mungu ili waombe kwa ajili yetu na kwa ajili ya watu watakaopata maisha tele ndani ya Kristo kupitiya ujumbe wetu.
Baadaye tuendelee kwa uhakika. Vita vya kiroho siyo rahisi. Mpinzani wetu anatushambulia kwa kila kipindi. Lakini aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yeye aliye duniani (1Yohana 4:4).
Sasa, wapenzi wapandaji wa makanisa, vaa silaha zote za Mungu. Omba bila kukoma. Hamasisha waombaji. Mpende jirani yako kama nafsi yako mwenyewe. Tangaza Habari njema katika nguvu za Roho Mtakatifu. Weka tumaini kwa Mungu ili kuokowa jamaa nzima na nguvu za adui, ili wao pia wawe na uzima tele ndani ya Kristo.
Ilikuwa ''ongezeka'', mimi ni Dean Davis. Nawaacha na swali hili :
''ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ? ''

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni