Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Siku kubwa inafika. Siku ya ajabu iko mbele yetu. Ni siku iliyo andaliwa na Yesu imepita miaka 1900. Ni siku ya furaha kubwa ! Sikia maneno ambayo Mtume Yohana alitumikisha kwa kuonyesha siku hii kubwa inayokuja: "Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;
wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.
Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,
wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele Amina !" (Ufunuo 7:9-12)
Ni siku ya ajabu ! Kundi kubwa. Ni mkutano mkubwa ambao hakuna mtu awezaye kuuhesabu. Na sio mkutano wa kawaida ; ni mkutano mkubwa wa watu ambao wamepata msamaha ndani ya Yesu-Kristo, Mwana Kondoo wa Mungu, mbaye kwa damu yake iliyomwangika () na kwa ufufuko wake wa ushindi zidi ya kifo, unatowa msamaha wa dhambi na wokovu kwa wote wanao mtumainia.
Watu walio ndani ya mkutano huo hawasemi lugha moja wala mbili, wanasema lugha za dunia mzima. Wanawakilisha mataifa ya kila kabila na kila taifa.
Wametoka wapi na wanafanya kazi gani? Wanatokea kila sehemu. Lakini zaidi, wanakuja kwa Kristo na wamesimama mbele ya kiti chake cha enzi kwa kumsifu sababu wanafunzi wa Yesu, ndani ya vizazi vyote, walitoka na walitangaza Habari njema. Mkutano umesimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kwa sababu mbili :
1) sababu Yesu alilipa deni zote ili waokolewe.
2) sababu wanafunzi wake walizidisha wainjilisti, wafanya wanafunzi na watumishi kutoka kila asilia ili kupeleka Habari njema kwa kila taifa, Kabila na Lugha.
Tukio hili la mkutano mkubwa mbele ya kiti cha enzi ni jambo litakalo kuja. Lilionyeshwa kwa Yohana katika maono imepita sasa miaka 1930. Tukio hili haliwezi kutokea kufuatana na mazingira tuliyo nayo leo, sababu bado kungali kabila nyingi na taifa ambazo hawana hata mtu moja aliye na kanzu nyeupe iliyo safishwa katika damu ya Mwana Kondoo. Jukumu letu ni kuzidisha wafanya wanafunzi ili tukio la Ufunuo 7 mbele ya kiti cha enzi iwe kweli kwa haraka iwezekanayo.
Sasa, kaka na dada zangu, muendelee kuvuka vizuwizi vya asilia ajili ya kumtambulisha Kristo.
Ilikuwa Ongezeka ! Na mimi Dean Davis nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni