Jumamosi, 5 Aprili 2025

UONGOZI WA MUWAKILI - Mfano wa Muwakili Mwaminifu na mMwenye busara Sehemu 1


 Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Kama ilivyo mwaka mpya, nilianzisha mtiririko mpya kuhusu Mada ya uongozi wa muwakili.

Mwandishi moja anatafsiria Mwakili kama ''mtu anaye ongoza rasilimali alizopewa na mtu mwengine ili kufikia malengo ya mwenye mali ''

Leo tunaendelea na somo letu juu ya mfano wa Mwakili mwaminifu na mwenye busara ambaye tunamukuta katika kitabu cha Mathayo 24:45-51 na katika Luka 12:42-48.

Kwa kifupi, Yesu alihadisia hadisi hii ili kufundisha wanafunzi wake kwamba matendo yetu yanaonyesha yale tunayo yaamini kweli. Wanaomtii Mungu watalipwa, lakini Wale wasiomtii wanaonekana kuwa siyo waaminifu na wanafiki kupitiya matendo yao.

Mfano huo unafundisha vile vile kwamba Mitume wa Yesu wanastahili kuishi wakiwa kila Siku tayari kwa kugonja kurudi kwake.

Yesu anauliza swali hili kwa vesi ya 45 kwa kitabu cha Mathayo :Ni mwanafunzi gani mwaminifu na mwenye busara (kwa kitabu cha Luka, neno hili linatafsiriwa ''Mwakili''), ambaye bwana wake amemuwaka juu ya watumishi wa nyumba yake ili kuwapa chakula kwa mda mwafaka?

Ningependekeza tuangalie hapa kwamba:

- watumishi waaminifu, wala Mawakili, waliwekwa juu ya watu wengine. Mwelekeo, wala uangalizi wa watu ao wa kazi za huduma, ni kipendeleo na wito wa Bwana wetu. Mwakili hakujichaguwa mwenyewe kwa kazi hiyo, ni Bwana ndiye aliyefanya hivo.

- watumishi waaminifu, ao Mawakili, wanawapa watumishi wengine ''chakula chao kwa mda mwafaka''. (Kifungo cha Luka kinasema anagawanya chakula chao'').

Sisi kama viongozi, ni majukumu yetu kujibu kwa maitaji ya wale tunao waongoza.

Katika VCP, ''chakula chao'' inaweza kuwa maono, kutiya moyo, motisha, mafundisho na mafunzo, marudilio ya somo wala mambo mengine. Viongozi bora na wachaMungu wanastahili pia kutowa vitu hivyo ''kwa mda mwafaka''.

Mfano unaendelea kwa vesi 46 na 47. Mtumishi ambaye wakati bwana wake aliporudi, atamkuta akitenda hivi atafurahi.  Nawaambia hakika, atamukabizi Mali zake zote.'' Yesu anafundisha - kama kwa mfano wa Talanta - kwamba Wale walio waaminifu watalipwa. Katika kipindi cha utangulizi wa huu mtiririko, niliongelea Mada Tano za mifano ya Yesu juu ya Uwakili.

Moja ya Mada hizi ni kwamba Mawakili waaminifu wanaendelea, ndivyo ilivyo onyeshwa hapa.

Kwa hatuwa hii, nitarejelea kwa tafsiri ya Luka, mahali ambapo tunasoma kwa vesi ya 45.

Lakini tuseme hivi kwamba Mtumishi atajiuliza : ''bwana wangu anakawia kurudi'', na akianza kuwanyima watumishi wenzake, wanaume na wanawake, chakula, kinywaji na kuanza kulewa pombe.

Mfano huo mbaya unatuonyesha kama Mawakili waaminifu wanastahili kuepuka kurizika na kushikilia heshima.

Kwenye kipindi chetu cha kufuata, tutaendelea na somo letu kuhusu Mwakili mwaminifu na mwenye busara.

Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wakikristo katika vijiji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...