Jumapili, 6 Aprili 2025

Kuomba na kutegemea Roho Mtakatifu



 Jambo, Tazama ''ongezeka''ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wakikristo katika vijiji.

Mimi ni Brad Snowden.

Kaka na dada, ni furaha kubwa ya namna gani kumtumikia Bwana na ni wito gani muzuri wa kupanda makanisa. Tuko na bahati ya kuona namna vijiji vinavyobadilishwa pamoja na kuwa na tumaini wakati Yesu anagusa maisha ya wengi.

Wito huo unaweza pia kupatwa na vipindi vya magumu mengi kwa utu wetu wa inje.

Tunapenda kufaulu na kuona kile kilicho ndani ya roho zetu kuwa yanatendeka.

Ni kipindi chetu kizuri cha kutembea pamoja na Kristo wakati anapoweka ndani ya roho zetu kile anachotaka kutekeleza. Ni kipindi kizuri sana kwa wapandaji wa makanisa, sababu ni kama vile tunaweza kuona ni kwa namna gani haya yanafananishwa  hata mbele ya hayo kuanza. Ni kipindi cha muhimu cha mpango wa Mungu kwa wale munao watumikia.

Mda huu unaweza pia kuwa moja ya magumu makubwa.

Nikigunduwa mimi kama Mchungaji, vipindi hivi vilinileta kwenye uwanja wa mapambano, nilijuwa kile Bwana alizalisha ndani ya roho yangu, na ningeweza kuyatarajia yote. Lakini hapo ndipo penye tatizo : sikujuwa ninani angeweza kupokea maono ambayo Mungu amenipa.

Sikujuwa namna gani ingezaa matunda, wala pia ni kwa namna gani tungeweza kupata pesa za kuiendelesha.

Vita haikukuwa juu ya uzoefu ao kwa yale ambayo nimejifunza kupitiya mafundisho niliyopokea. Hakuna kibaya kwa kuishi yale ambayo tuliyo fundishwa wala pia yale tuliyoyapitiya hapo nyuma. Shida ilitokea pale nilipotegemea katika vipindi vinavyo nihusu  siyo kwa maono mapya ya Mungu.

Ushindi mkubwa ambayo Mungu hajawai kuniruhusu kuishi ilifanyika wakati niliposema; ''sijue ni kwa namna gani utaichukuliya. Sijue ninani atatembea pamoja nami ili nione ginsi kazi yako itatendeka. Oh Bwana, naitaji unisaidiye kuelewa na kutekeleza kazi hii uliyoniitiya kutenda.

Yakobo 1;5 anasema; ''Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.''  Bwana hatuangalii kwa juu wakati tusemapo : ''sijue chakufanya'' ao ''sielewi kabisa kila napashwa kufanya''. Neno la Mungu linasema tuombe tu kwa unyenyekevu, sababu tuko na mtoaji mwenye huruma anayeweza kufunguwa macho yetu ili kuona. Tunaweza kutegemea sauti ndogo ya ukimya ya Roho Mtakatifu itakayo tupatiya uelewa mpya wa namna Mungu anataka kutenda ndani yetu na kupitiya sisi. Oh, Mpandaji wa kanisa, ushindi wetu unatokea wakati tunapoomba Roho Mtakatifu afanye kazi na ginsi tunavyojitolea kwake.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa.

Ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Mungu awabariki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...