Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Uaminifu ni moja ya tabia kubwa za kila mwanaume ao mwanamuke anaye mufuata Kristo. Mtu mwaminifu ni mkamilifu na mwenye haki. Copy iliyo nzuri ni ile inayofanana na ile ya asilia.
Moyo wangu unajaa furaha na tumaini wakati ninapokutana na wanaume na wanawake wanao mtumikia Kristo tangu zamani bila kuchoka.
Petro alitowa maelekezo yafuatayo kwa wanafunzi wake : ''kila moja wenu anastahili kutumikisha karama aliyo ipokea ili kuwahudumia wengine, kama vile Mwakili mwaminifu wa neema ya Mungu kwa hali zake zote.
Je! Wewe ni Mwaminifu ?
Mwanafunzi mwaminifu anawapa wengine kile alichopokea kwa bwana wake.
Na anatowa kwa uaminifu. Mwanafunzi mwaminifu habadilishi kile alichopewa.
Mtume Paulo kwa mwanafunzi wake Timotheo katika 2Timotheo 2:2 ni kifungu cha pili cha maandiko inayotajwa zaidi ndani ya VCP kisha Agizo kubwa.
Maneno hayo ni shurti yetu ya kutembea wakati tunapotumika kwa imani kwa kupanda kanisa ndani ya kila Kijiji cha Afika ifikapo mwaka wa 2050.
Paulo alimwambia mwanafunzi wake Timotheo : ''Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.'' Watu waaminifu, watu wanaofaa, watu wenye kujaa uaminifu. Watu watakao tumika kama Mawakili wema wa ujumbe wa tumaini watakao ipokea.
Je! Wewe ni Mwaminifu ? Wewe ni mfano wa watu ambao Petro alisema wakati alionyesha Mawakili waaminifu wanao tumikisha ujumbe wa tumaini kwa kufundisha wengine? Ao wewe ni Mwakili asiye mwaminifu, mtu anayepokea vizuri kwa mda lakini anagawanya pole pole? Siyo rahisi kwangu kuuliza swali hili, sababu najuwa wengi miongoni mwenu wanaotumika kwa bidii ili kuwasilisha yale waliofundishwa kwa ajili ya Kristo na kwa namna ya kutumikisha huduma yao ndani ya uwezo wa Roho Mtakatifu. Naona uaminifu wako. Japo hivo, nauliza swali : ''je! Wewe ni Mwaminifu ?'' sababu tunastahili kujiuliza mara kwa mara kuhusu Neno la Mungu.
Mwakili mwaminifu anasikia neno la Mwalimu wake, Mwakili mwaminifu anawasiliana na Mwalimu wake, anatumika, anapambana na kuomba ili kuelewa Neno. Mwakili mwaminifu anaweka mafundisho katika vitendo ndani ya maisha yake na katika huduma yake.
Mwanafunzi mwaminifu anafundisha wengine.
Je! Wewe ni Mwaminifu ? Mimi ni Mwaminifu ? Tafazali tuweke katika vitendo na kuwasilisha bila kukawia yale tuliyo fundishwa kutoka waalimu wetu waaminifu, ili wanafunzi wetu pia waweze kufundisha wengine.
Mimi ni Dean Davis nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni