Mimi ni Chuck Rapp na ''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji na waongozi wao.
Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Katika toleo langu la tarehe 23 Januari, nilielewa na kuwapa moyo viongozi kuwa waangalifu sana na watu wakaribu na kuchunguza pamoja na kufundisha viongozi wapya.
Leo, na katika vipindi vijavyo, natarajia kugawa mawazo mamoja kuhusu mwenendo ninao utafuta kwa viongozi wa baadaye. Pengine muko na tabia zingine ambazo munaendelea kutekeleza : ikiwa hivo, usisite kunijulisha. Nazingatiya pia kuonyesha kwamba ni mawazo na uchunguzi wangu binafsi. Wengine wanaweza kuwa na mawazo tofauti. Horoza hii haitoshi ; naamini kwamba kuko tabia zingine muhimu kwa viongozi wanaokuja. Ya kwanza, napata utambulisho wa kibinafsi unaopata mizizi katika Kristo. Wakolosai 3:3 inasema "Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.'' nafurahia matumizi ya neno '' kufichwa '' ya Mtume Paulo, sababu kiini cha kweli cha maisha ya mwamini iko ndani ya usalama na ulinzi wake katika Kristo.
Umenisikia pengine nikikazia katika podikasti zangu za mbele kuwa moja ya matokeo ya hatari sana ni ile ya mtu kuwa kwenye mstari wa uongozi kisha anakosa kujiamini. Kwa hatuwa tofauti, kiongozi ambaye usalama wake uko na mizizi ndani ya Kristo yuko na uaminifu ndani ya Bwana anaye muruhusu kutumikia wengine. Wafiliipi 2:4 inatufundisha kwamba ''Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.'' kwa hisia hii ya utambulisho wakibinafsi wenye mizizi ndani ya Kristo kunaongezeka unyenyekevu.
Ni tabia inayo jionyesha katika utumishi wa kutafuta faida kwa wengine.
Sikubaliani na wale wanao onyesha mwenendo wa kujinyanguwa ''kama watu maarufu''. Katika tafsiri ya J.B. Philips, tunasoma haya katika Warumi 12:3 . Mimi kama mwongozi wenu wa kiroho, ninawapa shauri hili :Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. Shauri gani kubwa namna hii! ''Msijidanganye kwa kunia makubwa, lakini mujitaidi kuwa na uhakika wa uwezo wenu... Ni shauri gani kubwa namna hii! ''Msijidanganye kwa kunia makubwa, lakini mujitaidi kuwa na uhakika wa uwezo wenu.'' Chuck Colson, kiongozi mkubwa katika maisha yangu, alizoeya kusema hivi : "anaye tarajia kuwa kiongozi akijizania kuwa ubinafsi wake unaenea tayari atashindwa.'' imenichukuwa miaka mingi kwa kuelewa somo hili muhimu.
Nitaendelesha mawazo yangu juu ya tabia za kutafuta kwa viongozi wabaadaye katika podikasti yangu itakayofuata.
Hii ni ujumbe wa kutiya moyo kwa wapandaji na viongozi wa makanisa katika vijiji.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni