Alhamisi, 13 Agosti 2026

Maendeleo ya Uongozi - Kuonyesha mfano, kushindikiza, Kuchunguza na kuachilia kutenda

 








    Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wa Kikristo katika vijiji.

Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Katika podikasti zangu mbili za nyuma, nilizungumza na Peter Baraka, kasisi makamo wa upandaji wa makanisa katika vijiji (VCP), pamoja na mke wake, Fidélité Ramla. Kiongozi wa Dynamic women kwa Bara la Afrika. Katika mazungumuzo yetu, Fidélité alionyesha mtindo wa maendeleo ya Uongozi ambao unazungumzwa mara kwa mara katika Shirika la VCP :

Kuonyesha mfano, kushindikiza, Kuchunguza na kuachilia kutenda 

- MAOL (MAWL)

Mbinu hii siyo ya VCP, wala siyo mpya. Kinyume chake, tunaona Yesu-Kristo na Mtume Paulo wakiitumikisha katika huduma yao. Hata naweza kusema kwamba mtindo MAOL (MAWL) ni muhimu sana kwa upandaji wa makanisa wa kizazi baada ya kizazi. Viongozi wakitume hawaishi katika hali ya kuboreka. Wanaandaa na kuwapa majukumu watu wengine ili kwamba waendeleshe kazi, wakiweka tumaini lao kwa Roho Mtakatifu ili kuwaongoza na kusaidia kizazi kijacho cha viongozi.

Kuonyesha mfano 

Tunaonyesha namna gani vitu vinafanyika. Paulo alisema : ''munifuate mimi, kama ninavyo mfuata Kristo.'' (1wakorinto 11 : 1)

Tunaonyesha ujuzi, njia ao mwenendo katika muktadha wa ulimwengu halisi. Viongozi wanaongoza kupitiya mfano kwa kueleza mawazo yao kadiri mda unavyoendelea.

Muniruhusu nirudilie : wakati tunapo tayarisha viongozi, hatuwaonyeshe tu namna vitu vinafanyika ; tunawaelewesha pia namna yetu ya kufikiri.

Paulo alikuwa na wanafunzi wengi ambao alitayarisha kuwa viongozi, kama vile Sila, Timotheo, Tito, Luka na wengine wengi.

Kiongozi wa VCP, ni viongozi gani anayejitokeza ambaye uko unatayarisha ?

Kushindikiza .

Kipindi cha kufuata kinahusu kufanya vitu pamoja. Tunatumika pembeni ya mwanafunzi. Tunampa marudilio ya hapo hapo, tunajibu swali zao na kuwatolea msaada ambao wanaitaji ili kutayarisha kwa pamoja uaminifu na ujuzi.

Barnaba alimshindikiza Paulo kwa mwanzo wa huduma ya pamoja. Tunasoma katika Matendo 11:25-26 : ''Kisha akatoka akaenda Tarso kumtafuta Sauli; 

[26]hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.''

Kuchunguza 

Kwa kipindi hiki, tunarudiya nyuma na tunachunguza. Tuna ruhusu mwanafunzi kuendelea mbele wakati sisi tunafuatilia kazi yake. Baadaye, tunamupa marudilio ya kujenga ili azidishe ujuzi wake na kuzidisha alama zake za uwezo.

Vipindi vya kushindikiza na Kuchunguza vinahusu kazi ya kurudiliya. Fursa nyingi za kutumika kwa pamoja na vipindi vingi vya uchunguzi ni vya muhimu kwa kurahisisha ukomavu wa kiongozi aliye katika majifunzo.


 Achilia kutenda 


Kwa mwisho, wakati kiongozi anayejitokeza yuko tayari, ni mda wa kumuachilia kutenda ili kurahisisha uhuru wa kujiamulia mambo. Tunastahili kuwa tayari kumwachia madaraka yote, tukiwa makini kwamba yuko na vifaa vyote, ujuzi na uaminifu muhimu ili kufaulu bila msaada wetu wa moja kwa moja.


Japo hiyo, tutakuwa tayari ili kumtolea, angalau, mashauri yanayoitajika.

Kumupa moyo pia kwa kila mara ni ya muhimu sana kwa kukomaa na kufaulu kwake.


Kuachilia kutenda mara nyingi ni kazi ngumu, lakini kipindi ni cha muhimu kwa maendeleo mema ya kiongozi.


Nafurahia sana Uongozi wa Peter na Fidélité, pamoja na utashi wao wa kugawanya nami haya mawazo.


Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Usikawize ubatizo

  Karibu kwenye ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa, kwa wachungaji na viongozi wa Kikristo. Mimi...