Jumamosi, 5 Aprili 2025

Kuwa mfano wa kuongezeka



 Tazama Daneille Snowden na Ongezeka.

Karibu kwenye Ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji, wachungaji na kwa viongozi wakikristo.

Leo, tutazungumzia namna ya kuwa mfano wa kuongezeka.

Kuwa kielelezo kwa mtu, inamaanisha kuwa mfano wa kuigwa (kufuatwa). Hii inamaanisha pia kujenga wala kuunda picha wala sura. Zaidi pia tendo kuongeza inamaana ya kuzidisha kwa hesabu, zaidi kwa namna iliyo juu. Mtume Paulo aliandika :  

''Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.''

1Wakorintho 11:1

Wengine wanaweza kujiuliza hii inatumika namna gani. Namna gani naweza kuongeza na hata kuzidisha ?

Kwa Siku hizi za nyuma, Andiko la Ahadi yangu ni vesi ya Agano la kale, Zekaria 4:6b inayosema :''... Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.''

Tunamaliza kazi hii kwa kutangaza ukweli wa Neno la Mungu. Neno la Mungu halistahili tu kukaa ndani yetu, lakini litumikishwe sabau ya kupanda mbegu nyingi ndani ya roho za watu.

Ni muhimu kutukumbusha kwamba udongo wa roho wa mwanadamu unastahili kutayarishwa na kulimwa ili kupokea mbegu hiyo.

Kwa kufanya hivo, upako mkubwa wa Roho Mtakatifu utawaka ndani ya moyo na kuzaa matunda mengi. Hiyo inafanana kuwa rahisi, sivyo? Ugumu wa jukumu hilo liko kwa ngambo yetu kwa kuacha na kutii.

Inatupasa pia kuendelea mbele na kutokuacha.

Katika Marko 8:34, Yesu anasema :''...Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate'' ni kwake tunapata mwelekeo na namna gani tunaifanya ! Kwa hiyo, inapashwa kumfuata Kristo kwa karibu sana, kukaa ndani yake na ndani ya uwepo wake. Tunafikilia kuachana na matakwa yetu (sababu kila Siku tunatumaini kwamba Bwana atajishugulisha nasi na maitaji yetu), na kwa mwisho, tunastahili KUCHUKUWA Msalaba wetu na kufuata mwelekeo na mfano wake.

Nafikiria maisha yangu ndani ya huduma na ninatambuwa kwamba vile miaka inavyo enenda, niliona mtu moja wa kawaida akiishi tu kwa kawaida maisha ya utii na ya kujitolea.

Je! Nimekwisha kila siku kutimiza yale Bwana aliniitiya kufanya? Apana hata kidogo.

Je! Nimeacha? Ebu kwa kuwa mkamilifu, kulikuwa wakati ambao niliitarajia. Lakini Yesu pamoja na upendo wake walisukuma moyo wangu na wakanipa Roho yake kwa ajili ya mioyo iliyopotea katika dunia hii.

Ninaweza kuwaambia kama, mara na mara, Yesu ananishika mkono, ananihakikishia nguvu yake na, kwa pamoja, tunaendelea kupenda wengine katika Ufalme wa Mungu!

Utafanya namna hii?

Mnifuate, kama ninavyo mfuata Kristo ! Na tutageuka sote kuwa wavuvi wa watu!

Ilikuwa Ongezeka, tunatarajia kwamba utabarikiwa na neno hili la leo ! Usikose kuligawanya pamoja na wengine na kutupata kwenye mtandao vcpencouragement.org

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...