Jambo kwa wote, naitwa Dean Davis, na tazama''ongezeka'' ni podikasti inayoleta neno la kutia moyo kwa wapandaji wa makanisa katika vijiji. Tunapowatazama viongozi, mara nyingi tunaona aina mbili: wale wanaowatumia wengine kuendeleza kazi zao, mamlaka, na madaraka, na wale wanaowatia moyo wengine kwa kufanya kazi pamoja kufikia malengo. Ulimwenguni, tunatarajia kupata viongozi wanaotumia fursa ya walio chini yao.
Lakini daima ni uzuni kugundua viongozi wanyanyasaji ndani ya kanisa. Hata hivyo, ni lazima tutambue kwamba baadhi ya viongozi wa Kikristo hutumia watu kujiendeleza badala ya kutumikia na kuunga mkono ukuaji wao. Yesu alituonya kuhusu viongozi hao. Siku moja, alipowaona wanafunzi wake wakigombania mamlaka, aliwaambia, “Mnajua ya kuwa watawala wa mataifa hutenda kwa mamlaka, na wakubwa wao huwatumikisha; haitakuwa hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkubwa kati yenu lazima awe mtumishi wa wengine, na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza lazima awe mtumwa wenu, kama Mwana wa Adamu, ambaye hakuja kutumikiwa bali kutumikia na kutoa uhai wake uwe fidia ya wengi.” Ni nini kinachoweza kuwa wazi zaidi? Yesu anatarajia wanafunzi wake wawaongoze wengine, kama vile yeye alivyowaongoza.
Yesu alikuwa mwalimu mkuu; alitumia muda mwingi kuwafundisha wanafunzi wake. Yesu alikuwa mpangaji mkuu. Alipanga huduma yake na ya wanafunzi wake. Yesu alionyesha nguvu za kiroho kwa kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Lakini yote haya yalifanyika kwa wema. Kumbuka maneno ya Yesu: Aliwaambia wanafunzi wake, kwa maneno yenye kujaa upole zaidi, "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."
Kama wafanya wanafunzi, tunawaita wanafunzi wetu kuishi kwa viwango vya juu. Tunawatarajia kwao watubu njia zao potovu. Tunawatarajia wafanye kazi kwa bidii katika huduma yao kwa Kristo na kanisa lake. Tunatarajia wasamehe wengine wanapokosewa. Tunatazamia wanafunzi wetu watoe wakati kwa maombi, kufunga, na kujifunza Neno la Mungu. Tunawaita wanafunzi wetu kuishi kwa viwango vya juu. Lakini hii haimaanishi kwamba tunapaswa kuwa wakali kwao. Yesu alisema, “Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo'' Yesu anatoa pumziko kwa ajili ya roho za wafuasi wake. Vipi kuhusu wewe? Je, wafuasi wako wanakujua kama mwanamume au mwanamke mkarimu au mkali? Unapowaita wafuasi wako kufanya kazi kwa bidii, je, unahakikisha pia kuwapa muda wa kupumzika na kuongeza nguvu? Wakati tabia zao zinahitaji kurekebishwa, je, unakumbuka pia kuwapa maneno ya kutia moyo na matumaini? Unaweza kuwa mkarimu na bado ukawa kiongozi hodari. Unaweza kuwa mkarimu na bado ukatimiza mambo makubwa. Roho Mtakatifu anataka kukusaidia. Kwa hivyo, neno langu la kutia moyo leo ni: “Enendeni katika Roho ; dhihirisha matunda ya wema. Usiwatawale wanafunzi wako, bali watumikie kwa wema. Kwa kufanya hivyo, Mungu atatukuzwa, wanafunzi wako watatiwa nguvu, na kwa pamoja mtatimiza mambo makuu.
Ilikuwa ''Ongezeka''na mimi ni Dean Davis nawauliza ni pamoja na wanani utagawanya nao leo neno hili la kutiya moyo ?

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni