Jumatatu, 31 Agosti 2026

Tayarisha waamini wapya kwa ubatizo

 









      Jambo kwa wote ! Naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Shurti lililotolewa na Yesu katika Mathayo 28 linatupa maelekezo ya umisheni. Bwana wetu alisema : "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 

na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari"

Wakati tunaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume, tunaona ni kwa namna gani Mitume pamoja na wanafunzi wao, walivyotii Agizo. Sehemu moja muhimu ya mafundisho ya wanafunzi inahusu kubatiza. Na katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kanuni thabiti inajitokeza :

Kubatiza bila kupoteza mda.

Siku ya Pentekoste, Petro liuliza wasikilizaji wake pa Yerusalemu kwamba "watubu na kila moja wenu abatizwe kwa Jina la Yesu-Kristo, kwa ajili ya musamaha wa dhambi zenu" (Matendo ya Mitume 2:38). Baadaye kidogo, watu 3000 wakabatizwa.

Wakati Filipo alihubiri wakaaji wa Samaria, wengi waliamini. Biblia inasema katika Matendo 8:12 : "Matendo ya Mitume 8:12

[12]Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake."

Baadaye kidogo, wakati yule Towashi mwethiopia alipo elewa Habari Njema ambayo Filipo alimueleza, akasema : "tazama maji ; ni nini basi kinanizuiya nisibatizwe ?" Na Filipo akambatiza.

Ubatizo wa Sauli katika Matendo 9, pia ule wa Kornelio pamoja na nyumba yake yote katika Matendo 10, pia ubatizo wa Lidia pamoja na nyumba yake, pia ule wa mlinda Gereza pa mji wa Filipi, akibatizwa pamoja na familia yake, wote wawili wakiripotiwa katika Matendo 16, pia ubatizo wa Crispus pamoja na nyumba yake yote katika Matendo 18, zinasimulia zote hadisi ya kufanana. Mitume na wanafunzi wao walibatiza wale walio sikia na kuelewa Habari Njema ya Yesu bila kupoteza mda.

Lakini ubatizo wa bila kupoteza mda, haukufanyika katika makanisa yaliyopandwa baada ya kipindi cha Mitume.

Makanisa mengi yalishurutisha vipindi virefu vya katekismu ao mafundisho ya kutayatisha ubatizo mbele ya kubatiza waamini. Wengine walipitisha mda mbele ya kubatiza sababu walitarajia kusubiri kuona matunda ya toba, wala tu hawakuwa na uaminifu na waamini wapya. Lakini hiyo haikuwa mtindo wala matendo ya Mitume.

Kanisa lako linatumika namna gani ? Wazee wanafundisha nini, wachungaji, wasimamizi ao maaskofu wa kanisa lako kuhusu mda unaofaa kubatiza na matayarisho yanayostahili kwa ubatizo ?

Kama haujue, nakuhimiza kutafuta hiyo habari kwa makini.

Lakini angalia kanuni moja ambayo naweza kuwapendekezea ili kuwasaidia kuhusu mda unaofaa kubatiza waamini wapya : muwabatize bila kupoteza mda.

Muhakikishe kama wameelewa injili.

Muongee nao ili muhakikishe kama wanamjuwa Yesu vizuri akiwa Mfalme wa maisha yao.

Muwafundishe ubatizo na maana yake.

Muhakikishe kama wameelewa damu inaosha roho zetu na kwamba maji ya ubatizo inamaanisha huo utakaso.

Muwasaidiye kuelewa kuwa wakati wanapotoka ndani ya maji baada ya wao kubatizwa, wanasimama ili kuishi maisha mapya ndani ya Kristo.

Muwasaidiye pia kugawanya Habari Njema pamoja na jamaa zao.

Lakini musikawize ubatizo wao.

Muhubiri Habari Njema. Mutayarishe kwa ubatizo wale wanaoelewa Habari Njema na wanaoweka tumaini lao kwa Kristo.

Muhakikishe kama hawa wanafunzi wapya wa Kristo wanabatizwa bila kukawa.

Ilikuwa ''ongezeka'' na mimi Dean Davis na ninawauliza swali hili : ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Usikawize ubatizo

  Karibu kwenye ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, kwa wachungaji na viongozi wa Kikristo. Mimi...