Tazama Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wa kikristo katika vijiji.
Mada yetu katika mwaka wa 2025 ilikuwa uwakili wa uongozi, na leo tumeanza mwaka mpya wa 2026 na mtiririko unaohusu maendeleo ya Uongozi. Mada ya mwaka huu inatokana na maongezi niliyokuwa nayo kwa mwanzo wa Disemba wakati wa shauri la ''coalition of the willing'' pa mji wa Lomé.
J.J, kiongozi wa kazi za ''coalition of the willing'' aliniuliza swali lifuatalo :
''Tufanye nini ili VCP izidishe maradufu kwa miaka mitano ijayo?''
Lilikuwa swali nzuri, ambalo nilifikiria kwa mda mchache.
Nawaza kwamba ni Bwana aliyenileta kwa haraka kwa kutekeleza kwamba tayari imezidisha maradufu kwa miaka mitano ya nyuma. Mbele ya COVID, VCP ilikuwa na vituo vya mafundisho 350 ndani ya inchi 19 ; leo , tunatumika ndani ya inchi 36 tukiwa karibu na vituo 900 vya mafundisho. Tunashukuru Mungu kwa ukuaji huo.
Kwa kurudilia swali la J.J, Bwana amenionyesha kuwa mipaka yetu siyo pesa. Bwana ameonyesha kwa mara nyingi akiba yake kwetu.
Naamini kwamba mipaka yetu kwa Sasa kwa ukuaji mkubwa zaidi unatokana na umuhimu wa kuchunguza, kusisimuwa, kuandaa na kuwaachilia viongozi.
Tuko na haja ya wakufunzi wengi, waratibu wengi, makasisi wengi wa VCP.
Tuko na haja ya warahisishaji wengi wa kuzidisha makanisa na watumishi wafazili katika inchi ya Marekani. Tuko na haja na wafundi wenye uzoefu katika Bara la Afrika, pamoja pia na wasimamizi wa miradi katika Afrika na Ulaya. Na kwa misingi ya hayo yote, tuko na haja zaidi ya watu wenye kujitolea katika maombi.
Kutokana na hayo, katika mwaka wa 2026, mtiririko huu wa podikasti utahusika zaidi na Maendeleo ya Uongozi. Makasisi na waratibu, najielekeza kwenu kwa mda huu. Ninaitaji msaada wenu kwa kutafsiri na kugawa vipindi hivi kwa wale mnao waongoza.
Nawaomba pia kuwa waangalifu katika juhudi yenu kwa kuchunguza, kuandaa, kufundisha, kuachilia na kuacha huru viongozi wanaopanda viwango. Tazama kanuni moja muhimu ya kuzingatiya :
Wasimamizi, wakati bado hamujatayarisha mtu wa kukugombowa, hauwezi kulinganishwa kwa kupanda cheo. Narudilia : wasimamizi, wakati bado hamujatayarisha na kuchunguza mtu wa kukugombowa, hauwezi kupandishwa cheo ; ungali peke yako tu mwenye uzoefu wa kutumika kwa wazifa wako wa sasa.
Nitahitimisha kipindi hiki kwa maono ya Yesu kuhusu uongozi, ambayo inatokana na Mathayo 20:25-28. Kulingana na Mungu, viongozi wameitwa kutumikia wale mnao waongoza.
Yesu akawaita nakusema :
''Mathayo 20:25-28
[25]Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.
[26]Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;
[27]na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;
[28]kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.''
Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na kwa viongozi wa kikristo katika vijiji

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni