Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis na tazama ''ongezeka'', ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji.
Bwana na Mwokozi wetu Yesu-Kristo alitowa neema kwa mwili wake, ambalo ni kanisa, ili sote tubarikiwe pamoja, ili kwamba tuishi kwa umoja na kutembea kwa imani. Neema, upendeleo na nguvu anazozitowa kwa kanisa zinaonyeshwa kwa njia mbali mbali. Lakini moja ya mambo muhimu na yenye kuvutiya ni kwamba Kristo alitowa neema yake kupitiya watu.
Hata kama sote tunakuwa viungo vya mwili moja, kila moja wetu anachangiya kwa namna yake.
Waefeso 4:7 inasema:
''Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.''
Mtume Paulo anaongeza kwa kueleza namna gani Kristo anatowa neema hiyo kwa kanisa.
Anasema katika Waefeso 4.11-13 :
''[11]Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
[12]kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
[13]hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;''
Ni ukweli unao onekana vile Paulo anatangaza kwa kanisa la mpya la Efeso. Kristo alitowa aina tano ya watu ili kujenga mwili wa Kristo. Anatowa aina hizi tano za huduma ili kwamba mwili wa Kristo ukomae na kuwa na nguvu : Manabii, Mitume, wainjilisti, wachungaji na waalimu.
Sasa, kama Yesu anawapa watu hawa kwa ujenzi wa mwili wake, je! Hatutawatafutiya miongoni mwa washiriki wa kanisa zetu?
Hatuwezi kujiuliza swali hili :
'' ni nani miongoni mwa washiriki wetu ni Mtume ambaye Mungu alitupatiya? Ni wanani Manabii? Na wachungaji na waalimu ?
Kwa kujibu kwa swali hizi, mara nyingi tunasubiri mshiriki moja wa kanisa asimame na kuchukuwa nafasi muhimu ya uongozi mbele ya kusema :
''Ah, huyu ni mwinjilisti'' , ao ''yule dada pale ni Nabii'' ao tena ''dada huyu ni Mwalimu''. Na wengi wanasita kuhakikisha kwamba mshiriki anaweza kuwa na karama za Utume. Neno ''Mtume'' liko na tafsiri nyingi. Kufuatana na asili za kanisa, neno hili limewekwa kwa ajili ya aina ya watu fulani.
Lakini ndani ya Agano Jipya, neno ''Mtume'' linamaanisha tu ''anayetumwa'' ao ''mwenye kupeleka ujumbe'' wamitume ni wenye kutumwa na Bwana na kanisa ili kueneza ujumbe wa wokovu na kupanda makanisa mapya.
Kwa mjibu wa Waefeso 4, Mtume ni mtu ambaye Yesu-Kristo alimpa neema, upendeleo, hekima na nguvu, ambaye matunda ni kutangaza ujumbe wa Kristo, upandaji na kuongezeka kwa makanisa katika maeneo mapya.
Ni akina nani ndani ya kanisa lako, walio na mwelekeo, maono na uwezo wa kuanzisha na kuongeza makanisa pale ambapo hayajakuwepo?
Ni vizuri kutambuwa hayo maoneo, kuomba kwa ajili yao, kuwapa moyo na kuwafundisha kwa ajili ya mavuno mengi.
Nani anajuwa? Unaweza fanya kwa watu hawa kile ambacho Barnaba alifanya kwa Mtume Paulo.
Alimbariki mbele ya wengine ambao walikuwa bado kutambuwa wito wake wa kiutume.
Kwa kufanya hivo, Barnaba alifata mfano wa Yesu katika ujenzi wa kanisa - tendo ambalo mpaka leo tunaona faida yake.
Mimi ni Dean Davis, nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni