Mimi ni Chuck Rapp na ongezeka, ni podikasti inayoleta neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wakikristo katika vijiji.
Mada yetu katika mwaka wa 2026 ni maendeleo ya Uongozi. Katika podikasti yangu iliyopita, tulijadili ginsi Yesu alivyokuwa akichukuwa mda wa kukaa pamoja na Mitume wake na ginsi ilivyoleta faida kwa maendeleo ya Uongozi wao. Leo, tunajadili swali hili kwa undani zaidi.
Yesu alifundisha makundi na kutowa maelezo na maelekezo ya kina zaidi kwa Mitume.
Tunapata ndani mfano kupitiya mfano wa mpandaji, unaotolewa katika Marko 4.
Kwa vesi ya 1 na ya 2, tunasoma :"Akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkubwa mno, hata yeye akapanda chomboni, akakaa baharini, mkutano wote ulikuwako juu ya nchi kavu kando ya bahari.
[2]Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, akawaambia katika mafundisho yake"
Mbali zaidi kwenye sura hiyo kwa vesi ya 10. Tunasoma :"Naye alipokuwa peke yake, wale watu waliomzunguka, na wale Thenashara, walimwuliza habari za ile mifano." Yesu akachukuwa vesi kumi zifuatazo ili kueleza mfano huo na kuelewesha hao Mitume 12.
Mbali tena zaidi katika 4, Yesu anasimulia mfano wa mbegu ya haradali, na hadisi inaishia kwenye vesi ya 33 na 34 :"Kwa mifano mingi ya namna hii alikuwa akisema nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulisikia;
[34]wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake mwenyewe mambo yote kwa faragha."
Sehemu ingine, katika Mathayo 13, Yesu alifundisha kupitiya mfano wa magugu. Kwenye vesi ya 36, tunasoma : "Kisha Yesu akawaaga makutano, akaingia nyumbani; wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Tufafanulie mfano wa magugu ya kondeni."
Wakati tutakapo tumikisha mtindo wa Yesu katika mwelekeo wetu wa maendeleo ya Uongozi, shurti ambalo ningependelea ni hili lifuatalo : hata kama Yesu alifundisha makundi kwa kawaida alielewesha mifano yake kwa watu wa karibu yake sana.
Ndivyo ilivyo mara nyingi leo na viongozi wa makanisa na viongozi wa VCP. Habari zinaweza, na zingestahili kugawanywa fasi nyingi, lakini maelezo kuhusu mafikiri na mazingatio yote yaliyosababisha kuleta maamuzi mara nyingi yanaachiwa kwa watu walio karibu na viongozi.
Hayo yanafanyika pia wakati tunapo shindikiza viongozi wanaojitokeza katika maendeleo yao.
Wakati tunapo chukuwa maamuzi yaliyo na faida kwao, mara nyingi ni muhimu sana kuwa na mawasiliano pamoja nao ili kuwaelewesha mafikiri yetu. Hii ni kwa ajili ya kuwasaidia kutengeneza vizuri uwezo wao binafsi wa Kuchunguza na kuwatayarisha kusimamia majukumu makubwa yajayo.
Ilikuwa neno la kutiya moyo kwa wapandaji wa makanisa na viongozi wakikristo katika vijiji.



.jpeg)
