Jumatano, 11 Machi 2026

RAMANI YAKO YA MAWASILIANO

 








       Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama "ongezeka" ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.

Hatujuwe habari zaidi inayo muhusu Mtume wa Yesu aitwaye Nathanaeli.

Lakini kitu kimoja ni kweli : iko na deni ya kumshukuru Mtume mwengine Filipo. Sikiliza Yohana 1:44-49 :"Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. 

Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. 

Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. 

Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.

Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. 

Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli." Amini ao usiamini, Nathanaeli hakujuwa la kufanya, alikuwa na mawazo mabaya zidi ya watu wa Nazareti, siyo wanazareti tu pengine hata pia na mkowa mzima wa Galilaya. Hakufikiri kwamba mtu mwema wala mawazo mazuri yanaweza kutokea Nazareti. Lakini rafiki yake Filipo alimuona Nathanaeli na kumshuhudia Yesu. Alikazia kwamba Yesu alikuwa Masiya ambaye Musa na Manabii walisema. Na, kitu cha kushangaza, ijapokuwa mawazo yake mabaya, wakati Filipo aliposema tu : ''njoo uone'', Nathanaeli akakutana na Yesu na akamjuwa kama Mwana wa Mungu. Ni urafiki gani uliyokuwepo kati ya Filipo na Nathanaƫl ? Walikuwa wandugu? Walikuwa wanaungana kwa kiapo? Wala walikuwa tu marafiki wazuri? Hatujuwe. Lakini ni wazi kwamba, walikaribiana sana, sababu Nathanaeli alikuwa mtu wa kwanza miongoni mwa watu ambao Filipo alisema baada ya kukutana kwake na Yesu. Filipo alifurahia wazo ya kukutana na Masiya ambaye wangestahili kugawana Habari njema. Akamwambia Nathanaeli, rafiki wa karibu. Uko na urafiki mzuri na mtu yeyote. Uko na Habari njema ya kumwambia, unamjuwa Yesu Masiya. Unajuwa kama ni Mwokozi wa ulimwengu. Unajuwa kama anatusamea dhambi, anatupa nguvu na anatupa uzima wa milele kwa wingi.

Sasa, andika ramani ya mawasiliano.

Chora kiviringo katikati ya karatasi na uandike ndani yake jina lako. Baadaye, chora mistari inayo unganisha kiviringo chako na majina ya marafiki na watu wakaribu yako ambao unajuwa wako mbali na Mungu. Kata mistari kwenye majina yao na marafiki zao na watu wa jamaa zao ambao nao pia wako mbali na Mungu. Utapata sasa ramani ya mawasiliano. Omba kwa ajili ya kila mtu aliye kwenye ramani yako. Baadaye, tarajia kwenda kuwaona ili kugawanya nao ushuhuda na Habari njema ya Yesu. Nani anajuwa? Kwa kwenda kuwaona, marafiki zako wanaweza kukushangaza. Wanaweza kuitikia mwito wa Yesu kama imani ile ile ya Nathanaeli wakati Filipo alipo muongoza kwa Bwana imepita sasa miaka mingi.

Ilikuwa ''ongezeka'', na mimi Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MIVIRINGO TATU AJILI YA KUWAFANYA WANAFUNZI

  Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa mak...