Jambo kwa wote. Mimi ni Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Wakati mtu anapo mpokea Yesu-Kristo kama Bwana na Mwokozi wake, wakati anapo zaliwa mara ya pili na kwa neema ya Mungu, anakuwa mtoto wa Mungu, anajiuliza kwa kawaida maswali mengi : ''na sasa ? Nini itatokea ? Haya maisha mapya ndani ya Kristo itafananishwa na nini ?'' baadhi ya waamini wapya wanapata jibu nzuri kwa swali hizi. Wengine, kwa bahati mbaya, hawapate majibu.
Unakumbuka kama uliwai kujiswali hizi swali ? Waamini wapya wengi hawaulize Mungu awajibu. Hawaulize hata kwa marafiki wao wakristo : ''ni kipindi gani cha kufuata kwangu kwa vile nimempokea Kristo ?'' wanajiuliza hizi swali wenyewe na mara nyingi, jibu sahihi wanayopata ni ''sijue'' cha kusikitisha, ni kwamba kama waamini wapya hawagundue kile Mungu anangojea kwa maisha yao mapya, wanarudilia namna yao ya zamani ya kuishi.
Ijapokuwa, Neno la Mungu linajibu swali hizi. Kipindi cha kufuata kwa mwamini mpya ni kujifunza kutii kwa amri za Yesu.
Yesu alisema katika Yohana 14:15 : mukinipenda mutazishika amri zangu.'' vesi zingine, zinaonyesha namna Bwana wetu anakazia haya mafundisho kwa kusema : ''anayeshika amri zangu nakuzitii, ndiye anipendaye. Anayenipenda atapendwa na Baba yangu ; nami pia nitampenda na nitajijulisha kwake ... Mtu akinipenda, atashika neno langu ; Baba yangu atampenda, tutakuja na kufanya makao kwake.''
Sisi kama wanaofanya wanafunzi, muwafundishe waamini wapya kumtii Yesu ili kwamba wafanye uzoefu wa upendo wa Mungu.
Mwamini mpya anaonyesha upendo wake kwa Yesu kwa kutii amri zake. Utii unakamilisha upendo alio nao kwa Mungu. Wakati tunapochaguwa sisi wenyewe kumtii Yesu, tunafanya uzoefu wa upendo, wa furaha na upole wa uwepo wake.
Ni uhakika wenye nguvu na wa wokovu.
Kufanya uzoefu wa uwepo wa Mungu kwa kutii amri zake inaleta furaha na amani.
Utii kwa Yesu unaleta baraka kwake anayetii, lakini pia kwa jamaa lake na jirani zake.
Lakini waamini wapya hawajajuwa hivo bado. Wanaitaji wafundishwe kutii kwa yote Yesu aliyo amuru. Yalikuwa maelekezo ya mwisho ambayo Bwana wetu alitowa kwa wanafunzi wake.
Aliwaamuru kwenda kwa mataifa yote na kuwafanya wanafunzi, ''kuwafundisha kuyashika yote niliyo waamuru''. Tunafanya wanafunzi kwa kufundisha watu kumtii Yesu. Namna hii ya kufanya wanafunzi inaitwa ''utume wenye msingi juu ya utii''.
Utume haihusike tu kabisa na kupokea mafundisho, wala kuishi maisha ya kiroho. Kuwa Mwanafunzi wa Yesu, mbele ya yote ni kumtii. Ni kwa utii huo tunamuheshimu Mungu kwa upendo wetu na ndipo tunafanya uzoefu wa uwepo wake kwa namna mpya na ya kina, ndipo anakuja kufanya makao kwetu.
Mimi ni Dean Davis, na ''ongezeka'' nawaacha na hili swali : ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni