Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Huduma mpya ya upandaji wa makanisa katika vijiji inaanza wakati Mkufunzi wa VCP anapokusanya wanafunzi ili kupanda makanisa katika vijiji visivyokuwa na kanisa.
Shabaha ya mukufunzi ni kukusanya wanaume na wanawake 15 waaminifu, waliyo tayari na wenye uwezo wa kufundisha. Kaka na dada hao walio tayari na wenye uwezo wa kufundisha wanajitolea kufuata miaka ine ya mafundisho ndani ya vituo vya mafunzo juu ya namna ya kupanda makanisa. Lakini wanajitolea kwa mema zaidi ya kujifunza. Wanajitolea katika kazi ya Mungu : kutumika kwa nguvu kwa kusudi ya kuzidisha wanafunzi, viongozi na makanisa.
Wanafunzi wa VCP wanakumbuka kujitolea kwao kwa fundisha na ongezeka waliyo chukuwa wakati walipoanza kutumika katika kituo cha mafunzo.
Lakini ..., Tuchukuwe mda kidogo kwa kukukumbuka kujitolea huko kunakopatikana kwenye ukurasa 24-32 ya kitabu ''mafunzo ya watumishi wachungaji na wewe''. Vile utakavyoendelea kusoma, chaguwa alama iliyo muhimu zaidi kwako ambayo pia kwako ni vigumu kuitekeleza.
Kujitolea kwa mwanafunzi wa Fundisha na ongezeka pamoja na msaada wa Mungu, najitolea kwa :
- kumpenda Yesu-Kristo na kuweka kipaombele utii kwa amri zake.
- kufundisha wengine kutii amri zote za Yesu.
- kutunza jamaa langu kwa upendo wa kweli (waefeso 5:25-33)
- kuombea kila siku Kondoo, rafiki zangu na wale ambao bado wangali na itaji ya kujuwa Kristo.
- kutumika kwa nguvu pamoja na wengine kwa umoja na upendo, kwa upeke pamoja na kanisa langu, na kusikilia Mwalimu wangu Fundisha na ongezeka na kuongeza kujulisha kazi zangu (Warumi 12:9-11)
- kutowa kiasi cha mda na pesa zangu ili kueneza Ufalme wa Kristo popote anaponiita kwenda (Mathayo 28:18-20)
- kuwa mwaminifu kwa uwezo wa Mungu ili kuruhusu kanisa kukomaa na kujizidisha (Marko 4).
- kufanya nguvu kutii shurti zinazo stahili kwa viongozi wa kanisa, kama vile zinavyoonyeshwa ndani ya 1Timotheo 3:1-7.
- Tangaza injili kwa bidii, upendo na uwazi ili watu waamini Bwana na kumtii. (Mathayo 28:19-20).
- kutafuta upandaji wa makanisa yenye afya ambazo zitajizidisha, kwa kipekee kwa maeneo ambako hakuna kanisa (Warumi 15:20-21).
- kuwa tayari kuteseka kwa ajili ya Kristo (2Timotheo 2:3).
- kufuata mashauri ya mukufunzi na kutekeleza kwa uaminifu majukumu zangu zote kwa kazi na mafunzo.
Ni alama gani kati ya hizi iliyo ya muhimu zaidi kwako leo ? Kwangu mimi, ni alama ya kwanza. ''kupenda Yesu-Kristo na kuweka kipaombele utii kwa amri zake zote ''. Alama hii inanipa mafasiriyo makubwa ya namna inavyonipasa kuishi maisha yangu. Inanikinga na majaribu na kunijulisha ni wakati gani napashwa kuungama na kutubu.
Naipenda sababu inaniongoza mimi kama mwanafunzi wa Yesu. Ni maamuzi gani iliyo ngumu kutekeleza kwako? Kwangu mimi, iliyo nguvu ni ''kukubali kuteseka kwa ajili ya Kristo ''. Sipendi kuteseka. Ninajaribu kuepuka mateso.
Lakini najuwa mimi kama mwanafunzi wa yule aliye vumilia msalaba kwa ajili yangu, nimeitwa pia kuteseka. Japo hiyo, wito huo unanihusu kwa sehemu kubwa. Kwa sasa vile munavyojitolea kufundisha wanafunzi ili kupanda makanisa mapya, muniruhusu niwape moyo kuwaonyesha kujitolea huku.
Muwaulize wanafunzi wenu wajiulize kwa ndani zaidi kujitolea kwa imani. Mungu anafurahi wakati watoto wake wanajitolea kumtii, kutangaza Habari njema na ''kutafuta upandaji wa makanisa yenye afya ambazo zitajizidisha, kwa kipekee kwa inchi maskini'', makanisa mapya yenye afya ambazo zitajizidisha kwa kipekee kwa maeneo ambako hakuna kanisa ''.
Mimi ni Dean Davis : ''ninawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni