Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.
Kama ilivyo mwaka mpya, nilianzisha mtiririko mpya kuhusu Mada ya uongozi wa muwakili kama ''mtu anaye ongoza rasilimali za mtu mtu mwengine ili kufikia malengo za mwenye mali''.
Leo, tunaendelea na somo letu la mfano wa talanta unaopatikana katika Mathayo 25:14-30.
Katika toleo langu la nyuma, tulijifunza kanuni tatu ambazo zimetolewa ndani ya hadisi; leo, tutajadiliana kanuni zingine ine.
- kila mfanyakazi (wala mwakilishi) atatowa ripoti ya yale aliyofanya kwa ile mifuko ya dhahabu aliyoipokea. 2wakorintho 5.10 inatuambia ''Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.'' kwa vesi ya 21 ya kifungu chetu, bwana anamsifu Mtumishi wa kwanza kwa kusema : ''ni vema, Mtumishi mwema na mwaminifu ! Ni ripoti gani tutaitowa mbele za Mungu kwa yote aliyotupatiya?
- kuko malipo kwa uongozi bora wa rasilimali. Angalia vile vesi ya 21 na 23 zinavyo fanana. bwana wake akamjibu : ''ni vema, Mtumishi mwema na mwaminifu ! Ulikuwa mwaminifu kwa mambo madogo ; nitakupa vitu vingi. Njoo tuchangia mema ya bwanawako. Mtumishi aliyepokea mifuko tano na ule aliyepokea mbili walizipokea sifa zilezile kutoka kwa bwana wao. Katika toleo langu la nyuma, nilitowa tahazari zidi ya mtego wa kulinganisha watu na wengine. Ndani ya VCP, wamoja wanatumika katika eneo ambao udongo wa kiroho uko na rutuba zaidi na ni mahali ambako mavuno ni mengi sana, na wengine wanatumika mahali pa nguvu sana. Matarajio ya bwana yanatokana na mazingira ya mahali ambako kila moja anatumikia.
- Mawakili wabaya watahamakiwa na kuhazibiwa. Ndivyo tuonavyo katika vesi za 24-30. Mtumishi ambaye hakufanya lolote na mfuko wake moja alio upokea aliambiwa Mtumishi ''mbaya'' pia ''mvivu''. Mfuko aliokuwa nao ulinyanganywa. Ndani ya utamaduni wangu, tuko na msemwa usio nanizamu usemao : ''unaitumikisha wala unaipoteza''. Baba yangu, leo tayari amekufa, alinirudilia msemwa huu mara nyingi kipindi cha mafundisho yangu. Je! Muko na msemwa unaofanana na huu? Hadisi hii inatowa ukweli ulio ndani yake.
- kwa mwisho, Mawakili wazuri watajikuta wamepewa zaidi. Kwenye vesi ya 28, tunaona kwamba mfuko ule ulionyanganywa kwa Mtumishi mvivu, ulipewa kwa yule Mtumishi ambaye alikuwa sasa na mifuko 10. Kanuni hapa katika VCP, na katika kila shirika, wale wanaoongoza vizuri rasilimali walizopewa watajikuta kwa mda fulani wamepewa zaidi... Zaidi ya majukumu, zaidi ya madaraka, na pengine zaidi ya mali.
Katika kipindi chetu chakufuata, tutaendelea somo letu juu ya uongozi wa Mawakili.
Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni