Jambo kwa wote naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Moja ya madai za ajabu sana kuhusu kanisa la kwanza, kanisa lililoanzishwa na mitume pa Yerusalemu Siku ya pentekoste, inapatikana katika Matendo 5:42 :
''Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.''
Hata kama wakati maisha inaendelea vizuri na matatizo ni machache, ni vigumu kufuata huduma ya muhimu bila usumbufu. Kwa mfano, niliwazia kama muundo mpya wa vitabu vya VCP ilikuwa jukumu langu la muhimu ndani ya huduma kuanzia mwaka wa 2019.
lakini kadiri nilivyojaribu kukaza fikira, nilizubaa na kushangazwa na muundo wa somo.
Kwa mwisho, kwa mwezi wa Disemba, nilimaliza sehemu yangu ya mradi huu kwa kuwasilisha somo za muhula wa 8.
Ni vigumu kufuata huduma ya muhimu bila usumbufu. Lakini kanisa la Yerusalemu ''halikuacha kufundisha na kutangaza Habari njema ya kwamba Yesu ni Masiya''.
Kama mulivyojifunza kwa kusoma huduma kenda za kanisa lenye afya, uinjilisti ni muhimu. Kanisa la Yerusalemu lilielewa hivo. Halikuacha kutangaza Habari njema ya Yesu.
Mateso hayakuwaziwia. Matendo 5:40 inatuambia kama viongozi wayahudi waliwapiga fimbo Mitume na kuwakataza wasitamke jina la Yesu. Lakini walipata fursa ndani ya ukumbi wa hekalu na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha.
Magomvi ya wao kwa wao ndani ya kanisa hayakuwaziwia Mitume wa Yerusalemu kutangaza Neno la Mungu. Wakati ulipotokea mgawanyiko kati ya waamini wa lugha ya kiyunani na wale wa lugha ya kiebrania kuhusu ugawaji wa chakula kwa wajane, kanisa, lililoongozwa na m
Mitume, lilipata haraka suluhisho.
Katika Matendo 7:7 inatuhadisia yaliyotendeka baada ya suluhisho ya tatizo ya ugawaji wa chakula. Imeandikwa ''Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.'' Hakuna kitu, hakuna kilicho zuwia kanisa la Yerusalemu kutangaza Habari njema ya Yesu.
Na hakuna chochote kingeweza Pia kuzuwia kanisa zetu. Kama kuko huduma ambayo tunastahili kuendelea kuifanya, ni vizuri kutangaza injili.
Muendelee basi kufundisha na kuandaa washiriki wenu ili watumikishe zana ine za Mpandaji na kutowa injili kwa mtindo wa miviringo tatu.
Fundisho moja halitoshi. Muendelee kuwatuma katika kijiji chenu na vijiji vilivyo kandokando.
Muendelee kuonyesha filamu ya Yesu.
Mufanye mupangilio wa kutumikia vionyesheo ili visibaki kwa mtu bila kutumikishwa na hapo vingeweza kutangaza Habari njema ndani ya Kijiji ambacho hakija sikia injili.
Kama kanisa lako, mfano wa lile la Yerusalemu, ''usiache kamwe kufundisha na kutangaza Habari njema ya kwamba Yesu ni Masiya'', kanisa lako nalo pia litakomaa na kupanuka.
Mimi ni Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni