Jambo, tazama ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji. Mimi ni Brad Snowden.
Juma lililopita, podikasti yetu ilihusika na : "sababu gani kufundisha amri 7 za msingi za Kristo ?"
Amri ya kwanza ya Yesu ni : tubuni.
Neno la Mungu katika Mathayo 4:17 :
""Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.""
Yesu alianza huduma yake na neno hili : TUBUNI.
Hiyo inamaanisha kubadilisha namna ya kufikiri. Ni mabadiliko makubwa na yenye nguvu ambayo yanastahili kuwepo.
Maisha yetu ndani ya Yesu inaanza wakati tunakubali dhambi kwa huzuni na kumuomba atusamehe. Anatuosha sasa na damu yake na kubadilisha roho zetu kuwa mweupe kama balafu kwa hali ya kiroho.
Kwa hiyo, siyo jambo linalotokea mara moja tu ndani ya maisha yetu. Namna yetu ya kufikiri inastahili kuendelea kubadilishwa kila siku.
Tunaweza kuwasaidia wengine kubadilisha namna yao tu, kwa kuwahubiri Habari Njema. Wakati wanasikia kwamba wanaweza kuwa na maisha tofauti, maswali mengi yanatokea : namna gani naweza kuwa na maisha tofauti ? Sina namna ya kuwa na maisha mengine. Ni mpaka kwa hatuwa gani haya maisha mapya yatanibadilisha ?
Horoza ya maswali inaweza kuwa ndefu, lakini kila mojawapo inatupa fursa ya kugawanya Habari Njema ya Yesu-Kristo.
Roho zinaweza kubadilishwa wakati wanaelewa ukweli huu rahisi : neno "toba" siyo neno mbaya. Kinyume chake, ni habari nzuri, sababu inafunguwa roho ya kupokea Habari Njema ya upendo, ya musamaha kwa ajili ya kesho.
Ni nani asingependelea kujuwa tumaini hili ?
Kwa dunia, kuwa na matumaini inamaanisha mara nyingi kuwa na pesa nyingi ili chakula kisikosekane. Japo hiyo, tumaini inayotolewa na Mungu inaenda mbali zaidi ya hayo.
Kwa kuwa Mwanafunzi wa Yesu, inafaa mabadiliko makubwa ndani ya namna yetu ya kufikiri.
Kumepita miaka mingi, msemwa moja umekuwa maarufu : WWJD-- "What would Jesus Do " yaani Yesu angefanya nini ?
Nafikiri kwamba swali hili lilihusika na kutusaidia kubadilisha namna yetu ya kuishi. Lakini linaweza pia kwenda mbali : linaweza kubadilisha namna yetu ya kufikiri.
Tunaweza kuomba namna hii :
"Bwana Mungu, natubu sababu mawazo yangu hayakukuwa na mwelekeo kwa Neno lako, na maisha yangu hayajaonyesha kabisa kwamba namna yangu ya kufikiri imebadilika."
Tusikie pia 2Mambo ya nyakati 7:14 :
""ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.""
Toba inahusu kugeuka kuacha maisha yako ya zamani ya dhambi ili kuishi maisha ya ujazo wa Yesu-Kristo. Ni kujinyenyekeza mbele ya Mungu na kusema :
" Bwana Mungu, nasikitika. Nisaidie kuzingatiya kwa namna nyingine maisha mapya ambayo umenipa. Nakubali hii Habari Njema, hii tumaini na haya maisha ambayo umenipa. "
Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni