Jumamosi, 5 Aprili 2025

Wote wamesikia Neno la Mungu




 Jambo kwa wote naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Mwanzilishi wa ''One Mission society'' ni mtu anayejulikana kwa jina la Charles Cowman, alipata wito wa kumtangaza Kristo. Alipata msukumo kutokana na kifungu cha Marko 16:15, mahali ambapo Yesu anawaomba Mitume wake kwenda ulimwenguni kote na kuihubiri Habari njema kwa kila kiumbe.

Cowman alipendelea kwamba kila mtu asikie Habari njema. Moja ya yale aliyoyafanya huyu mwanzilishi wa ''O.M.S.'' ilikuwa utekelezaji wa Kampeni kubwa ya Kijiji '' iliyo ruhusu kuleta injili kwa kila jamaa ya Japani mnamo miaka ya 1912 hadi 1918.

Cowman alitambuwa upendo wa Mungu kwa kila mtu na ndipo sasa akafanya nguvu ili kwamba kila mtu apate kusikia Habari njema ya wokovu ndani ya Krsto.

Kwa bahati mbaya, hata leo, pamoja na teknolojia tuliyo nayo, si vyepesi kwamba kila mtu kutoka  katika kila mkowa, jimbo wala inchi awe tayari amesikia Habari njema ya wokovu ndani ya Kristo.

Lakini kitabu cha Matendo ya Mitume kinatueleza kuhusu kipindi kikubwa cha miaka mbili mda ambao mkowa wote mzima ulisikia Neno la Bwana.

Paulo alikuwa Efeso, fasi ambayo kwa leo ni Uturuki. Matendo 19 inatufundisha kwamba Paulo alifundisha ndani ya Sinagogi kuhusu Ufalme wa Mungu.

Sikiliza Matendo 19:9,10 :''Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tirano. 

[10]Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hata watu wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani. 

Nini? Paulo anafundisha ndani ya ukumbi mkubwa kwa mda wa miaka mbili na wakaaji wote wa mkowa mkubwa wa Kirumi wanaisikia Neno la Bwana ? Hiyo ilitendeka namna gani? Kifungo kinatupatiya alama tatu.

Alama ya 1: Mungu alifanya miujiza ya ajabu kupitiya Paulo. Na hiyo ilileta msukumo mkubwa kwa watu wengi ambao hawangeweza kusikia Injili kwa namna ingine.

Alama ya 2: Paulo alikuwa na wanafunzi pamoja naye wakati alikuwa akifundisha na kufanya huduma yake ndani ya huo ukumbi mkubwa.

Wanafunzi wanafanya kila ambacho Mwalimu wao anafanya. Paulo aliongea kwa namna ya kushawishi kuhusu Ufalme wa Mungu, na wanafunzi walifanya namna hiyo. Paulo alikuwa akibishana kila Siku ndani ya ukumbi mkubwa wa Tirano, na hakuna Shaka kwamba wanafunzi wake, walifanya nao Pia mabishano kuhusu Yesu katika sehemu zingine za mikowa ya Asia.

Alama ya 3 inatusaidia kuelewa ginsi wakaaji wote wa mkowa walivyosikia Neno la Mungu. Wanafunzi, kama vile Paulo, walijazwa Roho Mtakatifu.

Vipi sasa kwako pia?

Utashinda tatizo la kumusaidia kila mtu wa kamati yako, Jimbo lako, mkowa wako kusikia Habari njema ?

Unafuata mfano wa Mtume Paulo na wa Charles Cowman ? Kama unatarajia kwa kweli majirani wako wote wasikie na kuelewa Habari njema, tafakari kuhusu Matendo 19:1-11 itakupa fursa nzuri ya kuanza. Ujazwe na Roho Mtakatifu, uombee wagonjwa, andaa na kuruhusu wanafunzi kwenda.

Uwe mwaminifu kwa Mungu ili huduma yako ya injili ipate kuenea na kuwa na matokeo makubwa.

Mimi ni Dean Davis nawauliza, ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...